Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
- Thread starter
- #61
Word!Juhudi za raisi ni kukusanya fedha binafsi za watu? Raisi siyo hakimu. Suala la Ruge liko mahakamani. Mahakaman itaamua kama alikwiba ama ni tuhuma zilizo kwenye msingi sahihi.
Ngereja ni papala siku zote za kufuata vishindo bila tafakuri. Kama Ruge alimpa fedha, na Ruge bila shaka fedha anazonyingi tu nje ya zile za Escrow. Kwa nini ngelezja hataki kuona kwamba fedha alizopewa na Rugemalila hazikutokana na mgao wa Escrow?
Haimpi ufahamu kwamba Ruge angeweza kutoa zawadi kwa marafiski zake kutoka vyanzo vingine zaidi ya Escrow? Nilidhani kitendo cha Ngeleja kisionekane kuwa ni busara ama uzalendo. Kwa mtazano ni kitendo cha hofu inayotokana na ukwlei anaoufahamu juu ya ushiriki wake katika Escrow na hivyo anajua kabisa kwamba ili haikuwa zawadi bali malipo ya biashara haramu.
Kwa nini sherika isimfuate naye kwa ushiriki wake katika mchakato wa wizi wa fedha za umma, ama asikamatwe kwa kuhodhi mali za wizi?
Kama sheria itazingatiwa na haki itendeke, bila shaka Ngeleja na wadau wenzake watamfuata Rege soon ili wajitetee pamoja. Wote ni syndicate ya wizi wa fedha za Escrow.
Sheria imeweka hukumu za wizi siyo tu kwa kuwa wameiba lakini pia ni namna ya kushambulia spirit ya wizi ambayo kama ikibainika kwamba wezi wanarudisha tu mali na kuachwa, bila shaka wengi wataiba sana , watafanya biashara na hizo fedha, watazitumia kwa nman yoyte watakavyo halafu baadaye watazirudisha, na halafu watanzania watafanya maandamano ya kuwapongeza wezi.
Aliyeibiwa aliumizwa kiasi gai?
Ni hasara gani katika maisha wanaipata wale wanaoibiwa?
Tuhalalishe wizi kuwa ni jambo la kawaida hapa nchini?
Halooo!. Ninaogopa.