Mheshimiwa the Don

Mogambi

JF-Expert Member
May 25, 2012
209
351
MHESHIMIWA THE DON
DAVID NGOCHO SAMSON

~1~

Geofrey Mtemvu alikulia katika familia yenye uwezo ya Mzee Ally Magubi Mtemvu baada ya wazazi wake kumtelekeza kwa kukosa uwezo wa kumlea. Alichukuliwa na familia ya mzee Ally, akiwa kichanga kabisa pale mama yake mzazi alipomtelekeza mlangoni mwa nyumba ya mzee huyo. Hivyo alikua na kusomeshwa na Mzee Ally hata kufika chuo kikuu. Hakuwahi kufahamu historia hiyo ya kutelekezwa hadi alipomaliza elimu ya chuo kikuu.

Akiwa shule ya sekondari alipata kukutana na binti mmoja aliyejulikana kwa jina la Asha, ambaye alidhani walipendana sana ingawa hawakudumu pamoja, kwa sababu Asha alihamishwa shule na kwenda kusoma huko Arusha.

Kwa kipindi hicho, miaka ya 90 Hadi 2000 mwanzoni, ilikuwa hakuna mawasiliano ya simu za mkononi, njia pekee na rahisi ilikuwa ni kuandikiana barua. Geofrey akawa anatuma barua mara kwa mara lakini hakuwahi kupata majibu kutoka kwa Asha, na hivyo, wakawa wamepotezana kabisa kila mtu akianzisha maisha mapya mbali na mwenzake. Hivyo ndivyo Geofrey alivyoamini. Hata hivyo, hakuvunjika moyo. Aliamini ipo siku wangekutana tena na mpenziwe Asha.

Baada ya kumaliza elimu ya sekondari kidato cha nne alifaulu na kwenda kidato cha tano ambako alijitahidi na kufanikiwa kufaulu kwenda Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Hakuamini macho yake alipomuona Asha. Geof akajua, Mungu alikuwa amewapa nafasi nyingine tena. Akamfuata Asha akiwa mwingi wa bashasha na tabasamu.

Akajaribu kumkumbushia zamani, kwamba daima alikuwa moyoni mwake na alimhitaji sana maishani mwake. Lakini wasemavyo waswahili, asiye bahati habahatiki. Tayari Asha alikuwa na mpenzi mwingine. Hivyo kwa huzuni, Geof alibaki mpweke.

Baada ya chuo kila mtu alitawanyika, na kuanza kuyasaka maisha ambayo yalionekana kuwa magumu licha ya elimu zao za chuo kikuu. Geof alifanikiwa kupata kazi mapema kwani mzee Ally alikuwa na marafiki wengi waliokuwa kwenye vitengo vizuri, na akiwa na digrii ya biashara , Geof aliajiriwa na Shirika la Umeme kama mhasibu jijini Dar es salaam.

Kwa mara ya tatu akawa amekutana na Asha na kwa kipindi hicho Asha alikuwa yuko peke yake, na atafutaye hachoki, Geof alifanikiwa kupata penzi la mwanamke aliyekuwa akimpenda sana, Asha. Geofrey aliamini kuwa walipendana sana. Hakutaka kuchelewesha mambo, akamweleza Asha kuwa alitaka wafunge ndoa mapema ili waishi kama mume na mke.

Hakufurahishwa na wao kuendeleza mahusiano bila ndoa. Asha hakuonekana kuwa na kipingamizi kwa wakati huo, hali hiyo ikampa Geof matumaini kuwa hatimaye angeishi na mwanamke wa ndoto zake. Ilifikia kipindi wakakubaliana kuoana, hatua ya kuanza kuandaa mipango ya kufunga pingu za maisha ili waishi kama mume na mke ikawa wazi.

Mambo yalizidi kupamba moto kuelekea harusi ya wawili hao, lakini kulikuwa na jambo ambalo lilikuwa litokee, jambo hilo lilikuwa moyoni mwa Asha kwa muda mrefu na alikuwa anajitahidi kujinasua lakini likawa linazidi kumshinda.

Historia yake ilichangia kulifanya jambo hilo, kila alipokumbuka limfanye ageuke mnyama, na kumpa taswira mpya kabisa juu ya wanaume. Ukweli ni kwamba, Asha hakuwa na imani na mwanaume. Alikuwa na chuki dhidi ya wanaume, kila siku alijiuliza ni kwa nini wanaume walikuwa laghai.

Hapo awali, Salimu, alikuwa mwanaume aliyekuwa mwanaume wa maisha yake na si Geof. Geof alikuwepo tu kutoa upweke aliokuwa nao, lakini hakuwahi kuingia moyoni mwake japo alijitahidi sana ampende Geof, hata hivyo haikutokea tu. Lakini kwa vile Geof alimpenda, hiyo ilimpa faraja ya kumfanya aonekane miongoni mwa wanawake wenye kupendwa, kwani nani asiyetaka kupendwa? Potelea mbali kupendwa na usiyempenda ilimradi usionekane wewe hupendwi kabisa.

Hiyo ni faraja kubwa, hasa baada ya uliyempenda kukuacha na wewe kujihisi huna thamani na mara tu, mwingine atokee akiwa hanenepi kwa jinsi anavyoelemewa na penzi juu yako! Ni faraja kubwa sana. Lakini pia, alimuonea huruma Geof, mwanaume alikuwa hakati tamaa, alikumbuka harakati zake tangu enzi za sekondari. Alikuwa akimpenda kweli kweli na ilimchukua muda kutamka kile alichokuwa amemwonesha kwa vitendo. Akamtolea nje kiguberi, bila chenga wala soni. Alipomtamkia,

“Sikupendi Geof, sitaki kukutia moyo bure.”

Ni hiyo kumbukumbu iliyomtia huruma walipokutana kwa mara ya tatu akibembeleza pendo. Hilo ndilo lililomuunganisha Asha kwa Geof. Lakini alipokumbuka kwamba alibakia dakika tu kufariki dunia hapo awali, upendo wa Geof kwake ulionekana usanii tupu. Penzi la Asha kwa Salimu lilipotezewa kama ilivyo rahisi kufumba na kufumbua macho. Alimpenda sana mwanaume huyo lakini mwanaume huyo alimwacha katika kipindi kigumu na kwa fedheha kubwa, kitendo kilichosababisha Asha kujinywesha sumu ili ajiue na kuepuka aibu na fedheha ya kuachwa.

Baada ya kupona kifo hicho, alijifunza kitu. Hakukuwa na cha maana kilichokuwa kimtoe uhai, huku mwanaume aliyekuwa afe juu yake akiwa hana habari ya kilichotokea. Mwanaume huyo alimwacha na kumuoa mwanamke mwingine, na hakuwa mwanamke mwingine tu bali rafiki yake mkubwa, waliyesoma na hata kulala pamoja huko chuo kikuu.
Eve!

Eve. Huyo akawa chanzo cha fedheha yake iliiyopelekea kujinywesha sumu, huku yeye akila raha na mwanaume aliyekuwa anampenda. Akamshuhudia kanisani mbele ya askofu wakiwa wanafunga pingu za maisha. Akatamani apae au hata atoweke kama jini, akashindwa na hapo ndipo alipopata wazo la sumu.

Kitendo hicho kiliyabadilisha maisha ya Asha na kumfanya adharau na kupuuza maneno matamu ya wanaume waliomtaka kimapenzi. Alijifunza kwamba, wanaume wote wana uwezo wa kusema maneno hayo. Hata pale Geof aliposema anampenda na alimaanisha, Asha aliitikia tu na kumwambia yeye pia alimpenda sana, lakini asimaanishe hata neno moja. Hakuna neno jipya alilopata kulisema Geof kwa Asha, kwani yote yalisemwa na Salimu hapo awali na matamu zaidi ya hayo.

Hali hiyo ikamjengea usugu moyoni mwake dhidi ya habari za mapenzi. Dhidi ya wanaume. Ikaumba chuki ya Siri dhidi yao, akiwa kila mara akitafakari jinsi gani angelipa kisasi dhidi yao. Hakuona njia nyingine zaidi ya kutumia njia ile ile iliyotumiwa na Salimu. Kukoleza penzi, likishakolea vya kutosha, kulimwaga na kuchukua mpenzi mpya. Akapanga maisha yake yote huo uwe utaratibu wake. Hakujali tena. Kama alionja kifo na kukitema kabla hakijamtenda ubaya, kwa nini wanaume wasikionje? Alijifariji kwa tafakuri hiyo.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
David
0629077792 WhatsApp

FB_IMG_1591786690360.jpg
 
2
Mheshimiwa the Don
David Ngocho Samson

Zilikuwa zimesalia wiki mbili hivi kabla ya tarehe rasmi ya kufunga ndoa Kati ya Geof na Asha, mambo yalipogeuka na kuwa kinyume cha matarajio. Geof hakuamini alichoambiwa na mpenzi wake Asha. Bila shaka ulikuwa ni muda mwafaka kwa Asha kutekeleza itikadi yake kwa vitendo ili kufurahisha mtima wake kama sehemu ya utaratibu wake aliokuwa kajiahidi. Asha alimtamkia, kwa sauti laini, akionekana kuwa na utulivu wa kutosha, ungehisi labda anafanya masihara.

“Geof dear, nasikitika hatutaweza kufunga ndoa kwa sababu...” hakuweza kumalizia kauli yake, Geof alidakia juu kwa juu, akikatiza kauli yake hiyo ambayo aliitafsiri haraka haraka kichwani mwake kama moja ya mizaha ya mara kwa mara ya mkewe mtarajiwa. Haikuwa mara ya kwanza kwa Asha kutoa kauli hasi kuhusu ndoa waliyotarajia kufungua siku chache za usoni. Hata hivyo, mara hii kulikuwa na utofauti kwa jinsi taswira yake ilivyotulizana kujaribu kuonesha ni kwa kiwango gani alikusudia kuonesha hana masihara. Geof sasa akiwa keshaanza kuuzoea utani utani wa Asha juu ya suala hilo, alipuuza na kutamka kwa utani vile vile;

“Unasema nini wewe? hebu acha utani kama huo, nikujulishe tu kipenzi, kwamba, Profesa McNeal wa chuo kikuu cha Dodoma amenithibitishia kuhudhuria kwake” Geoffrey alitamka, akilini mwake akichukulia kauli ya Asha kama utani na hivyo alikusudia kuucheza mchezo huo wa utani aliokuwa kauanzisha mkewe mtarajiwa.

Haikuwa utani. Maelezo yake hayo, yalionekana kama mkono uliozamishwa kwenye fuko lenye Sega la asali linalolindwa na nyuki watiifu na hivyo kuibua hasira dhidi ya mvamizi anayejaribu kuwachokonoa. Asha alifura kwa hasira na kuongea kwa sauti ikiyodhihirisha alichukizwa kwa kauli zake.

“Sasa hutaki kunisikiliza, huyo McNeal atahudhuria ndoa gani?” Asha aling'aka akidhihirisha kuchukizwa na namna mwanaume huyo alivyochukulia poa kauli zake. Kichwani kwa Geof kulisikika kitu Kama mlio wa tahadhari. Labda kwa sababu ya penzi lake zito, Geof hakuwahi kushitukia kuwa mapenzi yao, kwa kipindi chote hiki, ilikuwa burudani ya maigizo kwa Asha, burudani ambayo sasa ilifikia tamati. Na sasa Asha, kama ambavyo igizo likifika tamati, alikuwa anatafuta mlango wa kuondoka kwenye ukumbi wa sinema baada ya sinema hilo kufikia ukingoni. Geof alihisi mapigo ya moyo na hofu asiyojua maana yake kama vile ilikuwa inamnyemelea. Alimtazama mwanamke huyo kwa jicho la kidadisi huku akijihoji maisha yake bila Asha yangekuwaje. Pumbazo la huba likamvaa, akabaki ameduwaa akimhusudu mwanamke huyo mrembo. Mwanamke ambaye alitokea kumhusudu tangu aingie balehe yake kwa mara ya kwanza na kuhisi mvuto wa pekee kimahaba dhidi ya mrembo huyo nambari wani. Mrembo ambaye, alibaki moyoni mwake hata baada ya panda shuka za penzi lao kuyumba yumba kwa kuhama shule kwa Asha na hata kwa sababu ya mwanamke huyo kujihusisha na wapenzi wengine ilhali yeye daima alibaki mseja akimngojea na kumuomba Mungu awakutanishe. Ilimlazimu Geof kujikakamua na kutamka kwa utani, akitamani hofu iliyomvamia ghafla ibaki huko huko mawazoni, maana hakudhani kama angemudu kubaki peke bila Asha.

“Utani kama huu si mzuri, nataka nikuahidi mpenzi, kwamba, mimi na wewe ni mpaka kifo kitutenganishe, hakika nitakulinda kwa uhai wangu na kamwe sitaruhusu tena uondoke mikononi mwangu" Geof akaendelea kuchombeza huku akimbusu mchumba wake shavuni, akimaanisha maneno yake kutoka mvunguni mwa moyo wake. Jitihada yake hiyo, haikufua dafu, Asha mwenyewe alionekana pia akifanya jitihada za kukwepa busu hilo, huku sura yake ikidhihirisha ukali dhidi ya bwana wake huyo. Hakuwahi kumuona Asha katika sura hiyo, na kama hiyo haikutosha, mrembo huyo, mkewe mtarajiwa, alifanya kitendo kilichoupasua moyo wake vipande vipande.
Asha alisimama huku mwili wake ukitikisika, mkikono yake miwili akiwa kakishika kiuno chake, akamtupia Geof jicho la kusema, 'usintanie' kisha akaanza kuondoka. Akiwa ametembea hatua kama tano hivi kwa mwendo wa kuacha lawama kama ingekuwa anakatiza mitaa ya Kariakoo, Asha akamgeukia Geof na kusema;

“Ukishaondoa mawazo yako ya kufikiri utani, utakuja kwangu ili uelewe ninachokueleza.” Akavuta hatua na kuvuka kizingiti cha mlango wa sebuleni kwa Geof, akaubamiza mlango huo nyuma yake na kuondoka.

Fuatilia sehemu ya tatu
David
FB_IMG_1591786690360.jpg
 
3
Mheshimiwa the Don
Na David Ngocho Samson

Geof alimeza funda tatu mfululizo za wine halafu akaingia chumbani kwake. Usingizi ulimchukua kutokana na uchovu wa shughuli za kazi na ukiongezea harakati za maandalizi ya harusi yao. Aliposhituka tayari ilikuwa saa moja jioni na alishituka baada ya simu yake kuita. Alijinyanyua kivivu na kuikamata simu hiyo. Alitupia jicho lake kwenye kioo Cha simu hiyo. Jina 'My love' lilionekana kuchezacheza hapo. Ilikuwa namba ya mkewe mtarajiwa, Asha. Aliiweka sikioni akiwa mwingi wa bashasha na kutamka.

“Mambo mpenzi, najua heka heka za maandalizi ya harusi yetu ipo juu na inapandisha presha juu, huwezi amini, mimi pia najisikia hivyo, hata hivyo usijali, mambo yatakuwa poa, tuna watu ambao ni waandaaji wazuri wa matukio kama hayo, vipi, leo utakuja? Siku nyingi hatujalala pamoja!” Geof alitamka baada ya kupokea simu ya Asha. Tofauti na matarajio yake kwamba maneno yake yangempa faraja mpenziwe, maneno ya Asha yalimthibitishia kuwa mwanamke wake alikuwa na jambo moyoni. Jambo ambalo lilimfanya Geof ahisi unyonge. Huzuni ukatanda ghafla hali akijiuliza ni balaa gani lilikuwa linajaribu kuyakumba mahusiano yao.

“Hapana sitakuja, najua unachukulia maneno yangu kwa wepesi, lakini nadhani ni muhimu ukafika kwangu sasa hivi ili unisikilize. Tafadhali Geof niko siriazi, tafadhali njoo unisikilize,” Asha alilalama.

“Sawa mpenzi, nipe dakika tano tu nami nitakuwa hapo ASAP. Love you" Geof alijaribu kwa bidii kuyaondoa mawazo ya kufikiria kuwa kungekuwa na jambo baya dhidi ya penzi lao. Akajiaminisha moyoni mwake kuwa huu, ni moja miongoni mwa mizaha mingi ya Asha ambayo hivi karibuni alikuwa akimtishia nayo. Akaazimu kulazimisha furaha moyoni mwake japo wasiwasi ulizidi kutamalaki zaidi kihalisia.
Geof alibadili nguo na kisha akatoka ndani na kulifuata gari lake kwenye parking lot, akalitia moto gari lake na kuliingiza taratibu barabarani tayari kwa safari ya kuelekea kwa mpenziwe, Asha, umbali wa kitu kama kilometa tano hivi. Alibisha hodi getini kwa Asha na kukaribishwa ndani na Aminata, binti aliyemsaidia kazi Asha. Ndani alimkuta Asha amekaa sebuleni uso umesawijika kwa huzuni. Akajua ngoma inogile. Isijekuwa keshadaka Sasa analeta mashauzi ya kudeka? Geof aliwaza.

“Haya nieleze, jinsi ulivyo msumbufu mtoto wewe!” Geof aliongea akitarajia tabasamu mwanana usoni mwa Asha, lakini haikuwa hivyo, Asha alikuwa hana masihara. Hofu ile ya mwanzo, iliyomtia unyonge, ikajitokeza tena moyoni mwa Geof.

