Mhe. Chikawe, CCM na Tanzania viliuacha ujamaa lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhe. Chikawe, CCM na Tanzania viliuacha ujamaa lini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Dec 15, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Dec 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Waziri Chikawe asema Kikwete hawezi kuwabana mafisadi
  *Asema Rostam, Dk Hoseah hawakamatiki *Asikitika DPP, DK Hoseah kuparuana

  Na Leon Bahati  WAZIRI wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe amesema Rais Jakaya Kikwete hana uwezo kutumia mamlaka yake kuwapeleka mahakamani watuhumiwa wa ufisadi kwani hilo ni jukumu la vyombo alivyoviteua kuchunguza na kuchambua nani afikishwe huko baada ya kujiridhisha kwa ushahidi.  "Huu ni utawala wa sheria, Rais Kikwete hawezi kutoa amri za kukamata watu wakati kuna vyombo alivyoviteua kuchunguza na kuchukua hatua." Waziri Chakawe alisema hayo jana alipokuwa katika mahojiano maalumu na gazeti hili ofisini kwake jijini Dar es Salaam.  Alisema kitendo cha baadhi ya Watanzania kumshinikiza Rais Kikwete awafikishe mahakamani watuhumiwa wa ufisadi kinaashiria kuwa wanataka aamuru watuhumiwa hao wapelekwe mahakamani bila kutumia vyombo husika jambo ambalo haliwezekani katika mfumo wa kibepari.  "Enzi zile za mfumo wa ujamaa na chama kimoja cha siasa, hilo lingewezekana lakini wakati huu ambao nchi inatumia mfumo wa kibepari, haiwezekani," alisema Chikawe.

  Hivi karibuni, wanasiasa na hata baadhi ya viongozi waliowahi kuwa serikalini awamu zilizopita, wakichangia mada ya mustakabali wa taifa kwenye kongamano la taasisi ya Mwalimu Nyerere, waliitaka CCM imtose Rais Kikwete asigombee tena ili kumalizia ngwe ya miaka mingine mitano, iwapo atashindwa kufanya maamuzi magumu ya kuwachukulia hatua watuhumiwa wa ufisadi.  Alionya kwamba Rais Kikwete akikurupuka katika hilo, kesi nyingi zitakwaa kisiki mahakamani na itabidi hao wanaoitwa mafisadi kulipwa mabilioni ya fedha kama fidia ya usumbufu.  Chikawe alisema mawazo ya namna hiyo yanatokana na watu wengi kuendelea kuwa na mtazamo wa mfumo wa kijamaa na chama kimoja na kusahau kuwa tayari nchi imeingia katika mfumo wa kibepari.  Waziri Chikawe alitumia mfano wa enzi za waziri mkuu, hayati Edward Sokoine alipopambana na wahujumu uchumi kwa kutoa amri ya kukamatwa watu ovyo na kutaifishwa mali zao kuwa moja ya mifano ya uongozi katika mfumo wa ujamaa.  Alisema amri hizo zilikubalika kulingana na mazingira ya wakati lakini, ulipoanza kuingia mfumo wa kibepari waliopoteza mali kupitia operesheni hiyo walidai haki kupitia mahakama na walishinda hivyo serikali ikabidi iwafidie pamoja na usumbufu.  Waziri huyo mwenye dhamana ya kusimamia katiba na sheria za nchi, ambaye amekuwa kimya licha ya kuwepo na mijadala mingi inayokosoa utendaji wa vyombo vya sheria nchini hasa suala la ufisadi, alisema polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wana haki ya kuchunguza makosa ya jinai, lakini pia mkurugenzi wa mashtaka (DPP) ana mamlaka ya kutoruhusu kesi hizo zisiende mahakamani kama hakutakuwa na ushahidi wa kutosha.  Alitoa mfano wa Mbunge wa Igunga, Rostam Azizi (CCM) ambaye wengi wamekuwa wakimtuhumu kwa ufisadi kupitia kashfa ya kampuni tata ya Richmond iliyopewa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura mwaka 2006, akisema hakuna ushahidi wa kumfikisha mahakamani.  "Wewe jaribu kuipitia ile ripoti ya Kamati Teule ya Bunge ya (Dk Harrison) Mwakyembe, hata uipitie mara 10. Mimi nimeipitia mara nane, sijaona sehemu ya kupata ushahidi wa kumshtaki," alisema Chikawe.  Kuhusu anwani ya barua pepe ya kampuni ya Caspian ambayo inamilikiwa na Rostam kutumiwa na kampuni iliyoirithi Richmond, alisema: "Ni sawa, lakini hadi sasa hakuna mahali popote ambapo kampuni ya Dowans inatuhumiwa. Yenyewe ilipokea jukumu ambalo Richmond ilishindwa lakini wao wakatekeleza. Ingekuwa Dowans wana matatizo, basi hata Rostam angeweza kuhusishwa."  Alizungumzia shinikizo la kutaka Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hoseah awajibishwe kwa madai ya kuficha madhambi ya Richmond ambayo kamati ya Dk Mwakyembe iliyaweka wazi, alisema:  "Takukuru ilichunguza mwenendo wa utoaji wa zabuni kwa Richmond na kwenye ripoti yake ikaeleza haikuona fedha zilizotumika kurubuni mtu yeyote. Na hata kamati ya Dk Mwakyembe haikubaini kitu cha namna hiyo.

