Mheshimiwa Rais Kikwete nchi inasambaratika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mheshimiwa Rais Kikwete nchi inasambaratika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Watanzania, Jul 19, 2009.

 1. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa Rais nchi inasambaratishwa na udini, chanzo kikiwa ilani ya uchaguzi wa chama chako cha CCM kilichoingiza mambo ya udini katika ilani ya uchaguzi, Mh rais. wewe hauioni hatari hii?

  Uliapa hadharani kuilinda katiba ya nchi inayokataza udini, itetee sasa. Mh. rais bora ukose kura kuliko nchi isambaratike mikononi mwako. Mh. rais wewe uliomba kuwa rais kwa ridhaa yako ili uongoze nchi, sasa ongoza nchi, suala la kusambaratika kwa nchi siyo dogo. Toa uongozi unaoendana na katiba uliyoapa kuilinda. Nchi hii ni ya watanzania wote, dini mbalimbali na makabila mbalimbali, wote tuko sawa. Rudisha umoja wa watanzania, ulioapa kuulinda, Linda katiba, na vizazi vya watanzania vitakukumbuka daima. Vinginevyo mheshimiwa rais, utakumbukwa kwa kusababisha nchi kusambaratika kwa sababu ya udini ambao umeletwa na chama chako.
   
 2. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  naunga mkono hoja, muheshimiwa raisi, Kimya chako si dawa, mambo yanazidi kwenda ndivyo sivyo! Historia itakuhukumu!

  Watu wanatumia ahadi ya ilani ya chma chako kama ndiyo katiba ya nchi! walau wakumbushe kwamba ilani ya chama siyo muongozo wa taifa, na uwe muungwana uwaombe msamaha kwamba kweli chama chako kilikurupuka kuingiza ilani hiyo! Japo mlisema mtatoa ufumbuzi, wenzenu wameisha piga hatua mia mbele zaidi, na kudai mutekeleze siyo ufumbuzi tena, kwao ufumbuzi ni kuanzishwa, fumbua macho uone mkuu, jahazi linazama!

  Ama wasaidie kuwapa darasa kidogo, kwamba hakuna anaye pinga hiyo mahakama, swala ni kwamba serikali haiwezi igaramia, wajipange wenyewe waanzishe!
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Ndugu yangu Watanzania,
  Kuna mtu wa kukemea udini hapa sasa?
  Kama washauri wenyewe wa JK ni akina Kingunge, unategemea nini ndugu yangu?
  Unaongelea juu ya JK?, utakuta hana hata habari kama kuna harufu ya udini hapa, hivi hajasafiri saa hii?
  Aache kutafuta hela ya uchaguzi 2010, akusikilize wewe?
  Whether nchi itaingia na udini ama la kwenye awamu yake ya 2, hilo hajali, kinachotakiwa apate `urahisi`. Yaani hii ni yaleyale ya `PUNDA AFE, LAKINI MZIGO WA TAJIRI UFIKE`.
   
 4. Mnyisunura

  Mnyisunura Member

  #4
  Jul 19, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 69
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Ukiwa na rais mfu kama jk unategemea nini! Kiufupi hatuna Rais ila tuna anayejiita rais! Anyway kazi tunayo! Jamaa hajui analofanya hata kidogo ye tu mradi siku zinaenda!
   
 5. M

  Mugishagwe JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 295
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa kesha pewa sifa huko anako temblea kila mara hana shida na Watanzania tena kusambaratika .Yuko kimya anapanga safari ijayo aende wapi maana bado anajitambulisha kwa Dunia
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mwenye nyumba anasema kelele za milango hazimnyimi usingizi ,hivyo tungojee kuche au usiku wa manane lazima atakurupuka tu.
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Jul 19, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  JK alishatoa mwongozo siku nyingi kwamba hilo la kadhi hakuliweka yeye kwenye ilani ila alikuwa Ngasongwa, Kingunge na Mkapa! Our President is not serious really. Huwa anatoa majibu yasiyomaliza kiu ya wanaotaka kutoa dukuduku. Mnakumbuka hotuba yake ya Agosti, 21 2008? Wabunge walitaka kuijadili ikapigwa danadana mpaka leo. Sasa kama anafanya vituko hivi kabla ya 2010, je, akichaguliwa ungwe ya mwisho ya lala salama mwaka 2010 - 2015 atajali kitu kweli?
   