“Kaa chini,” ilikuwa amri. Sauti ya Asha ilitafsirika hivyo kwa Geof. Kwa muda wote huo, Asha alionekana kukosa utulivu kabisa.
Geof alikaa chini bila ubishi.

“Geof unafahamu kuwa nakupenda sana,” Asha alitamka. Alikuwa anatembea huku na kule mle sebuleni akiwa anajaribu kujielezea ili aeleweke. Haikuwa rahisi, maana alijua ni kwa kiasi gani Geof alikuwa anamzimia. Ndani ya moyo wake, sehemu fulani hivi ilikuwa inamrai asitende ukatili na usaliti huo aliokuwa kakusudia, lakini alipokumbuka habari za Salimu, roho yake ilimkereketa kwa fukuto la kutaka kulipiza kisasi.

“Najua unanipenda pia, ni uamuzi mgumu sana ambao imenibidi kufanya, na amini kuwa mimi pia najisikia vibaya. Geof, sikuwahi kukueleza kwa sababu mimi pia niliamini kuwa yaliyopita si ndwele na ni bora kuganga yajayo, lakini si yote yatokeayo yanakuwa kweli.” Asha aliendelea kujielezea kwa Geof. Alipofikia hapo, akanyanyua bahasha ya kaki na kutoa picha.

“Unaona hii picha,” aliiinua juu na kuielekeza usoni pa Geof. Geof aliyekuwa kakumbwa na gagaziko la fadhaa, aliitumbulia macho bahasha hiyo akiwa zuzu asiyejielewa anafanya nini.

“Huyo mwanaume alisemekana kufa kwenye ajali ya ndege, tulimzika lakini ukweli ni kwamba hakufa, yupo hai, na nimeonana naye hivi karibuni. Huyu alikuwa ni mpenzi wangu kabla ya ajali. Geof, sitaki kuwalinganisha lakini ananihitaji, na mimi nimegundua kwamba penzi langu lipo kwake bado. Samahani sana Geof!” Asha alihitimisha kauli zake akiwa amesheheni wasiwasi tele japokuwa alizuga kwa kujibandika ujasiri wa bandia. Viganja vyake vilitota kijasho chembamba. Haikuwa rahisi, na alifahamu hilo. Usaliti humuumiza zaidi msaliti hasa afikapo nyakati za majuto. Hiyo ndio hali halisi iliyomkumba Asha.

Ilikuwa kama hotuba, maneno ambayo Geof hakutarajia kuyasikia. Alibaki ameduwaa. Akatopea kwenye mawazo, akijiuliza swali la msingi, ‘ina maana muda wote huu mapenzi yake hayakuwa kwangu? Alikuwa ananichezea akili, hisia zangu na sasa ameamua kunidhalilisha? Au huu ni utani mwingine wa Asha?’ Geof aliendelea kujihoji pasipo na wa kumpa majibu. Heri basi angeliuliza. Alikuwa anajiwazia tu kwa unyonge.

“Geof.” Asha akaita kwa sauti tulivu!
Geof akazinduka baada ya kusikia sauti nyororo ya Asha. Akatamani aisikie tena ikisema, aah Geof, natania tu, lakini ikaishia mawazoni mwake. Geof alinyanyuka kwa unyonge, usoni mwake kukionekana chuki na hasira za wazi wazi, akaibeba ile bahasha na kurudi kwake bila kusema neno. Moyoni mwake ikajiotea mbegu ya chuki, chuki dhidi ya adui, adui aliyenuia kumtia fedheha wakati ambapo alikuwa kaweka mambo yote hadharani. Wakati ambao kila mtu angeliona fadhaa yake na kumuonea huruma. Asingekubali hilo litokee. Geof hakuwa tayari kukabili aibu ya kuachwa siku chache kabla ya harusi yake.

David
FB_IMG_1591786690360.jpg
 
4
Mheshimiwa the Don
David Ngocho Samson

Subira yavuta heri walisema wahenga. Geof alijipa moyo, 'hebu tuone itafika wapi, bila shaka huu ni utani mbaya sana' alizidi kuwaza. Alipofikia kutahamaki, tayari zilikuwa zimepita siku mbili kukiwa hakuna cha meseji wala missed call ya mpenziwe Asha. Kichwa kikamuuma, moyo ukafedheheka, hasira zikapata nafasi na kutia dosari wajihi wake. Hulka yake ikabadilka na kumpa taswira tofauti, hasa kwa marafiki zake na wale waliomtakia kheri ya fanaka kwa maandalizi yake ya harusi. Simu za marafiki juu ya harusi zikampandisha kichaa, ataficha wapi sura yake? Fedheha gani hii! Hapo akajivuta kivivu na kuweka simu sikioni baada ya kubonyeza bonyeza namba za simu ya Asha. Alitaka kusikia kauli ya Asha, huenda akawa amebadili msimamo. Kusema kweli, ni ile basi tu kwamba alikuwa amejikatia tamaa akitarajia muujiza.

“Hallow Geof,” ilisikika sauti ya Asha sikioni mwake baada ya simu kupokelewa.

“Hallow dear, ah leo ni siku ya pili na hatujawasiliana mpenzi wangu, tafadhali fikiri vema na fahamu kwamba unaniumiza Asha, tafadhali usintese mwenzio!” Sauti yake ikayatamka hayo ikiwa imejawa na huzuni isiyo kifani. Sauti ya mwanaume akinyenyekea na kujishusha chini kubembeleza penzi.

“My God, what shall I do, I know this is hard but just try to forget me G. We should try to let it go, I am going to marry Elinisa. I am sorry we came this far and it is affecting what we had. I am real sorry.” (Mungu wangu G, najua hili ni gumu lakini G, tafadhali jitahidi kunisahau, siwezi kuwa na wewe, nitaolewa na Elinisa, nisamehe sana G, nisamehe bure). Asha akajitetea na kusihi. Akili yake ilikwishaachana na habari za Geof, tayari moyo na akili yake, Asha alikuwa amevikabidhi kwa penzi jipya. Mwanaume mpya kutoka marekani. Elinisa. Kauli hiyo ikamfanya Geof akurupuke kutoka kwenye ile Hali ya unyonge iliyokuwa imeutawala moyo wake. Kauli ya Asha ikawa imemwamsha na kumuonesha jinsi alivyokuwa amelala wakati mwanaume mwingine anakula kwa ulafi penzi lake. Kama si dhihaka ni nini? Ungeutazama moyo na uso wa Geof, ungeelewa tafsiri rasmi ya chuki na hasira. Weusi wake ulikuwa si kitu tena, alikuwa mwekundu kama moto wa makaa ya moto.

“Going to marry him!?” (Unaolewa naye?!) Geof akauliza kwa dhihaka kisha akamalizia,
“Not when I am alive and breathing darling, I guess now we just started a war. It is either you marry me or he is...Did you say he died of an accident? But he didn't? It was fake news? He will die for real now, mark my words.” (Unaolewa naye umesema? haitatokea kama mimi niko hai kipenzi. Bila shaka hii ni vita, kiyama changu kiyama chake..... Ulisema alisemekana kufa ajalini, lakini hakufa, sio? Kwamba zilikuwa habari za uzushi sivyo? Nakuahidi sasa haitasemekana, itakuwa kweli).

Geof alikata simu na kujilaza kitandani. Mishipa ikimsimama wima usoni na kijasho chembamba kikaufanya uso wake ung'ae. Alivuta bahasha ya khaki aliyokabidhiwa na Asha kutoka kwenye meza ndogo pembezoni mwa kitanda chake na kuitazama vizuri, picha ya Elinisa. Hasira ziliikunja sura yake na kumfanya akaze meno mithili ya mjamzito anayehangaika kusukuma mtoto muda wa miezi kenda unapokuwa umewadia.

Alikumbuka vema kwamba, aliwahi kusoma na Elinisa kidato cha tano kabla ya jamaa huyo kuondoka kwenda Marekani baada ya mwezi mmoja tu wa kidato cha tano. Kwenda Marekani kusoma kulimaanisha kwamba, Ely kwao walikuwa na uwezo mzuri wa kifedha, ingawa ukweli ni kwamba Ely kusoma Marekani ilikuwa bahati tu ya ufadhili. Sasa, eti alitakiwa kumwachia mwanamke wake huyo jamaa aliyesomea Marekani, isingewezekana, potelea pote. Mawazo yalizidi kukitafuna kichwa Cha Geof.

'Mwanaume lazima asimamie mali yake kwa uhakika, lazima nipiganie haki yangu' alijiapiza kwa dhamira.

***

Majira ya jioni ya saa mbili, Elinisa alikuwa anarejea nyumbani kwake baada ya kumrudisha Asha nyumbani kwake. Akiwa anahesabu hatua zake mdogo mdogo, mara akasikia mlio wa simu ambao ulimjulisha kuwa simu yake imepokea ujumbe mfupi. Hivyo, akawajibika kuzamisha kiganja Cha mkono wake wa kulia kwenye mfuko wake wa suruali na alipoutoa, alikuwa na rununu yake ya kisasa, infinix hot 8. Akachora pattern kwenye kioo Cha simu hiyo na kuingia kwenye uwanja wa jumbe fupi. Haukuwa ujumbe wa kawaida, yeyote aliyeutuma alikuwa na hasira na chuki kubwa. Ujumbe ule ulisomeka; Achana na Asha, la sivyo, utakufa.

Elinisa aliusoma ujumbe huo lakini hayakumwingia akilini maneno hayo.. Akajaribu aupotezee kuwa huenda ni namba imekosewa, lakini uwepo wa jina la Asha, mpenziwe, ukamfanya atake kujua zaidi. Akashawishika arejee tena kwenye inbox lakini ujumbe ule haukuwepo. Ilikuwa ni flash message. Jumbe ambazo zikishasomwa hutoweka bila kuhifadhiwa kwenye simu ya mpokeaji. Tayari alikuwa amefika nyumbani, alipoingia ndani akawasha runinga kutazama taarifa iliyokuwa inaelezea habari za dunia, habari mahsusi ikiwa juu ya mlipuko wa gonjwa hatari Sana huko uchina linaloshambulia mfumo wa upumuaji.

Elinisa ambaye alikuja nchini kwa dhamira ya kupata mke huku, alidhamiria kurejea Marekani akiwa na Asha hasa kwa sababu alirejea nchini kutafuta mke baada ya mchumba wake wa siku nyingi, Tina kuachana naye na kuishi na mwanamke wa kizungu mahusiano dhalili ya usagaji. Sasa, akiwa Bado hajaweka mambo sawa, akashangaa anaanza kupokea jumbe za simu za vitisho, vyote hivyo, vikimhusisha mwanamke huyo, ambaye, kukutana kwao kwa Mara ya kwanza TU, kulimpatia uhakika kwamba alistahili kuwa mama wa wanae. Akali akitafakari Hayo, Simu yake iliita, namba ngeni ikicheza kwenye kioo cha simu hiyo ya kisasa

“Naam,” aliipokea simu na kuongezea swali

“Nani mwenzangu?”

“Huna haja ya kunifahamu mwanaharamu wewe, kwa tahadhari tu nakuonya tena, achana na Asha. Siku mbili tu zinatosha kuthibitisha hilo, la sivyo, you're a dead man” mzungumzaji alitamka halafu akapotea hewani bila kumpa nafasi Ely kujibu hoja au kuuliza swali kwa kusudi la kupata ufafanuzi wa kina.

Hofu ilimwingia moyoni Ely. Hakutaka vita na mtu. Huyu ambaye alikuwa anamsakama kuhusiana na habari za Asha, hakuwa muungwana. Na kama si hivyo, basi alikuwa mwoga wa kutupwa. Akajiuliza kwa nini mtu huyo ambaye alionesha kuwa anamhitaji Asha asimfuate Asha na kutia nia na kisha kuuza sera wapambane kwa sera za kumuwania mrembo huyo, badala yake anataka kutumia vitisho ili kumrudisha yeye nyuma kwenye kampeni yake ya kumchukua jumla mrembo huyo? Hilo lilimtatiza kwa sehemu. Akili yake ikamshawishi kuwa, mtu huyo, alikuwa ni mjinga mmoja ambaye hata kutongoza mwanamke mrembo kama Asha ulikuwa mtihani. Akajiuliza ingekuwa faida gani kwake hata kama angekubali kurudisha kikosi chake nyuma kutoka kwenye uwanja wa mapambano. 'Siamini hiki nachosikia, kwani ana nini huyu mwanamke?' Alijiuliza. Aliamua kupuuza lakini aliandika kwenye kijitabu chake cha kumbukumbu, kwamba kwa mara ya kwanza anaishi kwa hofu ya kutishiwa kuuawa na mtu asiyemjua, sababu ikiwa ni mwanamke.

Tufuatane kwa sehemu ijayo
FB_IMG_1591786690360.jpg
 
5
Mheshimiwa the Don
David Ngocho Samson

Kesho yake asubuhi, Elinisa alipata stafutahi maridhawa kisha akaelekea kwa Asha akidhamiria kupata jibu la kitendawili cha vile vitisho kutoka kwa mtu asiyejulikana hasa kwake binafsi, lakini bahati haikuwa yake. Hakumkuta Asha nyumbani! Hivyo, aliamua ampigie simu ili kufahamu wapi alipokuwa ili wapate wasaa wa kulizungumzia jambo hilo lililokuwa linamtatiza sana fikrani mwake. Alichukua simu yake na kubonyeza namba za Asha halafu akaipachika simu hiyo kwenye sikio lake la kushoto na kusikilizia wakati simu hiyo ilipokuwa inaita. Hatimaye ikapokelewa, na sauti tamu, laini, sauti nzuri ya kike ikasikika kwenye sikio lake.

“Yes babe,” alitamka Asha.

“Uko wapi?”

“Nipo saluni.”

“Sawa, ukitoka pitia kwangu ni muhimu sana.” Ely alitamka na kukata simu.

“Miss you babe.” akatamka Asha kwa bashasha.

Kwa hakika, Asha alijua vema kutumia nyama ya ulimi kuweka mambo yake sawa. Ilikuwa nyama tamu sana hasa alipokusudia kuitumia kunasa windo tamu kama Ely. Windo lenye nafasi na ukwasi wa kueleweka. Si kama alitumia mwili wake kutafutia fedha, la hasha, kwake yeye, aliwachukia zaidi wanaume wenye ukwasi kwa kule kudhani kwao kwamba wanaweza kununua binadamu wenzao kama vile wananua runinga ya kuwapa burudani wanapojisikia. Hasa Sana binadamu jinsia ya kike.

*†*†

Kama alivyoambiwa, Asha alifika kwa Elinisa baada ya kutoka saluni. Baada ya maelezo ya Elinisa kuhusu vitisho alivyokuwa kapata kwa mtu asojulikana, kwa wepesi kabisa, Asha alijibu kwa mkato huku akitoa msonyo uliokidhi kuelezea kuwa alidharau tabia hiyo aliyofanya mtu huyo. Yeye alikwishatambua, hakuwa na shaka kwamba Ni Geof mwenye kujua uhusiano huu mpya na ambaye angejaribu kutumia vitisho ili kujihakikishia umiliki wake kwake;

“Achana naye, ni mshenzi mmoja hivi amekuwa akinitaka na mimi namwambia simtaki lakini ni king'ang'anizi kama luba, anaitwa Geof.”

“Geof?” alihamaki Ely. Alikusudia kupewa taarifa za kina na sio jibu la mkato lisilokidhi haja na kiu yake ya kumtambua mtu huyo kinagaubaga.

“Geof Mtemvu, anafanya kazi na shirika la umeme TANESCO.” Asha alitamka huku akichukulia suala hilo kwa wepesi kabisa. Hasira zake dhidi ya Salimu ilimfanya Asha kuwachukulia wanaume wote kwa usawa, aliwachukulia kama pacha, akiwafananisha kitabia kwa kila hali.

Kutajwa kwa jina Geof Mtemvu kulimrejeshea kumbukumbu ya shule Elinisa. Miaka michache iliyopita, wakiwa kidato cha tano, walisoma na mtu aliyeitwa kwa majina hayo aliyoyataja Asha katika hali ya mzaha na kupuuzia. Ilikuwa katika shule ya serikali mkoani Lindi, Lindi sekondari. Alimfahamu hasa kwa vile Geof alionekana mtoto kutoka familia yenye ukwasi wa kutosha, akiwa mwanafunzi pekee darasani mwao aliyemiliki rununu janja huku akiweka bili ya chakula kizuri kwa mama mmoja, mke wa mwalimu, huku wao wakila ugali kwa maharage kila siku kwa mujibu wa ratiba ya shule. Geof alikuwa anafuatwa na gari binafsi, Land Cruiser, kila likizo, kutoka Lindi hadi Dar na kuletwa shuleni hali kadhalika. Hakupata shuruba za usafiri Kama alizopata yeye na wanafunzi wengine enzi zile hasa kutokana na ubovu wa barabara. Geof alikuwa Sharobaro wa shule. Kila siku alikuwa na mtoko tofauti. Hakuvaa nguo moja mara mbili. Huyo ndiye Geof aliyemkumbuka. Pamoja na ukwasi, ilijulikana wazi, Geof alikuwa domo zege! Mwoga kwa watoto wa kike. Hadi Elinisa anaondoka shuleni Lindi kwenda Marekani kwa masomo ya juu kwa ufadhili wa marafiki wa kanisa lao, hakuwahi kusikia Geof kuwa na msichana yeyote! Kumbukumbu hiyo, ikamfanya Ely aachie tabasamu laini kwenye pambizo za midomo yake.