  "Kamati ya Dk Mwakyembe imebaini udhaifu wa serikali kuchunguza Richmond kabla ya kuingia mkataba na hili ndilo lililofanya Lowassa na wenzake kujiuzulu na Baraza la Mawaziri kuvunjwa."  "Lakini uzuri ni kwamba Rais Kikwete alikuwa ameagiza wasipewe fedha hadi wawe wameleta mitambo nchini na hilo lilifanyika. Kampuni ya Richmond haikuchukua hata senti ya serikali. Kama ilihonga watu kwa siri huko, ilikula kwao. Ila tunachojua walishindwa kuleta mitambo ya kuzalisha umeme wakatoa kazi hiyo kwa Dowans ambao walifanikisha."  Pamoja na hali hiyo, Chikawe alisema Mtanzania yeyote mwenye ushahidi unaoweza kuwashtaki wanaotuhumiwa ni vyema akawasiliana na Mpelelezi Mkuu wa Makosa ya Jinai (DCI) au Takukuru.  Kuhusu majibizano yaliyotokea hivi karibuni baada ya Dk Hosea kumlaumu DPP, Elieza Feleshi kwa kukalia mafaili zaidi ya 60 ya kesi za ufisadi na baadaye Feleshi kumjibu kuwa ni muongo, Chikawe alisema ni jambo ambalo halikumpendeza.  "Kwa kweli imekuwa bahati mbaya vyombo hivi vya serikali kulumbana vyenyewe, lakini nafikiri ilikuwa ni bahati mbaya tu, wakati mwingine hilo halitatokea," alisema Chikawe.  Hata hivyo, alisema huenda lilichangiwa pia na vyombo vya habari kwa kuchokonoa mambo hayo hivyo kuwafanya kutoa kauli ambazo pengine zilionekana kuhitilafiana.  Chikawe ambaye ni Mbunge wa Nachingwea alisisitiza kwamba DPP amekuwa akipelekewa mafaili mengi na anapoona hayana ushahidi wa kutosha huwashauri wahusika mambo ya kufanya na pengine kuwaeleza kwamba hakuna kesi ya kujibu.  Maswali:
  - Chikawe wewe ndio waziri wa Katiba; hivi hii Katiba wenzetu mliibadilisha lini maana mara ya mwisho nilipoisoma inasema nchi yetu ni ya kijamaa (Ibara 3:1) na inafuata demokrasia ya vyama vingi. Hakuna mahali ambapo tumeutukuza Ubepari kama ulivyonukuliwa hapo.  - Chikawe hiyo kampuni ya Dowans wanahisa wake wa Tanzania ni kina nani?  - Chikawe wewe ni mbunge wa CCM, Katiba ya CCM bado inasema kuwa "Ujamaa na Kujitegemea ndio njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio huru na sawa" (Ibara 4:3). Sasa mwenzetu huu Ubepari umeingizwa CCM lini na kwa kikao kipi?


