panadol
JF-Expert Member
- Feb 11, 2012
- 349
- 44
Pendeni kuwa wakweli, tena napenda kutoa wito kwa Watanzania wote tuwe tunatafakari kwa kina na kujadili, pamoja na kupima mambo. Mimi ningependa watu watakao ingia kwenye siasa waingie kufuatana na hisia zao pamoja na msukumo wao wa kisiasa na si kwa ukanda wao. Hatuwezi kujenga nchi kwa kuacha watu ambao ni wazoefu au wanauwezo fulani eti kwa sababu ni wa kanda fulani, pia hatuwezi kuacha kutumia watu waliokomaa kisiasa na waadilifu halafu tukachukua watu ambao bado hawajakomaa kisiasa baadae zikatoka kauli za kukidhoofisha chama halafu tuseme eti itifaki ya ukanda ilizingatiwa.
Ili mafanikio yapatikane ni lazima kuwe na watu ambao wana hofu ya Mungu, wachapa kazi, waadilifu na wazalendo hivyo itakuwa rahisi kwa watu wa namna hii kupigania ukweli, na si vinginevyo.
kama mkutano umefanyika na watu waliopatikana kwa siku hiyo ndio hao, pengine wengine walishindwa kufika hakuna tatizo, na pengine hao waliokuwepo hawakuwa wamejiandaa sasa utalazimisha mtu azungumze.
tusipende kutumika na chama cha ccm kwa kuleta mijadala ambayo haina mantiki, nchi inaisha huku tunatumia sababu ambazo hazina msingi kuchafua chadema. Tulete hoja zenye mashiko mwisho wa siku wangezungumza watu mbalimbali mngesema waislamu walikuwa wengi kuliko wakristo au wakristo mbona walikuwa wengi kuliko waislamu.
Mtu anapojiunga na chama huwa akubaliwi au akataliwi kwa sababu ya kabila lake au dini yake bali kwa sababu ya utashi wake yeye mwenyewe na ana haki zote za kugombea nafasi za chama na kuwa kiongozi hivyo vvyote vinapatikana kulingana na sifra za mgombea huyo na si vinginevyo. sasa mnataka mtu akiwa anafaa akataliwe kwa sababu ya ukanda, huu ndio utakuwa ubaguzi.
wewe ni kijana wa chadema uko pale makao makuu mnapewa posho kwa ajili ya kuficha maovu ya chadema na kuisema vibaya CCM na Serikali yake ili kuijenga chadema kisiasa na kuidhohofisha CCM,ukweli ni kwamba chadema ni chama cha kidini na ukabila , hawafahi kupewa madaraka ya kuongoza nchi!