Rugemalira aamsha mzimu wa Escrow, aomba aachiwe azifuate kwa aliowagawia

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,551
2,000
RUGEMALIRA AAMSHA MZIMU WA ESCROW
:

MKURUGENZI wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira, amedinda kutubu na kukiri makosa anayotuhumiwa ya uhujumu uchumi, badala yake amemwandikia barua Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), akimtaka kumwachia huru ili washirikiane kupata Shilingi trilioni 37 anazoidai Benki ya Standard Chartered na pia Serikali itapata kodi ya zaidi ya Sh trilioni sita.

Wakati Rugemalira akidinda kutubu na kukubali kulipa ili aachiwe HURU, aliyekuwa mmiliki mwenza katika kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Kalasinga Harbinder Singth Sethi, ameandika barua kwa DPP akikubali kurejesha fedha kulingana na makubaliano watakayokuwa wamekubaliana.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi kwamba kesi hiyo ilikuja kwa kutajwa na anaomba tarehe nyingine.

Naye Wakili wa Rugemalira, Michael Ngalo alidai mteja wake aliandika barua kwenda kwa DPP, lakini hawajapata majibu, hivyo aliomba upande wa Jamhuri kusaidia yapatikane.

Baada ya Wakili Ngalo kueleza hayo, Wakili wa Serikali Wankyo alieleza kwamba ni kweli barua imepokewa na inafanyiwa kazi, majibu atapewa.

Alidai kuhusu upelelezi bado haujakamilika na hawawezi kuahidi ni lini utakamilika.

BARUA YA RUGEMALIRA

Rugemalira aliandika barua Oktoba 4, mwaka huu kwenda kwa DPP na kupokewa Oktoba 5, akiomba aachiwe huru ili aweze kushirikiana na Serikali kupata Sh trilioni 37 kutoka Benki ya Standard Chartered na washirika wake.

Mshtakiwa huyo ameainisha vielelezo kadhaa vinavyoonyesha Standard Chartered ilivyohusika katika sakata la IPTL.

Miongoni mwa vielelezo hivyo ni gharama zilizokuwa zinatozwa na IPTL dola za Marekani 1.06 kwa kWh ni za chini kuliko zilizokuwa zinatozwa na Songas dola za Marekani 4.31 kwa kWh.

Kielelezo kingine ni barua aliyomwandikia Gavana wa Benki Kuu (BoT) Januari 17 mwaka huu akiomba majina ya watu waliolipwa Sh 144,947,669,844.2 zilizokuwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow kati ya Julai 5, 2006 na Machi 19 mwaka 2014.

Wakati sakata la Escrow lilivyoingia bungeni mwaka 2014 na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi wa akauti hiyo kwa maelezo ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ilielezwa kuwa fedha za Rugemalira zilikuwa kwenye akaunti ya Benki ya Mkombozi ambazo baadhi aligawa kwa watu waliotajwa.

Pia inaelezwa fedha nyingine za PAP, ziliwekwa katika akaunti ya kampuni hiyo ya Sethi ambapo taarifa ya PAC bungeni ilisema zilisombwa kwa sandarusi na watu ambao hawakutajwa na sasa Rugemalira anataka majina ya watu hao kuwekwa wazi.

Pia katika barua yake hiyo kwa DPP, Rugemalira pia anadai alieleza PAP kukiri kulipwa na Benki Kuu Sh 164,513,630,314.15 na dola za Marekani 22,198,544.60 na si Sh 309,461,300,158.27 na dola za Marekani 22,198,544,.60 kama ilivyokuwa katika hati ya mashtaka kwenye kesi ya uhujumu uchumi namba 27/2017.

Aliambatanisha pia nakala ya barua ya BoT yenye kumbukumbu namba NC.130/170/01 iliyoandikwa Februari 18, 2018 (2019) ikiwa ni majibu ya barua yake ya Januari 19, 2019.

