Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Nimefurahishwa sana na vita nzito ambayo serikali imeianzisha dhidi ya wezi wote wa kazi za wasanii. Kumuona waziri Nape Nnauye mwenyewe akiingia front kwenye mapambano dhidi ya wote ambao wanachangia katika kuwapatia umasikini wasanii, ni jambo ambalo linahitaji kuungwa mkono kwa nguvu zote.
Wanamuziki, wachekeshaji na waigizaji ni kundi la jamii ambalo limedhulumiwa kwa miaka mingi sana. Hivyo kuiona serikali kwa maana ya waziri akiingia ndani ya duka moja baada ya jingine, kwa kweli inatia moyo sana. Kuna wanamuziki wengi sana ambao walikatishwa tamaa na dhuluma za kazi zao.
Ring tone za simu zimewapa utajiri mkubwa wenye makampuni huku wanamuziki wenye sauti na vipaji, wakikatiza mitaani wakiwa na maisha ya kawaida sana. Mara nyingi wanamuziki wakiridhika kununua magari ya kupigia misele mitaani, ambayo pia hayana thamani inayolingana na kazi yao inayosikika radioni na kuonekana runingani.
Wapo wananchi wenye kupenda sana kumsema vibaya mheshimiwa Nape Nnauye, katika zoezi hili la kuwakamata wote wanawadhulumu wasanii, kwa kweli mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.