Mhe. Rais hajui athari za kauli zake... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhe. Rais hajui athari za kauli zake...

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by ngoshwe, May 12, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  May 12, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Wakati akiwahutubia wazee wa ccm wa mkoa wa dar es salaam kuhusu mgogoro kati ya serikali na tucta ni dhairi kabisa mhe. Rias alionekana ni mtu mwenye jabza, asiyejua utawala bora na aliyolewa madaraka.

  Akisema kuwa yeye ategemei ushindi katika uchaguzi mkuu toka kwa wafanyakazi na kuwaponda wafanyakazi mhe. Rais hata kama hakushauriwa vizuri, kama kingozi wa watu na aliyekuwa madarakani (katika nyazifa mbalimabli nyeti) alipaswa kufikiri sana kabla ya kukurupuka, kuitisha kikao na kuanza kuropoka mbele ya wanachama wenzake wa CCM (sio watanzania wote) kauli zisizoendana na dhamana aliyonayo kama Rais wa watanzania (bila kujali matabaka, dini, rang, kabila na mlengo wa kisiasa).

  Kwa kauli yake ya kuonyesha hajali kabisa wafanyakazi na madai yao hayatekelezeki, Rais amejitia doa na asijue yafuatayo ambayo yanaweza kumwangusha:

  1. kwa kukataa kura za wafanyakazi mbele ya wana CCM wenzake, ameonyesha wazi kuwa anauhakika wa kusshinda kwa mbinu zozote zile na kuwa wafanyakazi wa nchi hii hawana ulazima wowote wa kuwepo katika orodha ya wapiga kura wa CCM (ubaguzi wa hadhira).
  2. akae akijua kuwa wale wazee aliokuwa wakimpigia makofi siku ile kwa mbwembwe wao ni wazazi wa hao wafanyakazi na kuwa wafanyakazi wanaweza kuwashawishi ndugu na jamaa zao wote ambao wanategemea misadaa na huduma zao kutompa kura kabisa yeye na wagombea wote wa ccm ili kumwonyesha tu kuwa wafanyakazi hawafanyiwi mchezo!
  3. ajue kuwa kwa kauli ile ya kukataa hadharani kura za wafanyakazi alionyesha kuwa yeye ni mbinafsi na asie fikiria kuwepo kwa wanasiasa wenzake ndani ta CCM ambao wanahitaji hizo kura ili ziwape ushindi katika ngazi mablimbali za uongozi kuanzia tawi mpaka taifa. Hivyo, kamwe wasingethubutu kuwabeza wafanyakazi.
  4. ameonyesha unafiki kwa kuwa yeye ndie aliekuwa akihubiri kila siku kuwa cheo ni dhamana kuwataka wafanyakazi wa umma kuheshimu wateja kupitia mikataba ya huduma kwa wateja (CLIENT SERVICE CHATER) huko Serikali ambayo inawataka watumishi wa umma yeye akiwa mmoja wapo kutotumia lugha za dharau, kuwasikiliza na kuwajali wateja. Tulitegemea yeye kama kiongozi mkuu wateja wake ni watanzania wote ikiwemo wafanyakazi, hivyo alipaswa awasikilize kwanza baada ya Waziri husika (Kapuya) kushindwa na sio kukurupuka na kwenda kuanika hadharani misimamo yake binafsi ambayo kimsingi ilionyesha ni jisni gani Serikali yake isivyo na subira pia na inavyoichuka maamuzi kwa kukurupuka na kinyume na kanuni za utawala bora ambao anadai Serikali inaufuata.
  5. Akiwa mwenye dhamana ya nchi, hakupaswa kutamka kuwa yeye ndo "mwajiri Mkuu" na kusahau kuwa watanzania ndio waliomwajiri yeye na kuwa hali bora ya maisha yake na viongozi wengine wa chama na Serikali ilipaswa iendane kipoato halisi cha mtanzania na hivyo busara si kusimamai kwenye kadamnasi na kuelezea jambo ambalo angeweza kulitatua ndani ya vyombo vya Serikali yake.
  6. ameonyesha jinsi gani ambavyo Mawaziri wake kama Msomi Prof Kapuya wasivyokuwa na uwezo wa kushughulikia masuala yahusuyo Wizara zao mpaka yeye mwenyewe ainigilie kati jambo ambalo ni dharau kwa hao mawaziri wake.
  7. akae akijua kuwa hao wafanyakazi ndio waliomsaidia ushindi wa uchaguzi uliopita na ndio wanaomfanya ajivunie mafanikio ya serikali yake.
  8. ajue kuwa kuvuja kwa siri za serikali pengine kunatokana na viongozi wa serikali yake kutosikiliza matatizo ya wafanyakazi.
  9. ajue kuwa kuendelea kuwepo kwa ufisadi wa wazi na ule wa siri siri ni kutoka na wafanyakazi kutolipwa vizuri na atahri zake ni kujenga tabaka la watumishi wa umma wasio waadilifu.
  10. ajue kuwa amewapa kiburi maafisa wa usalama kuhusiana na jinsi ya kukabilina na matatizo yanayohusu migomo ya wananchi iwe wafanyakazi, wanafunzi na wengine kwa kauli yake ya kurejea kauli ya hatua ambazo serikali ilichukua dhidi ya mgomo wa kilombero na ambao kimsingi wawez kutokuwa na sura linganifu na hii inayotoke sasa.
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Ajue kwamba wafanyakazi ndio wanasimamia hata kura!
   
 3. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Well said mzee!

  Wahenga wanasema usimtukane mke wakati ukijiandaa kwa tendo la ndoa na wala usimkashifu mpishi wakati chungu kipo jikoni!!!

  Hao hao wafanyakazi ndio wanamlinda yeye na familia yake, na ndio watakao saidia kufanya kura zile za maruhani za kubadili matokeo zitimie.#

  Ajui hata hao polisi na wana usalama ni wafanyakazi hata kama si wanachama wa TUCTA lakini bado ni wana ndugu za hao anaowapuuza!.
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hana adabu na imeonyesha jinsi gani alivyokosa staha kwa watu anaowaongoza...very low for him
   
 5. masharubu

  masharubu Senior Member

  #5
  May 13, 2010
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wana wa JF kisa hiki cha jk kuwakana wafanyakazi mbele ya hadhira na kusema haitaji kura zao ananikumbusha na mimi kisa kimoja cha ndege mmoja anaitwae kozi (Eagle). Siku moja aliruka juu umbali mrefu sana na akiwa juuu alisema natumia uwezo wangu na manyoya ya pembeni yakasema na sisi tumo. Hapo akakasirika na kurudi chini akisema nitawakomoa leo,kilichofuata alijinyonyoa manyoya yote. Kilichofuatia kila akijaribu kuruka alishindwa na alikoswakoswa kuliwa na wanyama kama mbwa kwa muda wa siku kadhaa mpaka manyoya yalipoota na ndipo aliweza kuruka. Siku ya kwanza kuruka tena alipaa zaidi ya pale na alisema tena natumia akili yangu, manyoya yakasema tena na sisi tumo naye akajibu shime.

  Kwa kisa hicho jk asijifanye kozi ambae aliona hana haja na manyoya anweza kuruka mwenyewe. Na kwakiasi kikubwa raisi alijitahidi kuonyesha kwamba yeye ni mkweli hapendi kuwadanganya wananchi wake kuwa hawezi kulipa laki 315, basi ukweli huohuo na atueleze nishule gani leo hii watoto wanapewa madaftari, niwapi umeme unafikishiwa majumbani bila gharama, ni hospitali gani unatibiwa bureeee bila kulipa kama alivyoainisha katika kutilia mkazo hutuba yake?
   