 8. B

  Bull JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2009
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuweko mahakam ya Kadhi sio kuwa ndo nchi inasambaratika, Hizi mahakam ziko sehemu nyingi zina operate na hizo nchi ziko safi. CCM ilitoa ilani kwenye uchaguzi baada ya kuona kuwa mahakama ni muhimu kwa waislam, Hawakukurupuka.

  Tanzania inakusanya Zanziba na tanganyika, kama Zanzibar Kadhi kuti ipo, kwanini bara isiwepo? wakati ni nchi moja?

  Mahakam inaweza kuwepo na haipingani na katiba ya nchi, mahakama tayari ipo Zanzibar ambayo iko ndani ya katiba
  Acheni wasiwasi wa roho nchi iko stable unles mkatae mahakam!!
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Jul 19, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mahakama za Kadhi na Uvunjaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977!!

  1. Je, ugharamiaji wa Mahakama za Kadhi unaweza kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977? Ndiyo!
  Ibara ya 19 (2) inaeleza kwamba “Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari la mtu binafsi, na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za ma mamlaka ya nchi”. Kwa kuwa Waislamu wamesema kwamba uendeshaji wa Mahakama za Kadhi ni kuendesha ibada Mamlaka ya nchi haitakiwi kuingilia ibada hizo bali wahusika waachwe waendelee na uendeshaji ambalo ni jambo la mtu binafsi.

  2. Je, kuwepo kwa Mahakama za Kadhi Zanzibar ni kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Hapana!
  NYONGEZA YA KWANZA ya Katiba hiyo imetaja Orodha ya Mambo ya Muungano na suala la Uenezaji wa Dini, Kufanya Ibada, Kutangaza Dini sio la Muungano. Pia suala la Mahakama zote isipokuwa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano sio jambo la Muungano. Kwa hiyo suala hili ni la Tanzania Bara pekee ambapo utangazaji wa dini upo nje ya Mamlaka ya Nchi. Katika Ibara ya 99 (2) (b) ya Katiba ya Zanzibar, 1984 imeandikwa kwamba Mahakama ya Rufaa ya Jamhuri ya Muungano haitahusika na mambo ya Kiislamu ambayo yameanzia katika Mahkama za Kadhi. Kwa hiyo Mahakama za Kadhi za Zanzibar zimeanzishwa kwa Sheria za Zanzibar kama zilivyo Mahakama zingine hadi Mahakama Kuu, isipokuwa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.

  3. Je, kuna mtu amewakataza Waislamu kuunda Mahakama za Kadhi? Hapana! Wafuate Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 kuhusu uenezaji wa dini na sio kunukuu Katiba za Kenya, Ethiopia, Uganda, n.k.!
   
 10. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Jamani watoa mada wote kuna kitu kikubwa mnakisahau nacho ni idadi ya Waislamu kwenye hizo nchi zinazotolewa mfano kama Kenya, Uganda na hata Afrika Kusini. Waislamu ndani ya nchi hizo ni asilimia ndogo sana ya wananchi kwa ujumla wao na hivyo athari (impact) ya kuanzishwa kwa mahakama hizo inakuwa ndogo. Lakini kwenye nchi zenye idadi kubwa ya Waislamu kama Nigeria au Somalia yametokea matatizo makubwa kwa sababu ya mwingiliano uliopo baina ya wananchi kwa ujumla wao. Zanzibar kwa mfano ambapo idadi kubwa ya wakazi wake ni Waislamu na tunashuhudia matatizo makubwa yanayowapata wananchi wasio wa dini hiyo ingawa yanafagiliwa chini ya kitanda.