Kiambatanisho kingine ni cha gazeti la Financial Times la Julai 20/21 2019 lililotoa taarifa kuwa wadau wameituhumu Benki ya Standard Chartered kwa Serikali ya Marekani kwa kutoa dola bilioni 57 isivyo halali na benki hiyo ilifikia makubaliano na mamlaka za nchi hiyo kwa kukubali kulipa faini ya dola bilioni moja.

“Ninatumaini kwa maelezo hayo yaliyoainishwa katika nyaraka hizi zilizotolewa na ofisi yako kati ya Juni 18, 2019 na Julai 22 2019 utaweza kutumia mamlaka yako chini ya kifungu cha 29(6) cha Sheria ya Makosa ya Uhujumu Uchumi kuniachia huru katika kesi ya uhujumu uchumi namba 27 ya mwaka 2017 ili niendelee na juhudi zangu za kuisaidia Jamhuri kurejesha zaidi ya Sh trilioni 37 kutoka Benki ya Standard Chartered,” alieleza.

Alieleza hana tatizo na Jamhuri kwa kuwekwa mahabusu kwa muda wote aliokaa huko, kwa kuwa anaamini hatua hiyo ilichukuliwa kwa Jamhuri kupotoshwa na Benki ya Standard Chartered.

Alimuomba DPP kutumia mamlaka yake aliyopewa katika Kifungu cha 29(6) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 2016 kuagiza aachiwe huru ili achukue hatua katika kesi zake dhidi ya Benki ya Standard Chartered kupitia Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa.

“Iwapo nitaondolewa mashtaka yanayonikabili, itaniwezesha kuendelea na kesi nilizozifungua dhidi ya Standard Chartered na washirika wake ambapo nadai Sh trilioni 20, kiasi ambacho kitaiwezesha TRA kukusanya kodi kutoka kwenye hiyo fedha Sh trilioni 6,” alisema.

Katika barua yake, alieleza kuwa viambatishi vingine ni nakala ya tozo iliyokuwa imeandaliwa na Tanesco ikionyesha tozo zilizotakiwa kutozwa na IPTL, ambazo zilikuwa ndogo kuliko za kampuni nyingine.

Ameainisha pia kuwa tozo nyingine ni ya taarifa ya Dk. Camilo Schutte ya Oktoka 12, 2012 kwenda Benki ya Standard Chartered (SCB), Benki ya Standard Chartered (Hong Kong) Ltd (SCBHK) na Benki ya Standard Chartered Tanzania Ltd (SCBTZ) kuwa iwapo hawataondoa malalamiko yao ya kisheria dhidi ya Tanesco katika kesi ya ICSD namba ARB/10/20, Kampuni ya VIP itaibua madai ya zaidi ya dola milioni 485 kama gharama za usumbufu.

Pia ameambatanisha nakala ya taarifa yake kwa Benki ya Standard Chartered Tanzania Ltd na Jamhuri ya Juni 11, 2013 ikieleza kuwa VIP imechukua hatua ya kukata rufaa kwenye mahakama ya juu ya New York nchini Marekani kwa madai hayo ya dola milioni 485.

Ameambatanisha pia nakala ya Kampuni ya VIP yenye kumbukumbu namba Ref: VIPEM: JB/41/2013 kwenda kwa Gavana wa BoT ya Desemba 5,2013 kutoiruhusu PAP kulipwa fedha kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow kutoka BoT kwa niaba ya IPTL.

Nyingine ni nakala ya barua yenye kumbukumbu namba NC.53/135/085 ya Desemba 12, 2013 kutoka kwa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, Beno Ndulu ikimweleza Rugemalira kuwa kwa hati ya mahakama iliyotolewa Septemba 5, 2013 Serikali na IPTL malipo yote yameshatolewa kwenye akaunti ya Escrow na kuhamishiwa IPTL Novemba 28, 2013.

