Jana Alkhamisi usiku kulikua na kipindi cha MALUMBANO YA HOJA. mada ilikuwa MJADALA JUU YA UAMUZI WA BUNGE KUTOKURUSHA VIPINDI VYA BUNGE MOJA KWA MOJA. wageni wa meza kuu walikua muh. mnyika, afisa wa bunge na mwananchama wa ccm.
wachangiaji waliokua ukumbini walitoka katika vyama mbalimbali vya kisiasa pamoja na asasi a kiraia. mjadala ulikua mzuri. wapo waliyounga mkono kutooneshwa kwa bunge moja kwa moja na waliyo wengi hawakuunga mkono usitishwaji wa kurusha vipindi vya bunge moja kwa moja.
muheshimiwa mnyika ni kijana mwenye akili na ni mzuri wa kujenga hoja. ni mtafiti mzuri kwa sababu kawaida yake yake huwa hachangii kitu bila ya kukifanyiwa utafiti. anatekeleza usemi usemao "no research, no right to speak".
licha ya kupenda michango ya mnyika, huwa nattizwa na jazba anayoitumia pindi anapo changia. muh mnyika jana alipandwa na hasira hadi akawa anazungumza kwa tabu sana kutokana na kukosa pumzi. alikua tayari kuzipiga na mjumbe wa ccm. walipopewa dkk za mwisho kuhitimisha, mnyika aliongea kwa jazba sana hadi waendesha kipindi wakawa wanaingilia kati kumtuliza. walimuambia muda umekwisha lkn aliendelea kuzungumza huku akipandisha midadi.
ndugu mnyika, ukitaka kufikisha jambo lako vizuri kwa ufasaha, tulia na jiepushe na jazba. jana ulidhihirisha usivyo na subira katika mijadala! si jambo zuri hata kidogo. wewe ni jembe! wewe ni kichwa! nakukubali1 lakii ili ufanikiwe zaidi, tulia unapo jenga hoja. utatisha zaidi.
nimetoa ushauri huu nikitanguliza uzalendo na maslahi ya taifa. sina chuki na mnyika bali ni mmoja kati ya mashabiki wake.