Mhe Mnyika, hapa unaniangusha - Mfumuko wa bei

Majoja

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
611
185
Mnyika azidi kucharukia mfumuko wa bei

Na Tamali Vullu

(Tanzania Daima 24th Oct 2011)

"Kutokana na kukithiri kwa mfumuko wa bei za bidhaaa mabali mbali mchini. Mbunge wa Ubungo John Mnyika,anakusudia kuwasilisha muswada binafsi Bungeni ili Serikali itunge sgeria ya kudhibiti bei za bidhaa muhimu.

Akizungumza na waandishi wa hahari jijini Dar es salaam, Mnyika alisema kutokana na mfumuka wa bei za bidhaa muhimi, hali ya maisha ya Watanzania imezidi kuwa ngumu kila kukicha.
Alisema hali hiyo ikiachwa hivi hivi ni hatari kwa uchumi wa nchi na kwamba Taifa linaweza kuingia katika machafuko makubwa."

My Take:

Mtazamo wa utatuzi wa mfumuko wa bei nchini nasikitika kucomment kuwa si wa kisomi sana na nilitegemea fikra zaidi kutoka kwa Mh. mnyika juu ya hili.Nakubaliana na Mnyika as far as the EFFECTS za mfumiko wa bei na si zaidi ya hapo.

Si jambo linaloeleweka kuwekea sheria mfumuko wa bei-to the layman yes.
Tulikubali wenyewe zaidi ya miaka ishirini na tano iliyopita juu ya kutumia nguvu ya soko katika kuendesha uchumi.Sijui ni wangapi wanaoikumbuka SCOPO ya Ndg Wilfred Mwabulambo.

Ilifanya kazi tu katika misingi ya ujamaa na controlled economy. Leo tukipanga aei za vitu muhimu wakati uzalishaji hakuna hilo halieleweki wala si sustainable. Nilitegemea Mh Mnyika akazanie UZALISHAJI mali wa bidhaa hizo kwa nguvu zote na kwa tija ili bei ziweze kushuka.
Leo ukipangia bei ya sukari kuwa Tshs 1,900 wakati demand yake inadictate at Tshs 2,500 ni kujidanganya.

Bidhaa inakuwa muhimu kwako pale tu unapoweza kumudu kuinunua, bidhaa hiyo ikiwa nje ya uwezo wako ina-cease kuwa na umuhimu kwako.
Wabunge wetu vijana nawashauri msome sana hizi economical dynamics ili muweze kutumika vizuri katika vyombo mnavyo wawakilisha wananchi.

Kikubwa zaidi ni serikali yenyewe kubana matumizi yake ili matumizi yalingane na kipato chake. Kinachoelekea kuwa kimetokea (mfumuko wa bei)ni kuwa Serikali inaendelea kuchapisha fedha zisizo na backing ya uzalishaji, hivyo more money chasing the few commodities at large.Serikali ikiendelea na msimamo huu tuatuwa na pesa nyingi sana kwenye mzunguko wa biashara, fedha ambazo si halali kuwepo.

Nina uhakika economists waliobobea wana cheka juu ya hii suggestion ya Mh Mnyika kwa vile haitekelezeki.
 
VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,195
1,336
Hii it never works.., huwezi kuleta wawekezaji na ushindani at one hand alafu kwa upande mwingine uwapangie bei, hii italeta scarcity na magendo.

Cha kufanya ni kuongeza production.., tena Ndugu Mbunge angepeleka muswada wa kuzuia huu ugawaji ardhi kwa wawekezaji ili walime bali hii ikiwa mikononi mwa jamii / state / vyama vya ushirika na kuzalisha surplus bei itashuka.. Alafu kumbuka hizi taasisi zitakuwa pale sio kwa ajili ya profit bali service.., hivyo basi wanaweza kuzalisha bidhaa za kutosha kwa bei nafuu kwa mwananchi.