MASHTAKA YANAYOWAKABILI

Vigogo hao walifikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Juni 19, 2017, wakikabiliwa na mashtaka 12 yakiwemo ya utakatishaji fedha.

Rugemarila, ambaye ni Mkurugenzi wa VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL na Sethi ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa PAP, wanadaiwa kutenda makosa hayo katika Jiji la Dar es Salaam na nchi za Afrika Kusini, Kenya na India.

Miongoni mwa mashtaka yanayowakabili washtakiwa hao ni kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kughushi, kutoa nyaraka za kughushi.

Pia wanadaiwa kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh bilioni 309.

Washtakiwa wanadaiwa kati ya Oktoba 18, 2011 na Machi 19, 2014 Dar es Salaam walikula njama ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India.

Katika shtaka la kujihusisha na mtandao, washtakiwa hao wanadaiwa kati ya Oktoba 18, 2011 na Machi 19, 2014 jijini Dar es Salaam wakiwa si watumishi wa umma, walitekeleza mtandao wa uhalifu kwa lengo la kujipatia faida.

Sethi anadaiwa Oktoba 10, 2011 katika Mtaa wa Ohio, Dar es Salaam, akiwa na nia ya ulaghai, alighushi fomu namba 14 a ya usajili wa kampuni na kuonyesha yeye ni Mtanzania anayeishi kiwanja namba 887 Mtaa wa Mrikau Masaki wakati akijua ni uongo.

Baada ya kusikilizwa maelezo hayo ya pande zote, Hakimu Shahidi aliiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 24, kwa ajili ya kutajwa.
....
WAFUATAO WALICHOTEWA MABILIONI YA ESCROW KUTOKA KWENYE ACCOUNT YA RUGEMALIRA: KWA NINI HAWASHTAKIWI?

WANASIASA
Andrew Chenge (MB) CCM - Bilioni 1.6
Anna Tibaijuka (MB) CCM - Bilioni 1.6
Paul Kimiti (CCM) - Milioni 40.4
William Ngeleja (MB) CCM - Milioni 40.4
Daniel Yona (CCM). - Milioni 40.4

MAJAJI
Jaji Mujulizi - Milioni 40.4
Jaji Ruhangisa - Milioni 404.25

WATUMISHI WA UMMA
Mkurugenzi Mkuu TIC, Emanuel Daniel Ole Naiko - Milioni 40.4
Lucy Appollo (TRA) - Milioni 80.8
Dkt. Enos Bukuku (Mjumbe Bodi Ya Tanesco).
Philip Saiboko (RITA) - Milioni 40.4

VIONGOZI WA DINI
Askofu Msaidizi Jimbo Katoliki La Bukoba, Methodius Kilaini - Milioni 80.9
Askofu Msaidizi Jimbo Kuu Katoliki La DSM, Alphonce Twimannye Simon - Milioni 40.4

Mkurugenzi wa TAKUKURU wakati huo alisema kuwa kurudisha fedha zilizochotwa katika akaunti ya Tegeta Escrow hakumsafishi mtu dhidi ya tuhuma za uhujumu uchumi zinazomkabili na kusisitiza kuwa ni lazima sheria ichukue mkondo wake bila kujali cheo cha mtuhumiwa.

Swali ni Je mbona ni miaka mitatu sasa tangu Kalasinga Seth na James Rugemalira wakamatwe kwa tuhuma za uhujumu uchumi, mbona hawa washirika wakuu wa ufisadi huu bado wangali uraiani wakila maisha wengine bungeni na hata wengine Makanisani?

Kwa nini walioshirikiana uhujumu uchumi na Seth na Rugemalira wao wapo mtaani wanakula maisha Bungeni na hata Makanisani?