"Vipi mpenzi, kipi kinachokuchekesha Sasa ilhali dakika kadhaa zilizopita ulikuwa umejawa na simanzi na hofu hatari?" Asha akauliza, alishangazwa na tabasamu lile la ghafla. Elinisa alicheka, safari hii kwa sauti kubwa na halafu akamshika Asha begani na kumsimulia Kidogo alivyomfahamu Geof.

“Nilisoma naye kidato Cha tano, nadhani kwa miezi mitatu hivi kabla sijakwenda Marekani” Elinisa alimweleza Asha. Kile kitisho sasa alikichukua kwa wepesi na kupuuzia. 'Yule domo zege atanifanya nini?' akajiwazia, moyo wake ukitulizana kifuani mwake. Hofu akaitupilia kule!

“So absurd!” Alijisemea Elinisa kwa kimombo. Hakujua watu hubadilika, yeye mwenyewe akiwa mfano hai wa mabadiliko halisi. Fikra zake juu ya Geof wa shuleni kidato cha tano bado alizitumainia kumpa liwazo katikati ya kitisho chenye ukomo wa siku mbili. Kosa la kifalsafa.

David
0629077792 WhatsApp
FB_IMG_1591786690360.jpg
 
6
Mheshimiwa the Don
David Ngocho Samson
0629077792 WhatsApp

*†*
Ile mbegu ya chuki iliyokuwa inaota moyoni mwa Geof ilianza kunawiri na kustawi ikikuza mizizi yake panapo mvungu wa moyo wa Geof na matawi yake mapana yalitokeza kwenye pua zake na kufanya mapafu yake yavute na kutoa hewa ya chuki kwa wingi.

Sasa alijua adui yake ni nani, mwosha huoshwa. Maneno aliyomtamkia Asha juu ya Elinisa yalianza kuumba kitu. Tayari Elinisa alionekana maiti katika taswira ubongoni mwa Geof, isingekuwa ngumu. Alijua nini cha kufanya.

Muda usiopita mwaka mmoja uliopita Geof alikutana na mzee Mabruki, huyu alikuwa mwanasiasa maarufu sana nchini Tanzania, harakati zake za kibiashara ndicho kilikuwa chanzo na kiunganishi kikubwa cha wait kufahamiana. Mzee huyo Mabruki, alikuwa mkwasi kwelikweli na haikuwa Siri kwamba Vijana waliosaka mafanikio, wakimtazama Kama kipimo Cha mafanikio ambayo walitamani kufikia. Baada ya mikutano kadhaa na mzee Mabruki, Geof alionesha wazi matamanio yake ya kufuata nyayo za Mabruki, mtu ambaye alitokea kujinyakulia umaarufu mkubwa kutokana na utajiri wake uliotukuka. Alijulikana zaidi Kama Mheshimiwa the Don. Mzee huyo alimkaribisha Geof katika ushirika wao wa siri, uliokuwa unawapa wanachama fursa mbalimbali za kujifunza namna ya kufanikiwa kibiashara na kisiasa.

Geof aliyekuwa na hamu ya kuwa mfanyabiashara mkubwa aliona ni bahati ilioje kuingia katika biashara kwa msaada wa mzee Mabruki ambaye siku zote alihusudu mafanikio yake. Mengi yalikuwa ni siri kama sera za umoja wao zilivyosema na hilo alijua lingemwezesha kufanikiwa kwa tatizo hili lililokuwa linamkabili.

Baada ya tafakuri nzito ya kina, Geof alimpigia simu mzee Mabruki na kuomba kuonana naye kwa mazungumzo.

Mbali na kuwa mfanyabiashara mkubwa, mzee Mabruki alikuwa ni waziri katika serikali iliyokuwa madarakani. Nafasi hizo za kisiasa na kibiashara zilimpa jina kubwa ndani ya jamii na taifa kwa ujumla. Mwanasiasa mbobezi, tajiri asiyejua ubahili, hizo zilikuwa sifa zake madhubuti, zilizompa jina katika jamii ya walalahoi, kwa sababu alitoa misaada mingi na kusimamia sera mbalimbali za Serikali na ilani ya chama chake kwa ufanisi. Mheshimiwa the Don, alikuwa mtu wa watu. Huo ukiwa Ni upande mmoja wa sura ya mzee Mabruki.

Kwa sura ya pili, huyu mheshimiwa alikuwa mtu hatari kwa usalama wa taifa lake, alijihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya na biashara haramu ya kuuza binadamu. Alimudu kuuza wasichana warembo waliopelekwa Ulaya kufanyishwa biashara za ngono na kucheza picha za ngono pia. Kama hiyo haitoshi, huyo mzee alikuwa mshirikina wa kutupwa, akihusishwa na kununua viungo vya albino na ngozi za binadamu.

Mzee Mabruki almaarufu The Don, kama alivyofahamika vyema miongoni mwa makundi ya vijana, alikuwa na kikosi maalum kilichohusisha baadhi ya vijana kutoka Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa na wale wasomi wabobezi wa taaluma mbalimbali, alimradi alikanyaga kila idara muhimu hapa nchini. Hao, walikusanya habari mbalimbali na kuandaa mipango kabambe ya kimkakati ya kibiashara na kijasusi, kitu kilichomfanya awe mtu hatari sana.

The Don, asingeruhusu mtu yeyote yule aingilie mahali penye maslahi yake, huyo lazima angetangulia huko wanakokwenda wafu. Alikuwa tajiri mkubwa na kwa utajiri wake aliishi maisha ya anasa kubwa. Kitu gani alihitaji asipate? Magari? Majumba? Starehe? Fedha? Mapenzi?. Hivyo vyote vilikuwa chini ya uwezo wake. Alipoamua, alilala Paris Ufaransa kwenye madanguro ya kisasa na kula starehe kwa kadri alivyotaka, safari za ulaya na Marekani ilikuwa sawa na kutoka Mbagala kwenda Posta tu. Alikuwa kiungo maridadi kabisa cha wauza madawa ya kulevya wale papa kutoka mataifa ya Amerika ya kusini, Columbia na Mexico. Alikuwa msimamizi wa usambazaji wa mikanda ya ngono iliyohamasisha ngono za jinsia moja na kinyume na maumbile kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati. Ni huyu huyu the Don, aliyekuwa kiungo maalum kabisa kwenye ile taasisi ya siri, iliyozingatia sadaka za binadamu na hivyo kuhamasisha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi - alibino, vikongwe, watoto na wale wazee wenye vipara-ngoto!

Kwa mujibu wa mitandao yake ya kiintelijensia, The Don alikuwa na orodha ya watu ambao kwa kuwa kinyume na mipango yake, walikuwa lazima wafe. Miongoni mwa orodha ya wafu watarajiwa, alikuwa kijana mtata na makini sana aliyeitwa Maisha Nchagwa. Huyu alikuwa ni mkurugenzi mtendaji wa shirika la haki za binadamu, maarufu kwa kifupisho chake, HRO. Hii ni kutokana na kwamba kijana huyo machachari alianika uozo wa mzee huyo na kuchimba chimba mambo ya mheshimiwa huyo. Hilo lilikiuka sera ya ngome ya mzee Mabruki na lingehatarisha usalama wa ngome hiyo. Kuchunguza harakati za Don na watu wake, lilikuwa kosa ambayo adhabu yake isingehitaji mjadala. Adhabu yake ilikuwa ni kifo tu. Iwe kwa mbinde au hiari.

Maisha alikuwa ni kitoto kidogo kinachopigia kelele wakubwa. Hivyo, kulikuwa na namna moja tu ya kurekebisha tatizo hilo. Kukinyamazisha. Njia pekee ilikuwa kumchafua kijana huyo na kumfanya asisikilizwe tena na raia au kumpoteza kabisa asionekane kwenye uso wa dunia.

The Don alijing'ata kwenye papi za midomo yake alipolitafakari suala la Maisha, usoni kwake mikunjo ya ndita ilidhihirisha chuki ya waziwazi dhidi ya kijana huyo. Hakutaka masihara kabisa katika suala la Maisha. Alimtaka awe mfu! Na huyu, mtu huyo katili 'The Don', ndiye mtu ambaye tafakari ya Geof ilimwambia angemsaidia katika kumuondolea kikwazo dhidi ya furaha yake, yaani mapenzi yake na Asha.

Geof alitafakari kutumia uzoefu wa kimafia wa Don ili kumfutilia mbali adui yake mkubwa Elinisa.

Endelea kufuatana nami
David
FB_IMG_1591786690360.jpg
 
7
Mheshimiwa the Don
David Ngocho Samson
0629077792 WhatsApp

NDANI ya ofisi yake kubwa na ya kifahari, kwenye moja ya majengo yake Bora kabisa nchini, Mabruk Complex, The Don aliketi kwenye kiti chake cha leather, kinachonesa nesa, mdomoni mwake kukiwa na cigar ya gharama. Alikuwa akinesa nesa kwa mtindo wa kubembea mbele nyuma mbele nyuma, akimsikiliza kijana wake machachari, Estivan Brown.

"Mzee, mipango yetu ipo hatarini kwa sababu Machera amepata habari na yupo mbioni kufichua mambo, taarifa za uhakika ni kwamba anashirikiana na Maisha wa HRO kuchimba kisha kuyapeleka mambo yetu kwenye jamii, katika kile wanachoita 'taarifa za utekelezwaji wa haki za binadamu nchini'. Taarifa hizo zimekuwa zinarushwa na vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini, na vina mwelekeo wa kutuhusisha na ukiukwaji wa haki za binadamu. Tunahitaji kucheza kabla hawajacheza.” Estivani ambaye katika genge la Don alikuwa ndiye mkuu wa kikosi pelelezi na kitengo cha habari cha ngome ya The Don, alitoa ripoti kwa bosi wake. Alipomaliza kutoa ripoti hiyo ikiwa na pendekezo la kufanya kitu mapema kabla ya kushitukiwa, Estivan alisimama kikakamavu akisubiria kupata mwitikio wa bosi wake, The Don.

Estivan Brown alikuwa kijana mkakamavu na mwenye mafunzo ya hali ya juu ya ukomando. Huyu ndiye hasa alikuwa injini ya ngome ya The Don hasa kwa vile Don mwenyewe mara nyingi alilazimika kujificha kwenye kivuli cha uwaziri na ile taswira makini aliyomudu kuijenga miongoni mwa raia, yaani, tajiri asiye na ubahili. Mara nyingi, Estivan ndiye aliyekuwa anatekeleza mipango yote na alifanya uamuzi wote muhimu wa kiutendaji. Alikuwa mtu katili na muuaji wa kutisha. Mauaji aliyotekeleza Estivani Brown kwa niaba ya Don, yalikuwa ya aina yake. Kwa maana kuwa, kila alipotekeleza mauaji, basi aliyapatia namba kulingana na mtiririko wa matukio hayo ya mauaji. Namba 1, 2, 3 ......39....na kuendelea. Huyu uraibu wake ulikuwa ni kuua. Mauaji yake yaliambatana na mhanga kuvalishwa mkufu wenye kidani cha fuvu la binadamu.

Estivani Brown Mzaliwa wa nchi jirani ya Rwanda, ni muuaji aliyeacha vimikufu vyenye mfano wa fuvu za binadamu kwenye kila tukio la mauaji alilotekeleza mwenyewe kama utambulisho wake, lakini hakuna aliyepata kutafsiri utambulisho wake huo. Mauaji ambayo yaliumiza intelijensia ya vikosi vya usalama nchini wakitafuta ufumbuzi bila mafanikio. Mauaji yaliyoacha taharuki na bumbuwazi kwa namna yalivyotekelezwa kikatili. Miongoni mwa vitendo vya kikatili alivyofanya Estivan Brown, vya kutisha na kukerehesha ni pamoja na kuwachuna ngozi wahanga wake, kuondowa sehemu zao nyeti, mauaji ya albino kwa ajili ya viungo vyao ambavyo iliaminika miongoni mwa wanajamii, hasa wenye kuamini kwenye ushirikina kuwa vilikuwa na thamani katika kupata utajiri wa mali . Alibobea kwenye mambo hayo.

Estivani Brown, alizaliwa miaka kumi kabla ya mauaji maarufu ya kimbari nchini Rwanda. Mauaji ambayo alilazimishwa kushuhudia mauaji ya ndugu zake ambao walichinjwa kama vile kuku kwa majambia yenye makali ya kutosha. Naam, mauaji ambayo hakutakiwa kutoka uchozi wake kuwalilia wazazi wake, dada na kaka zake. Alikuwa amevalishwa nguo za kike, na hasa kutokana na ukweli mchungu ambao pia alilazimika kuishi nao, ukweli kuwa Estivani Brown alikuwa ni mtu mwenye jinsi mbili na hivyo utotoni sura ya kike ilishamiri zaidi. Kwa kumdhania kuwa alikuwa ni msichana wahutu wale waliokusudia kuwaondoa watutsi kwenye ardhi ya Rwanda walimtelekeza Estivani Brown kwenye dimbwi la damu ya nduguze. Akilia moyoni, macho makavu yakigoma kudondosha chozi na kuruhusu moyo wake kuvuja matone ya machozi ya damu ndani kwa ndani.

Hilo halikutosha, baada ya wazazi na nduguze kuchinjwa kwa majambia na yeye kuzimia kwa kutohimili yale aliyoyashuhudia, akaokotwa na mfaransa Rousseau Pierre, muumini wa dini ya kishetani, iliyotamalaki kwenye mizoga ya warwanda mithili ya ndege tai, ikihamasisha mauaji zaidi kwa lengo la kutimiza ibada zao.
Rousseau Pierre akambeba na kwenda naye Paris! Katika moja ya ibada yao ya kishetani, ilikuwa Estivani apandishwe kwenye altare ya mauti kama sadaka, pale alipogundulika kuwa na jinsi mbili. Kwa taratibu za ibada yao, huo ulikuwa mkosi, ambao kwake uligeuka muujiza. Asingefaa kuwa sadaka, alikuwa ni alama ya muungu waliyouabudu. Kisa hicho kikabadili kusudio, Estivani akapewa mafunzo ya kuwa mvunaji wa sadaka badala ya kuwa sadaka yenyewe. Mafunzo yake yakamgeuza mnyama! Akiwa mtu mwenye kiu ya damu, damu ya binadamu wenzake. Naam, Estivani raha yake pekee ilikuwa ni kumwaga damu! Damu ya binadamu!!

Sasa baada ya kufanywa mvunaji, alikuwa ni sehemu ya jamii yenye nguvu. Sehemu ya malipizi ya kisasi. Sehemu ya utawala mpya. Akilini mwake, tangu utotoni alipoyashuhudia mauaji ya kutisha kwa familia yake, alijua waliuwawa kwa vile hawakuweza kujitetea. Hawakuwa na nguvu za kujilinda, hawakuwa na mafunzo ya kujihami. Hawakuwa na itikadi.

Alitema mate chini kwa dharau kila alipokumbuka matukio hayo ya kikatili, yalioondoka na familia yake nzima. 'Kwa nini walikubali kuchinjwa kama kuku bila hata kujaribu kujihami? Kwa nini wasingejaribu hata kukimbia basi wafe katika kujiokoa? Mbona walihiyari ukatili ule? Au walikuwa wamechoka maisha. Waliona ndio njia ya wokovu? Kuokoka dhidi ya mateso na manyanyaso! Kuokoka dhidi ya njaa iliyokuwa imewadhoofisha! Umaskini uliokuwa umevamia kaya yao kwa kasi! Kuokoka dhidi ya kuishi bila tumaini? Tumaini la kusaidiwa!?

Mataifa Jirani, mataifa mashuhuri duniani, umoja wa mataifa, hakuna msaada ulioonekana. Hata ilipobaki watutsi kwa watutsi, kwa ukatili uliokuwa unaendelea, kila familia ilijitazama yenyewe, umoja, ushirikiano kati ya jamaa na jamaa haukuwepo tena. Walikimbia huku na huku bila msaada. Hata walipokimbilia kwenye nyumba za ibada, huko walikuta maiti yamejazana. Bila shaka hata Mungu hakuonekana kusaidia. Inawezekana ndio sababu walihiyari kuchinjwa bila jitihada. Walikwishachoka! Kikombe kile hawakuwa na namna ya kukiepuka.

Estivani alipowaza mambo hayo mara zote alijipata akiangua kilio cha mtoto mdogo na kujikunyata kama kifaranga cha kuku kilichompoteza mama yake, halafu kikanyeshewa kwa mvua. Hisia za maumivu zilimnyong’onyesha. Hapo uanamke wake ulidhihirika, alilia mithili ya mwanamke aliyefiwa mume na wanawe wote kwa mpigo. Halafu taratibu, hasira zilipomjaa, alirejea kwenye uanamume wake! Ni hapo ambapo alipata lile tabasamu la kifo, tabasamu la kuua, tabasamu lililomfariji kuwa kamwe asingekufa kizembe. Asingehiyari mauti bila jitihada, ni hapo alipojikuta hajui hofu ni nini! Ni hapo aliposisimkwa kwa raha aliyoijua mwenyewe kila alipotekeleza mauaji.

