Mhe. Bashe kwanza hongera sana kwa kuingia bungeni baada ya kufanyiwa figisu nyingi 2010 na hatimaye ukaenguliwa eti wewe si mtanzania. Na kwa kipindi kifupi tu jina lako limeanza kuingia vichwani mwa watanzania wachache wanofuatilia bunge manane ya usiku.
Nakuja hapa kukutaka utengue kauli yako iliyonukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari kwamba "ualimu ni kichaka cha waliofeli". Binafsi sijakusikia wala kukuona moja kwa moja kwa kuwa hilo bunge lenu linalooneshwa manane ya usiku wala sina habari nalo. Lkn kwa kuwa hujakanusha nukuu hii iliyoenea katika vyombo vyote vya habari bila shaka uliitoa kauli hii.
Kauli hii inawezekana uliitoa kwa dhamira njema kabisa lkn hukufikiria madhara yake kwa ualimu na walimu. Maana inatweza na kudhalilisha ualimu na walimu. Kwa mtu wa hadhi yako unayesifika kuwa mwanasiasa machachari unayechipukia unapaswa kuwa makini kabla ya kufungua kinywa chako.
Jiulize maswali yafuatayo mhe. Bashe.
1. Kufeli maana yake nn?
2. Taasisi nyingine za serikali hakuna waliofeli?
Elimu ni uwezo wa kutambua na kupambana/kukabiliana na changamoto zilizopo ktk mazingira. Anaye elimika anapaswa kuwa huru kifikra na kiuchumi.
Kimsingi elimu ktk taifa letu haimpi msomi ujuzi na uwezo wa kutambua na kupambana na changamoto zinazomzunguka. Tumeshuhudia mkuu wa mkoa aliyekuwa mstari wa mbele kuhimiza vijana wajiajiri akilia njaa baada ya kuondolewa kwenye nafasi hiyo.
Yawezekana hata wewe Bashe unajiona mwenye kufaulu kwasabb tu umepata ubunge. Nje ya ubunge huna mbinu ya kupata mlo au kuendesha maisha
Tunaona maprofesa wakililia mikataba ya kuendelea na kazi hata baada ya kufikia umri wa kustaafu. Hii ni ishara tosha kuwa hawana ujuzi na uwezo wa kupambana nje ya ajira.
Lkn kama taasisi nyingine zina waliofaulu. Inakuwaje walimu waliofeli wakaingia kwenye ajira ili hali mifumo ya kuajiri serikalini imeshikwa na walioelimika??
Mhe. Bashe ulikuwa too specific katika kauli yako. Ingekuwa vema ungesema "serikalini ni kichaka cha waliofeli".
-bungeni hakuna waliofeli?
-polisi hakuna waliofeli?
-mahospitalini hakuna waliofeli?
- jeshinini hakuna waliofeli?
- wizarani hakuna waliofeli?
-tra, pccb, ewura, n.k hakuna waliofeli huko?
Nionavyo mm watanzania wote wamefeli. Ndiyo maana hata chama chako kikakuzushia kashfa zisizo na miguu kuwa wewe ni msomali ili tu usiwe mbunge. Waliofaulu wanaweza kufanya hivyo?
Lkn waliofaulu wamefanya nn ktk nchi hii? Mm naona kuna walioenda shule na kupata vyeti tu. Ndiyo maana nchi ina kila kitu halafu umaskini umekithiri. Mpk leo nchi inaagiza vijiti vya kuchokonolea meno!!!? Hao waliofaulu wako wapi?
Majengo, yanaanguka hovyo, miji yetu yote haijapangwa, viwanda vinakufa kuna waliofaulu kweli? Kuna watakao kuja na majibu ya watunga sera na sheria. Hawa pia wamefaulu??
Daah!! Niishie hapa.
Wako Kigodoro.