Mhe. Bashe tengua kauli...

Mhe. Bashe tengua kauli...

Wanaodai kuwa wenye div 1 or 2 hawaendi ualimu sio kweli labda kwa form four kwa sababu wengi wanaweka FORM 5 kuwa chaguo la kwanza,ila kwa 6 ni uamuzi wa mtu na wengi wanaenda ualimu kwa sababu kuu mbili 1.Mkopo ni 100% wachache sana wanapata pungufu ya hiyo % 2.Ajira ni ya uhakika sio ya kutafuta ni kusubiri tu. Sababu kubwa ya kuwepo hizo sababu mbili ni HALI YA KIPATO CHA FAMILIA WALIKOTOKA kuchangia lakini 5 chuo kikuu ni vgumu bado amalize aanze kuhangaikia ajira nauli tu za usaili mikoani shida. Kwenye Qualifications hamna utofauti kabisa na kada zingine utofauti kidogo sana kwenye michepuo SCIENCE vs ARTS,Science PRINCIPAL PASS mbili tu umequalify kozi kibao, tuseme kutokana na umuhimu wa hii sekta kuna haja ya kubana kwenye qualifications level zote ASTASHAHADA STASHAHADA SHAHADA na hata UZAMILI na UZAMIVU huku changamoto zingine zikiwa zimefanyiwa kazi.
 
Ni muendelezo wa mitazamo hasi na mgando juu UALIMU.Taaluma haiko hivyo kama mitazamo hiyo migando inavyojiri.Imejengeka dhana yenye fikra mgando katika jamii yetu ya kitanzania kwamba Walimu ni watu walioeli kuendelea na malengo yao ya awali wakajikuta hawana jinsi ikabidi wakimbilie huko.Dhana hii yenye FIKRA MGANDO JUU YA UALIMU imefanya wanafunzi wengi kuogopa kusomea ualimu kwa kuonekana ni duni na hawana uwezo wa kufikiri.Wengi sasa huchukua ualimu kama plan B.Je kila mtu mwenye maarifa anaweza kuwa mwalimu? Ni lini ualimu utapewa hadhi sawa na taaluma nyingine?Taaluma hii imekosa mtetezi,hata wenye taaluma nao hawako pamoja.Sasa kila mtu anaweza kutamka NEGATIVE PERSPECTIVE bila kufikiria kuathiri wanafunzi na walimu wao.Itafika wakati hakuna mwalimu atakayependa kudumu kwenye taaluma hii na kukimbilia taaluma zinazoheshimika.Kuomba radhi kwa kauli hiyo ni bora.
 
Kwa kweli binafsi mtu anayesema walimu ni waliofeli ni mpumbavu na lofa (Nukuu ya Mkapa) Kwa kuwa vigezo vya kuwapata walimu viko sahihi.

Nchi haihitaji wenye division ones kuwa shule ya msingi. Kwani kuwa mwalimu wa darasa la saba au la kwanza huhitaji division one, mwalimu huandaa kipindi. Same applies kwa secondary.

Kada zingine kwa mfano afya na uhandisi wanaoenda certificate ni waliopata division four form four. Wanaenda kusomea clinical officer na kozi za awali kwenye uhandisi na ni wazuri kweli kwenye kutenda kazi kwa kuwa wamelelewa toka chini.

Uhasibu ni hivyo hivyo kwa mfano Chuo cha uhasibu (TIA) kina vijana waliopata division four na wakaanzia Singida, Mtwara, Mbeya na wakanolewa vyema na sasa ndiyo wako MA wizarani.

Kila wizara ina vyuo vyake. Nadhani kitu asichojua Bashe ni kwamba kati ya wahitimu wa form four 400,000+ wanaopata division one hadi three ni kama elfu ishirini tu!!! Kwa hiyo kama fikra yake ni kuwa hao wamefeli, basi yeye ndiyo kafeli

Hii nchi ni yetu wote, swala la kufeli linahitaji tafiti kwani mimi naamini ukiwachukua walimu wa vyuo vikuu wafundishe darasa la kwanza au la saba matokeo yanaweza kuwa yaleyale au mabaya zaidi lakini kamwe hayawezi kuwa bora!!!
 
Sekta zingine- Take note hata jeshini wanakwenda waliofeli (sijui siku hizi). Lakini jeshini wana utaratibu wa kuingia kule siyo free kama kwa walimu. Hivyo attention ya jamii haiko huko kwa vile hakuna direct impact kwa mtu wa kawaida. Pili umuhimu wa sekta yenyewe. Huu ni uhai wa taifa kwa kila nyanja even at individual level. Mzazi anataka mtot wake aelimike apate kazi nzuri. Shule za kata wote (???) wanafeli! Lazima watu wapige kelele!
Hebu tafsiri kwanza kufeli ni nini halafu tuendelee na mjadala........
 