“Huyo mtu ni hatari sana, nafahamu utekelezaji wake wa kazi, anaaminika sana serikalini, ni lazima tuwe makini, la sivyo mambo yataharibika kweli, sijui una mpango gani?” mheshimiwa Mabruki alisema na kuhoji akiwa bado anabembea kwenye kiti chake kwa mtindo ule ule.

Estivan alishika tama na kutafakari halafu kwa sauti tulivu akatamka, “Ni muhimu afe.” alipotamka hayo, akamtazama Mabruki usoni na kusema,
“Waziri Masebo na Machera watakuwa na kikao pale Kilimanjaro Hotel, unafahamu tuna watu wetu pale hao watawahudumia, ni kikao cha siri lakini tumefanikiwa kupata habari kupitia kwa Amosi, na itakuwa rahisi tu kuwanywesha sumu. Ni sumu ambayo inaanza kufanya kazi baada ya saa mbili” Estivani Brown alielezea mkakati wake.

“Una maana Masebo naye afe?” Mabruki akahoji.

“Ikibidi,” Estivani akajibu kwa mkato.

“Masebo ni ndugu yangu” Mabruki akalalama! Naam, ni kweli kuwa waziri wa mambo ya ndani Mheshimiwa Sebastian Masebo, alikuwa Ni binamu yake kabisa.

“Sasa mzee, unadhani itakuwa rahisi Machera kunywa sumu peke yake?” Estivan alitamka alijitahidi kuficha hasira zake dhidi ya bosi wake kwa kuleta mambo ya kujuana kazini. Ni vile tu alikuwa bosi wake, lakini alitaka kumkaripia kwa kuweka udugu kazini.

“Nadhani mpango wa sumu si sahihi, kwanza utasababisha upelelezi juu ya kifo cha waziri wa Mambo ya Ndani ambao unaweza kutuzoa na sisi, na pili Masebo ni ndugu yangu kabisa.” Mabruki akazidi kuupinga mkakati husika.

“Sawa, kwa hiyo?” Estivani akahoji akionekana kuchoshwa na wasiwasi wa bosi wake.

“Tafuta njia nyingine ya kumuua huyo mshenzi Machera haraka iwezekanavyo, eti mpelelezi?” akamlizia maneno 'et mpelelezi' kwa bezo! Mabruki akatoa agizo. Estivani, damu ikachemka mishipani mwake kwa kule kusikia tu habari ya kuua.

The Don na Estivan Brown ndio watu Geof anataka wamsaidie kumuondolea kikwazo chake dhidi ya Asha, pata picha itakuwaje?! Usikose sehemu inayofuatia.

David Ngocho Samson
FB_IMG_1591786598873.jpg
 
8
Mheshimiwa the Don
David NGOCHO SAMSON
0629077792 WhatsApp

Machera lilikuwa jina maarufu sana nchini. Mpelelezi aliyetukuka na kukwamisha hujuma mbalimbali za maadui wa taifa, lakini yumkini alifahamika na watu wachache sana. Hata waandishi wa habari walioandika habari lukuki za kumsifu kijana huyo, si ajabu kwamba hawakuwahi kumwona kwa macho yao.

Machera alikuwa kirusi hatari sana kwenye kompyuta za maadui wa nchi kikitafuna vibaya mipango yao kabambe na kuwaacha wakilaani, yeye mwenyewe alitembea mitaani na kuonekana kijana wa kawaida na hakuna aliyejua kwamba kijana huyo wa kawaida sana ndiye alikuwa anauza magazeti mengi mitaani kwa vichwa vya habari vilivyosheheni jina lake.
Huyo alikuwa maumivu ya kichwa kwa mzee Mabruki, akifichua habari na mipango yake mingi na kumtia hasara ya mamilioni ya dola!

Akiwa na wenzake Kened na Anastazia walifanya ugunduzi wa ajabu. Wakibaini namna watu waliojiita wazalendo, viongozi wa serikali walivyoifilisi nchi kwa tamaa zao binafsi, wakitengeneza matabaka ya tajiri wakubwa na maskini wa kutupwa miongoni mwa raia na wadau wa nchi.

Sifa mojawapo ya Machera, ilikuwa ni huruma kwa watu walioonewa bila sababu. Hakupenda kuona amani ya mtu inatoweka kwa sababu mtu mwingine anataka kuona ufahari kwa gharama ya maskini huyo. Moyoni mwake alikuwa na kisasi cha kulipa, kumlipia mnyonge asiyejiweza. Alidhamiria kumwadabisha mla rushwa na fisadi yeyote yule aliyethibitika. Ni hapo ambapo alikutana na Maisha na pamoja wakafanya kazi ya kutetea maskini, ajue haki yake na aipate.

Hapo akagundua uozo wa mzee Mabruki, jinsi alivyowatumia wasichana warembo kuingiza dawa za kulevya shuleni na vyuoni. Wao walivaa mavazi katika mitindo ambayo ingeamsha ashki za mapenzi na kuwatia majaribuni vijana barobaro na shababi. Kama hiyo haikutosha, wasichana hao walifunzwa kujitongozesha kiasi kwamba hata madomo zege walijikuta wakiwamega kirahisi kabisa, lakini wakaishia kuwa si wamegaji tu, bali walijikuta wakifundishwa ubwiaji wa madawa ya kulevya na kugeuzwa mateja. Hivyo, ngome ya Don ilikuwa na hakika ya biashara kwa sababu soko halikuwa na mshindani na lilikuwa la uhakika. Wanawake na wasichana hao, hawakuushia tu mitaani, la hasha, walivuka mipaka na kuingia mashuleni kama wanafunzi, hasa hasa vyuoni na kuendesha biashara ya dawa za kulevya. Vijana wengi, kwa kupenda mserereko na kushobokea Mali na umaarufu bila juhudi, wakakumbwa na kimbunga cha matumizi na wengine kujiingiza kwenye biashara hizo.

Mitaani nako hivyo hivyo, warembo hao waliuza miili yao na dawa za kulevya. Hata pale polisi walipofanya msako, wangewapita warembo hao huku wakifukuzana na mateja ambao hawakujua mwenye biashara ile. Kila siku vilisikika vilio miongoni mwa raia juu ya vifo vya kutatanisha vilivyohusisha watu kuchunwa ngozi na albino kukatwa viungo mbalimbali vya miili yao na Vijana kufa kwa aidha kuzidisha matumizi ya dawa za kulevya au ugomvi tu uliohusiana na dhulma katika biashara hizo.

Pamoja na yote hayo kuwa dhahiri shahiri, hakuna raia hata mmoja ambaye angekubaliana nawe kama ungetaja jina la “The Don” kuwa ndio mhusika wa masaibu yote hayo. Si ajabu kwamba wangeandamana kuwa unamchafulia jina mtetezi wao. The Don, aliwawezesha kuishi maisha ya kisasa. Hata serikali iliposuasua kupeleka fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali, The Don alizama mifukoni mwake na kutekeleza. Vikundi vya kina mama na vijana, vilipewa mikopo nafuu kujiimarisha kibiashara. Vijana walijiajiri kwa msaada wa The Don. Vijiwe vingi mijini na vijijini kulibandikwa chata za The Don. Hata ungekuwa una shida gani, kama ungefanikiwa kuonana na The Don, ungefanikiwa kuitatua. Huyo ndio Mabruk waliyemfahamu.

Mabruki alikuwa na taasisi za kusaidia watu kwa kila nyanja. Ndio, wapo wanafunzi waliosomeshwa kwa ufadhili wa Mabruki, wapo wagonjwa wasiojiweza waliotibiwa kwa ufadhili wa Mabruki. Kwenye jamii, Mabruki alikuwa ni shujaa. Mtetezi wa wanyonge bungeni. Waziri mtekelezaji. Mtu wa watu! Ungesema nini dhidi ya Mabruki mbele ya umma urudi salama nyumbani kwako?

Tutaendelea
David
FB_IMG_1591786598873.jpg
 
9
Mheshimiwa the Don
MTUNZI: DAVID NGOCHO SAMSON

***
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Taifa, mheshimwa Sebastiani Masebo, mzee wa makamo, mrefu mwenye haiba ya kimazoezi alikuwa miongoni mwa viongozi wa serikali waliokuwa na uzalendo wa kweli na nchi yake. Huyu alichukulia suala la usalama wa taifa kwa kipaumbele, akitetea maslahi ya nchi kwa nguvu na uwezo wote wa cheo alichopewa dhamana kukisimamia.

Harakati zake katika nafasi hiyo zilimkutanisha na Machera, kijana mwajiriwa katika wizara yake, wakashirikiana katika masuala mbalimbali ya usalama wa raia.

Gunduzi mbalimballi zilizofanywa na Machera na wenzake, zilimfanya Masebo aduwae. Hakuamini kwamba binamu yake Mabruki alikuwa na roho ngumu kiasi kile. Na kisa nini? Utajiri. Hilo likampa hamasa zaidi ya kuendeleza mapambano dhidi ya mafisadi hao mufilisi.

Leo aliamka asubuhi mapema saa kumi na moja, akafanya mazoezi kidogo kuweka mwili sawa kabla ya kuingia bafuni na kuyaruhusu maji kutoka kwenye shower yautalii mwili wake na kumpa burudani ya pekee. Baada ya hapo, alipata kifungua kinywa maridhawa kisha akalifuata gari lake lenye usajili wa Waziri wa Mambo ya ndani. Dereva wake alikuwa tayari kwenye usukani akimngojea Mheshimiwa Waziri ili kutimiza wajibu wake wa kumpeleka ofisini. Kazi zake za ofisini zilikuwa nyingi na kwa sehemu kubwa zikiwa zile za uhamiaji.
Alitekeleza majukumu hayo ya kitaifa, na aliponyanyua uso wake kutazama saaa ya ukutani mle ofisini, mshale ulikuwa kwenye tarakimu ya kirumi iliyomjulisha ni saa nane za mchana. Kazi zilikuwa nyingi Kiasi kwamba muda ulionekana kwenda mbio za mkata upepo Usain Bolt. Alinyanyuka kitini, akanyoosha mkono kuchukua miwani yake iliyokuwa pembeni upande wa kulia ea kompyuta yake ya ofisi, akaipuliza kidogo kwa hewa kutoka mdomoni mwake na kuipangusa kwa kitambaa kidogo maalum kwa kazi hiyo. Aliporidhika na usafi huo, akaipachika machoni. Aliweka ofisi yake vema tayari kutoka, lakini akatulizwa na katibu wake muhtasi ambaye alimpasha habari kuwa tayari alikuwa kamwandalia cha mchana, hivyo, alipata mlo wa mchana halafu akaelekea Kilimanjaro Hoteli kuwahi miadi yake ya kukutana na Machera.

Alipowasili hotelini, alikuta Machera tayari yupo eneo la tukio, wakaketi katika moja ya meza iliyokuwa imeandaliwa kwa wageni wa hadhi ya Waziri katika moja ya kumbi zilizopo ndani ya Hoteli ile ya kisasa. Walipokwisha kutulia, Machera akachomoa bia mbili zinazozalishwa na kampuni moja la wazawa kwenye bahasha kubwa ya khaki na kuweka mezani. Ilikuwa bia ambayo Mheshimiwa Waziri alipendelea kutumia, halafu akamkaribisha mheshimiwa ambaye alipokea kwa shukrani.

Wakati Amos, yule mshirika wa Siri wa Estivani Brown alipowasili na kinywaji kilichokusudiwa kuteketeza maisha ya wawili hao, mpango ambao Estivani Brown alikusudia kuutekeleza licha ya onyo la the Don, akawakuta wazalendo hao wakiburudika na kinywaji chao huku wakiendelea na mazungumzo ambayo yalikuwa muhimu Sana bila shaka. Kwa namna hiyo, jaribio la sumu kwenye vinywaji ili kuwapoteza Mheshimiwa Masebo pamoja Machera liligonga mwamba na kurudi mikono mitupu.

Miongoni mwa mada katika mazungumzo ya kikao chao, kubwa lilikuwa juu ya mauaji ya albino mkoani Mbeya ambayo upelelezi ulithibitisha kuhusika kwa The Don. Muuaji alikiri kutumwa kufanya kitendo hicho kwa malipo ya shilingi laki tano pekee. Machera alimweleza Mheshimiwa Masebo.

“Laki tano tu?!" Waziri Masebo alihoji, mshangao ukidhihirika usoni mwake kama vile hakuwa tayari kuamini.
“Naam mheshimiwa, hii ni baada ya kufuatilia mlolongo wa utekelezaji wa matukio hayo kwa kutumia intelijensia ya juu sana. Mtekezaji wa mauaji hauyo alidai lilikuwa ni agizo la mganga wa kienyeji katika kutekeleza matakwa ya kujipatia utajiri. Kilichotushangaza, ni mazingira anayoishi huyo mganga. Jumba la kisasa lenye ulinzi wa CCTV na wa kampuni. Mganga wa kienyeji anayeishi maisha hasa ambayo wanaousaka utajiri wanayatamani. Sio waganga wale wanaopatikana maporini kwenye vichaka wakitopea kwenye umaskini wa kutisha huku wakiahidi kuwapa watu utajiri ambao hawana. Huyu mganga, yeye binafsi alikuwa ni mfano halisi wa utajiri waliosaka wateja wake. Kwa hakika mheshimiwa, mtu yeyote mwenye kusaka utajiri kwa njia za ushirikina, lazima angekubali kutekeleza masharti yoyote yale ambayo angepewa na mganga yule.!" Machera alimweleza waziri Masebo na kuweka kituo hapo, alimtazama Waziri akiyasharabu maneno yake huku akitikisa kichwa kwa masikitiko.
Waziri alitoa sauti ya mguno huku akionekana kuzama katika kuyasharabu maelezo aliyotoa Machera.

"Kwa jinsi hiyo ni dhahiri kuwa hicho ndicho chanzo cha kuongezeka mauaji mkoani Mbeya.' Waziri Masebo akatamka kwa namna ya kuonesha masikitiko makubwa halafu akamalizia kwa swali. ''Kwa hiyo mliweza vipi kubaini kuwa ni Mabruki anahusika.?" Waziri Masebo akahoji.

"Tulimkamata mganga, lakini jioni yake, mganga yule alifanikiwa kutoroka kituoni. Kulikuwa na kila dalili kuwa kuna mtu wetu si mtu wetu tena kwenye Jeshi la polisi, ni mtu huyo ambaye alihusika kumtorosha. Hatujamfahamu bado, lakini tunaendelea kufanya upelelezi kimya kimya. Hata hivyo, imetushangaza sana jinsi watu hao walivyojipanga, kwa sababu, habari zimeenea kote jijini Mbeya, kuwa Mganga huyo baada ya kukamatwa alitoka mkononi mwa Jeshi la polisi kwa njia za kichawi, na hivyo, ameendelea kujitengenezea jina kubwa kwa wale wenye kuamini ushirikina. Si ajabu kuwa, sasa jeshi letu la polisi bila kuridhia, limetumika kama promo kubwa kwa mganga huyo, Jambo ambalo linalitia kashfa jeshi la polisi." Machera alimeza funda kadhaa za kinywaji chake halafu akaendelea kueleza.

"Hata hivyo, tuliendelea na upelelezi wetu na hapo ndio tulipogundua kuwa, ule mjengo alioishi mganga, Wala si wake bali ni moja ya mali za kampuni moja wapo za mheshimiwa Mabruki."

"Kwa maana nyingine, bado hawezi kusimama kizimbani kwa tuhuma hizi?!" Waziri Masebo akataka kujiridhisha na uwezekano wa kukamatwa kwa Mabruki binamu yake.

"Kusema kweli bado hatuna kitu cha maana cha kusema tunaweza kumsimamishia mbele ya hakimu. Tunajua kwa hakika kuwa ni yeye anayehusika, lakini hatuna kitu cha kumhusisha moja kwa moja. Isitoshe, huyu ni mtu ambaye katika kujilinda, ameweka mapandikizi wake kwenye idara muhimu za kiintelijensia, ambapo kila hatua tunayopiga kumwelekea, anakuwa tayari ana taarifa. Utakumbuka pia, kwamba anamiliki kampuni ya uwakili, ambayo imekuwa ikitetea wahalifu wote wanaohusishwa naye na wamekuwa wakishinda mara zote. Maana baadhi ya mawakili wenye uwezo kwenye fani hiyo, wapo kwenye orodha ya marupurupu manono kutoka kwa Mabruki!" Machera akaendelea kueleza. Waziri Sebastian Masebo akajipata njia panda. Hakika alihisi kuwa kazi hiyo ya uwaziri ulikuwa mzigo wa misumari ambayo alitwishwa kwenye kichwa chenye kipara mithili ya vijana wa jkt mafunzoni au wafungwa wa kule Segerea.

Jeshi la polisi tayari lilikuwa linakumbwa na kashfa kibao za rushwa na uonevu. Na sasa kashfa kubwa ilikuwa inaendelea kusambaa mitandaoni na magazetini, juu ya Mganga maarufu jijini Mbeya kupotea mkononi mwa Jeshi hilo tumainiwa kwa namna iliyoupa ushindi upande wa adui. Ni kashfa hiyo iliyomlazimu kuitisha kikao hiki na kijana pekee aliyemwamini katika idara hiyo ambayo ilionekana kuoza kwa udhalimu na rushwa huku mauaji ya watu na matukio ya kutisha yakilikabili taifa, kana kwamba Jeshi hilo halikuwepo. Kibarua chake kilikuwa kwenye njia panda.

