Mogambi
JF-Expert Member
- May 25, 2012
- 213
- 359
- Thread starter
- #21
16
Mheshimiwa the Don
David Ngocho Samson
0629077792 WhatsApp
Maisha alimpigia simu mchumba wake Neema, ambaye alikuwa mhadhiri wa chuo kikuu cha Mzumbe na kumueleza masahibu yaliyokuwa yamempata jana ya siku hiyo. Alidai kwa hali ilivyokuwa, ni dhahiri alikuwa anakabiliwa na kesi ya mauaji, ambayo ushahidi ulimwonyesha yeye kuhusika kwa sababu aliacha kitambulisho kwenye mifuko ya koti alilokuwa ametelekeza kule shambani.
Ilikuwa habari nzito ambayo Neema aliazimia kufika Dar ili kupata uhalisia wa hayo aliyokuwa ameelezwa, ambayo yalionekana sasa kumchanganya akili. Ilikuwa imebaki miezi kadhaa kwa wawili hao kuumba mwili mmoja na kuanzisha familia, habari ile ilimshitua vibaya sana Neema.
Alijikuta anafuta machozi yaliyokuwa yameanza kumtiririka usoni, kisha akaweka chini simu na kutoka bustanini ili kuvuta pumzi na kuchukua hatua sahihi.
Kwamba mmewe mtarajiwa, mtetezi wa haki za binadamu maarufu sana sasa ibainike ni muuaji. Nini angekisema sasa kimpe unafuu na kipate kibali machoni mwa walimwengu? Na je? suala hilo lilikuwa linamweka upande gani yeye binafsi? Hakuwa tayari kuona wanafikia hapo. Kwa vyovyote vile alipaswa kuwa faraja kwa mchumba wake Maisha. Huu ulikuwa muda mwafaka wa kuonesha mshikamano kwa mwanaume aliyemtambulisha kwenye ulimwengu wa wakubwa. Ambaye hakujali umaskini wake na kumpa sapoti wakati akisoma chuo kikuu. Ndio, huyu ni mwanaume ambaye hakujali ule uvumi kwamba mchumba hasomeshwi na kufanya kile kilichompendeza kufanya.
Hakumsomesha ili baadae amuoe. Hata suala la mapenzi kipindi hicho halikuwamo akilini mwake. Ni yeye Neema mwenyewe aliyekuja kuliibua suala hilo. Na, akatumia uwezo wake wote kuhakikisha anamtunuku Maisha zawadi ya ushindi. Hakuishia hapo, bali alidhamiria kumkabidhi maisha yake yote. Alimpenda haswaa! Hivyo basi, wala kuhisi hata kidogo kuwa labda Maisha ametekeleza suala hilo la kikatili, Ni jambo ambalo halikupita kabisa kwenye fikra zake Wala kuleta maana.
Alirejea ndani na kupaki nguo mbili tatu na kuziweka sawa. Halafu aliingia kwenye gari lake ist nyekundu na kuchoma mafuta, breki ikikanyagwa chuoni Mzumbe. Alipokwisha paki gari lake eneo husika, Neema aliteremka na kupanda ngazi katika jengo la utawala kuelekea katika ofisi yenye maandishi Deputy Vice Principal - Human Resources and Education. Alizama ndani. Akafanya mazungumzo na wahusika wa ofisini hiyo. Alipotoka, alikuwa na uhakika na safari yake. Akiwa na ruhusa ya kuondoka kazini.
Hakurejea nyumbani. Tayari alikwishajiandaa kwa safari. Alichofanya ni kupita kwenye kituo cha kujaza mafuta, akajaza Lita za kutosha za petroli, ambazo zingemudu hata safari ya Dar hadi Mwanza, akaingiza gari barabarani kulitafuta jiji la Dar es salaam.
***
Ilikuwa asubuhi sana majira ya saa moja, na alihitaji sana kuonana na Elinisa baada ya kumkosa siku ile. Anastazia aliendesha gari lake kwa mwendo wa wastani tu na hatimaye akafika getini kwa Elinisa na kubisha hodi bila mafanikio. Leo asingerudi bila kuonana na Elinisa, alikuwa na maswali mengi yakimkereketa moyoni mwake na alihisi angepata majibu yake kutoka kwa Elinisa hasa sana juu ya ndugu yake Elineema Urio.