Ni siasa hakuna aliyeipenda UPE na walikuwa wanafundisha darasa la kwanza tu! Nina mdogo wangu ni UPE lakini mpaka sasa bado unaona kuna pengo- bahati mbaya hakujiendeleza.
Mbona unapotosha wakati waliobaki baki wa nafundisha hadi darasa la saba tena Maths na Sayansi? Na nina ushahidi wa Ilala jijini Dar
 
Ualimu ni sehemu nyeti huwezi kulinganisha na sehemu ulizozitaja.Wote uliowataja wanatokana na mwalimu, hivyo mwalimu akiwa mbovu kila kitu kinakuwa kibovu.
Let us face the reality! Kuna mwanafunzi aliyepata division 1 or 2 (nadhani hata three??????) akaenda ualimu?
Tupo mm n Mwalimu nafundisha Secondary-Kahama, csee nilipata div3 point 22, Acsee nilipata div2 point 10, BA(ed) ya DUCE nina Upper second with honors! Sasa hii hoja ya ualimu n chaka la waliofeli linahusu walimu wa ngazi IPI? Kama n primary yawezekana kabsa wapo waliofel wanafundsha huko! Ukitaka nikuthbitishie niliyosema kuhusu elimu yangu njoo PM' ntakutumia vyeti vyangu vyote kuanzoa 0-level hadi university
 
Sina hakika Mkuu. Ngoja waje.

HONGERA KWA 2ND UPPER! Nilitaka nisijibu maana sababu nimezitoa kwa nini mtu wa div 1,2 anakwenda ualimu. Soma humu. Umemaliza lini? Shule zipi? DUCE nimesoma pale 1979 wakati huo ikiwa Chang'ombe (sikumaliza nilikatisha). Lecturers wanawatoa wapi walio competent hapo chuoni! Kuna vyuo ukisema nimesoma pale Tanzania, kila mmoja anakuwa na mashaka na competence yako (sisemi DUCE) ujue hilo. Hata wa ST Joseph bila kugundulika ingelikuwa na product mitaa za hovyo-nasikia pale kuna first class nyingi tu!
 
DUCE nmemaliza 2013, lecturer weng ndio wanaofundisha main campus-udsm' o-level na A-level nmesoma government schools! Hii hoja ya kuwa "ualimu n kichaka cha waliofeli" haina uhalisia kiasi hicho ambacho watu wanaamini
 
Sawa, una sabau za msingi kama vile kupata mkopo, kupata ajira. Haiwezekani ukaenda ualimu kama huna sababu ya msingi na una div 1,2.
Hakuna sababu ya msingi kama kuipenda kazi unayoenda kusomea
 
Huwezi kupenda kusomea umasikini ,kukosa heshima kwenye jamii, kupigwa viboko na DC, etc
Kwaiyo wewe unaamini hakuna Mwl mwenye hali nzuri nchi hii?? Kuuondoa umasikini ni zaidi ya kutegemea kazi uliyoajiliwa Nayo ni vile utatumia muda wako kuchekecha akili zako tofauti na pato upewalo na mwajiri wako! Kuna wafanyakaz wa benki wengi tu wanalipa mishahara sawa au chini ya mia 5 elfu anayopokea Mwl acha mawazo mgando hayo Nenda Ubungo Bus Terminal Ulizia gari inaitwa KIPACHA inafanya safari za Handeni -Dar-Songe alafu ulizia mmiliki wa iyo gari ni nani? Ni Mwl wa shule ya Msingi Handeni kwa taarifa yako ilukitumia muda vizur umasikini unaepukika bila kuhitaji ajira au mshahara mkubwa
 
Hapana sikufundishwa na hao please. Nimemaliza University 1983! Hapakuwa na upuuzi wa sasa. Afterall University ilikuwa moja usingelithubutu kwenda huko bila sifa
Umesomea ualimu kwa vile labda kwa ajili ya uhaba wa ajira/mikopo- wazazi kutokuwa na uwezo kifedha. Watoto wetu wanakwenda huko na div 1 ya form six (kupata ajira with hope kuwa kwa vile form six pass zangu ni nzuri nitabadilisha mbele, na wengi wamefanya hivyo kama vyeti vyao vya form six ni vizuri) not form 4.
kua na adabu mzee, unasema bila aibu kua umemaliza university 1983 ukaa bila kusaidia kuweka utaratibu mzuri was kupata walimu alafu unakuja kulaumu watu ambao hata primary hawajamaliza kwa upuuzi wenu nyie wazee. Unaongea utafikiri miaka hiyo kuna mwenye PHD alikufundisha sekondari...Kweli Magufuli alisema kweli kua nyie Wazee ndo mmearibu nchi hii
 
Ualimu ni sehemu nyeti huwezi kulinganisha na sehemu ulizozitaja.Wote uliowataja wanatokana na mwalimu, hivyo mwalimu akiwa mbovu kila kitu kinakuwa kibovu.
Let us face the reality! Kuna mwanafunzi aliyepata division 1 or 2 (nadhani hata three??????) akaenda ualimu?

Je na maslahi yao yanaendana na huo unyeti,au ni unyeti katika majukumu tu????
 
Naunga mkono kauli ya Bashe,ualimu ni sekta nyeti na msingi wa mafanikio ya sekta zingine.Nchi haifanyi vyema kwenye seka zingine pia ni kutokana na msingi mbovu wa walimu..Lazima serikali ianze kudahili watu wenye ufaulu kuanzia daraja la 2 kwenda juu na wapewe motisha hapo automaticaly wengi watajitahidi kupata alama za juu ili wawe walimu na heshima ya ualimu irudi.mfano mzuri ni shule binafsi zina walimu bora na matokea mnaona,pia shule za bweni za zamani zilikua zinafanya vyema kozi walimu walikua bora lakini walimu wenu wa saizi ni poor kabisa na matokeo mnayaona,hawa hata wapewe malipo makubwa watoto watafeli tu
 
Back
Top Bottom