"Tunafanyaje sasa?" Waziri akauliza hatimaye, usoni kwake kukisomeka kila dalili ya kushindwa na kuelemewa. Ni kweli alijitahidi kufanya kila liwezekanalo lakini kwa hali iliyokuwa inaendelea nchini, alikuwa amebakiwa na hatua moja tu. Kujiuzuru wadhifa huo, ambao sasa ulionekana kuwa mzigo. Naam! Ilikuwa heri kujiuzuru kuliko kutumbuliwa. Mbaya zaidi, mbaya wake alikuwa ni mtu ambaye walihusiana kikazi na kifamilia. Alikuwa ni waziri Mabruki, wakikutana kwenye baraza la mawaziri mahali ambapo angeweza kulielezea suala hili kwa mheshimiwa Rais. Lakini, angewezaje sasa ikiwa hakuwa na taarifa mahsusi ya kumnyooshea kidole kwenye baraza la mawaziri?

Huyu Mabruki ambaye ilijulikana wazi ni binamu yake. Hata kama angethubutu kumtaja kama mtu hatari, je! Isingeonekana kuwa ni ugomvi tu wa kifamilia? Masebo alihisi kichwa kikizunguka. Hakuna namna, kulikuwa na kila haja ya kumshirikisha mtu kitendawili chake hicho. Machera alikuwa mtu sahihi.
"Nadhani sasa nina uamuzi mmoja tu wa kufanya. Ninatakiwa kujiuzuru wadhifa huu mara moja kabla sijatumbuliwa. Hizi hoja za kukiri kuwa mauaji yanafanywa na watu wasiojulikana hazinipi taswira ya maana kwa taifa." Waziri Masebo akakiri. Uso ukiwa umesawijika kwa uzito wa fikra.

"Hapana mheshimiwa, nikuombe uwe na imani kidogo, naamini kuna uwezekano wa kumtia hatiani. Vumilia walau mwezi mmoja zaidi, kuna taarifa tunaifanyia kazi, tukifeli basi mimi mwenyewe nitakushauri kuchukua maamuzi hayo!" Machera alishauri. Wakakubaliana.

Itaendelea
David
FB_IMG_1591786598873.jpg
 
10
Mheshimiwa the Don
David Ngocho Samson
0629077792 WhatsApp

*†*
Jioni ya saa mbili za usiku, Machera akiwa na Anastazia, walikuwa wakipata mlo wa jioni katika Hoteli ya Kilimanjaro, kwenye viwanja maridadi vya hoteli hiyo kubwa ya kisasa. Walikuwa wamevaa kimichezo. Mengi ya mazungumzo yao yakiwa juu ya shughuli zao na utani mwingi wa kimapenzi. Walikuwa hapo kwa kazi maalum. Kwa asiyewafahamu, hakika angejua tu hawa ni wapenzi waliotoka kufunga pingu za maisha na wapo hapo kwa fungate lao mujarabu.

Meza ya nyuma yao kwa mbali kidogo walikaa Elinisa na Asha. Elinisa alivalia suti yake nyeusi na miwani myeusi. Asha alivaa sketi fupi na blauzi iliyoacha wazi sehemu kubwa ya mabegani na kifuani na kumfanya avutie kimahaba.

Miguu yake iliyojengeka vema ilitosha kuwa kishawishi cha kumfanya mwanaume rijali apagawe achilia mbali vishimo vilivyobonyea shavuni mwake na tabasamu lililochanua vema kwenye sura nzuri yenye ngozi laini na rangi ya watu kutoka mashariki ya kati. Nywele zake, alizitengeneza kwa mtindo ambao ulimpendezea haswa, huku fungu la nywele hizo likifunika moja ya jicho lake kiaina, ikawa kama anachungulia kwa jicho moja, lakini Mara moja moja alifanya kuzisogeza nywele hizo na kuruhusu jicho Hilo kuonekana pamoja na nyusi zake pia, kope zake ndefu, zilivutia kwelikweli na kumpa mwonekano wa pekee. Alivutia Sana.

Kwenye upande wa kushoto wa ziwa lake, hapo alining'iniza miwani yake ya macho ambayo pia iliongezea kwenye ulimbwende wake. Walikuwa wenye furaha mno. Lugha ya Kiingereza waliyoongea, ingemfanya mtu ahisi ni watalii kutoka Marekani. Muda wote huo Anastazia alikuwa anawapiga jicho la udadisi wawili hao kiwizi wizi.

Mara Ana aliwashuhudia wakianza kufukuzana, Asha mbele na Elinisa nyuma huku wakicheka na kutupiana tumaneno twa kimahaba.
Akiwa katikati ya mazungumzo, Anastazia alinyanyuka ghafula huku akimwangalia Elinisa kwa jicho la wasiwasi zaidi! Hali hiyo ikamshangaza Machera.

“Hey, vipi bibie?” Machera alihoji akijaribu kuzungusha shingo yake ili macho yake pia yapate kushuhudia kilichomduwaza mwenzie.

“Yule mwanaume namfahamu kama si kumfananisha,” Anastazia alijibu huku akivuta makini zaidi kumchunguza yule mwanaume, Elinisa!

“Kivipi?” Machera alihoji, akitia bidii ya kumchunguza mwanaume yule pia. Hata hivyo hakuna alichong'amua.

“Miaka mitatu iliyopita alisadikika kufa kwa ajali ya ndege, ile iliyoanguka maeneo ya New York ilipojaribu kutua. Kabla ya kifo hicho alikuwa anatafutwa na interpol kwa makosa ya wizi wa fedha kwa njia ya elektroniki kwenye benki zaidi ya tano kubwa duniani ikiwamo Barabank na ADB,” Ana alisimulia.

“Hizo habari hata mimi nilizisikia, lakini simfahamu. Sasa wewe umemtambua hata sura?” Machera akahoji kwa udadisi.

“Ni kweli, mimi niliona picha yake kwenye mtandao na jina lake lilionekana katika orodha ya waliosafiri na ndege ile. Lakini hata hivyo binafsi niliwahi kukutana naye kwenye semina moja Arusha, na tofauti na wewe yeye alinipenda akanitongoza na tuka-‘do’. Na hapo ndipo nilipomfahamu” Ana alizidi kumchambua mwanaume yule huku akijaribu kumtia wivu Machera kwa kuchomekea suala la mahaba.

“Anaitwa nani?” alihoji Machera.

“Elineema….Yeah, Elineema Urio”

“Sawa, enhee, nipe maelezo ya kina ni nini anafanya hapa nchini kama ni marehemu, sawa mpenzi ila, nisikilize vizuri hapa, usi-do naye” Machera alizungumza huku akidhihirisha wivu kama alivyotarajiwa na Ana.

“Nani mpenzi wako? Ukome na ukomae! Siku zote nimekuwa nateseka kwa mapenzi juu yako na hakuna kitu umenifanya zaidi ya maneno tu. Nionyeshe mapenzi ya kweli, nipende Machera, mbona mimi ni mzuri na wanaume wengine wananimezea mate kila wakiniona, wewe tu! Una nini wewe mwanaume?” alilalamika kwa hisia.

“Ombi lako limepata majibu, leo umenipata wala usijali, tumalize kula halafu utamjua Machera” aliongea Machera huku akimshika mkono Anastazia kwa huba, Ana alinyanyuka na huku wakiwa wameshikana viunoni. Wakaelekea hotelini.

*†*

Baada ya kutoka pale viungani, Anastazia hakupata utulivu, moyo wake ulikuwa unamkereketa kuhusiana na mwanaume yule Elinisa. Yeye akimtambua kama Elineema Urio. Ndio, ilikuwa siku nyingi sasa tangu kiripotiwe kifo chake, taarifa zikidai jamaa huyo alikuwa hacker mmoja hatari na ambaye utajiri wake ulitokana na wizi wa fedha kwa njia za kielektroniki. Ajabu sana. Ni taarifa ambayo ilimwacha njia panda. Mwanaume huyo, alikutana naye Arusha. Katika moja ya mambo ambayo yalimfanya Ana ampende mwanaume huyo na kuhakikisha anashirikiana naye kimapenzi ni hulka yake ya upole na ustaarabu, hakuwa mtu wa papara wala majigambo. Alimpenda na kuruhusu mwanaume huyo kuuchezeana mwili wake ingawa hakuna makubaliano yoyote maalumu waliyowekeana. Hilo likiwa suala ambalo bila wao kujua, kila mmoja alilifurahia mno. Hakuna kati yao aliyekuwa tayari kwa commitment. Ana kwa asili ya kazi yake, na Elineema pia kwa asili ya kazi yake. Kila mmoja alificha ukweli, na penzi lao la muda mfupi likaacha alama kwa Ana.

Asingeweza kumsahau kijana yule mpole, ambaye aliamua kuanzisha taasisi ambayo ilishirikiana na serikali ya Tanzania, lengo likiwa ni juhudi za dhati za kupambana na umaskini. Kukutana kwao pia kukiwa ni katika moja ya harakati ya taasisi ya kijana yule kuandaa semina shirikishi juu ya vita dhidi ya umaskini.

Ana alipopata taarifa za kifo cha Elineema Urio, hakika alijihisi mkiwa, alikuwa sawa na mke wa marehemu aliyeondokewa na mumewe. Aliomboleza, akikumbuka raha na starehe zote alizoshiriki naye. Hivyo, asingekubali kirahisi kumuona hapa, tena akiwa hai, akivinjari na mwanamke mwingine, ikiwa alifeki kifo. Anastazia alihakikisha anafahamu alipoishi Elinisa baada ya kuwafuatilia usiku ule. Halafu akarejea hotelini ambapo alimkumkuta Machera akiongea kwenye simu.

“Nani huyo unaongea naye?” alihoji Ana kwa wivu.

“Rafiki yangu.” Machera alijibu huku akiiweka ile simu kwenye meza ndogo pembezoni mwa kitanda. Ana alimwendea Machera pale kitandani na Machera akampokea kwa mikono miwili.

“Machera, kweli unanipenda?” Ana akahoji. Alikuwa kachanganywa kabisa na kumuona Elinisa, yeye akimdhania ni Elineema Urio.

“Kwa nini nikuchukie?” Machera akajibu kwa masihara.

“Unajua mimi nakupenda sana Machera, kwa hakika niko radhi kwa lolote juu yako.” Ana Sasa alikuwa anajaribu kupima kina cha maji kwa mguu.

“Sasa unahofu nini napokuambia nakupenda?”

“Utanioa?”

“Kuoa? haitowezekana Ana, nadhani nilishakueleza toka awali sababu yangu ya kushindwa kufanya hivyo.”

“Mimi? Hujanieleza chochote!”

“Acha hizo bwana au ndo unataka kuninyima mwenzio furaha”

“Basi nieleze nijue au huna mpango na mimi?”

“Mwenzio nina mke.”

“Mke? Mke? Kweli maskini haokoti, akiokota huambiwa kaiba, nilidhani tutaoana.”

“Sasa nifanyeje Ana?”

“Njoo,” alitamka Ana huku akimvuta Machera karibu yake na kumkumbatia. Akili yake ikimuwaza Elinisa.

*†*

Asubuhi ya saa mbili hivi, Ana alielekea kwa Elinisa na safari hii alifanikiwa kumkuta peke yake. Alikaribishwa ndani. Macho yake yalidadisi sura na mwonekano wa mwenyeji wake ili agundue kama ni Elineema au siyo. Hakukuwa na shaka kwamba huyu mwenyeji wake ndiye Elineema, ila mbona ajifanye kutomfahamu kabisa! Ahaa.... anataka kuficha ukweli wake! Ana alijiwazia mwenyewe.

“Kuna maziwa na kahawa, ungependelea kinywaji gani?” Elinisa alihoji baada ya kumkaribisha mgeni huyu aliyemvamia asubuhi na mapema.

“Kahawa tafadhali” Ana akajibu kikamanda. Waliketi mezani Ana akiendelea kufanya udadisi.

“Inawezekana kwamba hunikumbuki kabisa?” uvumilivu ulimkimbia ghafla, akauliza swali lililokuwa linamkereketa moyoni.

“Sijui, labda unikumbushe, tulishawahi kukutana?” Elinisa naye akarejesha swali.

“Semina Arusha, mkakati wa kupambana na umaskini” Ana akajibu kwa kujiamini akiamini kumbukumbu zingemrejeshea kukutana kwao mwenyeji wake huyu.

“Hapana, Arusha kwenye semina? Hapana” Elinisa alijibu huku akimtazama kwa udadisi zaidi mwanamke huyu jasiri, aliyekuwa, kwa maoni yake, anajaribu kujigonga kwake.

“Sawa, jina lako nani?” Ana akahoji tena. Safari hii akijiaminisha kwamba huyu alikuwa ni Elineema ambaye bila shaka asingependa ifahamike hivyo, ndiyo, asingependa ifahamike hivyo kwa kuwa tayari alikwishauaminisha ulimwengu wote kuwa yeye ni mfu. Iweje sasa akiri ni yeye ikiwa dunia nzima inafahamu yeye ni marehemu. Tabasamu laini likatokeza kwenye kingo ya kushoto ya mdomo wake kwa kuubaini ukweli huo. Wacha nisikie jina bandia alilojipachika. Anastazia akajiwazia.

“Elinisa Urio na wewe ni?” Elinisa akajibu huku akimtupia swali. Anastazia akatoa macho ya mshangao na kujibu kwa kifupi.

“Anastazia.” hakutarajia jibu hilo kama ambavyo hakutarajia kushikwa na mshangao.

“Sawa Anastazia, kama hutaona taabu unaweza kunieleza nini kinaendelea hapa maana maswali yako yamekaa kimtego vile!”
Elinisa akaamua kuutua mzigo mzito wa wasiwasi aliokuwa anajaribu kuficha.

“Bila shaka nimekufananisha” Ana akajibu, usoni mwake akijitia kuona haya.

“Umenifananisha na nani?” Elinisa akauliza akiwa anamtazama barabara usoni.

“Marehemu, mpenzi wangu”

“Marehemu?” Ely akauliza kwa hamaki. Akajiuliza huyu mwanamke alikuwa anafanya mchezo gani.

“Ndiyo marehemu, kwa sababu alikwishakufa yapata miaka mitatu sasa, cha ajabu ni kwamba mnafanana mno na ubini wenu unafanana pia. Alikuwa akiitwa Elineema Urio.” Ana akatamka huku akiwaza 'haya sasa tuone kiswahili kingine utakacholeta hapa!'
Ni hapo ndipo Elinisa alipopata kung'amua nini kilikuwa kinaendelea.

“Unamuongelea kaka yangu, tulikuwa pacha lakini yeye kama ulivyosema...”Elinisa akathibitisha. Mshangao ukamshika Anastazia. Hakuwa amefikiria uwezekano huo.

"Wewe si mtu wa kwanza kunidhania kuwa ni Elineema, hasa kutokana na kashfa aliyopata kabla ya kifo chake. Hata serikali ya Marekani ilikwisha nitia mbaroni kwa kudhania mimi ni yeye, kilichoniokoa ni utofauti wa fingerprints zetu. Mungu ni fundi hakika!" Elinisa alizungumza kwa namna ambayo alimuondolea mashaka Ana.

'Mh, Mungu kweli fundi, yaani sauti na kila kitu ni vile vile' Anastazia aliwaza halafu akatamka;
“Sasa napata picha! Unajua, niliwaona pale Kilimanjaro Hotel na ulikuwa na mrembo mmoja hivi, nikajiuliza, Elineema amefufuka? Hivyo nilikufuatilieni hadi nikapafahamu hapa na ndio maana niko hapa” Ana akaweka wazi dukuduku lililompeleka mpera-mpera kwa shemejie huyu.

“Karibu sana shemeji, jisikie huru, nasikitika nimekukumbusha habari za majonzi,” Elinisa akasikitika.

“Asante shem, Maadam nimepafahamu kwako, mbona utachoka kuniona? Ah, nashukuru kwa kahawa shemeji, lakini naomba kwa sasa nikukimbie kidogo, kuna sehemu natakiwa kufika muda huu.. Nikiri wazi kuwa kwa muda nilihisi ni Elly, hata hivyo nimefurahi sana kufahamiana nawe” Ana alijieleza huku akijinyanyua tayari kuondoka.

“Na ni kweli mimi ni Elly, sema Elly huyu ni Elinisa! Nimefurahi kukufahamu pia Ana” Elinisa akatamka huku wakishikana mikono na vicheko vikiwatoka. Ni kwenye vicheko hivyo, Anastazia alipobaini utofauti kati ya Elineema na Elinisa. Naam, mpangilio wa safu za meno midomoni mwao na ile hali ya kuungulia meno iliyokuwa kama alama ya ukanda wa kaskazini. Ana aliitambua tofauti hiyo.

Itaendelea
David Ngocho Samson
FB_IMG_1591786598873.jpg
 
11
Mheshimiwa the Don
David Ngocho Samson

GEOF alifika kwenye makazi ya mzee Mabruki na kujitambulisha kwa walinzi ambao walimruhusa aingie kwenye ofisi kubwa ya kisasa ndani ya kasri hilo la The Don. Kila kitu ndani ya jengo hilo kilikuwa cha kisasa na cha gharama. Lilikuwa jengo la ghorofa tatu. Alipandisha vidato vya ngazi kupanda orofani akiwa anatafakari lini na yeye angefikia kiwango cha utajiri aliomiliki the Don. Kadri alivyokuwa anapanda ngazi hizo na kutazama picha za tingatinga zilizopamba kuta za jengo hilo, mifano ya wanyama hai kama swala, ngiri na wengineo waliowekwa kwa ustadi katika korido za jengo hilo, Geof akajikuta akitamani muda uende kasi afikie kiwango cha utajiri wa Don kwa mujibu wa taratibu za umoja wao ule wa siri.

