Sijawahi wala sitawahi kuunga mkono au kushiriki kwenye ufisadi wala mafisadi

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,517
Wakuu,nalazimika kujibu,ingawa ni kwa ufupi,mwanaJF mwenzetu Troll JF aliyenituhumu kuwaunga mkono na kuwatetea mafisadi.

Kwenye Jukwaa hili la Siasa,mwanaJF huyo amenituhumu mimi pamoja na Mkuu barafu kumtetea na kumuonea huruma Mzee Rugemalila wa Escrow.

Pamoja na kwamba nimemjibu kwenye uzi wake huo,niwieni radhi ili nami nimjibu na kumtaka alete ushahidi wa anachokidai hapa. Nasema, with confidence,sijawahi wala sitawahi kuunga mkono au kushiriki kwenye ufisadi. Siivi na mafisadi,waropokaji,matapeli na wapotoshaji.

With due respect, Mkuu Troll JF huwa hana uwezo wa kusoma na kupambanua hoja tuziletazo. Kwakuwa amejaa uchama na kujianika kama kada mtiifu wa CCM,hukurupuka na kupotosha mada.

Binafsi,nimezungumzia suala la Escrow mara moja tu. Tena,ni juzi tu ambapo Mbunge Ngeleja alirejesha mgawo wake wa milioni arobaini toka kwa Mzee Ruge. Hoja yangu ilikosoa timing na sehemu alipozirudisha pesa hizo na athari kwenye kesi iliyo mahakamani. Sikutetea wala kumuonea huruma fisadi.

Tangu utoto wangu,na aina ya maisha niliyokulia,nachukia na kujitenga na wizi,ufisadi na jinai yoyote. Lakini,napenda mno kusema ukweli na kuwa huru kimtazamo. Dhana hiyo ya kuwa huru imenizuia kuwa na chama cha siasa kama mwanachama wake hadi sasa.

Namuomba na kumshauri Troll JF alete hapa ushahidi wa alichokidai. Pia,namshauri awe anasoma hata kwa kusaidiwa mada niziletazo zenye uhuru na ukweli. Tena,asiwe analeta siasa kwa kila jambo. Mwisho,namsihi kuepuka kulazimisha uadui au urafiki.
 
Mkuu kumbuka CCM wamezoeya kulipwa na mafisadi ili kutetea ufisadi.

Refer hizi pesa za ESCROW 2014 October makada hawa-hawa wa CCM walitokwa hapa mapovu ya damu kwa kutetea kuwa hizi pesa za ESCROW sio za umma, ila leo wamejikuta wanameza yale mapovu yao machafu na kusadiki kuwa hizi ni pesa za umma.
 
Mbona unatumia nguvu sana kujisafisha na tuhuma.

Mara ulipokuwa mtoto sie tuna uhakika gani ulipokuwa mtoto hukupenda wizi maana sio ajabu ulipokuwa mtoto ulikuwa mdokoni(nadhani)

Usitumie nguvu sana kujisafisha ndugu shutma ni kawaida kwa binadamu ila wengine wanaonekana wabaya kwa vile walikamatwa.

Kuna mtu alishasema 'kama Mungu asingesamehe basi mbingu zingekuwa wazi'
 
Haya ngoja tapitia hayo mauzi yenu ili niweze kujua ni yupi mkweli hasa kwenye suala la escrow, maana huwa mnatudanganya kwa kujifanya mnajua mambo!
 
Mbona unatumia nguvu sana kujisafisha na tuhuma.

Mara ulipokuwa mtoto sie tuna uhakika gani ulipokuwa mtoto hukupenda wizi maana sio ajabu ulipokuwa mtoto ulikuwa mdokoni(nadhani)

Usitumie nguvu sana kujisafisha ndugu shutma ni kawaida kwa binadamu ila wengine wanaonekana wabaya kwa vile walikamatwa.

Kuna mtu alishasema 'kama Mungu asingesamehe basi mbingu zingekuwa wazi'
Nakuhakikishia,sikutumia nguvu kubwa.
 
Hivi mkuu inakuaje unatumia mda wako mwingi kumjibu mtu kama yule wakati mwingine unatakiwa utulie iwe jibu tosha kwa mjinga.

"the different between stupidity and genius is that genius has its limit" Albert Einsten.
 
Mkuu,nisingekuwa Verified ningekaa kimya. Hata uongo na utapeli huaminiwa Mkuu.
 
alichoandika yule jamaa heading ni nzito kuliko content za thread yake.
maana ktk maelezo yake hayajaonyesha kile alichotuhumu kwenye heading.

ila kama kweli mnatetea mafisadi muache.
 
Back
Top Bottom