Haitofautiani na kale kakipima joto ka ITV na Redio one ni upotezaji wa muda tu. Maswali elekezi tupu. Mfano kipima joto kinauliza " Kukithiri kwa uchafu katika soko la---je, haihatarishi afya ya walaji'? Sasa hilo swali kweli au kwa sababu lina alama ya kuuliza. Sasa likiwa swali la kisiasa na hasa linapotakiwa kuonyesha serikali imeshindwa linaulizwa hivi, "Wanafunzi kusomea chini ya miti, nani alaumiwe?" Sasa hapo unataka jibu gani na ili iwe nini! Kwanini swali kama hilo ITV isiliweke ifuatavyo, "Wanafunzi kusomea chini ya miti, nini kifanyike? Unajua vyombo vya habari vinaweza kujenga au kubomoa kama vitakuwa haviko wazi. Kama chombo cha habari kina mlengo wa chama fulani au dini fulani kijiache wazi-ni haki ya chombo chochote cha habari kuwa na upande,mfano gazeti la Tanzania Daima ni gazeti la propaganda la chadema kama lilivyo Uhuru kwa CCM. Hivyo, haitatokea hata siku moja Tanzania daima ikaisifia CCM na serikali yake wala haitatokea gazeti la Uhuru kuisifia chadema na kuiponda serikali. Hiyo ndio tunataka, sio chombo cha habari kinaonekana wazi kiko upande gani lakini bado kinataka tuamini hakina upande-huo ni udhaifu.