Mhe. Makonda mfungulie kesi Askofu Gwajima

Mhe. Makonda mfungulie kesi Askofu Gwajima

Ni kama anajitahidi kumshambulia kuzuia wengine wasiongee wayajuayo juu yake, kiongozi wa dini kujaa chuki na kufurahiwa inanishangaza.

Makonda oyeeee
 
Utata wa Daudi uko mtandaoni tu! Huko kijijini kwao wanajua vizuri tu Daudi na bwana yule wanahusianaje! Ukiwaita wanakijiji waliosoma naye bwana yule wamtambue Daudi mahakamani inaweza kuwa kioja! Necta pia wana picha ya Daudi aliyotumia kwenye usajili, Pamba Sekondari wana Paswa kuwa na picha ya Daudi kwenye faili lake! Kufunika kombe ni vigumu sana! Dawa nzuri kwake ni hii aliyoichukua ya kuwa kimya! Ili maadam mwajiri wake haimsumbui (haelekei kuwa na haja hata ya kuhakiki) hakuna tatizo labda!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Double standard katika ubora wake!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mheshimiwa Makonda pole sana kwa jina lako kuendelea kuchafuliwa pasipo kuchukua hatua za kisheria. Kipindi cha nyuma ulishawahi kuagiza
Mhe. Kubenea akamatwe na kufikishwa Mahakamani kutokana na kutumia lugha ya matusi ambapo alipatikana na hatia na kuhukumiwa kutumikia kifungo cha nje.

Vivyo hivyo nakushauri ukafungue kesi dhidi ya Gwajima ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaotoa taarifa za uongo kwa jamii kwa lengo la kukushushia hadhi yako. Kuendelea kukaa kimya kutamaanisha kuwa yalioongelewa ni ya kweli.
Khaaa,,,[emoji845] kwani bado hajafungua.[emoji844] ..
Nenda kamfungulie mkuu.
 
Akafungua kesi thubutuuuuu yake atakopoulizwa na kibatala, Generali ulimwengu na Tundu lissu athibitishe kweli paul makonda ni jina lake halisi atathibitishaje? Mbona hapo ndo atakuwa kajipeleka mwenyewe kwenye mdomo wa mamba
 
Hivi inawezekana tumbili kumfungulia kesi mkulima kuwa amemsingizia kula mahindi yake!
Tumbili: mheshimiwa hakimu mkulima alinikuta shambani kwake nikiwa nimejisitiri jua kwenye kivuli cha mahindi shambani kwake, sasa ananichafua mitaani kuwa mimi nilikula mahindi yake!
Hakimu: Je bwana tumbili wakati umejisitiri jua shambani. uliona mahindi yoyote yakiwa yameliwa!
Tumbili: Sijui mheshimiwa unachouliza maana msamiati wa kula mahindi siujui!
Hakimu: Mkulima una kielelezo chochote cha kuthibitisha madai yako kuwa tumbili alikula mahindi yako?
Mkulima: Ndiyo mheshimiwa, shambani niliweka automatic camera iliyokuwa inachukua picha za mnato na mtembeo.
Hakimu: Mkulima tuonyeshe hizo picha!
Tumbili: Nina pingamizi na hizi picha mheshimiwa! Ninaamini zinatokana na Photoshop! Naomba zisionyeshwe!
Hakimu: Tuzione kwanza, then tutaona kama ni halisi au vipi!
Mkulima: Anaweka mkanda wa video, angalieni wenyewe tumbili anavyojinoma na mahindi yangu!
Mahakama iliangua kicheko ilipoona tumbili akiyashughulikia mahindi kisawa sawa!
Hakimu: Tumbili Huyo anayeonekana kwenye mkanda ni Nani na anafanya nini?
Tumbili: Naona ni kiumbe Fulani anayefanana na mimi si unajua duniani wawili wawili! (Mahakama kicheko!) Anachokifanya sikijui maana sijawahi kukiona! (Mahakama kicheko!!)
Ndivyo itakavyokuwa kama Bwana yule akishitaki! Kuna picha za Daudi toka primary, Sekondari, na necta Zitakazolinganishwa na yule anayedhaniwa kuwa ndiye Daudi na mahakama itaangua kicheko!
 
Wee hana thubutu hiyo Daudi Bashite na vyeti vyake feki. Amepata zero amezungusha yaan, zero yaan, sio four zero yaan fafafa
Yaani zero maanake hujui kila kitu! Daah! Ila ngwajima noma sana
 
Amfungulie mashaka kwa kosa gani,au washtakiane na ninani akiyemdhalilisha mwenzie kati ya hao wawili na ukae ukijua hao ni ndugu ww ulitakiwa ukae kimya ndugu wakigombana masika hii chukua jembe ukalime!
 
NA HAWA MODS NITAWAFUNGULIA MASHITAKA KWA SABABU WANA LAO JAMBO NGOJA KWANZA TUMALIZE HILI LA KOLOMIJE
IMG-20170302-WA0006.jpg
 
Nauliza tu: Nini implication ya mamlaka husika zilizokuwa zinapigia kelele vyeti hewa kukaa kimya kwenye sakata hili? Je hazijasikia? Je zinaona hazihusiki? Je zinaogopa? Je zinaona hakuna madhara? Je zinasubiri nini? Je zinaelewekaje?
 
Afungue kesi ya nn, hiv ni nani aliyemdhalilisha mwenzie kati yao, kwani makonda unamuona mbumbumbu, ugonvi wao uache kama ulivyo au na ww msukuma, kama wote ni kabila moja waende usukumani wakashtakiane kule kuna jaji wa Kamila wa sungusungu hataki longo longo isitoshe hana chama!
 
Yan makonda bana alifkir maovu yake hayatagundulika jamaa anavyopenda sifa ingekua anasingiziwa siku nyingi angeshaita waandshi wa habar awaonyeshe vyeti ngwajima na mange wote wangeshafunguliwa mashtaka skunying sana
sasa wanamwita bure anakimbia na vyeti vyake
 
Mheshimiwa Makonda pole sana kwa jina lako kuendelea kuchafuliwa pasipo kuchukua hatua za kisheria. Kipindi cha nyuma ulishawahi kuagiza
Mhe. Kubenea akamatwe na kufikishwa Mahakamani kutokana na kutumia lugha ya matusi ambapo alipatikana na hatia na kuhukumiwa kutumikia kifungo cha nje.

Vivyo hivyo nakushauri ukafungue kesi dhidi ya Gwajima ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaotoa taarifa za uongo kwa jamii kwa lengo la kukushushia hadhi yako. Kuendelea kukaa kimya kutamaanisha kuwa yalioongelewa ni ya kweli.
Ina maana unapigilia mstari kwa yaliyongelewa kuwa ni kweli?

Ukweli ni kama moja (1) haugawanyiki.
 
Muuza madawa ya kulevya utamjuwa tu jinsi anavyotokwa na povu. Failure, una data zake au unafuata upepo tu?
Tatizo siyo failure maana kufeli siyo jinai! Tatizo huyo bwana anasemekana anatumia cheti ambacho siyo chake! Na ameshindwa kujinasua kwa kuweka taarifa zake za SHULE tangu primary na vyeti hadharani ili kuweka kumbukumbu sawa!
 
Back
Top Bottom