Kwamba kushtakiwa au kutoshtakiwa nayo inahitaji connection? Kwamba ukifanya uhujumu uchumi kama huna connection ujue utakamatwa na kushtakiwa lakini kama ukifanya ufisadi na uhujumu uchumi ila una connection za kutosha wewe utakuwa salama hutokamatwa wala kushtakiwa maana kwa connection yako ukiguswa tu wataguswa mpaka wakubwa waliostaafu ambao una connection nao? Hakika bongo kila kitu kinahitaji connection, hata ukifa ili msiba wako upewe air time connection inahitaji sana. Yani kwa connection tu leo wahujumu uchumi wengine wanakula maisha ndani ya CCM, ndani ya makanisa, ndani ya bunge, ndani ya taasisi mbali mbali, mitaani huku wahujumu uchumi wasio na connection wakinyea debe magerezani. Kabla huja hujumu uchumi jiulize kwanza, je una connection?

Wakati mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Kalasinga Habinder Sethi na Mfanyabiashara James Rugemarila wao wameendelea kusota rumande kwa mwaka wa tatu sasa kwa kile kinachoitwa eti ni kutokana na upelelezi wa kesi yao ya utakatishaji fedha kutokamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Hakimu Mwaikambo ameahirisha kesi hiyo hadi Oktober 10, 2019 na washitakiwa wamerudishwa rumande.
_
Mtemi Andrew Chenge, Mbunge wa Bariadi (CCM) aliwahi kusema hadharani kwamba "wakumkamata yupo lakini haoni mtu wa kumshitaki". Na kweli hadi leo si kukamatwa tu bali hata kushtakiwa hajashtakiwa.

Ni katika ufisadi huu tulimsikia Anna Tibaijuka ambaye ni Mbunge wa Muleba Kusini (CCM) akisema zile bilioni 1.6 alizochotewa na Rugemalira ni " tuhela twa mboga". Tukamsikia Chenge akisema alichopewa yeye ni vijisenti tu. Yaani kama bilioni 1.6 aliyopewa Change ni vijisenti tu hebu jiulize hao wengine ambao hawatajwi katika huu ufisadi walipewa nini? Na pengine ndio sababu ya Chenge kusema wa kumkamata yupo Ila haoni wa kumshtaki kwa kuwa anajua akishtakiwa ataenda kuchomoa betrii katikati ya hekaheka za uchotaji mafuta na wote wataungulia humo. Na pengine ndio sababu badala ya Chenge kukamatwa na kushtakiwa amepewa cheo cha kua Mwenyekiti wa Bunge katika Bunge na Serikali inayojinasibu kupambana na UFISADI.

Binafsi sina tatizo na kuwekwa ndani Seth na Rugemalira, tatizo langu ni KWA NINI WALIOSHIRIKIANA NA HAWA JAMAA WAPO KITAAN WANAKULA MAISHA na hata wengine tunawaona huko Bunge? Orodha ya washirika wa ufisadi huu iliwekwa wazi na kiwango cha pesa mafisadi wenza walichochotewa, wengine ni Maaskofu. Mbona wako uraiani.

William Ngeleja, Mbunge wa Sengerema (CCM) alitangaza kurudisha fedha alizochotewa, tukasikia kila mtu akizikana si TRA sio nani. Leo nani anajua zile fedha alizotapika Ngeleja ziko wapi?

Leo nasikia na Prof. Anna Tibaijuka naye kashikwa na kichefuchefu na kutangaza kutapika zile bilioni 1.6 (hela za mboga). Sijui nazo kila mtu atazikana?

Can you imagine watu wako gerezani miaka mitatu sasa kwa kile kinachoitwa upelelezi haujakamilika, alafu leo mtu anatokea na kusema njooni kwangu mtubu enyi wenye DHAMBI na kulemewa na mizigo, mlipe mpate UHURU kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi. Lazima tujiulize ni nani anachelewesha kesi hizi, ni nani anachelewesha ushahidi na upelelezi. Je ni upande wa upelelezi, serikali au Mahakama? Kwa nini hatua zisichukuliwe ikiwa kuna nia ya dhati?