  Yaani mnatukuza kuvunja Katiba? Kama mnataka tufuate ubepari na vikolombwezo vyake badilisheni Katiba yetu vinginevyo wote mmepoteza uhalali wa kuwepo nyinyi mteteo Ubepari na kuukana ujamaa. Si mliapa kulinda Katiba ama?
   
 2. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Hivi huyu Chikawe ana elimu gani?,amesoma sheria,engineering,social science au.....maana siku hizi siasa imekuwa kama dini,when it comes to politics mtu anaweka proffessional yake pembeni,hata kama ni mwanasheria aliyekubuhu hutashangaa akitoa comment zinazokinzana na katiba yetu(as if hajawahi kuigusa kabisa).Utakuta mtu ni msomi tena ana Masters in Electrical engineering lakini comment zake kuhusu hali ya umeme nchini hutaamini kama alishawahi kugusa vile vitabu vya akina Hughes.Siasa bwana....
   
 3. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  MM,

  Zaidi ya kusema kuwa tuko kwenye mfumo wa kibepari, kautukana ujamaa na mfumo wake kwa kusema mambo ya kukamata kama vile wakati wa ujamaa ilikuwa ni udhalimu mkubwa. Zaidi aliposema kuwa Sokoine na kamata kamata ya ovyo!

  Sasa wao na ubepari wana sera ya achia achia ovyo, hivyo tuikubali?

  Si umesikia Ole Naiko anadai wana ardhi heka laki mbili kwa wawekezaji wa Kilimo Kwanza lakini hataki kusema ardhi hii iko sehemu gani eti ni suala nyeti?

  Gademu Shiti!
   
 4. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Kiongozi anapokiuka katiba ya nchi, au anapotofautiana na sera ya Serikali anatakiwa kujiuzuru mara moja. Chikawe anapaswa kuachia madaraka mara moja. Kama ataendelea na maneno yake hayatakanushwa sitakuwa nimejinyima heshma wala kuikosea nchi yangu kwa kutamka wazi kwamba nchi yetu imeoza.

  Tatizo ni kwamba (most of Tanzanians) mambo makubwa tunayaona madogo na madogo tunayaona makubwa.
   
 5. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #5
  Dec 15, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  kinachotokea ni kua Watendaji ambao wameteuliwa na Rais kushika nafasi za juu za kuendesha mashitaka hawatimizi wajibu wao hadi JK aseme, kumbuka juu ya watuhumiwa wa EPA na Richmond, ilimpasa JK kutoa kauli kwanza ili wenyewajibu wao wafanye kazi.
  Jamii inaamini ni lazima Ikulu iseme ili kina DPP, na wengine watimize wajibu. kweli hawawajibiki ndo maana tunamtaka Rais aamue jambo moja kuwafukuza kazi kwa kushindw kutimiza wajibu wao.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Dec 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Maana... ndio maana JK na matatizo yake yote (sitaki kuyataja) hajawahi kuita kinachoendelea sasa kuwa ni "ubepari" mwenyewe na wenzake wanaita "mfumo wa soko".. whatever that means.

  Sasa waziri wa Katiba anapodai kitu ambacho hakipo kisheria na kubeza kile kilichopo anaweza kuendelea na nafasi yake?
   
 7. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
   
 8. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #8
  Dec 15, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  And there we go again................ Chikawe, Hosea, DPP, Sophia Simba, Makamba........... the list goes on ni viongozi kweli? Hawa wote wanafanana kitu kikubwa kimoja kwamba hawatafakari kabla ya kuzungumza. Anywayz labda ndiyo staili ya awamu ya nne!!!!!!!
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Dec 15, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,312
  Likes Received: 1,783
  Trophy Points: 280
  Hapo sasa! Ninaanza kuona ukweli wa yale yaliozungumzwa katika mkutano wa taasisi ya Mwalimu Nyerere. Uongozi wetu, kwa haya mambo ambayo viongozi wetu wanayasema, una onyesha weakness ya hali ya juu maana unapingana na misingi yenyewe wanayodai kusimamia
   
