Mheshimiwa Mbowe, Wananchi na Wanachadema wanasubiri uwasomee maazimio ya kamati kuu juu ya Maridhiano na suala la ngorongoro

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,505
51,108
Kwako mheshimiwa Mbowe,

Miezi miwili iliyopita, ulitutangazia kuwa Kamati kuu iliyokaa mwezi huo iliazimia mambo mengi, miongoni mwayo ni suala la bandari, Maridhiano na suala la ngorongoro.

Lakini katika kusoma maazimio hayo, ulijikita zaidi kwenye suala la bandari, ukasema kuwa masuala mengine yanayohusu ngorongoro na Maridhiano utayasoma siku nyingine ili kutoa nafasi kwa suala la bandari kujadiliwa kwa mapana.

Sasa ni dhahiri, suala la bandari tumelijadili, tunalijadili na turaendelea kulijadili ila tunadhani ni wakati Muafaka sasa uje utusomee maazimio ya kamati kuu ya chama juu ya mambo mengine.

Hii ni muhimu sana hasa ukizingatia kuwa, tunaona rais Samia akianza kukwepa suala la katiba mpya kinyume na alivyotuaminisha awali.

Lakini pia tunaona manyanyaso ya wananchi huko ngorongoro na hata kufikia viongozi wa chama kuzuiliwa kufanya mikutano huko ngorongoro.

Mheshimiwa,
Tunaomba kabla hamjafanya kukao kingine cha kamati kuu, tunaomba utusomee kirefu maamuzi ya kamati kuu iliyopita.

Natanguliza shukurani.

Wako katika ujenzi wa Taifa
Missile of the nation.
 
Back
Top Bottom