Uwekezaji uletwe kwenye issues kama viwanda na usindikaji sababu huu utaleta ajira kwa watu
 
tembaisdor

Member
Sep 19, 2011
29
7
Mh. Mnyika hebu angaika na jimbo lako kwanza umetusahau ss tulikuchagua achana na hiyo idea haitekelezeki. Barabara mbovu, uchafu, maji n.k
 
VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,195
1,336
Mh. Mnyika hebu angaika na jimbo lako kwanza umetusahau ss tulikuchagua achana na hiyo idea haitekelezeki. Barabara mbovu, uchafu, maji n.k

Hapana mkuu anaweza kufanya yote na mengi zaidi ya hayo..., lakini sio anachotaka kufanya sasa, wewe hakikisha production inakuwa kubwa zaidi au kulingana na demand basi bei itashuka tu.., Siwezi kukuuzia wewe X kwa tshs 500/= wakati najua nikienda kwa kujificha Y anaweza kulipa 1,000/=; lakini kama mimi nauza kitu kwa Tshs 500/= wakati wengine wanauza kwa tshs 300/= basi sina budi kushusha bei.

Ila tofauti yangu mimi na wengine wengi badala ya serikali kutegemea hii production ifanywe na private sectors (au wawekezaji) nataka hii itoke serikalini / vyama vya ushirika (hususan kwenye kilimo na mazao ya chakula).
 
Gad ONEYA

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
2,633
168
Tatizo ni kwamba kwa kwetu bongo wafanyabiashara wengi hawako honest na huwa wanatafuta hata asilimia 100 au zaidi ya faida na kwa kuwa walaji ni walalamikaji katikanchii ambao huwa hawawezi kufanya movement yoyote...lazima kuwe na sheria kama hizi japo zinakuwa anti-free market! Lakini pia, nchi kama yetu vitu kama hivi lazima viwepo kwani haiwezekani kila mtu ana-peg bei yake kwenye dola halafu watu wakae kimya eti soko huria. Tazama karo za shule zetu sasa hivi baadhi ya shule na vyoo ambavyo viko tz vinachaji karo kwa dola tena kwa watanzania ambao hawauzi chochote kuipata hiyo dola!
 
Rejao

JF-Expert Member
May 4, 2010
9,232
4,042
Hivi Mnyika ana taaluma gani? Jamaa anaweza kuwa na degree ya LANGUAGE sijui ndio Linguistic! Mambo ya Inflation atayajulia wapi?
 
Lua

JF-Expert Member
May 19, 2011
704
305
Mh. Mnyika hebu angaika na jimbo lako kwanza umetusahau ss tulikuchagua achana na hiyo idea haitekelezeki. Barabara mbovu, uchafu, maji n.k
kwani bei ya bidhaa ikishuka itakuwa imemsaidia pia mkazi wa jimboni kwake na hata pia watz wote, na khs maji siku ya tarehe 5/9/2011 mbunge aliandamana na wakazi wa ubungo hadi makao makuu ya dawasco na kukutana na afisa mtendaji mkuu ndg midala kilifanyika kikao cha shinikizo la nguvu ya umma kwa masaa 5 na hali ya maji kwasasa wananchi wa ubungo wanasema kuna mabadiliko makubwa na pia huyo midala atakuwa na ziara na mbunge mwanzo wa mwezi wa 11 kwa ajili ya kutazama hali ya upatikanaji wa maji ktk jimbo la ubungo, khs barabara kuna zinginemeshanza kutengenezwa kama ya temboni hadi kwa abbas, brbr ya milenia ya3, golani na nk. na hili jambo linawezekana la kuwa na sheria ya bei na sio wakina pinda kusema kuwa sukari ishushwe na hakuna anayeshusha zaidi ya kupanda na ni kauli za kisiasa na pia uzalishaji ni mwingi na ndio maana zinapelekwa kuuzwa nchi za nje, mahindi watu wanalima, mpunga pia unalimwa kwa wingi, tunayo gesi asilia, nk hivyo vyote kama tukuwa na sheria inayosimamia tutafanikiwa na si kuwa soko holela, inayosababisha leo watz tunalipa ada ya chuo in terms of dollar, na hata bidhaa leo unakwenda kwy maduka mengine unanunua bidhaa kwa dollar. hii ni kutokana na soko holela.
 
VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,195
1,336
Tatizo ni kwamba kwa kwetu bongo wafanyabiashara wengi hawako honest na huwa wanatafuta hata asilimia 100 au zaidi ya faida na kwa kuwa walaji ni walalamikaji katikanchii ambao huwa hawawezi kufanya movement yoyote...lazima kuwe na sheria kama hizi japo zinakuwa anti-free market! Lakini pia, nchi kama yetu vitu kama hivi lazima viwepo kwani haiwezekani kila mtu ana-peg bei yake kwenye dola halafu watu wakae kimya eti soko huria. Tazama karo za shule zetu sasa hivi baadhi ya shule na vyoo ambavyo viko tz vinachaji karo kwa dola tena kwa watanzania ambao hawauzi chochote kuipata hiyo dola!

Mkuu huku ni ku-tackle tatizo kwa njia ambayo sio sahihi.., badala ya kulazimisha mtu auze sukari kwa 2,500/= hakikisha supply inaongezeka.., alafu kumbuka hakuna mfanyabiashara honest popote pale.., na hata kule kwa wenzetu competition inakuwa kubwa sababu ya purchasing power ya watu ni kubwa kwahiyo hata ukiuza vitu kwa bei ndogo sana sababu ya volume kubwa unayouza bado unapata faida..

Kwahiyo mkuu ndio maana nikasema na nitasema tena na kuendelea kusema.., hii serikali iache hadithi za Abunwasi za kuleta wawekezaji hususan kwenye kilimo na ijitose yenyewe na kuanzisha vyama vya ushirika na kwa manufaa ya wananchi walime na kuhakikisha wanauziwa wananchi kwa bei ndogo sana na kinachobaki kuuza nje faida irudi kusomesha na kutibu wananchi wake bure...

Zaidi ya hapo hizi ni story za Abunwasi ambazo mwisho wake ni kupingwa bungeni kwa Sioooo ya Nguvu zote lazima tuweke plan from A to Z jinsi ya kufanya mambo na tuwe na vision ni wapi tunataka kufika
 
Lua

JF-Expert Member
May 19, 2011
704
305
ulipaswa wewe kusema taaluma yako ndio uulize ya mwezio kwani unaweza ukabisha kumbe fani yako ni hotel management.
Hivi Mnyika ana taaluma gani? Jamaa anaweza kuwa na degree ya LANGUAGE sijui ndio Linguistic! Mambo ya Inflation atayajulia wapi?
 
VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,195
1,336
Another point to remember...!!! kuna mazao yanaozea mashambani huko vijijini cha kufanya ni kushinikiza serikali ipeleke miundombinu mpaka huko ili mazao yaweze kufika sokoni kwa urahisi uone kama bei hazitashuka automatically...

Ni mengi ya kuyafanya na yote yanakuja kwenye jibu moja tu.., Serikali haifanyi kazi yake wala hakuna vision wala objectives ya nini wanatakiwa wakifanye.., nchi inaendeshwa kwa auto-pilot (ila kupanga bei sio solution) it has never worked anywhere
 
Majoja

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
611
185
Tatizo ni kwamba kwa kwetu bongo wafanyabiashara wengi hawako honest na huwa wanatafuta hata asilimia 100 au zaidi ya faida na kwa kuwa walaji ni walalamikaji katikanchii ambao huwa hawawezi kufanya movement yoyote...lazima kuwe na sheria kama hizi japo zinakuwa anti-free market! Lakini pia, nchi kama yetu vitu kama hivi lazima viwepo kwani haiwezekani kila mtu ana-peg bei yake kwenye dola halafu watu wakae kimya eti soko huria. Tazama karo za shule zetu sasa hivi baadhi ya shule na vyoo ambavyo viko tz vinachaji karo kwa dola tena kwa watanzania ambao hawauzi chochote kuipata hiyo dola!
Gad , kuendesha uchumi inahitaji taaluma na si hisia.
The Law of Demand and Supply ndio kitu kinachocheza katika soko huria, kama kuna bidhaa zipo chache bei inapanda automatically na hakuna cha mfanya biashara wala mchuuzi.
Price ya kitu ina kuwa determined at the source.
Hata hizo shule zikiwa nyingi za kutosha na kuzidi bei ya karo ni lazima itashuka tu.
Jaribio lolote la kufix bei basi unasukumiza bidhaa hiyo underground na itauzwa kwa bei mbaya zaidi.
 
John Mnyika

JF-Expert Member
Jun 16, 2006
712
1,238
Mnyika azidi kucharukia mfumuko wa bei

Na Tamali Vullu

(Tanzania Daima 24th Oct 2011)

"Kutokana na kukithiri kwa mfumuko wa bei za bidhaaa mabali mbali mchini. Mbunge wa Ubungo John Mnyika,anakusudia kuwasilisha muswada binafsi Bungeni ili Serikali itunge sgeria ya kudhibiti bei za bidhaa muhimu.

Akizungumza na waandishi wa hahari jijini Dar es salaam, Mnyika alisema kutokana na mfumuka wa bei za bidhaa muhimi, hali ya maisha ya Watanzania imezidi kuwa ngumu kila kukicha.
Alisema hali hiyo ikiachwa hivi hivi ni hatari kwa uchumi wa nchi na kwamba Taifa linaweza kuingia katika machafuko makubwa."

My Take:

Mtazamo wa utatuzi wa mfumuko wa bei nchini nasikitika kucomment kuwa si wa kisomi sana na nilitegemea fikra zaidi kutoka kwa Mh. mnyika juu ya hili.Nakubaliana na Mnyika as far as the EFFECTS za mfumiko wa bei na si zaidi ya hapo.

Si jambo linaloeleweka kuwekea sheria mfumuko wa bei-to the layman yes.
Tulikubali wenyewe zaidi ya miaka ishirini na tano iliyopita juu ya kutumia nguvu ya soko katika kuendesha uchumi.Sijui ni wangapi wanaoikumbuka SCOPO ya Ndg Wilfred Mwabulambo.

Ilifanya kazi tu katika misingi ya ujamaa na controlled economy. Leo tukipanga aei za vitu muhimu wakati uzalishaji hakuna hilo halieleweki wala si sustainable. Nilitegemea Mh Mnyika akazanie UZALISHAJI mali wa bidhaa hizo kwa nguvu zote na kwa tija ili bei ziweze kushuka.
Leo ukipangia bei ya sukari kuwa Tshs 1,900 wakati demand yake inadictate at Tshs 2,500 ni kujidanganya.

Bidhaa inakuwa muhimu kwako pale tu unapoweza kumudu kuinunua, bidhaa hiyo ikiwa nje ya uwezo wako ina-cease kuwa na umuhimu kwako.
Wabunge wetu vijana nawashauri msome sana hizi economical dynamics ili muweze kutumika vizuri katika vyombo mnavyo wawakilisha wananchi.

Kikubwa zaidi ni serikali yenyewe kubana matumizi yake ili matumizi yalingane na kipato chake. Kinachoelekea kuwa kimetokea (mfumuko wa bei)ni kuwa Serikali inaendelea kuchapisha fedha zisizo na backing ya uzalishaji, hivyo more money chasing the few commodities at large.Serikali ikiendelea na msimamo huu tuatuwa na pesa nyingi sana kwenye mzunguko wa biashara, fedha ambazo si halali kuwepo.

Nina uhakika economists waliobobea wana cheka juu ya hii suggestion ya Mh Mnyika kwa vile haitekelezeki.

Majoja,

Nashukuru sana kwa maoni yako. Natamani sana kama kuna mwanahabari ambaye alikuwepo kwenye mkutano wangu wa jana aeleze kwa kina zaidi niliyoyangumza jana. Suala la kupeleka muswada wa sheria ya udhibiti wa bei ya bidhaa muhimu ilikuwa ni moja tu ya orodha ndefu ya njia nilizozieleza ambazo Tanzania inapaswa kuzichukua kama sehemu ya hatua za dharura za kukabiliana na kupanda kwa gharama za maisha ambako kwa sehemu kubwa kumechangiwa na mfumuko wa bei na kuporomoka kwa sarafu ya Tanzania. Suala la kuongeza uzalishaji nililisisitiza na kutaka hatua za dharura kwa msukumo wa Rais na Bunge. Katika kuongeza uzalishaji wa ndani naamini katika kupanua fursa kwa wazalishaji wadogo na wa kati katika sekta za kilimo na viwanda kama jambo la haraka. Hapa tutashughulikia tatizo la kutokuwa na uwiano wa urari wa kibiashara (balance of payment) ambapo sasa taifa letu ni la wachuuzi badala ya wazalishaji; tunanunua kuliko tunachouza. Lakini nilikwenda mbele zaidi kwa kueleza kwamba kutokana na matatizo katika nchi za magharibi hasa athari za mdodoro wa uchumi duniani na sasa matatizo ya kifedha Eurozone na udhaifu wa utegemezi wetu toka nje; hali ya kifedha ya nchi ni mbaya kwa kuwa serikali haijafunga mkanda- bado kuna ubadhirifu, ufisadi na matumizi mengine ya anasa wakati hali ya mapato hairidhishi. Kwa vyovote vile hatua za dharura zinahitajika na nikatoa mwito kwa Rais Kikwete akutane na tume ya mipango na baadaye akutane kwa dharura na baraza la mawaziri kuweka msukumo wa haraka kwa kuwa tunapokwenda kama taifa hali itakuwa tete; mfumuko wa bei umefikia 16.8%, kubadili dola moja kwenda shilingi ni 1700. Ni maoni yangu kwamba hatuwezi kuamini Wizara ya Fedha na Benki Kuu pekee katika kushughulikia hali hii; tunapaswa kuunganisha nguvu ya wadau wetu wote: wataalamu, sekta binafsi nk. Uongozi Mkuu wa nchi unapaswa kutoa msukumo unaohitajika kufikia azma hii. Naelewa kwamba gharama za vyakula na nishati zinamchango mkubwa sana katika mfumuko wa bei. Hata hivyo, ieleweke kwamba matatizo yetu ya chakula ni zaidi ya uzalishaji na ukame; tuna tatizo pia la usambazaji. kwa kuwa hivi sasa wakati ambapo kuna maeneo yana njaa na maeneo yenye chakula cha bei juu; kuna maeneo ya nchi yetu chakula kinaoza au kinauzwa bei chee. Ushahidi wa kwamba kuwa tuna matatizo ya kimfumo na kiuongozi ni kuwa hata chakula kutoka hifadhi ya taifa ambacho kilitolewa kwa maelezo kuwa kinakwenda kupunguza bei kwa gharama yako na yangu lengo husika halijafikiwa; bei bado iko juu na sehemu ya chakula hicho kinatoroshwa na kuuzwa kinyemela nje ya nchi. Matamko ya viongozi pekee ya kwamba bei ya sukari na sembe iwe kwa kiwango kilichotangazwa hayajasaidia. Walau kukiwa na sheria, tutapata nguvu nyingine ya kuwabana badala ya kutegemea kauli zao za kisiasa pekee. Tunaona kwamba pamoja na udhaifu wa EWURA katika upangaji wa bei elekezi na pia serikali kushindwa kupunguza kodi kwa kiwango tulichopendekeza bungeni na kuweka mifumo mizuri zaidi ya haraka ya uagizaji wa mafuta; bado walau bei elekezi inayotolewa inafuatwa kwa kuwa hatua hizo zinafanyika kwa misingi ya sheria sio kauli tu za kisiasa za viongozi. Hivyo; pamoja na taasisi zetu za fedha kuchukua hatua za kisera kudhibiti mfumuko wa bei na kuporomoka kwa shilingi; pamoja na hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa na Rais, Bunge na vyombo vingine za kimfumo na kitaasisi za kuboresha uzalishaji na usambazaji hususani wa vyakula na nishati (umeme, gesi asilia), tunahitaji pia kuweka mifumo ya kisheria. Mimi ni muumini wa mrengo wa kati, naamani katika soko la kijamii- yaani uchumi mchanganyiko; kwa kuweka pamoja misingi ya dola kuhusika katika uchumi (ambayo hutumiwa zaidi katika ujamaa) na uhuru wa soko (ambao hutumiwa zaidi katika mifumo ya kiliberali na kibepari). Hata hivyo, nasikitika kwamba nchi yetu haifuati ujamaa wala soko huria; ni nchi yenye mfumo wa soko holela. Wakati nikitoa mwito kwa Rais na Bunge kuzisimamia taasisi nyingine na kuongoza sekta binafsi na umma kunusuru hali ya mambo kwenye uzalishaji na usambazaji ili kupunguza mfumuko wa bei na kuporomoka kwa shilingi yetu; napenda pia pawepo na nguvu za kisheria hususani katika bidhaa chache na muhimu; Tanzania haitakuwa nchi ya kwanza kufanya hivyo; hata baadhi ya nchi zenye kuamini katika soko huria, serikali na dola huingilia kati pale soko linaposhindwa au pale ambapo kuna ulazima wa kulinda maslahi ya umma. Ugumu wa maisha unaochangiwa na kupanda kwa bei na gharama ni tishio kwa uchumi na usalama wa nchi na wananchi ni suala ambalo tunahitaji kuunganisha nguvu kulishughulikia; tusipoziba ufa tutajenga ukuta. Na kwa kweli ni kati ya mambo ambayo wananchi wa jimbo la Ubungo wamenituma niwawakilishe, nilihoji suala hili kwenye mikutano ya hadhara, na nimepata ridhaa yao. Tuendelee kujadiliana kupata maoni zaidi

JJ
 
Mundali

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
749
164
Thanks Mnyika. Mawazo mazuri sana inahitaji wenye uwezo wa kufikiri kama wewe kuyajadili na kuyatenda. Lakini kwa magamba mmmh! Yangu macho.
 
Topical

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
5,174
931

Mkuu maji goba mkuu hiyo ni ahadi iliyosimama..

Achana bei ya bidhaa maji goba please
 
Narubongo

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
2,769
2,724
hii idea ya mnyika kuna nchi zinaitumia mfano malaysia [mixed economy] govt wanacontrol bei za bidhaa basic kama sukari, mchele etc huwa hazipandi na hata zikipanda basi ni baada ya miaka 3/4/5 na ni <8%, nadhani jk alipouliza wampe mbinu walizozitumia mpaka kufika walipo ni lazima walimwambia na hili

go on mnyika
 
Majoja

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
611
185
Asante sana Mh. Mnyika kwa mawazo yako na ufafanuzi wako.
Nitayapitia kwa kina mawazo haya kabla ya kuchangia zaidi.
Sisi wengine tulikuwepo toka enzi za "mwendo wa kuruka" wakati wa awamu ya kwanza.Hata hivyo nakupongeza sana kwa mchango wako wa haraka.
 
KERENG'ENDE

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
398
31
Nimeupenda mjadala huu! Mnyika umeeleza ukweli na umefanya vizuri kujitokeza kujibu hoja hii kwa sababu wa kosoaji wa lileta taarifa ambayo sio sahihi na uka onekana umefikiria kwa kiwango cha chini sana na kupata hitimisho la sheria ya udhibiti wa bei.Ni sahihi kabisa kuangalia uzalishaji wetu na kwa asilimia kubwa kilimo ndio msingi wetu ingawa hauja pewa mikakati ya kutosha, wa kubwa walidhani mpango wa kilimo kwanza ungelinyanyua taifa baada ya kuandika mipango yake na kuisoma kwenye majukwaa yakisiasa na wengine wa kadhani kilimo kwanza ni kununua ma power tiller hapo ndipo tulipo chemka na tuna hitaji mjadala mkubwa kuondokana na hii dhana.........

Nchi imegeuka ya matapeli na madalali wanao takakuuza zaidibila kuzalisha ndani ya nchi wanauza zaidi bila kununua ndani ya nchi hapandipo utapeli unapoanza wa kubwa wanazidi kuwa wezi na kuficha matatizo yao wana issue parallel notes kwenye mzunguko wa uchumi bila sababu za msingi za kiuchumi wa kitolea maelezo eti noti za zamani sio bora hii haini ingii akilini kabisa nahii sababu ya ubora sio ya msingi kabisa kwa sababu noti mpya ndio mbovu kuliko zazamani lakini haya ni madili ya wakubwa.......

Dollarlization mfumo mchafu katika uchumi BOT wamekaa kimya kwasababu wanamaslahi yao nyuma hii nihatari nalo mnataka mlikalie kimya kweli tuta kuwa hayawani ...Mkulo aliwahi kusema wakati anawakilisha budget yake kuwa bei zote zitakuwa in TZS tukaona anaakili sasa sijui kulitungiwa sheria ya jambo hili au ulikuwa mkakatiwa kupitisha budget maana hapa kuna mikakati mingi kamavile ya kina Jairo.Kweli nalo tusitungie sheria tuliachekamal lilivyo hapana lazima ifike sehemu kuwepo na taratibu ikikiukwa maana yake nikosa na mkosaji ahukumiwe kulingana nasheria. Napo hapa kuna dili lawakubwa......

Mafuta yamekuwa mwiba kwa ustawi wa jamii maana bei zake hazieleweki mmeachia UWURA ambao meno yao ni ya kuazima hapa napokitendawili kingine mpaka bwanamkubwa aje kutegua.Bei ya mafuta ina panda kiholela na athari zake ni mtambuka kila kitu kina panda bei, Wakulima wa najitahidi kulima mazao yao wanashindwa kuyatoa mashambani nakupeleka kwenye masoko ili wauze angalau kwa bei ya kuwa lipa kwasababu usafiri upo juu matokeo yake matapeli/madalali wanaenda kuwa langua na kukimbizia nje ya nchi wakiacha watu wetu maeneo ambayo mazao hayakupatikana wana kufa na njaa nalo wakosoaji wanaona hilina tija mnyika akae kimya .....

Tusaidiane nchi hii ni yawote msiwakosoe wabunge na kuwabana wa baki majimboni kwao tuu acheni wa fikirie nje ya box ili watusaidie wote tulie kaliwa na matapeli....
 
mwana wa africa

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
548
128
nadhania mnyika anayo hoja ya msingi ya kutaka kama taifa tutazame sera na taaisi zetu zinazosimamia uchumi kama zinalichukua tatizo hili kama bomu linalijijenga taratibu ndani ya taifa au la. hii ni ajenda ya kujadili na kuiboresha ili hata atakapokuwa anaiwasilisha bungeni kama hoja binafsi iwe na mashiko. moja ni kuangalia mwenendo wa uchumi wetu amabao kwa kiasi kikubwa watanzania wanaanza kutupwa nje ya ulingo wa umiliki wa uchumi unaolenga kuwaondolea umasikini na kukuza vipato vyao. upaikanaji na umilikaji na wa arhi una urasimu mkubwa. na tumejikita zaidi na wakekezaji kutoka nje . tuone ni kwa kiasi gani tunawawezesha wazalishaji wa ndani na uwekezaji ambao utakuwa na impact ya moja kwa moja kwa watanzania wa kawaida.tujikite katika uzalishaji wa mazao ya chakula hasa nafaka kwa kwa kuwajengea uwezo wakulima wetu kupitia vyama vya ushirka na taasisi nyingine za fedha.
 
NewOrder

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
2,045
2,639
Hii it never works.., huwezi kuleta wawekezaji na ushindani at one hand alafu kwa upande mwingine uwapangie bei, hii italeta scarcity na magendo.

Cha kufanya ni kuongeza production.., tena Ndugu Mbunge angepeleka muswada wa kuzuia huu ugawaji ardhi kwa wawekezaji ili walime bali hii ikiwa mikononi mwa jamii / state / vyama vya ushirika na kuzalisha surplus bei itashuka.. Alafu kumbuka hizi taasisi zitakuwa pale sio kwa ajili ya profit bali service.., hivyo basi wanaweza kuzalisha bidhaa za kutosha kwa bei nafuu kwa mwananchi.

Uwekezaji uletwe kwenye issues kama viwanda na usindikaji sababu huu utaleta ajira kwa watu

Nadhani huelewi vizuri maana ya Mb. Mnyika. Labda una ufahamu kuhusu uchumi lakini unajua kitu kinaitwa "consumer protection"?? Kwa taarifa yako tu, EWURA ni moja ya taasisi zinazoangalia hilo. Kushindwa au kufanikiwa kwa EWURA ni topic nyingine lakini ndiyo taasisi inayoangalia bei za nishati na maji. Sijasikia watu walilalamikia kupungua kwa bei bali kuongezeka.

Point ya mnyika ni hii - kuna bidhaa muhimu kama sukari, unga, mafuta ya kupikia, madawa ya mifugo na binadamu. Vitu ambavyo ni basic needs. Hazungumzii mvinyo, almasi, dhahabu, nk. Huko tulikuiga mfumo huria, bidhaa muhimu au zina kodi ndogo au hazina kabisa. Hiki kitafanya wawezekazi wawe wengi katika uzalishaji wa bidhaa hizo. Au serikali ianze kuwekeza katika uzalishaji wa bidhaa hizo. Ukitaka kuelewa hili vizuri, pandisha bei ya sembe ktk nchi za Zambia na Zimbabwe!!

Bidhaa muhimu lazima ziwe regulated na serikali. Serikali ina wajibu kwa wananchi wake, ndio maana hata nyingine zina unemployment benefits!! Hapa pasipo na unemployment benefits, pasiwe na price regulations pia??
 
Rejao

JF-Expert Member
May 4, 2010
9,232
4,042
Unajua Mnyika sometimes una akili, tatizo ni hicho chama tu ulichopo.
 
5 Reactions
Reply
Top Bottom