 10. bona

  bona JF-Expert Member

  #10
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  watanzania tunatakiwa tuanze kufunguka macho kua kwenye ubepari ni mfumo wa kilaghai hata sheria zake ziko ivyoivyo, hakuna ataefungwa kwa sababu kinachoangaliwa ni tafsiri ya sheria sio ukweli wa mambo, zombe si alipiga mtu risasi ya kichwa lakini hakimu akasema hamna ushahidi hakusema zombe hajaua ila haman ushahidi.
  mwendo ndio uleule hata kwenye kesi za kifisadi hakuna atayefungwa hata kama hela zimechotwa benki ila kama hakuna eti ushahidi hafungwi mtu, na waziri anatoa kauli za kebehi eti mwenye ushahidi apeleke, vyombo husika vinafanya kazi gani?
  rushwa katika nchi za kibepari haiishagi na nchi inavyoota mizizi ya kibepari rushwa inakua vilevile, ni sifa pacha dunia nzima.
   
 11. GY

  GY JF-Expert Member

  #11
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Viongozi wetu (wakiwemo makatibu wakuu) hupewa ilani ya uchaguzi ya CCM (ambayo hua haitekelezeki) mara tu wanapoteuliwa kushika uongozi wa juu, badala ya kupewa katiba ya nchi (ambayo wengi wao hawajawai hata kuitia machoni). Sishangazwi hata kidogo waziri kutoa kauli ambazo zinapingana na katiba yetu.

  National interests zilishaenda na kina Nyerere na Sokoine, sasa ivi ni interest za wenye pesa. Na Chikawe yupo sahihi kabisa, serikali ya nchi hii haiwezi kamwe kuthubutu kumpeleka Rostam mahakamani, haiwezi aslan.

  Mahakama gani itakayoweza kusikiliza na kuhukumu kesi ya Rostam, mtu aliyempeleka rais wa nchi (ambaye ndio anateua jaji mkuu na majaji wengine ambao hawasafishwi hata chembe na bunge) madarakani?

  Ukipeleka ushahidi wowote unaohusu ufisadi wa huyu bwana, serikali itauficha, na hutausikia tena. Labda itokee miujiza ya mfumo wa kiutawala wananchi turuhusiwe kuwashtaki mafisadi kwenye nchi yeyote tunayodhani itasikiliza kwa haki madai haya, na mimi ntakua wa kwanza kumpeleka huyu wetu uchina.
   
 12. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #12
  Dec 15, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hili suala la ujamaa katika katiba yetu Prof Shivji alilitolea mtazamo wake wakati akijumuisha mada yake aliyotoa wakati wa Kongamano la kujadili mustakabali wa Taifa liloitishwa na Mawalimu Nyerere Foundation hivi karibuni. Kuna watu waliokuwa wakitaka kujua kama kuna uwezekano wa kufungua kesi ya katiba kuhusu ukiukwaji wa katiba kwa upande wa serikali katika suala hilo.

  Prof Shivji kwa maoni yake alisema hilo haliwezekani kwani katiba inasema kuwa tunajukumu la kujenga taifa la kijamaa na kujitegemea ambalo kwa mujibu wake katiba hiyohiyo imetoa nafasi kubwa ya kumanipulate maana halisi ya taifa linalofuata siasa za ujamaa na kujitegemea.

  Kwa mujibu wake, ukifuata mwanya huo wa kikatiba utakuta kuwa hata Marekani ni waumini wazuri wa ujamaa na kujitegema....

  Hayo siyo yangu ni Kamarade Shivji...

  omarilyas
   
 13. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #13
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Chikawe is trying to be clever by half!! Kama Rais JK hana mamlaka ya kuwachukulia mafisadi hatua za kisheria ilikuwaje akatoa amri kwa mafisadi hao hao warudishe pesa za EPA la sivyo.......
   
 14. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #14
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Duh..ukisikia lile kosa hasa kwenye masuala ya ajira wazungu wanaita "Gross Misconduct" huu ni mfano wake sahihi kabisa. Yaaki kosa ambalo halina msalia mtume, huwezi kuomba samahani ukasamehewa na kuendelea na kazi...ni kosa pekee linaloweza kukufukuzisha kazi dakika hiyo hiyo.

