Mhe. Ngeleja, Mzee Rugemalira amekukosea nini hadi 'umhujumu' hivi?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,196
25,515
Fact No. 1: Katika urafiki wenu, Mzee Rugemalira alikupa milioni zaidi ya 40 mwaka 2014.

Fact No. 2: Pesa alizokupa Mzee Rugemalira zilitokana na mgawo wake kwenye masuala ya hisa na Escrow kwa ujumla.

Fact No. 3: Ni wewe tu ndiye unayeujua ukweli kama ulifahamu chanzo cha fedha ulizopewa na Mzee Ruge au la na mlichozungumza hadi akakupa.

Fact No. 4: Mzee Rugemalira ameshaburuzwa mahakamani kwa mashtaka yahusuyo sakata la Escrow na ameyakana mashtaka yake yote.

Fact No. 5: Kisheria, Mzee Ruge kukana mashtaka ni kuwa na nia na wajibu wa kutetea uhalali wa fedha zake na mgawo wote alioufanya.

Fact No. 6: Kama waliogawiwa ukiwemo Ngeleja, wanataka kurejesha pesa, wanapaswa kuzirejesha kwa aliyewapa ambaye ni Mzee Ruge ili azitetee pesa zake mahakamani anaposhtakiwa.

Fact No. 7: Kuzirejesha pesa Serikalini ni 'kuchongea' kuwa chanzo hakikuwa halali na hivyo kuweka ukakasi hadi kwenye mashtaka dhidi ya Mzee Ruge.

Kwa urafiki wenu na muda wote uliopita tangu ugawiwe mwaka 2014, kwanini wafanya haya ya marejesho sasa? Huku si 'kumhujumu' Mzee Ruge?
 
siku ukinikana mbele ya rafiki zako nami nitakukana....................................................................
 
Aliyetoa mwingine,anayerudishiwa mwingine.
Vipi kuhusu riba ya miaka mitatu?
Ina maana mgawo uliolipiwa kodi unapaswa kuongezewa kodi?
Ngeleja katika hili umeiabisha taaluma yako ya sheria,kwani hata logic za kawaida zinakataa.
TRA rudisheni hizo pesa kwa Ngeleja ili azirudishe alikozitoa na sheria ya maadili ya utumishi wa umma ichukue mkondo wake.
TRA isitumike kutakatisha watu waliokuwa wamejificha,otherwise TRA itakuwa ni sehemu ya kutakatisha fedha haramu zinazohojiwa na serikali kupitia mahakama.
 
Binadamu tunaruhusiwa kutubu.

Awasaidie tu takururu kuwapa habari zote na kuwataja wote na kila kitu ilikuwaje na ikawaje.

Cheo chake kileeeeeeeeeeeeeee
 
amezirudisha kwenye escrow account zilikotoka zikaendelee kusubiri maamuzi.
 
Back
Top Bottom