Geti lilionyesha kila dalili kwamba toka alivyoondoka siku ile basi hakuna kiichofanyika pale, kulikuwa na kila dalili ikionyesha kwamba, Elinisa hakuwepo. Hata hivyo, Ana hakurudia getini, aliusukuma mlango wa geti kwa nguvu akitegemea kupata upinzani wa kitasa kwa ndani, lakini akajikuta kidogo adondokee ndani pamoja na mlango ule uliokuwa mwepesi kulinganisha na nguvu aliokuwa ameuwekea katika kuusukuma.
Aliingia ndani na kupitiliza hadi mlangoni mwa nyumba aliyoishi Ely na kubisha hodi. Jitihada zake hazikufua dafu, akajaribu Mara nyingine, Hola! Kuugusa mlango,ukachanua kea uwazi. Ulikuwa wazi, bila shaka tokea juzi. Runinga ilikuwa inafanya kazi, lakini kulionekana kama kwa siku mbili hivi Elinisa hakuwa amerudi.
Kichwa kikazunguka, sasa alipata hofu juu ya Elinisa kwa habari ya tishio alilokuwa amepewa na Geof, tukio lile la mazungumzo kati yake na Asha, likavamia fikra zake. Mazungumzo yao yalianza kujirudia ndani ya ubongo wake.
Kulikuwa na simu ya mkononi ya Elinisa juu ya meza pale sebuleni na aliona wallet ndogo pia kwenye meza hiyo. Ana akahisi kwamba mwanaume huyo aidha alitekwa au kukumbwa na lolote bila kujiandaa, baada ya kutoka nje kwa kusudi la kurejea ndani bila kutumia muda mwingine nje, na ndio maana hakuondoka na simu Wala wallet. Akiwa angalia bado anafakari uwezekano huo, Ana akapata wazo jipya. Vipi kama labda umauti ulimkuta mwanaume huyo humo ndani? Ndio, lisingekuwa Jambo geni. Watu hufa usingizini, Kuna magonjwa Kama shinikizo la damu huondoa uhai wa mtu Kama masihara. Na pia alishasikia kesi za watu waliokufa kwa kuanguka vibaya, hali wakiwa ni wagonjwa wa pumu, kifafa na wengine kwa kujizidishia dozi ya dawa za hospitalini na hata za kulevya.
Akili yake ikamtuma kuzuga kuita jina la mwenyeji wake endapo alikuwa bafuni akioga au kitandani amelala. Hakupata mrejesho, na badala yake akajisikia sauti yake kwa mwangwi na ukimya wa kuogofya kwenye nyumba hiyo.
Akapiga hatua moja ikifuatiwa na nyingine, mkononi akiwa na bastola yake thabiti, alikusudia kufanya upembuzi yakinifu wa nini kilikuwa kinaendelea hapo. Akaufikia mlango wa chumba cha kwanza, kilikuwa kitupu zaidi ya kitanda kilichotandikwa vizuri kabisa.
Akatoka hapo na kufuata korido hiyo na kuufikia mlango wa pili, huko pia kulikuwa hakuna cha maana. Hatua zake zikamuongoza kwenda chumba alichoamini ndio master bedroom aliyotumia Ely. Alikuwa sahihi. Hata hivyo, zaidi ya kukuta kitanda ambacho kilikuwa safi na maridadi, pamoja na mali kadha wa kadha za Ely, hakukuwa na mtu yeyote na kila dalili ilionesha hakuwa amekitumia kitanda na chumba hicho kwa siku mbili hivi.
Moja kwa moja, Ana akajikuta amerejelea yale mazungumzo yake na Asha. Hisia zake zikamweleza, Geof atakuwa ama amemteka Ely au kaamua kumpoteza kama alivyomwahidi.
Akarejea sebuleni na kuichukua ile wallet ndogo na kuamua kuifungua. Mlikuwa na fedha Kiasi pamoja na vitambulisho mbalimbali vya Elinisa. Pembeni ya iliyokuwa bwallet na simu, akaona shajara ndogo ambamo Elinisa alitunza kumbukumbu zake muhimu. Ghafula simu ile ya Elinisa ilianza kuita. Haraka Sana akainyanyua akitaka kujua nani aliyekuwa anampigia Elinisa. Huenda akawa yeye mwenyewe anataka kujua kama kuna usalama nyumbani kwake. Akaona jina Asha kwenye simu hiyo. Ana aliipokea simu, jambo lililomfurahisha Asha. Alikuwa amemtafuta mwanaume huyo na sasa hatimaye ilikuwa imepokelewa. Lakini, kusikia sauti ya kike ikiijibu simu ya mpenzi wake, moyo ulimuuma kwa wivu.