 6. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  hatuna Prezidaa ameonea kama Mzee wa Kijiweni...amewakosea heshima Wafanyakazi wa Tanzania
   
 7. Eng. SALUFU CA

  Eng. SALUFU CA Senior Member

  #7
  May 13, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kuwa huu ni wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu na kwa kuwa yeye ni miongoni mwa Candidates, alikuwa anajaribu kuteka kundi la watu wengi ili TUCTA waonekane wamechemka, miaka ya tisini sisi tulipokuwa chuo kugomea cost sharing tulionekana manyang'au na vibweka vingi kwamba tunataka hela za matanuzi wakati sio kweli, wakati ule hata vijana waliandamana kuunga mkono kuwa sisi tulioandamana tulichemka matokeo yake ndo haya sasa hivi huna kitu chuo sahau kwani hata hiyo mikopo yenyewe inatolewa kiduchu. Kwa hiyo kauli ile ilikuwa ni kupata sapoti ya watu wengi ambao hawakupewa nafasi ya kueleweshwa kisayansi juu ya mchakato mzima wa kima cha chini cha mshahara. Sisi tujitahidi kujitokeza kupiga kura ili tupate viongozi safi, tukumbuke kwamba kura yako moja ni muhimu sana kumuweka mtu madarakani.
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  May 13, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Ngoshwe unajua Kiburi chake huletwa na ugoi goi wa maaamuzi mazito ya hawa Watumishi, Kikwete hawaogopi kwa maana anajua fika watamchagua tu, ni waoga wamageuzi, wamelelewa kwenye mazingira ya mkuu wa nnchi ndie mwenye uwezo pekee wa kufikiri.
  kwa kuujua fika udhaifu huo, yupo tayari kuwatukana matusi makubwa na yanguoni....haogopi na wala hanahofu nao.
   
 9. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #9
  May 13, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  MISEMO IFUATAYO YA KISWAHILI INA MAANA KUBWA SANA HAPA!
  • Ngoma ikilia sanaaa.....................?
  • Si yote yang'aayo ...............?
  • Ajizaniaye amesimaaa................?
  • Asiyefunzwa na Mamaye....................?
  • Hakuna Marefu..................................?
  >>>>>>SASA KWA TAARIFA YAKE: MUHESHIMIWA MKUU ATAMBUE KWAMBA MAREFU YAKE SASA YAMEFIKIA NCHANI....!
   
 10. MLATIE

  MLATIE Senior Member

  #10
  May 13, 2010
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 174
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ukweli ni kwamba rais wetu hajatambua kama watendaji wake wanampeleka ndivyo sivyo kama ni kweli yale yote yaliyosemwa na TUCTA ni kweli muda mfupi tu baada ya JK kuhutubia kweli hapo kuna tatizo.Rais aangalie upya baraza lake la mawaziri na achanganue jambo kabla ya kuanza kulitolea maamuzi.
   
 11. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #11
  May 13, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kama kweli watanzania wakulima na wafanyakazi bado wana ile hofu ya mbwa kuficha mkia mbele ya tajiri ili wapate mkate, hali halisi sasa wanaiona wenyewe. Hapo ni miaka mitano tu..sasa kiburi kitapanda pale mitano mingine ikiongezwa, na mnavyomuita wenyewe "Mcheshi", Kijana nk ...msije kujuta siku ambapo matasikia hata Katiba imebailishwa kuongeza mitano mingine na mingine...(yeye ana taaluma ya Jeshini na Siasa) basiiii!. Na mwaona wenyewe sasa imekuwa kama sala ya asubuhii, kila kiongozi ataka mwanae nae arithi nyayo..Nadhani watoto wa Marehemu Baba wa Taifa tu wameonekana ndo pamoja na kubebwa sana, wameshindwa kutokana na maadili waliyolelewa na Mwalimu (R.I.P). Mungu awasaidie kuepuka hii dhambi ya kupenda madaraka hata kama huna sifa.