  Waziri Chikawe hakutakiwa awe bado ni Waziri mpaka dakika hii...kweli Tanzania ya leo haina Rais.
   
 15. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #15
  Dec 15, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Hivi jamani kweli hakuna mtanzania anayeweza kuwa na huruma akatuokoa na kututoa katika jinamizi hili?
   
 16. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #16
  Dec 15, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Azimio la Zanzibar malengo yake haswa yalikuwa ni yapi??
   
 17. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #17
  Dec 15, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Sijapata ona viongozi wenye dharau,ngebe na ujivuni kama hawa wetu....
  .... Tuombeane uhai 2010
   
 18. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #18
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waziri Chikawe asema Kikwete hawezi kuwabana mafisadi[​IMG]*Asema Rostam, Dk Hoseah hawakamatiki
  *Asikitika DPP, DK Hoseah kuparuana

  Na Leon Bahati

  WAZIRI wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe amesema Rais Jakaya Kikwete hana uwezo kutumia mamlaka yake kuwapeleka mahakamani watuhumiwa wa ufisadi kwani hilo ni jukumu la vyombo alivyoviteua kuchunguza na kuchambua nani afikishwe huko baada ya kujiridhisha kwa ushahidi.

  "Huu ni utawala wa sheria, Rais Kikwete hawezi kutoa amri za kukamata watu wakati kuna vyombo alivyoviteua kuchunguza na kuchukua hatua." Waziri Chakawe alisema hayo jana alipokuwa katika mahojiano maalumu na gazeti hili ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

  Alisema kitendo cha baadhi ya Watanzania kumshinikiza Rais Kikwete awafikishe mahakamani watuhumiwa wa ufisadi kinaashiria kuwa wanataka aamuru watuhumiwa hao wapelekwe mahakamani bila kutumia vyombo husika jambo ambalo haliwezekani katika mfumo wa kibepari.

  "Enzi zile za mfumo wa ujamaa na chama kimoja cha siasa, hilo lingewezekana lakini wakati huu ambao nchi inatumia mfumo wa kibepari, haiwezekani," alisema Chikawe.

  Hivi karibuni, wanasiasa na hata baadhi ya viongozi waliowahi kuwa serikalini awamu zilizopita, wakichangia mada ya mustakabali wa taifa kwenye kongamano la taasisi ya Mwalimu Nyerere, waliitaka CCM imtose Rais Kikwete asigombee tena ili kumalizia ngwe ya miaka mingine mitano, iwapo atashindwa kufanya maamuzi magumu ya kuwachukulia hatua watuhumiwa wa ufisadi.

  Alionya kwamba Rais Kikwete akikurupuka katika hilo, kesi nyingi zitakwaa kisiki mahakamani na itabidi hao wanaoitwa mafisadi kulipwa mabilioni ya fedha kama fidia ya usumbufu.

  Chikawe alisema mawazo ya namna hiyo yanatokana na watu wengi kuendelea kuwa na mtazamo wa mfumo wa kijamaa na chama kimoja na kusahau kuwa tayari nchi imeingia katika mfumo wa kibepari.

  Waziri Chikawe alitumia mfano wa enzi za waziri mkuu, hayati Edward Sokoine alipopambana na wahujumu uchumi kwa kutoa amri ya kukamatwa watu ovyo na kutaifishwa mali zao kuwa moja ya mifano ya uongozi katika mfumo wa ujamaa.

  Alisema amri hizo zilikubalika kulingana na mazingira ya wakati lakini, ulipoanza kuingia mfumo wa kibepari waliopoteza mali kupitia operesheni hiyo walidai haki kupitia mahakama na walishinda hivyo serikali ikabidi iwafidie pamoja na usumbufu.

  Waziri huyo mwenye dhamana ya kusimamia katiba na sheria za nchi, ambaye amekuwa kimya licha ya kuwepo na mijadala mingi inayokosoa utendaji wa vyombo vya sheria nchini hasa suala la ufisadi, alisema polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wana haki ya kuchunguza makosa ya jinai, lakini pia mkurugenzi wa mashtaka (DPP) ana mamlaka ya kutoruhusu kesi hizo zisiende mahakamani kama hakutakuwa na ushahidi wa kutosha.