Utajiri wa Don ulimwezesha kuishi kama yuko peponi. Maisha matamu. Biashara zake zilikuwa za mamilioni ya fedha za Kimarekani. Kila kitu alichoshuhudia Geof kwenye jengo hilo kilikuwa cha thamani halisi, bora kabisa, na wazungu husema, 'genuine'. Hatimaye akakifikia chumba cha mapokezi kwenye ofisi ya Don, hapo aliketi msichana mrembo mwenye asili ya Kihindi. Geof akamweleza shida yake ya kuonana na mheshimiwa.

Alielekezwa kusubiri kwa dakika moja wakati binti yule akiwasiliana na Mheshimiwa Mabruki juu ya ujio wake. Pamoja na kuwa hakuwa ameweka miadi ya kuonana na Don, kutajwa kwa jina lake na binti yule kulimpatia tiketi ya kuonana na Don, japo ilikuwa kama kwa hati ya dharura. Kwa kawaida, Don alipenda kujionesha ni mtu wa watu, lakini alikuwa keshaweka utaratibu. Ukitaka kuonana naye, sharti uweke miadi walau kwa siku moja kabla. Don aliuvunja utaratibu huo kwa vile Geof alikuwa mmoja kati ya vijana ingizo jipya kwenye chama chao cha siri, na alikuwa na ajenda yake binafsi kwa kijana huyo.

Binti yule alipoutoa mezani mkonga wa simu ile, alimtamkia Geof kwa utani;
"Kwa hakika kaka una bahati ya mtende wallahi, ni kwa nadra see ukute mzee anakubali wito usio na appointment. Karibu pita, yupo ndani anakusubiri."

Mzee Mabruki alikuwa ameketi juu ya kiti chake akitazama habari za kwenye mitandao kwenye smart TV ya nchi 32 iliyokuwa imebandikwa ukutani mwa ofisi hiyo. Taarifa zile zilitokea kwenye simu janja yake na kuonekana mubashara kwenye kioo cha runinga ile. Alikaribishwa na wakasalimiana kwa ishara zao za usharika wao wa siri halafu mazungumzo yakachukua nafasi yake.
Geof akamsimulia the Don madhila yaliyokuwa yamempata ghafla kutokana na mtu aliyejukikana kwa jina la Elinisa. Alisimulia kwa maumivu makubwa kana kwamba the Don alikuwa na namna ya kumwepusha nayo. Mwishowe akaweka ombi lake wazi.

"Najua hili kwako si kubwa, ukisema neno na watu wako naamini muda si mrefu furaha na amani yangu vitarejea tena. Muhimu afe kabisa huyo mjinga" Geof alimrai the Don.

“Unaweza kuniambia kwa nini ni lazima tumuondoe huyo mwizi wako?” alihoji The Don.

“Mzee unamjua Asha, yule mchumba wangu, ameamua kuniacha kwa sababu ya huyu mshenzi kumdanganya, na unajua mipango ya harusi imekwishafanyika, nimeingia gharama na anataka kunitia aibu mzee, mimi naona nimtoe tu sadaka” Geof akatamka huku sura yake ikidhihirisha chuki isiyo kifani.

“Oh, wanawake wengi bwana Geof, ukitaka nitakupa watoto wazuri wenye mbinu kibao za mapenzi, umemuonaje huyo secretary wangu hapo? Unadhani anaweza kuziba pengo la mchumba wako? sema tu, si unamuona mtoto rangi ya mtume” The Don akatamka kwa dhihaka.

“Hilo si tatizo mzee, aibu ndo tatizo, wewe una kadi ya harusi na umeshachangia, nitaweka wapi uso wangu?” Geof alisema kwa hisia.

"Sawa, unafahamu uhai wa mtu si kitu kidogo, ni kazi kubwa hata kama unataka kutoa kafara. Kama unahitaji msaada wangu kuna gharama bwana Geof, kwa hiyo sijui unasemaje? Naa.. nikutahadharishe tu, kwa vile ni sadaka itabidi uweke ombi linaloambatana na sadaka yako kwenye kitabu chetu pamoja na saini yako. Lakini pia kuna taratibu za kuifanya ibaada hiyo ya sadaka, inahusisha mambo fulani ambayo, sharti yafanyike ili kukamilisha suala husika. Je, Unadhani bado uamuzi wako ni huo huo?" Don akamtupia swali.

Geof alishangaa, hakujua kama kitendo cha sadaka zao kilikuwa na mlolongo huo, Don alimfafanulia kwa kina taratibu hizo, moja ikiwa ya kuingia kwenye chumba cha siri kilichokuwa chini ya jengo lile ambamo mlikuwa mwanga hafifu sanawa njano na alipaswa kufanya ibada ya kishetani kabisa kwenye giza hilo na kutakiwa kufanya zinaa na mtu aliyesemekana kuwa ni kiongozi wa ibada hiyo, ikiwa ni sehemu ya mchakato wa sadaka yake. Kutokana na ukweli kuwa, roho ya kisasi ilikuwa imemtawala, Geof alifanya maamuzi ya kuingia kwenye taratibu hizo. Akaingia kwenye chumba hicho cha siri, chini ya jengo hilo.

Tofauti na alivyodhania hapo awali, kule chini alikuta sio chumba kidogo, la, ilikuwa ni ukumbi mmoja mkubwa kabisa.
Alivuliwa nguo akakabidhiwa kikombe kilichokuwa na kimiminika mfano wa damu. Alipaswa kunywa kimiminika chote kwenye kikombe hicho. Hapo akakutana na ladha mbaya hajapata kuonja maishani mwake, lakini akalazimika kunywa hivyo hivyo. Wakati akiendelea kukamilisha zoezi hilo, huku sura ameikunja kama anayeonja ndimu chachu, akatokeza binti wa kukadiria miaka ishirini hadi ishirini na mitano hivi. Mrembo wa haja. Alikuwa yu uchi kabisa mbele yake. Akamkaribia na kuanza kulambalamba michirizi ya kimiminika kile mfano wa damu iliyokuwa imejitokeza midomoni mwake kushuka kidevuni mwake, huku akiutoa ulimi wake mrefu na kuzamisha mdomoni mwa Geof. Kama hiyo haikumsisimua Geof, ambaye tayari kimiminika kile kilikuwa kimeanza kuonesha athari zake, binti huyo alizidi kuutalii mwili wake kwa ulimi hadi maeneo ambayo Geof alizidiwa na uvumilivu, akajikuta anamvutà binti yule na kama hayawani, wakaanza kufanya ufuska wa hatari mle ndani. Taa iliyokuwa mle ndani ilitoa mwanga hafifu wa njano na hivyo iliwawezesha wawili hao kuonana miili yao. Hata hivyo, kwa athari za kile kinywaji alichonyweshwa, ilionekana kama sura ya binti yule ilikuwa ikibadikika badilika hata hakuweza kuihifadhi kwenye kumbukumbu zake. Alikuwa amelewa kwa kinywaji asichokijua.

Kitendo kile kilimjaza Geof roho ya kishetani, kiasi kwamba alipotoka mle ukumbini alikuwa ni mnyama, mnyama katika roho yake na shetani, kasoro mkia. Baada ya zoezi hilo lililohusisha ngono isiyo ya kawaida, Geof alivalishwa mavazi yake na kurejea ofisini kwa Mabruki.

Hawakukaa humo, ajabu ni kwamba mzee Mabruki alimsifu Geof kwa kufuzu vema hatua yake ya kwanza ya usharika wao na kumwambia bado kulikuwa na hatua kadhaa bado alizotakiwa kufuzu. Halafu alimshika mkono na kumwambia Geof amfuate, walishuka kwa lift ile iliyomleta mle ofisini. Ilionekana kwamba, lift ile ilianzia ofisini mle na kushuka ardhini kwenye ukumbi ule ambao baadaye alikuja kubaini, ilikuwa ni eneo maalumu kwa ibada za chama chao cha siri.

Lift hiyo, ilikuwa imefichwa ukutani, kiasi kwamba kwa mtu asiyejua hilo, isingekuwa rahisi kubaini uwepo wake. Na switch ya kufungua lift hiyo, ilikuwa ni codes ambazo aliingiza kwenye simu. Waliingia tena kwenye lift ile, safari hii wakiwa wawili tofauti na awaki ambapo alielekezwa kuipanda na kushuka kule chini mwenyewe. Walipokwisha kuteremka kule chini, huko waliingia kwenye chumba kingine, hicho kilijaa uchafu na ufuska wa mzee Mabruki. Ukutani mlikuwa na picha za mzee Mabruki akiingiliwa kinyume cha maumbile na nyingine zikimwonyesha akiwafanyia kitendo hicho wanawake kadhaa kwa kutumia nyeti za bandia, wanawake ambao walifahamika jijini kwa utajiri na ufanyabiashara mkubwa.

Kulikuwa na skirini kubwa ikionyesha picha hizo chafu na watu mbalimbali mashuhuri wengine wakiwa viongozi wa dini mbalimbali; Wakristo kwa Waislamu; wapagani kwa Wahindu; wanasiasa kwa wasomi na kada mbalimbali za watu. Ushetani wao ukawapanda vichwani mwao na bila aibu wakarudiana, Mabruk akidhihirisha alikuwa shoga aliyekubuhu! Hayo yote yakiwa matokeo ya kutaka kumuondoa Elinisa katika uso wa dunia. Mbali na yote hayo, bado alilazimika kugharamia kwa fedha taslimu pia. Jumla yake ikiwa malipo ya shilingi milioni tano.

Itaendelea
FB_IMG_1591786598873.jpg
 
12
Mheshimiwa the Don
David Ngocho Samson

*†*
Baada ya Geof kujikuta kwenye masharti magumu kwa Don, alirejea nyumbani kwake na kusubiria matokeo ya kazi aliyompa mzee Mabruki. Siku ya kwanza ikapita, kimya, hakupata mrejesho wowote, hali alikuwa roho juu akitamani kusikia tu, kwamba Elinisa hayupo tena duniani. Akaamua kumpigia simu Asha. Simu ikaita bila kupokelewa. Haikuwa kawaida ya Asha. Wakati akiendelea kujihoji kulikoni Asha kufikia kiwango cha kutopokea simu yake, Mara simu yake ikapata ugeni. Kwenye kioo cha simu hiyo, jina Hussein likaonekana barabara.

Kwa kawaida waliwasiliana na kaka yake Hussein mara kwa mara, lakini safari hii, wito wa simu ya kaka yake ulimtia wasiwasi. Hii ni kutokana na ukweli kuwa Hussein alikuwa kwa wiki mbili mfululizo, anashughulikia matibabu ya mama yao aliyekuwa kalazwa hospitalini KCMC kutokana na maradhi ya mgongo.

“Habari za huko kaka?” alihoji kwa kimuhemuhe.

“Siyo nzuri, mama bado yupo hospitalini KCMC anaumwa sana, unahitajika Moshi” Hussein akaeleza kwa sauti iliyojaa majonzi na huzuni mwingi.

“Sawa kaka na poleni kwa kuuguza. Ngoja nifanye mpango wa usafiri wa haraka”. Geof akaeleza, kichwani akiwaza namna ya kuwahi Moshi haraka iwezekanavyo.

Huyo alikuwa mama yake, ingawa hakumzaa, lakini alimnyonyesha wakichangia ziwa na kaka yake Hussein ambaye alikuwa na miezi sita wakati yeye anaokotwa akiwa na siku mbili au tatu. Alikurupuka na kuelekea Ubungo ambako alipata gari la mwisho kuelekea Moshi.

Aliwasili hospitalini KCMC na kukaribishwa na taarifa mbaya, kwamba mama yake huyo aliyemlea toka uchanga wake alikuwa ameaga dunia. Hakuwa naye tena, Geof akaomboleza. Mama yake hakumsubiri, akaondoka bila kumuaga. Musiba ulipaswa kufanyika kijijini kwao huko Mbeya. Walifanya mpango wa usafiri na kusafirisha mwili kwenda Mbeya kwa mazishi.

***
Elinisa alikuwa amemsindikiza Asha na sasa alikuwa anarejea nyumbani kwake. Mara ghafula alitokea mtu amevalia kinyago usoni, akashituka, lakini haikumchukua mtu huyo mwenye kinyago usoni muda kumfikia Ely. Kwa muda, Ely akajipata ameganda kwa bumbuwazi, ni kama hakuhisi chochote.
Alijaribu kupiga kelele lakini akaishia kuzisikia mwenyewe. Alipopata akili ya kujitetea, akakunja ngumi na kumtandika adui yake katikati ya miguu. Adui akaanguka chini.
Elinisa akapata upenyo wa kutoroka, lakini alichelewa kidogo tu, akajishudia mwili wake ukipingana na kusudi la roho yake iliyomtaka kukimbia, hakuenda mbali, mwili ukashindwa kuhimili kunyanyua mguu kutafuta hatua ya kusonga mbele, akaanguka na kutoa sauti kali ya maumivu, halafu kimya kikachukua nafasi yake.

Risasi ilikuwa imepenya mgongoni na kujikita kwenye moyo wake na kumfanya apoteze uhai wake. Dakika mbili mbele, uliokuwa mwili wa Elinisa, ulikuwa ndani ya gunia kwenye buti ya gari aina ya Toyota Mark 2.

Kwenye usukani alikaa kijana miaka 29, Sura yenye makovu ikimtambulisha kama mtu hatari kwenye shughuli za namna hii. Jina lake alijulikana kama Chirundumusi. Jina lilitokana na utani wakati akisoma sekondari. Yeye alikuwa anatokea huko Sumbawanga, na kwa kusudi la kujiwekea ulinzi dhidi ya waonezi, wezi na wengineo, akajiita jina hilo. Hali hiyo, ikamjengea ngome imara dhidi ya watu sampuli hiyo, hasa kwa kuzingatia uonezi uliofanyika sana zamani hizo mashuleni. Hivyo ndivyo alivyojiita katika kujitengenezea usalama wa mali zake, huku akiwaaminisha kuwa, kwao ulikuwa ukoo wa kichifu wenye nguvu za kutosha za kichawi. Aliogopwa kama tetemeko la ardhi, jina hilo la utani likimaanisha tetemeko. Akitishia kushusha tetemeko la ardhi kwa mtu yeyote yule ambaye angemletea za kuleta.

Kijana ambaye alikuwa miongoni mwa vijana waliofuzu kozi maalumu za ukomando kwa lengo la kutumikia taifa, naam, alikuwa ni afisa wa kutumainiwa na taifa ambaye alithubutu kuliasi Jeshi ili kumtumikia The Don. Sasa alikuwa ni mali ya The Don akitumikishwa kinyume kabisa na lengo la mafunzo yake. Tena akiaibisha mafunzo yake kwa kupambana na watu ambao hawakuwa na mafunzo yoyote ya kujitetea. Pesa ilimpa amri kuliko taaluma yake. Alikuwa radhi kutumikia pesa, pesa aliyopewa maradufu na The Don.

Alikanyaga mafuta, gari likaitikia barabara, lami ikaugulia maumivu ya tairi zilizoikanyaga kama vile zinataka kuchomoka. Mwendo wa dakika ishirini hivi, tayari Chirundumusi alikuwa amechepuka barabara kuu ya Kilwa, na kuilamba ile inayoelekea Mbande kutokea pale Mbagala rangi tatu. Mwendo wa dakika kadhaa, tayari alikuwa anaacha makazi ya watu waliokuwa wameanza kujenga eneo hili lililoonekana kuwa nje kidogo ya jiji hili la raha na karaha. Jua la saa kumi na moja likiwa na nguvu bado ya kutoa jasho miili ya wanajiji, hasa wale watembeao kwa miguu.

Hakusimama hapo, lengo lake lilikuwa ni kutoka nje kidogo kulikokuwa bado mashambani. Kule alitakiwa kufikisha maiti yale ya Elinisa kwenye shamba la mheshimiwa Maisha Nchagwa.

Alipofika Chamazi, Chirundumusi akachukua simu yake ndogo, akampigia mzee Mabruk,
“Mzee, kazi yako iko tayari” Chirundumusi aliongea kwenye simu.

“Ok, sasa hakikisha hamjaacha unyayo wowote hapo, tenganisha kichwa na kiwiliwili, halafu mtaelekea Mbande, huko mtamkuta Chale mtamwachia maiti hayo, kazi yenu itakuwa imekwisha,” The Don alitoa maagizo kwa sauti ya kawaida kana kwamba walikuwa wanaongelea habari za kuchinja kuku, kumbe alimaanisha binadamu.

*†*
Orodha ya wafu watarajiwa waliomsumbua mzee Mabruki ilizidi kupungua na siku ya kumuondoa Maisha Nchagwa ilikuwa inakaribia, kumwondoa au kumchafulia sifa na hadhi katika jamii na kumpoteza kabisa kutoka kwenye ushawishi wake kwa jamii. Mipango ilisukwa vema. Baada ya kifo cha Elinisa, ambapo maiti ya kiwiliwili cha Elinisa ilizikwa shambani kwa Maisha, taarifa za mwili wa marehemu kukutwa shambani kwa mtetezi wa haki za binadamu, zingepata kiki ya kutosha mitandaoni na kwenye vyombo mbalimbali vya habari. Kama hiyo haitoshi, ingevujishwa video ya kijana huyo machachari Maisha Nchagwa, akionekana eneo la shambani hapo.