  MKUMBUKE ZAMANI KATIKA SHAHADA YA KUPIGIA KURA WALITUWEKA "PICHA YA MTU" NA "KIVULI" LEO TUNAJIVUNIA KUWA NA "PICHA ZA WATU" KAMA WOTE NI WABOVU BASI NI HERI TUKAJARIBU MBOVU MWINGINE KWA STAILI YA KUCHEZA KARATA KULIKO KUMPA MTU AMBAE AMESUSA WAZI WAZI TENA KWA MATUSI YA HADHARANI!!!.
   
 12. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #12
  May 13, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,604
  Likes Received: 4,731
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni kuwa jk ni mvivu wa kufikiri kazi ya kufikiri amewachia REDET na jopo la wachawi. Ataisoma namba oktoba
   
 13. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #13
  May 13, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu Presida wetu hutemeblea hili jamvi? Tunaweza kumshauri zaidi kuliko hao watu wake like Kapuya AKA AKUDO .
   
 14. o

  obseva JF-Expert Member

  #14
  May 13, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 80
  Nawaomba chonde chonde wadau wa jamvi, kama kana mahari tunaharibu nikutopiga jiandikisha na kupiga kura, ama kwasababu hatuoni mtu wa kumpigia au kwa sababu ya kukata tamaa. kwa kutofanya hivyo tunawapa wale wazee walikuwa wakipiga vijembe wakati wa hotuba kupiga kura na kuleta ushindi wa kishindo wa asilimia 9 ya watanzania wote.

  Narudia kuwaomba tarehe 22 na 23 jiandikisheni natukapige kura kuwachagua tuwatakao, usiiache kura yako nyumbani hatakama humuoni unaye mtaka basi chagua wapili wake ili kura za tusiowapenda zisiwe nyingi kwasababu tu hatukushiriki kuchagua.
   
 15. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #15
  May 13, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  hapa tutaongea weeeh lakini kama watu wetu, wapigakura wetu hawataamka, tumeliwa, lazima watu wajifunze kua jukumu lakumng'oa Jk nilakila mmoja, waache wale wazee wajinge waendelee kumpigia makofi wakati wenzao wanagalagala pale Hazina kwakunyimwa haki zao.
  mimi nasema adui ya Watanzania wenzangu ni hofu na uwoga wakudhani kua kuna mwenye jukumu lakuleta mabadiliko kisiasa, wanadhani mtu kama Mrema ataweza kazi hiyo, tuunganishe mikono yetu, tuungane na wapenda mageuzi wengine kuwang'oa hawa vibaraka na wanyonyaji wa Taifa letu.
   
 16. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #16
  May 13, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kama inavyoonekana kwenye Signature ya Baba_Enock
   
 17. masharubu

  masharubu Senior Member

  #17
  May 13, 2010
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  We babaake Enock umerogwa?
   
 18. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #18
  May 13, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Jamaa alibwabwaja kiasi nikisikia mtu akiita ile ni hotuba nashindwa kumuelewa maana haifanani kabisa na hotuba...sijui kama ilikua ni ushauri aliopewa ama alitumia kilevi fulan yaani naonahata aibu kutamka kuwa ni rais wangu.
   
 19. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #19
  May 13, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  yawezekana kwenye ile chupa ya maji ya kilimanjaro hakukuwa na maji halisi...ni wakati wa kujifunza sasa kutokana na kauli zake, hakika Mwalimu alilijua hilo tokea mapema na hakusita kutuasa watanzania juu yake lakini huko aliko aliko Mwalimu ambapo tunamwombea apumzike kwa amani hawezi kuwa na amani hata kidogo kwa jinsi ambavyo watanzania hatujaonyesha kum enzi kwa vitendo.
   
 20. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #20
  May 13, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  tulisahau jamani,mwalimu alisema hajakomaa tungemwuliza tusubirihadi lini? naona bado kama miaka ishirini hivianshindwa kuelewa moja nambili ni ipi inatangulia.sasa kama yeye ni mwajiri namba moja yeye kaajiriwa na nani? au ni mfalme? haki ya mama inakula kwake mwaka huu.tena ajira yake ni ya mashaka kuliko hao anao wadharau.akili za kuambiwa?
   
Loading...