  Hebu tuliangalie jambo hili kwa kulilinganisha na mfumo wetu wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kwa sababu ya udogo wake na uchache wa raia wake na ili kuhakikisha inaendelea kuwapo iliweza kubakiziwa serikali yake ndani ya muungano. Je, ingekuwaje kama serikali ya Tanganyika ndiyo ingebaki na serikali ya Zanzibar kumezwa ndani ya Muungano ? Hata kwa akili ya kawaida waweza kuona kuwa hali kama hiyo ingeleta tafrani na hatari kubwa ya Zanzibar kuonekana kama mkoa au wilaya tu ndani ya Jamhuri ya Tanzania. Hivyo kukatolewa mwanya kwa sauti ya kikundi kidogo cha Watanzania milioni moja kusikika ndani ya kundi kubwa la Watanzania milioni arobaini.
   
 11. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #11
  Jul 20, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Anzisheni mahakama ya kikiristu ,kama mna sheria au sheria zake mnazijua tuone kama mna ubavu ,afu sijui kama mtazifuata maana hamjazizoea na wala sijaona kanisa linazifundisha ,sasa ugonvi upo wwapi? Au rudini katika misitu ya Kongo huko historia inaeleza ndipo wengi mlipotokea ,si raia wa pande hili la Tanzania au sivyo.
   
 12. Mtimti

  Mtimti JF-Expert Member

  #12
  Jul 20, 2009
  Joined: Feb 23, 2008
  Messages: 912
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 60
  mkwere kaelemewa jama....
   
 13. S

  Shamu JF-Expert Member

  #13
  Jul 20, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakuna ushahidi wowote kwamba nchi inasambaratika kwa sababu ya Kikwete. Tatizo si Rais, ni FREEDOM iliyopo sasa hivi. Zamani wakati wa Nyerere, Makanisa na Wakristo walikuwa na sauti kubwa kuliko Waislamu. Waislamu wengi hawakupata nafasi za kusoma nje ya nchi au kuongoza Taifa letu. Hali ya kimaisha ya Waislamu ilianza kubadilika wakati wa Mwinyi. Waislamu wengi wameweza kusoma na kupata nafasi za kuongoza Taifa letu. Kwa mujibu wa takwimu nyingi zinaonyesha kwamba Waislamu ni wengi zaidi kuliko dini yoyote ndani ya Tanzania. Sasa hivi tunaona hayo ktk uchaguzi nyingi ambazo madiwani ni Waislamu au katibu kata ambao pia ni Waislamu. Mabadiliko haya yanaonyesha kwamba Waislamu watakuja kudominate ktk kila kona ya siasa, biashara, kazi nk. Mabadiliko haya yamewafanya hadi Makanisa kuanza kumlaumu Rais; hata hivyo Rais hana uhusiano wowote na udini ktk uongozi wake. Zipo njia nyingi za kutatua haya matatizo.
   
 14. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #14
  Jul 20, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  mko more concerned na Mahakama ya kadhi kuliko ile anti terrorism law ambayo imekunyanganyeni liberty zenu zote kama binadamu

  mnakazi kweli kweli nyie
   
 15. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #15
  Jul 20, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Nina mashaka kama wewe (Mwiba) ni Mtanzania kweli! Lugha yako inaonyesha u mgeni nchi hii. WaTz kamwe hatubaguani kwa dini. Unalihusishaje kanisa na masuala ya mahakama ya kidini? Usichanganye mambo! Mbona Wakristo mara zote wanaungana na Waislamu kulaani kutukanwa dini ya Kiislamu. Kumbuka Rushdie alipoandika kile kitabu chake cha AYA ZA SHETANI (The Satanic Verses), hata Wakristo hawakufurahia na walishirikiana na Waislamu kulaani. Au unataka waanze kutafsiri hicho kitabu na kukisambaza? Patatosha kweli? Acha kushabikia na kuingiza chuki kwenye haya mambo ya dini, ni hatari sana!
   
  Last edited: Jul 20, 2009
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Jul 20, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,076
  Trophy Points: 280
  Nchi inatikisika kwa uongozi dhaifu- Lipumba
  Monday, 20 July 2009 07:11

  Tumaini Makene na Salum Pazzy
  Majira

  MATATIZO yanayoitikisa Tanzania na kutishia mgawanyiko mkubwa miongoni mwa jamii kwa misingi ya ukabila na udini ni matokeo ya uongozi dhaifu usiokuwa na majibu kwa wakati muafaka.

  Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba alipokuwa akihutubia Mkutano wa Hadhara wa chama hicho katika Kata ya Mwananyamala.

  Prof. Lipumba alidai kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete imeonesha udhaifu katika kuyatolea ufafanuzi na maamuzi masuala makubwa yanayoitatiza nchi na kutishia mgawanyiko miongoni mwa Watanzania.

  Aliyataja baadhi ya masuala yanayoitikisa nchi kwa sasa kuwa ni pamoja na Mahakama ya Kadhi, Tanzania kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislam (OIC), ufisadi miongoni mwa viongozi nchini na kuongezeka umaskini miongoni mwa Watanzania.

  "Ndugu zangu nawaambia yote mnayoyaona yakitokea sasa ni matokeo ya serikali dhaifu inayoongozwa na Kikwete (Rais Kikwete) mliyemchagua 2005, ni hatari sana kuchagua kiongozi dhaifu, legelege ambaye hawezi kusimama na kukemea maovu au mambo hatari yanayotishia uhai wa taifa," alisema Prof. Lipumba.

  Prof. Lipumba huku akifafanua dhamira ya CUF kuwazindua wananchi kupitia 'Operesheni Zinduka' ili wananchi wazinduke na kuona udhaifu na ufisadi wa viongzi wao, alisema umasikini wa Watanzania unazidi kuongezeka huku viongozi wakizidi kujineemesha kwa kula rushwa na kupora rasilimali za nchi.

  "Ripoti ya Serikali iliyotolewa mwaka jana ilionesha kuwa idadi ya masikini wa kutupwa imeongezeka kutoka milioni 11.4 mwaka 2001, hadi milioni 12.9 mwaka 2007, hii maana yake ni kwamba masikini wameongezeka kwa milioni 1.5 sasa haya ndiyo Maisha Bora kwa Mtanzania mliyoahidiwa na CCM?," alihoji.

  Akizungumzia suala la Mahakama ya Kadhi, Prof. Lipumba, alisema kuwa Rais Kikwete alipaswa kuwa amelitolea ufafanuzi na uamuzi wa suala hilo ambalo liko katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005 ambayo ndiyo iliyotumika kumwingiza madarakani.

  "Katika Ilani hiyo sura ya 8, ibara ya 108 b, CCM iliahidi kuhakikisha kuwa tatizo la kukosekana kwa Mahakama ya Kadhi, linatafutiwa ufumbuzi lakini sasa hivi cha ajabu wanawaambia waislam waunde Mahakama hiyo wao wenyewe, nje ya Serikali, sasa wakiunda mahakama kama za Somalia itakuwaje?," alihoji tena Prof. Lipumba.

  Prof. Lipumba alisema kuwa katika hilo, Rais Kikwete alitakiwa kumuuliza Rais wa Kenya, Bw. Mwai Kibaki, alipotembelea juzi nchini kwani nchi hiyo ina Mahakama ya Kadhi na wala haina tatizo lolote.

  Alisema kuwa kwa kipindi cha miaka minne madarakani serikali ya CCM chini ya Rais Kikwete imeshindwa kutumia fursa ya kijiografia ambayo Tanzania imebarikiwa kuwa na bahari, maziwa makuu, mito mikubwa na madini mbalimbali.

  "Mwaka jana Tanzania imesafirisha dhahabu yenye thamani ya dola milioni 800, lakini Serikali iliambulia dola milioni 24 tu na zingine zote zimepotea kwa misingi ya kifisadi na mikataba mibovu,"

  Alidai kuwa katika kesi za ufisadi Rais mstaafu, Benjamin Mkapa anapaswa kuwa namba moja kwa sababu aliruhusu ukwapuaji mkubwa wa rasilimali za nchi hii hasa katika awamu yake ya mwisho ya utawala.

  Alisema aliposhutumiwa juu ya hilo baadhi ya viongozi waliwataka wanaomtuhumu watoe ushahidi. Alidai kuwa sasa ushahidi umepatikana tena kutoka kwa Taasisi ya Kuchunguza Ufisadi ya Uingereza (SFO) ukiwahusisha baadhi ya viongozi waandamizi wa Serikali na ufisadi wa rada.