Itaendelea
FB_IMG_1591786598873.jpg
 
13
Mheshimiwa the Don
David Ngocho Samson

Kwa kawaida, alikuwa na siku ndefu kuliko wafanyakazi wengine, huenda kwa sababu hata alipotoka ofisini alijikuta akifanya kazi nyingine mbalimbali na hakupata muda wa kukaa peke yake. Mara nyingine ungemkuta katika makongamano mbalimbali akielimisha juu ya haki za binadamu, au akitoa ushauri juu ya jambo fulani lililohusiana na haki mbalimbali.

Alikuwa kipenzi cha wengi, wanasheria, waandishi wa habari, wanaharakati mbalimbali, wanafunzi wa vyuo vikuu kadha wa kadha, wanafunzi wa sekondari na mashirika mbalimbali yaliyomtumia kama mtu wa mfano kwao. Huyo aliitwa Maisha Nchagwa, msomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadaye Edinburg huko Uingereza, mwanasheria na mkurugenzi mtendaji wa shirika la kisheria na haki za binadamu lililojulikana kwa kifupi HRO (Human Rights Observers).

Mbali na HRO, alijishughulisha na miradi mbalimbali ya kijasiriamali, akiwa na shamba kubwa kabisa Morogoro, shamba lingine likiwa Mbande nje kidogo ya Jiji la Dar na ranchi kubwa tu ya mifugo huko mkoani Katavi. Kwa historia yake, mifugo na kilimo alivipa umuhimu wa juu kwani bila hivyo asingekuwa Maisha huyu aliyekuwa akijulikana ndani na nje ya Tanzania. Umuhimu huo ukizingatia ukweli kwamba, kupitia kilimo na mifugo, familia yake ilimudu kumsomesha.

Alisoma katika mazingira yaliyowashinda wengi hata wakaishia darasa la saba tu. Akiwa na umri wa miaka tisa, alibahatika kuchukuliwa na mjomba wake aliyekuwa mwanajeshi, akaenda kuishi naye huko jijini Mwanza. Huyo alimwezesha kupata elimu sitahili tofauti na waliyopata wenzake kule kijijini kwao ambako kulikuwa na mwalimu mmoja tu wa hesabu.
Mwalimu huyo walimtegemea afundishe madarasa yote saba. Mwalimu wa historia alifundisha madarasa yote saba huku akitakiwa pia kufundisha masomo mengine kama Kiingereza, Maarifa ya Jamii na Uraia. Kwa jumla walikuwa na walimu wanne tu.
Mjini Mwanza, alikuta kila somo lina mwalimu wake kwa kila darasa. Hali hiyo ilimpa mwanzo mzuri wa kujiendeleza kielimu huku akifurahia masomo yake kila kulipokucha.
Alijiona mwenye bahati kupata elimu na kazi aliyokuwa nayo ukizingatia wenzake wenye uwezo darasani kule kijijini kwao, walikwamishwa na mazingira kuoiga hatua kubwa kielimu.

Aliishi na mama yake nyumbani kwake Masaki, baba yake alikwishatangulia mbele za haki na ndugu zake tayari walikuwa na maisha yao. Kaka yake mkubwa alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa wa ng’ombe akiwa na mabucha ya kuuza nyama kanda ya ziwa na kila kona jijini Dar es Salaam. Yeye alikuwa wa pili kuzaliwa. Wadogo zake wa kike wawili, mmoja alikuwa kaolewa na yule mdogo zaidi akisoma huko Marekani kwa ufadhili wa Chuo kikuu cha John Hopkins baada ya kufanya vema kwenye mtihani wake wa kidato cha sita. Huko Marekani, akisomea shahada ya kwanza ya udaktari.

Katika vitu vilivyomfurahisha mama yake, ni vile ambavyo kijana wake alivyokuwa ameshikilia kilimo, hilo lilimpa faraja na maneno ya baraka yakamtiririka kuhusu mwanae. Ni kijana gani ambaye alipata elimu kama ya Maisha aliyethubutu kushika mpini wa jembe! Kijana wa miaka 32 akiwa na nyumba za kisasa tatu, maduka kadhaa Kariakoo na daladala tano, bado ashike mpini wa jembe kwa shida gani haswa? Huyu mwanaye, hakika alimpa faraja, yeye mwenyewe akisema;
“Jembe limenipa maisha, hii ni kuonyesha fadhila zangu za dhati kwa 'mheshimiwa kilimo'”

Alikuwa na mchumba, jina lake Neema, mrembo, mwenye tabia safi na elimu ya kutosha. Maisha na Neema wakapendana pendo la ukweli, lisilo na hila, wakati huu Neema akiwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe. Maisha pamoja na Neema wakajaliwa maisha yaliyosheheni neema. Mapenzi yao yakakubalika kwa wazazi wa pande zote mbili kama zilivyo desturi za Kiafrika. Wakawa wanaendelea na mipango ya kufunga ndoa na kuishi pamoja kama mke na mume, Huku jina lake likitamkwa midomoni mwa raia na umaarufu wake kuongezeka maradufu kutokana na harakati zake HRO.

*†*

Jioni ya saa moja, Maisha alikuwa anaondoka shambani kwake Mbande. Alirejea alipopaki gari lake akiwa ameridhika na kazi iliyokuwa imefanywa na vijana wake wa kazi ambao walikuwa wamerejea makwao. Aliinama na kufungua turubai lililokuwa limefunika uwazi wa carrier ya gari yake aina ya Toyota Pick up Double Cabin, ili kuingiza baadhi ya matunda kama nanasi na maembe aliyokuwa amevuna shambani humo. Hakika yake, hakuamini kile alichokishuhudia kwenye gari lake!, moyo ulimpasuka paa! Mapigo ya moyo yakaenda kasi na jasho jembamba likaaanza kumtiririka usoni.

Ndani ya gari lake mlikuwa na kichwa cha binadamu, kijana wa kiume! Mshituko alioupata, hakika ulimtia wazimu. Akili yake ikashindwa kutafakari kwa kina. Hamaniko lililompata, halikumwachia nafasi ya kukumbuka kwamba yeye ni msomi wa sheria, tena mbobezi katika masuala ya haki za binadamu. Ni kama alichanganyikiwa ghafla asijue kimemkuta nini. Mara, alivua koti lake, hamadi bila kufikiria anafanya nini, akalitumia koti hilo kubeba kichwa hicho na kwa hali ya kuhamanika asijue la kufanya, alikwenda kwenye kichaka na kutupa koti lake pamoja na kile kichwa. Aliporejea kwenye gari lake, alikuwa na wazo moja tu, kutoweka eneo hilo haraka sana. Aliingia kwenye gari, akalitekenya likacheka na bila kupoteza muda, akalitia moto na kutoka mbio kurejea nyumbani.

Huko nyuma, mzee wa makamo, mwenyeji wa maeneo yale alikuwa akipita kuelekea nyumbani kwake akitokea katika shughuli zake za kila siku. Katika hali ya mshangao, mzee huyu aliyejulikana kwa jina la Hashimu, alimwona Maisha katika harakati zile za kutupa koti lake. Kichwani kwake alipata wasiwasi, nini kimempata Maisha, kijana ambaye alikuwa maarufu sana nchini. Alipata kumfahamu vema kijana huyo pindi alipotembelea Masaki. Bintiye alifanya kazi ya kusaidia shughuli za nyumbani kwa tajiri mmoja muuzaji wa vipuri vya magari, kazi iliyojulikana zaidi kama 'uhausigeli'. Ni hapo alipomshuhudia kijana huyo akizungumza kwenye runinga, akielezea kwa kina masuala ya haki za binadamu na kutuhumu serikali kuyakalia kimya mauaji holela kwa walemavu wa ngozi na hata watu wenye vipara ambayo alidai yalikuwa yanaongezeka kila uchao. Katika kuonesha alijua anazungumzia nini, kijana huyo alidai, tafiti zao zikionesha kuwa kuna vigogo wakubwa serikalini waliohusika na kashfa hiyo ya kuendekeza mauaji ya watu kwa sababu za kukidhi malengo yao na nafasi zao kwa ushirikina.

Mzee Hashimu alielekea pale lilipotupwa koti, koti la gharama na la kisasa, bahati ilioje! Alitabasamu kwa furaha akilifuata like koti. 'Dah, matajiri ama kwa hakika wanafuja mali, koti jipya kalichoka, kaamua kuliacha shambani' Hashimu alijisemea huku akiendelea kulipekua kwa pupa lile koti. Pekua yake ikamtunuku zawadi. Katika moja ya mifuko ya koti hilo, alikuta wallet ya kijana yule ikiwa imetuna vema kwa salio la noti kadhaa za elfu kumi pamoja na kitambulisho chake.
Alilinyanyua koti lile na kulikung'uta vema tayari kulibeba aondoke nalo. Macho yake yakaona kitu, akashituka. Mbele kidogo alishuhudia kitu cha ajabu, alimanusura adondoke kwa mshituko wa moyo. Akajishikiza kwenye tawi la mpera jirani yake, akihemea juu juu kama mfukuza upepo anayemalizia mbio zake. Kichwa cha binadamu jinsia ya kiume. Kimeanza kuharibika lakini kilionekana kuwa huyo mtu ameuawa muda si mrefu.

Dunia imeharibika na halikuwa jambo geni sana kuwahi kutokea, lakini ilimshitua sana mzee Hashimu kufikiri kwamba mtu aliyepata kumsikia akikemea mauaji ya albino kuwa yeye pia ni muuaji. Ushahidi wote ulimwonyesha wazi kwamba Maisha alifanya yale mauaji. Aliondoka kuelekea nyumbani kwa mwendo wa haraka haraka kuhofia kukutwa eneo la tukio hilo kwa sababu hawakawii waswahili kumbambikizia mtu kesi, kisa amekutwa kwenye tukio.

Itaendelea

Je, umepata nakala yako ya kitabu 'MATEKA WA HUBA' ? Usingoje Sana. Vianelekea kuisha sokoni. Changamkia nakala kwa Bei ya taifa, TSH 10,000/= TU. Ni boonge moja la story, Sio ya kusimuliwa, utamu wake uisome wewe mwenyewe!
Karibuni kwa maulizo. 0629077792 WhatsApp
David
FB_IMG_1591786598873.jpg
FB_IMG_1592108536669.jpg
 
14
Mheshimiwa the Don
David Ngocho Samson

Mzee Hashimu aliyeshuhudia harakati za Maisha mara baada ya kuhamaki kukuta kichwa cha binadamu kwenye gari lake, alifika kwake hatimaye, moyo ukimwenda mbio asiamini ukatili wa binadamu kwa binadamu mwenzake.

“Watatumaliza, lakini ndo hao hao, nikisema nikaripoti itasaidia nini ilhali askari wetu wamejaa njaa na shida na mwenye pesa ndo mtuhumiwa na kuna hatari nitakufa. Cha msingi nina vitambulisho vyake, nitamfuata anikatie kidogo nifiche siri. Binadamu si watu tena.” Mzee Hashim alitafakari.

Akiwa anatafakari nini cha kufanya, mlango wake uligongwa, akalipuka hofu moyoni, kidogo adondoke chini kwa mshituko.

“Karibu, pita ndani” alijitutumua mzee Hashim kwa kihoro.

“Asante, naona mzee uko peke yako” mgeni alipiga hatua na kuingia ndani huku akiuliza swali ambalo Mzee Hashim alilipuuza.

“Nikusaidie nini kijana?” Hashim akauliza huku mshangao mkubwa ukisomeka usoni pake dhidi ya mgeni wake aliyejitokeza bila taarifa huku akiulizia vitu ambavyo hakutegemea kuulizwa.

“Mzee una mpango gani na vile vitu” mgeni akahoji akiweka tabasamu la bandia usoni mwake. Swali hilo likazidi kumchanganya vibaya mzee wa watu!

“Vitu? vitu gani kijana?” Hashim akajibaraguza kwa hamaki. Hakutaka kuamini kilichokuwa kinaendelea. Siri aliyokuwa aitunze mwenyewe na aitumie kubadili mboga, kuna mvamizi huyu aliyeonesha kila dalili ya kutaka kuuharibu mpango wake.

‘Haitakuwa rahisi’ alijiapiza kimoyomoyo.

“Vitu ulivyochukua pale shambani kwenye koti,” kijana yule aliyeonekana mkakamavu mwenye macho ya paka, Hashim alimkadiria kuwa na umri kati ya miaka ishirini na nane hadi thelathini na mbili hivi, alidhihirisha kuwa si mtu wa kawaida. Kwa vyovyote vile, ama alikuwa na sura mbaya tu au alikuwa mtu katili sana kwa jinsi mwili wake mwembamba, mrefu, uliokakamaa, ulivyoonesha makovu na majeraha yaliyopona.

Alikuwa na macho yaliyoonesha kuua mtu lisingekuwa jambo geni kwake. Yalikuwa macho ya mdogo wake ziraeli yule malaika anayevuna uhai wa waenda zao! Macho madogo yasiyoweza kupepesa, muda wote, yakitazama kama vile amevuta makini kutungisha uzi kwenye sindano. Kijana alikusudia kupewa majibu, majibu stahiki. Mzee Hashim hakuamini masikio yake.
‘Nafikiri vitu ambavyo havipo!?,’ aliwaza Hashimu kisha akajenga taswira ya hasira na kutamka!

“Sijui kama nimekuelewa kijana na nahisi huo si utani kwa sababu kwanza, sikujui na pili sijui unaongelea vitu gani!” Alitamka huku kihoro cha woga kikimtetemesha moyoni. Mapigo yake ya moyo yalikuwa yanadunda mara mbili zaidi ya kawaida.

“Mzee, nimekushuhudia ukipekua lile koti na najua umechukua vitu kwenye lile koti. Nafahamu pia kwamba kuna kichwa cha binadamu pale, nachotaka ni hivyo vitu na wewe mwenyewe ili tulifikishe suala hili kwenye vyombo vya sheria, matajiri wamezidi kutuonea na kutuua kwa tamaa zao za mali.” Kijana yule alitamka huku akijaribu kumwingia kiakili mzee yule. Hata hivyo, kijana yule hakuelewa kwa nini alizidi kumkawisha Mzee huyu kulamba mchanga, huku muda ukizidi kuelekea magharibi. Bila shaka umri. Umri wa Mzee Hashim, haiba na hata mwonekano wake haukuwa tofauti na wa baba yake mzazi, Mzee Mwanambeti, ambaye aliamini mwanae alikuwa afisa wa kikosi maalum cha kulinda usalama wa taifa. Hivyo ndivyo alivyojisifia kwa wazee wenzake huko Sumbawanga. Hilo ndilo lilimfanya Chale, mtu katili asite kumpoteza mzee huyu. Alimkumbusha baba yake kwa kila kitu.

“Wewe kijana ni nani?” Hashim akahoji kwa hamaki.

“Mimi mzee, ni mpelelezi kutoka usalama wa taifa na hapa nilipo ninafuatilia nyendo za huyu tajiri kwa sababu amekuwa akivaa kofia la haki za binadamu kumbe yeye ndo mvunjaji mkubwa wa haki hizo.” Kaka jambazi akadanganya.

“Sawa kijana nimekuelewa, na naungana nawe lakini ni muhimu polisi wafahamu habari hii ili waendelee na upelelezi,” Mzee Hashim akapendekeza.

“Sawa kabisa mzee, hicho hasa ndicho nachofanya hapa, hivyo vithibitisho ndio vitawezesha kukamilisha upelelezi na nadhani ni muda mwafaka wa kulifanya hilo.” Chale akazidi kujifanya afisa usalama!

*†*

Chale Mwanambeti alikuwa miongoni mwa majambazi vibaraka wa The Don, na kwa muda wote ule alikuwa anachukua video ya tukio la Maisha na kichwa cha binadamu kwa lengo la kuiweka kwenye mtandao ili kumchafulia jina, na hapo ndo alipoonekana mzee Hashimu na kuvuruga kabisa mpango wao! Hivyo ikambidi kubadili gia angani na kujiita mpelelezi!
Walipokubaliana na mzee Hashimu, safari ikaanza kuelekea kituo cha polisi. Kijigiza cha magharibi kikiimeza nchi kidogo kidogo na hatimaye kuimeza kabisa!

Walizidi kusonga mbele huku mzee huyu akimweleza Chale kwamba binti yake naye yupo Masaki, jijini Dar es salaam, anafanya kazi ya uhausigeli, muda nao ulizidi kusonga mbele huku Chale akipata hofu kwani kutokana na mauaji mengi yaliyokuwa yanaendelea, wananchi waliamua kufanya ulinzi wa sungusungu.

“Mzee umekumbuka kuchukua vile vithibitisho bila shaka?” Chale akahoji kwa msisitizo. Macho yake hasa ndio yalionesha huo msisitizo.

“Oh. Uzee kijana wangu, nimesahau juu ya meza” Hashimu akamjibu Chale. Hakuwa ameamini kabisa hadithi ya kutunga ya kijana yule ambaye mwonekano wake ulithibisha ni mtu hatari kabisa.
Kusikia hivyo Chale alitamani amtafune huyu mzee.