Ni vigumu kuamini unaweza washitaki hawa bila kuwashitaki/kuwahusisha walioshirikiana nao ambao ushahidi wa nyaraka uliwekwa wazi.

Bwana yule Mungu aje amlipe kutokana na matendo yake!!

Mwaka wa tatu eti upelelezi haujakamilika, na watu kila siku wanaingia kazini/ofisini na mwisho wa mwezi wanalipwa mishahara na posho!!

Hata kama kweli walifanya makosa, ila kuwaweka watu ndani miaka mitatu huku kila wakati mkidai upelelezi haujakamilika, si kuwatendea haki hata kidogo. Leo mnawaambia watu watubu watubu nini, kazi ya Mahakama ni nini? Nini lengo lililojificha nyuma ya pazia la hii toba? Je zile Mahakama za mafisadi zinafanya kazi? Je tunatafuta kwa nguvu fedha kwa ajili ya kampeni za uchaguzi?

namuona Kalasinga Seth ameamua akubali ili aepuke mateso makali ya gerezani ila Rugemalira ameamua KAMA ni kufa basi wacha afe.

Amesimamia KWELI ya nafsi yake. Moyo wake umeota sugu, haogopi tena kulala chini, kuumwa na mbu, chawa, kunguni wala viroboto vya Jela. Ameheshimu nafsi yake na kukubali kuwa kila mtu ataonja mauti.

Huenda anaewasababishia USUMBUFU huu akafa kabla wao hawajafa (Mungu ni Msiri) sana.

Hata wale walioshindwa kuvumilia mateso makali ya gerezani na kuamua kutubu hata kama wanajua hawana makosa au walibambikiwa kesi na kwa kuona kuwa hata hukumu ikija toka hawatopewa HAKI kutokana na kesi na ushahidi kuingiliwa basi nao Mungu ni muaminifu atawalipia kisasi.

Mene Mene Tekel na Peres!

Remmy Cameroon
Sauti ya wasio na sauti
 
All TRUTH

JF-Expert Member
Nov 20, 2011
4,474

Ngoja tusubiri T6

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
53,178
2,000
Bila sheria kuchukua mkondo wake, ufisadi hautakwisha...

Mbata zaidi huenda baadhi ya mashtaka/tuhuma zinakigusa chama chetu pendwa au watu wake au maslahi yake...

Kuendelea na hizi kesi kwa kufuata haki itakuwa sawa na kujichimbia kaburi...
 
idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
23,976
2,000
Naona Ruge anataka kufukua Makaburi...

Kama anamaanisha anachokisema serikaki inaweza kumsaidia kwenye baadhi ya madai yake...

Hasa kuwatafuta watu waliopewa pesa kwenye masandarusi.!
 
Themagufulianz

JF-Expert Member
Apr 15, 2017
4,000
2,000
true.... ishakuwa hasara na wengine walioko kwenye hizi scandals hawagusiki... na hata hizo pesa hawana tena..

Serikali ije na terms nzuri washirikiane nae zipatikane zitakazopatikana na warudishe waliopewa etc ili aachiwe huru...

Mungu amjalie JPM huruma na uelewa zaidi katika hili kwakuwa system ya wakati ule ndio imefikisha haya mambo hapa
Maadam rais Magufuli amesamehe, wasamehewe waendelee na maisha yao.
P
 
Bad Man Tivu

Senior Member
Jan 16, 2019
146
250
"Sometime Mafisadi Wacha Magufuli Awabinye Tu Kila Mtu Abinywe Kivyake Mimi Nabinywa Kwenye Democrasia Wao Wanabinywa Kwenye Wizi Na Ufisadi"

Ingawa Na Yeye Ni Fisadi Wengine Watambinya Uko Mbeleni Atawajibika Pia.
Jamaa amesema chenge alyesema 1.6 B ni vjcent katunukiwa uenyekiti wa bunge kweny bunge la huyo huyo unyesema anwabinya mafisadi!!!WTF???
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom