Mhe Mnyika, hapa unaniangusha - Mfumuko wa bei

Mhe Mnyika, hapa unaniangusha - Mfumuko wa bei

Majoja
Nasikitika wewe ndo hukumwelewa mnyika na unaposema eti point yake siyakisomi basi yako ndokabisaa haina hatakichwa wala miguu
Unajidai msomi lakini sisi wachumi ndo tunakucheka wewe badala ya mnyika

Wawezaje kuongeza uzalishaji wasukari kwa wakati huu tunaokumbwa na mfumuko wabei?
Unasema hatuwezi kucontrol mbona imewezekana kwenye mafuta?

Nawasiwasi utakua umetumwa na hao magamba .

Nimpemnyika hongera kwa mawazo mazuri tunahitaji vijana wanaoweza kufikiri kama mnyika
Bei ya mafuta inajulikana duniani, na pia hutegemea formula fulani (nenda mtandao wa EWURA). uKIONA THAMANI YA SHILINGI IMEPUNGUA, UJUE BEI YA MAFUTA ITAPANDA NA CONSEQUENTLY BEI YA VYAKULA. Solution siyo kuongeza uzalishaji, bali ufanisi ili mafuta kidogo yaweze kuzalisha bidhaa nyingi. Tunaweza:-
1.Kuchochea matumizi ya usafiri wa umma, kwa kuweka Sheria za kuruhusu only High occupancy vehicles kuelekea mjini kabla ya saa kumi na mbil jioni kuanzia saa kumi na moja asubuhi....
2. Kutokuagiza magari au kutoza kodi kubwa magari yanayotumia mafuta mengi(miguu ya jini)....
3.Kutumia makaa ya mawe ambayo subhana wa taala katujalia mengi tu hapa nchini kwetu.
4. Maji, umeme rahisi mno! kwanini tunashabikia mafuta?
5.Mafuta ni adui mkubwa wa nchi yetu na dunia kwa ujumla, hata tukiweza kuyachimba tuwauzie mafala wengine, sisi tutumie hiyo hela kuvuna vyanzo vingine vya nishati pamoja na kulinda mazingira yetu.
6.Haya mambo ya kupanga bei ni kupoteza muda tu, waulizeni wakenya.
 
Hivi Mnyika ana taaluma gani? Jamaa anaweza kuwa na degree ya LANGUAGE sijui ndio Linguistic! Mambo ya Inflation atayajulia wapi?

Kila mwanasiasa nchi hii ni mchumi!!! Jinsi wanasiasa walivyo wataalamu wa uchumi ni kama wa-tz walivyo wataalamu ktk malaria! ukijisikia kahoma na kabaridi kidogo tu halafu ukamwambia mwenzako, utasikia "malaria hiyo...!"
 
Hivi hii sukari mnafanyia nini exactly? Ni kuweka kwenye Chai au kuna la ziada?, maana malalamiko kuhusu sukari ni mengi sana, sasa labda kuna kitu ninamiss.

Mkuu, sukari hivi sasa deal kwa sababu huu ni msimu wa mihogo ya kukaanga a.k.a chips dume! Ukienda kwa mama muuza mihogo na kupata vipande vyako 5 na kurudi navyo gheto kisha akachemsha maji pamoja na majani ya sh. 50, hapo ni bonge la supper mazeya! na kama hilo menyu unalipiga asubuhi wakati unaenda mzigoni, ukaunganishia na ki2 mneli ; ha! raha tupu! mida ya lunch unajifanya upo bze...chips dume na chai ya rangi vinakupa stimu!!
 
Back
Top Bottom