Mhe. Ngeleja, Mzee Rugemalira amekukosea nini hadi 'umhujumu' hivi?

Aliyetoa mwingine,anayerudishiwa mwingine.
Vipi kuhusu riba ya miaka mitatu?
Ina maana mgawo uliolipiwa kodi unapaswa kuongezewa kodi?
Ngeleja katika hili umeiabisha taaluma yako ya sheria,kwani hata logic za kawaida zinakataa.
TRA rudisheni hizo pesa kwa Ngeleja ili azirudishe alikozitoa na sheria ya maadili ya utumishi wa umma ichukue mkondo wake.
TRA isitumike kutakatisha watu waliokuwa wamejificha,otherwise TRA itakuwa ni sehemu ya kutakatisha fedha haramu zinazohojiwa na serikali kupitia mahakama.
 
Binadamu tunaruhusiwa kutubu.

Awasaidie tu takururu kuwapa habari zote na kuwataja wote na kila kitu ilikuwaje na ikawaje.

Cheo chake kileeeeeeeeeeeeeee
Na hawa waliyopokea warudishe

Ova
 

Attachments

  • Screenshot_2017-07-10-22-22-26.png
    Screenshot_2017-07-10-22-22-26.png
    402.7 KB · Views: 27
Hajamsaliti....isipokuwa amefanya kile nafsi inaona inafaa zaidi kuunga mkono juhudi za Rais kupambana na ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma.



From Kibiti
Ye mwenyewe fisadi, mbona hajarudisha kipindi cha JK?asitulaghai akaona akili zetu zimeganda. Kwanza yeye ndiyo alibinafsisha hadi Tanesco, Umeme uwe wa shida ili wafanye biashara zao za majenereta. Yeye ni jipu tu na mama ake wa pesa za mboga. Wasituone kimya Watz tuna hasira nao kweli kweli.

Sent from my TECNO-L5 using JamiiForums mobile app
 
Zawadi iliyorudi baada ya miaka 3 zawadi gani iyo au ya wizi?Kwani pesa kamrejeshea ruge au TRA? Kwa nn asimrejeshee aliempa?
Jibu lake ni muhujumu uchumi kama wahujumu wengine.

Sent from my TECNO-L5 using JamiiForums mobile app
 
Binadamu tunaruhusiwa kutubu.

Awasaidie tu takururu kuwapa habari zote na kuwataja wote na kila kitu ilikuwaje na ikawaje.

Cheo chake kileeeeeeeeeeeeeee
kwan zile hela zilikua za serikali?????
mbona rais mstaafu alisema zilikua sio za umma lumumba wakapiga makofi ???

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
 
Huyo mbunge akili zake si sawa yaani nikupe pesa kisha ukaipa serikali and then unatangazia Dunia kuwa umenirejeshea...

We mzee ni mnafiki kiama....

Ruge ukitoka lupango mshitaki huyu mbunge akurejeshee pesa yako aliyotutangazia... hata usipotoka nduguzo wamdai
 
Fact No. 1: Katika urafiki wenu,Mzee Rugemalira alikupa milioni zaidi ya 40 mwaka 2014.

Fact No. 2: Pesa alizokupa Mzee Rugemalira zilitokana na mgawo wake kwenye masuala ya hisa na Escrow kwa ujumla

Fact No. 3: Ni wewe tu ndiye unayeujua ukweli kama ulifahamu chanzo cha fedha ulizopewa na Mzee Ruge au la na mlichozungumza hadi akakupa.

Fact No. 4: Mzee Rugemalira ameshaburuzwa mahakamani kwa mashtaka yahusuyo sakata la Escrow na ameyakana mashtaka yake yote.

Fact No. 5: Kisheria, Mzee Ruge kukana mashtaka ni kuwa na nia na wajibu wa kutetea uhalali wa fedha zake na mgawo wote alioufanya.

Fact No. 6: Kama waliogawiwa,ukiwemo Ngeleja,wanataka kurejesha pesa,wanapaswa kuzirejesha kwa aliyewapa ambaye ni Mzee Ruge ili azitetee pesa zake mahakamani anaposhtakiwa.

Fact No. 7: Kuzirejesha pesa Serikalini ni 'kuchongea' kuwa chanzo hakikuwa halali na hivyo kuweka ukakasi hadi kwenye mashtaka dhidi ya Mzee Ruge.

Kwa urafiki wenu na muda wote uliopita tangu ugawiwe mwaka 2014,kwanini wafanya haya ya marejesho sasa? Huku si 'kumhujumu' Mzee Ruge?
Hivi wewe bado chuo kikuuu UDSm bado wanakuendekeza kuwa Mwanasheria wao? no no no
 
Huyo ngeleja anajaribu kujibembeleza kwa pombe,hana lolote!! Ndio hawa tunawaita wanasiasa uchwara

Sent from my TECNO W5 Lite using JamiiForums mobile app
 
Ningekuwa Valentine Mlolowa wa pccb ningehakikisha leo ngeleja analala ndani
 
Hajamsaliti....isipokuwa amefanya kile nafsi inaona inafaa zaidi kuunga mkono juhudi za Rais kupambana na ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma.



From Kibiti
Kwa Mujibu wa Dr Kikwete , ambaye alikuwa Rais wa Tanzania na kiongozi wa juu kabisa wa ccm , Alipoongea na wanaccm mafukara na waliochoka wa DSM , ambao walipachikwa jina la uongo la Wazee wa DSM , Alisema kwamba HELA ZILE SI ZA UMMA .

Sasa Msaliti Ngeleja kwanini asimrudishie mzee wa watu hela zake ?

Kisa ni huo uwaziri wa Muhongo ?
 
Fact No. 6: Kama waliogawiwa,ukiwemo Ngeleja,wanataka kurejesha pesa,wanapaswa kuzirejesha kwa aliyewapa ambaye ni Mzee Ruge ili azitetee pesa zake mahakamani anaposhtakiwa.
Hiki ndicho alichopaswa kufanya huyu Bashite mwingine Ngeleja...kwa hiyo kimsingi Mzee Ruge akimalizana na serikali atapaswa kudai hela zake kwa huyu mnafiki Ngeleja, pmbv zake!
 
Back
Top Bottom