  "Katika ufisadi wa rada wataalam walishauri Serikali inunue rada yenye thamani ya dola milioni 5, lakini wao wakanunua kwa dola milioni 40, huku Kampuni ya BAE System iliyowauzia ikimhonga dalali Saileth Vithlani, dola milioni 12 naye akawahonga wakubwa serikalini " alisema

  Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF, Bw. Ismail Jussa, alisema kuwa CCM imekamilisha kazi yake ya kuwaletea uhuru watanzania lakini imethibitisha kuwa haiwezi kuleta maendeleo kwa nchi hii.

  "Kwa muda wa miaka 48 ya uhuru na minne ya Rais Kikwete Watanzania wameshuhudia utawala wa 'kisanii' na 'kishikaji' ambao sasa umefikia mahali pa kuvuruga umoja na mshikamano wetu kwa kushindwa kusimamia maslahi ya nchi hii," alisema Bw. Jussa.
   
 17. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #17
  Jul 20, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  huenda wakisema viongozi wote wa upinzani haya, labda wananchi wanaweza kuamka na kupigia kura angalau wabunge wengi zaidi wa upinzani.
   
 18. F

  FM JF-Expert Member

  #18
  Jul 20, 2009
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama ishu ni kusema nadhani viongozi wote wa upinzani na wana ccm wazalendo wanasema sana. Tatizo huko wanakosemea. Ni bahati mbaya sana kwamba mambo haya yanasemwa kwenye maeneo ambayo kwa kiasi fulani wanaujua ubovu wa JK na serikali yake lakini bahati mbaya zaidi watu wenyewe wala si wapiga kura. Nadhani jitihada hizi sasa zikaelekezwa vijijini ambako ndiko kwenye watu wengi na wakihamasishwa vizuri wanaweza kufanya mabadiliko maana huko ndiko kwenye wapiga kura wengi.Ni mtazamo tu!
   
 19. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #19
  Jul 20, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hongera Lipumba umekata kichwa kingine.
   
 20. M

  Mwanaluguma Member

  #20
  Jul 20, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Ni kweli,Kikwete hawezi kuhandle suala la udini unaochipukia kutoka kwa kuwa ana washauri wabovu,pamoja na mwenye kuwa na uwezo mdogo katika kushughulikia masuala mazito kama hayo.
  Mfano suala la udini Mwl NYERERE alisema katika hotuba yake kuwa suala la kuzuia udini kuchipukia lisiposimamiwa litaibuka ndicho tunachoshuhudia leo hii,mfano hivi enzi za nyerere waislamu hawakuhitaji Mahakama ya kadhi au OIC? haya mambo kwa nini yalianza tu baada ya mzee yule kututoka duniani?
  Kikwete anajifanya kunyamaza kimya labda ataonekana safi kwenye kushughulikia mambo,ukweli ni kwamba amechemsha sana kwani mambo kama hayo ambayo yanaweza kuigawa nchi yakijitokeza yanaitaji hotuba ya kitaifa kuyaweka sawa. Najua waislamu ni delicate kuwahandle kumbuka mbokomu butchery Manzese ingekuwa wakristu wasingefikia vife,kumbuka picha ya madona ya kuwambwa msalabani kama yesu iliyooneshwa Italia alipotaka kufanya shoo zake,kilichofuatia kwa wakristu ni kukemea tu na sio jazba za kuharibu mali.
  Kwa hiyo Kikwete ambaye watu wengi walimsifu kuwa ni rais anayefaa leo hii anaoneka hopless kabisa,kazi kuzunguka dunia kwa kisingizio cha kutafuta misaada. Tofauti yake na mkapa ni kuwa mkapa alikuwa na jazba ndio maana nchi ikazalisha wakimbizi Pemba,angeweza kuongeza askari wengi kusimamia maandamano yaliyokuwa yafanywe na CUF ili yasiwe na vurugu damu ya watu isingemwagika ila jazba zilizidi,
  Kikwete yeye kazi yake kutabasamu tu lakini tabasamu lisilotusaidia chochote.
   
Loading...