“We nani na mwenye simu hiyo yu wapi!?” alihoji Asha.
“Mimi Ana, nimekuwa simpati kwa simu yake ndo maana nimeamua kuja huku ili kujua kulikoni lakini ndo hivyo, Elinisa anaonekana kupotea katika mazingira tatanishi.” Ana akamweleza.
“Nipo njiani nakuja” Asha alitamka na kukata Simu.
Kama kawaida yake, Asha alimpigia dereva teksi simu, akamfuata, akawa yuko njiani akielekea kwa Elinisa ili kujua namna ya kutatua kitendawili kile.
Alimkuta Ana amekaa kitako anakunywa juisi ya Pera kwa raha zake.
“Leo ni tarehe nne, lakini kwa mujibu wa Elinisa, alipata ujumbe wa kutishia kuuondoa uhai wake ndani ya siku mbili kama asingeliachana na wewe. Leo ni siku ya tatu toka amepata ujumbe huo, na haonekani, unadhani ni nini kina endelea hapa?” Ana alihoji akiwa anamwangalia kwa makini Sana Asha. Ukiwa mpelelezi ni shida kweli. Kila mtu unamtilia mashaka kuwa ni mtuhumiwa.
Asha akaisikia kengele ikilia kichwani mwake. Ikawa kama anayasikia mazungumzo yake na Geof kipindi kile. Sauti ya Geof ikitamka kwa uthabiti, ‘not when I'm alive and breathing darling’
Akatengeneza ubongoni mwake sura tulivu ya Geof ilivyofyonya kwa hasira na uchungu wakati akiyatamka maneno hayo. Haikuwa siri, alimjua Geof kwa muda sasa, bila shaka ilikuwa kosa pale alipoyapuuza maneno hayo, Geof alidhamiria na haikuwa na shaka kwamba Geof amehusika na tukio hilo.
Moyo ulianza kwenda mbio, kwa mara nyingi, hakufikiri angekuwa chanzo cha tukio kama hili. Aliyajua machungu ya mapenzi, alikwisha umizwa, ilikuwa vipi asahau? Angesahau vipi ilhali tabia hii ilitokana na machungu ya mapenzi, kumwacha Geof, au basi kumpenda, alichohitaji Geof ni kupendwa lakini ni nini alipata kwake?
Alianza kuhisi hisia aliyopata pindi alipoachwa na Salimu na kitendo cha kunywa sumu, sasa, yeye mwenyewe alichukua uamuzi kama huo! Labda yeye alikuwa mwoga, alishindwa kumkabili adui na kwa kihoro akataka kujimaliza, labda Geof alikuwa tofauti, alikuwa tayari kumkabili adui, adui ambaye sasa alikuwa Elinisa. Vipi hakufikiri juu ya hili. Vipi ilivyo rahisi kwa mwanadamu kusau! Vipi ilivyo ngumu mwanadamu kujifunza!
Alinyanyua macho yake kwa upole na kuyatua usoni kwa Ana aliyekuwa akimtazama kwa muda huo akijaribu kuhisi alichofikiri mchumba wa Elinisa, Asha.
“Nadhani namfahamu aliyehusika na kupotea kwa Elinisa, nadhani Geof anahusika” alivuta pumzi kwa nguvu.
“Mungu wangu nimefanya nini? Nimefanya nini mimi?” Asha alilalamika. Usoni kwake kulionekana wingu zito la huzuni mithili ya blanketi la Sufi.
Ana alimwangalia tu,
“Sasa tutafanya nini?” Asha alihoji.
Kuwepo kwa Ana pale kulitengeneza mhimili wa kuegemea, ni kama alihisi unafuu kidogo kwa uzito wa yale aliyokuwa akiyafikiri pale alipoyasema na kupata masikio ya kuyapokea.
“Labda tuwasiliane na huyo Geof ili kupata
uhakika, ingawa hata kama ni yeye anahusika sidhani kama atakiri. Tunaweza kupata kitu kwa kusikia sauti yake. Pili, tunapaswa kuripoti kwa mamlaka husika ili uchunguzi ufanyike haraka iwezekanavyo.”
Ana alimalizia kuongea huku akiukabili mlango wa kutoka ndani ya nyumba hii, nyuma akiitwa na Asha aliyekuwa anamkimbilia.
Itaendelea