Rc Makonda ndiye mteule pekee wa Rais JPM anayefanya kazi na kuwatumikia wananchi
Siku za nyuma niliandika waraka wangu kuonesha kwamba Makonda anastahili nafasi ya juu kabisa ya kuwatumikia watanzania wote na sio Dsm pekee
Makonda anastahili cheo cha juu kabisa kwa sasa
Makonda aliahidi kujenga viwanja vitatu vya mchezo wa soka mkoani DSm
Leo hii balozi wa china akiambatana na mkuu huyu wa mkoa wameweka jiwe la msingi la kuanza ujenzi wa uwanja wa bandari kwa gharama ya dola 450,000/=
Na pia balozi huyu ameahidi kujenga viwanja vingine ndani ya mkoa wa dsm baada ya uwanja wa bandari kukamilika na pia kuwapatia ajira vijana zaidi ya ya 24,000 wa kitanzania katika makampuni ya kichina yanayotegemea kuanza kazi hivi karibuni
Huyu ndio aina ya kiongozi anayetakiwa hapa Tanzania
Makonda ni mfano tosha kwa sasa
Hivi kweli ni bora tuwe na maprofesa wenye vyeti lukuki lakini wasiwe na utendaji kazi kama huyu kijana?
Hivi tumkose makonda kisa hao wauza unga?
Nani anaitaji cheti cha makonda zaidi ya utendaji kazi wake?
Tunawaona wawakilishi wetu wasomi wakiwa bungeni kazi wanazofanya na sheria wanazopitisha
Majimbo yote yenye wabunge wasomi yana hali mbaya sana ya maendeleo
Wakishachaguliwa wanaamia mbezi na masaki majimboni adi kampeni zikikaribia
OMBI LANGU KWA MH RAIS
Makonda tunamuitaji sana sisi wanyonge kuliko wasomi wengine
Wasomi hawa ndio waliokuwepo kwenye escrow, richmond na Epa
Mikataba yote mibovu hapa nchini ilisimamiwa na wasomi
NDIMI
RAPHAEL LUKINDO