  Alitoa mfano wa Mbunge wa Igunga, Rostam Azizi (CCM) ambaye wengi wamekuwa wakimtuhumu kwa ufisadi kupitia kashfa ya kampuni tata ya Richmond iliyopewa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura mwaka 2006, akisema hakuna ushahidi wa kumfikisha mahakamani.

  "Wewe jaribu kuipitia ile ripoti ya Kamati Teule ya Bunge ya (Dk Harrison) Mwakyembe, hata uipitie mara 10. Mimi nimeipitia mara nane, sijaona sehemu ya kupata ushahidi wa kumshtaki," alisema Chikawe.

  Kuhusu anwani ya barua pepe ya kampuni ya Caspian ambayo inamilikiwa na Rostam kutumiwa na kampuni iliyoirithi Richmond, alisema: "Ni sawa, lakini hadi sasa hakuna mahali popote ambapo kampuni ya Dowans inatuhumiwa. Yenyewe ilipokea jukumu ambalo Richmond ilishindwa lakini wao wakatekeleza. Ingekuwa Dowans wana matatizo, basi hata Rostam angeweza kuhusishwa."

  Alizungumzia shinikizo la kutaka Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hoseah awajibishwe kwa madai ya kuficha madhambi ya Richmond ambayo kamati ya Dk Mwakyembe iliyaweka wazi, alisema:

  "Takukuru ilichunguza mwenendo wa utoaji wa zabuni kwa Richmond na kwenye ripoti yake ikaeleza haikuona fedha zilizotumika kurubuni mtu yeyote. Na hata kamati ya Dk Mwakyembe haikubaini kitu cha namna hiyo.

  "Kamati ya Dk Mwakyembe imebaini udhaifu wa serikali kuchunguza Richmond kabla ya kuingia mkataba na hili ndilo lililofanya Lowassa na wenzake kujiuzulu na Baraza la Mawaziri kuvunjwa."

  "Lakini uzuri ni kwamba Rais Kikwete alikuwa ameagiza wasipewe fedha hadi wawe wameleta mitambo nchini na hilo lilifanyika. Kampuni ya Richmond haikuchukua hata senti ya serikali. Kama ilihonga watu kwa siri huko, ilikula kwao. Ila tunachojua walishindwa kuleta mitambo ya kuzalisha umeme wakatoa kazi hiyo kwa Dowans ambao walifanikisha."

  Pamoja na hali hiyo, Chikawe alisema Mtanzania yeyote mwenye ushahidi unaoweza kuwashtaki wanaotuhumiwa ni vyema akawasiliana na Mpelelezi Mkuu wa Makosa ya Jinai (DCI) au Takukuru.

  Kuhusu majibizano yaliyotokea hivi karibuni baada ya Dk Hosea kumlaumu DPP, Elieza Feleshi kwa kukalia mafaili zaidi ya 60 ya kesi za ufisadi na baadaye Feleshi kumjibu kuwa ni muongo, Chikawe alisema ni jambo ambalo halikumpendeza.

  "Kwa kweli imekuwa bahati mbaya vyombo hivi vya serikali kulumbana vyenyewe, lakini nafikiri ilikuwa ni bahati mbaya tu, wakati mwingine hilo halitatokea," alisema Chikawe.

  Hata hivyo, alisema huenda lilichangiwa pia na vyombo vya habari kwa kuchokonoa mambo hayo hivyo kuwafanya kutoa kauli ambazo pengine zilionekana kuhitilafiana. Chikawe ambaye ni Mbunge wa Nachingwea alisisitiza kwamba DPP amekuwa akipelekewa mafaili mengi na anapoona hayana ushahidi wa kutosha huwashauri wahusika mambo ya kufanya na pengine kuwaeleza kwamba hakuna kesi ya kujibu.
   
 19. O

  Omr JF-Expert Member

  #19
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  malaya wa rostam huyu
   
 20. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #20
  Dec 15, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  wanasiasa karibu wote hapa bongo wako kwenye payroll ya Rostam, watamkamata vipi?
   
Loading...