“Kwa vile hatujaenda mbali sana, hebu turudi haraka sana” Chale aliamuru akionekana kunung'unika moyoni.

Walianza safari ya kurejea nyumbani kwa mzee Hashimu, giza sasa lilifunika nchi kabisa na sasa walitumia mwanga wa tochi aliokuwa nayo Chale. Mbele walikutana na sungu sungu, ilikuwa yapata saa mbili usiku. Tabasamu mororo likatanda usoni mwa Hashimu.

“Wapi mwaenda bwana Hashimu na huyo hapo ni nani?” aliuliza mzee Mwinjuma kiongozi wa sungusungu wale.

“Samahani ndugu zanguni, huyu kijana ni mgeni maeneo haya kutoka usalama wa taifa, kuna matukio anapeleleza.” Hashim akajieleza kwa kifupi. Alichokuwa anataka kilitimia. Alikusudia kupoteza muda ili hatimaye wakutane na sungusungu. Huu ungekuwa uhakika wa usalama wake kuliko kuambatana na mtu ambaye alishamtilia shaka, kwenye giza totoro. Hofu ya umauti iliyokuwa imemvaa sasa ilitoweshwa na furaha ikamjaa moyoni kwa kule kukutana na awa raia wenzake..

“Upelelezi gani, hebu tuonyeshe kitambulisho” Mwinjuma akaamuru akimpiga jicho la amri kijana yule, Chale. Lilikuwa swali gumu kwa Chale.

“Sijaja na kitambulisho kwa sababu za kiintelijensia, kwa hiyo tuacheni tuendelee na kazi ya kitaifa” Chale hofu ilimvaa na katika kupoteza lengo akaongea kwa kitisho ili kuwapunguza kasi sungusungu wale walioonekana tayari kumkabili kwa silaha zao za jadi. Angeweza kutumia bastola, lakini risasi tatu zingefaa nini kwa kundi hili lenye silaha za jadi ambalo lilikuwa na munkari wa kushambulia wakati wowote kama ingetoka amri! Alijikuta ananywea kama kuku aliyenyeshewa!

“Na kijana unatarajia kwamba tutaamini maneno yako matupu?” Mwinjuma akatamka halafu akamgeukia Mzee mwenzake

“Mzee Hashimu wewe ni shahidi wa matukio yanayotokea hapa, unafanya nini mzee kukaribisha wageni wasio na vithibitisho vyovyote? Kwamba hujui Taratibu za mtaa?” kamanda wa sungusungu alihoji na kumwagiza sungusungu mmoja miongoni mwao.

“Mtie pingu huyo, mengine yatafahamika huko mbele.”

Chale alitiwa pingu mikononi na usiku huo huo akaongozwa kwenda kituo cha polisi Mbande.

*†*

Asubuhi ya saa mbili, Anastazia alikuwa anabisha hodi kwenye geti la nyumba alimoishi Elinisa, aligonga kwa muda na kusikilizia lakini hakukuwa na majibu. Mara alijitokeza mwanamke aliyekuwa na Elinisa kule Kilimanjaro Hotel, yaani Asha.

Alikuwa amevalia fulana ya kampuni fulani ya simu iliyofanya maziwa yake ya mviringo yaonekane yamesimama wima na kutia hamasa na mvuto. Nywele zake alizilaza kuelekea nyuma na alitembea kwa mwendo wa maringo mithili ya twiga mbugani. Umbo lake zuri na urefu wa wastani vilimpa upekee wa peke yake miongoni mwa wanawake warembo. Alikuwa ameshuka kwenye teksi na kutembea kuelekea kwenye geti la Elinisa.
Anastazia alisimama getini akisubiri mwanamke yule, Asha, afike. Bila shaka angekuwa anafahamu alipo Elinisa.

“Za saa hizi anti?” Asha alimsalimu Ana huku akielekea getini akimpita na kumwacha amesimama pale bila kumtilia maanani.

“Nzuri, inavyoonekana huyu bwana hayupo” alijibu Ana kwa kujibaraguza. Alikuwa na shida, alipaswa kutulia. Moyoni mwa Asha mlikuwa na swali la nini Ana alikuwa anafanya pale. Alipuuza maneno ya Ana na kupiga simu ya Elinisa iliyoita bila kupokelewa. Kuona hivyo alimgeukia Ana na kumuuliza

“Unafanya nini hapa?” lilikuwa swali lenye shari zaidi kuliko heri.

Ana alijua tayari Asha alikuwa anaonyesha ushindani fulani na wivu ulimtafuna vilivyo. Hata hivyo hakutaka shari na mwanamke huyo, na hivyo taratibu na kwa sauti ya upole alijibu,
“Nimekuja kumuona Elinisa lakini naona ni kama hayupo.”

“Yeye ni nani yako?” hasira za Asha sasa zilikuwa bayana. Aliwaza huyu ni nani anayemuulizia Ely wake!

“Ni shemeji yangu, marehemu kaka yake alikuwa mume wangu, sijui mwenzangu ni nani?” Ana akauliza pia akijaribu kumwingiza Asha kwenye kumi na nane zake kisaikolojia.

“Mi ni mchumba wa Elinisa, haya kwaheri. Nitamuona hata baadaye” Asha aliongea kimashauzi akibetua midomo yake kwa bezo huku akiwa anaondoka.

“Mimi pia naondoka na kama ukipenda naweza kukusogeza unapoenda” Ana akikusudia kujua mengi, hivyo akapuuza dharau ya mwenzake na kupendekeza kumpa lifti.

Ana alipendekeza wazo lililopata majibu aliyotaka.

“Mie naenda Posta” Asha alijibu, safari hii akijiheshimu!

“Oh! Mimi pia napita huko,” alijieleza Ana, ukweli ni kwamba hakuwa na mpango wa kwenda huko lakini sasa aliona hiyo ingekuwa nafasi nyingine ya kupata undani wa Elinisa na Elineema.

Waliingia kwenye gari dogo aina ya Toyota spacio. Ana aliliondoa gari kwa mwendo wa wastani wakawa wako njiani kuelekea Posta kupitia Barabara ya Ali Hassan Mwinyi wakitokea Oysterbay. Njiani waliongea mengi na lililomgusa zaidi ni habari ya Geof.

“Oh maskini, kwa hiyo sasa yuko wapi?” Ana alihoji.

“Labda nimpigie simu” Asha alitamka huku akibonyeza namba kadha wa kadha kwenye simu yake.

“Halo Geof, mambo?” Asha alizungumza simu ikiwa sambamba na sikio lake.

“Si mazuri, nipo msibani, amefariki mama” Geof alitamka upande wa pili kwa sauti iliyobeba majonzi yasiyo haba!

“Oh pole bwana, mbona tusijulishane au tumefika hatua hiyo?” Asha akasaili kwa sauti tulivu, sauti ya upole.

“Wala, sema mambo yamekuwa ghafula sana, hivi nipo Mbeya baada ya kutoka Moshi alikopatwa na umauti” Geof akatamka kwa sauti iliyojaa majonzi tele.

“Oh pole sana Geof; nimesikitishwa sana na taarifa hiyo;”Asha akampa pole.

“Asante, sote tutakwenda wacha atutangulie” Geof akajifariji. Alimgeukia Ana na kusema;
“Amefiwa na mama yake na yupo Mbeya kwenye msiba.”

“Inasikitisha sana, lakini huoni kama unaweza kuwafanya wauane?” Ana akachombeza kuendeleza mazungumzo, sasa hawakuwa maadui tena, bali marafiki.

“Nifanyeje ndugu yangu, mimi pia niliponea chupuchupu kufa kwa sababu ya mwanaume. Wao pia hawana huruma.” Asha akatamka huku akisimulia kile kisa chake na Salimu.

Itaendelea
David

Usikose nakala yako ya MATEKA WA HUBA.
FB_IMG_1590917892882.jpg
FB_IMG_1597699307149.jpg
 
15
Mheshimiwa the Don
David NGOCHO Samson

AFANDE Masiko alikuwa kaoa mke wa pili hivi karibuni baada ya kupita miaka miwili tangu afariki mke wake wa kwanza mama Chacha. Mkewe huyu alimuoa baada ya kushauriwa na wanawe wakubwa kwamba ni jambo zuri la kufanya ukizingatia majukumu aliyokuwa nayo hali akiishi peke yake katika nyumba kubwa tu aliojijengea miaka mingi iliyopita.

Mwanzoni hakuona tatizo, lakini lilipokuja suala la mkewe kuanza kulalamika juu ya ufanisi wa Masiko katika suala la unyumba, Masiko alijikuta akipata msongo wa mawazo na hasira nyingi. Asingethubutu kuachana na mkewe huyo kwa kuhofia kwamba kufanya hivyo kungesababisha walimwengu kuhoji kulikoni na kwamba wangebaini ugonjwa wake aliokuwa ameupata hasa baada ya kugunduliwa kuwa na maradhi ya kisukari.
Hata hivyo umri nao ulikuwa umemtupa mkono na alikuwa amebakiza miaka minne tu kustaafu.

Leo akiwa nyumbani, saa sita za usiku alipigiwa simu na Koplo Magumashi akimtaarifu kuwa, kulikuwa na mtuhumiwa wa mauaji na walitaka kupata mwongozo wake namna gani wamhifadhi kwa kuhofia usalama, kwa sababu kituo hicho kidogo cha polisi hakikuwa na mahabusu ya kuweka watu kama huyo.

Magumashi alidai jambazi huyo alikuwa na silaha nzito aina ya Colt 45 yenye kiwambo cha kuzuia sauti. Hofu kubwa aliyokuwa nayo Magumashi ni kwamba huenda jambazi huyo hakuwa peke yake na kwamba kwa kufahamu kwamba mwenzao yuko pale kungesababisha kuvamiwa kwa ajili ya kumuokoa mwenzao.

Afande Masiko hakuwa akipenda matukio haya ya usiku, ingawa aliipenda kazi yake hiyo, lakini kuamshwa usiku daima ilikuwa kero kwake. Kwa miaka mingi aliifanya kazi hii na hata sasa alipokuwa anaelekea kustaafu bado aliandamwa na matukio haya!

Aliamka, na... ingawa alikereka, alipata ahueni kwani alipata sababu ya kumuacha mkewe huyu asiyeridhika na huduma yake, mkewe alikuwa na miaka 33 tu ukilinganisha na yeye aliyekuwa amefikia miaka 61 sasa halali, tofauti na ile 56 ya kwenye vyeti.

Alichukua bastola yake na kuiweka usawa wa kiuno upande wa mkono wa kulia halafu akatia moto Land Rover lake kuukuu na kuelekea kituoni umbali wa kilometa 20 hivi.
Yapata saa sita na nusu, aliwasili kituoni na kumkuta huyo jambazi akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi. Aliagiza jambazi huyo apelekwe ofisini kwake kwa mahojiano.
Wakati akiwa ndani akimhoji jambazi yule, ilisikika milio ya risasi nje tu ya kituo hicho cha polisi, hofu ilitanda. Kwa mara ya kwanza maishani mwake, Masiko aliachia ushuzi kwa hofu na kuhisi harufu ya umauti. Kifo, kifo ambacho aliona kitu cha kawaida sasa kilimtia hofu mno na mara moja aligundua kwamba hakutaka kufa aslani.

Akili iliyomwijia haraka ilikuwa ni kusimama atafute sehemu salama ya kujificha, ili asikutwe kirahisi na majambazi hao ambao aliamini walikuwa na nia ya kuwaua ili kumnusuru mwenzao.

Alipiga hatua moja, akaanguka chini kama mzigo, puu! Aligeuka kutazama kulikoni na ndipo alipogundua kosa alilokuwa amefanya, katika kuhamanika na milio ya risasi nje ya kuta za chumba kile, alisahau kwamba alikuwa anachukua maelezo ya jambazi sugu mle ndani.

Jambazi hili sasa lilikuwa limedaka mguu wa Afande Masiko na lilitishia kuuvunja asipofunguliwa pingu. Lo! Salale! Mkosi gani huu?! Alijihoji afande. Maumivu ya kwenye goti yalianza kusambaa mwilini kwani jambazi lile lilitumia pingu zile ili kumtia maumivu afande Masiko. Siwezi kufa kizembe hivi! Alizidi kuwaza Masiko.

Alijiviringisha kwa haraka kitu ambacho hakikutarajiwa na jambazi na kujikuta amemimina risasi tatu mfululizo katika kifua kipana cha jambazi lile na kushuhudia damu zikivuja mithili ya chemichemi.

Huko nje kulikuwa hakufai ikiwa inasikika milio ya risasi kwa majibizano kati ya jambazi na askari. Askari kwa kutumia mbinu zao, walifanikiwa kuwazingira watu waliosemekana kuwa majambazi na kumuua mmoja wao huku wengine wakikimbiza mbawa zao kama kunguru.

Waliwaweka chini ya ulinzi watu wale waliokuwa eneo zingirwa na hapo ndipo walipobaini kuwa mmoja kati ya watu hao, alikuwa amepigwa pingu hali wengine wakiwa na silaha mbalimbali za kijadi na short gun moja. Baada ya mahojiano na watu wale iligundulika kwamba wengi walikuwa ni sungusungu na kwamba yule aliyepigwa pingu alikuwa amekamatwa akihusishwa na tukio la uuaji na kwamba wakiwa njiani ndio walipatwa na msukosuko wa kuvamiwa na majambazi wengine wakidhamiria kumuokoa mwenzao kabla ya kufikishwa pale kituoni. Jambazi hili lililokuwa limekamatwa lilijulikana Kwa jina la Chale.

Tukio la kukamatwa kwa jambazi Chale iliwapa changamoto kubwa polisi hao wakiongozwa na Masiko, kwani maelezo waliyopata yaliwatatiza. Mzee Hashimu, aliyehusishwa na jambazi hilo, alilikana na kusema hajui chochote kwani lilimfuata baada ya kumshuhudia akibeba vitu katika tukio lililomhusiha mtetezi wa haki za binadamu, Maisha Nchagwa kutupa koti lake lililobainika lilibebea kichwa cha binadamu na kwamba lilidai kuhitaji kupeleka vithibitisho vile kituo cha polisi kwa upelelezi, huku likidai lenyewe ni usalama wa taifa.

Baada ya kumsikiliza jambazi Chale, yeye alidai kuwa alitumwa na Maisha kuhakikisha kwamba hakuna mtu atakaye shuhudia wakati wa kutekeleza utoaji sadaka ili kufanikiwa utajiri, kitendo ambacho alimshuhudia Hashimu akikishuhudia.

Kwa vile lilipaswa kuwa tukio la siri, ilibidi kunyang'anya vithibitisho vile ili kumlinda bosi wake na kuvuja taarifa za mauaji aliyotekeleza.
Hilo likuwa jambo jipya ambalo liliwashitua akina Magumashi na wenzake wasiamini kabisa kuhusika kwa Maisha, lakini maelezo ya Mzee Hashimu na jambazi lile yaliwapa utata mkubwa juu ya habari zenyewe.

Kusikia vile, Masiko alipata hasira, akajikuta kamnyanyua juu Chale na kumbwaga chini mithili ya gunia huku akimshushia kibano kizito na kumpotezea Chale meno mawili ya mbele.
Dakika chache zilizopita Masiko alikuwa amejiona kwenye jeneza, kwa sababu mapigano yale bila shaka yangemtoa uhai kwa ile hofu aliyokuwa ameipata.

Masiko aliagiza Chale afungiwe kwenye chumba pale kituoni na kuwekewa ulinzi madhubuti ili afanyiwe mahojiano zaidi kesho yake.

***
MAISHA alirejea nyumbani akiwa amechoka sana, wasiwasi ulisomeka bayana machoni pake. Shati lake lilikuwa limelowa jasho. Kwa jumla hakuwa Maisha waliyemjua.
Hilo lilionekana wazi katika macho ya mamaye aliyekuwa amekula chumvi nyingi za kutosha.

“Vipi mwanangu mbona hivyo, kulikoni?” alihoji mama yake, sauti yake tamu zamani za usichana wake sasa ilififia na ilitoka kwa mwangwi hafifu.

“Vaiii” aliita kwa sauti Maisha.

Vai aliyekuwa msichana wa kazi za ndani hakuwahi kusikia bosi wake akimwita kwa sauti ile, yeye pia aligundua kwamba kulikuwa kumetokea tatizo huko alikotoka bosi wake.

“Hebu niletee kahawa mara moja.”

“Sawa boss” Vai alitoka na kufanya yale aliyoagizwa.

“Huyu mtoto mbona siku hizi haelewi, nimeagiza juisi ameleta kahawa” Maisha alingaka!

“Kuna nini Maisha maana leo haupo katika hali nzuri kabisa,” mama alizidi kudadisi.

“Yaliyonikuta sijui nitafanya nini mama, kwa kweli binadamu wana hila mbaya sana.” Alitamka Maisha akimtazama mama yake ambaye alipatwa na wasiwasi mkubwa juu ya mwanae.

“Mama nimekuta kichwa cha binadamu ndani ya gari langu nilipokuwa shambami kule Mbande na katika kuhamanika nilivua koti langu na kulitumia kubeba kichwa hicho na kukitupa porini, hivi ndo nagundua kwenye koti mlikuwa na vitambulisho vyangu na fedha kidogo.

“Yeso rugia!!” Mama alitamka kwa kilugha na kubaki ameduwaa.

Itaendelea
David
FB_IMG_1591786598873.jpg
 
Back
Top Bottom