Omutwale
JF-Expert Member
- Feb 4, 2008
- 1,429
- 1,053
Bwana Bashiru Ally, Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Hivi majuzi Bwana Bashiru alishiriki mjadala wa DW juu ya miaka 15 ya mapambano dhidi ya ugaidi. Msimamo na utetezi wa mtazamo wake juu ya jinsi vita hii inavyopiganwa nakubaliana nao kwa asilimia 100-"Mbinu zinazotumika kupambana na ugaidi ni za kigaidi na hivyo zinazidisha ugaidi"
Bwana Bashiru ni mtu aliyejipambanua kuwa na msimamo usiyoyumba katika masuala ya Kitaifa na yale yote anayoyaamini baada ya kuyatafiti kwa kina. Si mtu wa papara na kuropoka. Hisia zake juu ya jambo lolote hazijathibitika kufungamana na imani au itikadi. Kiufupi ni mtu-huru, mwenye fikra chanya kwa mustakhabari wa jambo lolote analoshiriki kulitenda au kulipendekeza. Tuna uhaba wa watu wenye sifa hizi katika utungaji wa sera na kuisimamia serikali. Kumuacha aendelee kuongea na makaratasi au kuwasilisha hoja zake kwa Power Point mikutanoni na kisha akitoka ukumbini hakuna wa kuzitekeleza ni matumizi mabovu ya rasilimali watu wa nchi hii.
Ili Taifa liweze kunufaika na weledi wa Bwana Bashiru, naomba ashawishiwe kujiunga rasmi na siasa za majukwaani na atafutiwe jimbo ili kuanzia 2016 inshallah Taifa linufaike na vipawa vyake. Binafsi sijali atajiunga na CHADEMA, CUF, NCCR, TLP, n.k ilimradi tu asijiunge na ccm, mahali ambako mawazo mapya na utendaji ni dhambi. Akitaka Jimbo nitamchagulia Bukoba Vijijini na nitakuwa tayari kuanza kumpigia kampeni. Naamini maeneo yenye wapiga kura wengi kama Ibwera na Katoro hatutakuwa nahaja kabisa ya kupita kupiga kampeni.
Eid Mubraak!
Cc: FaizaFoxy, Ritz, omar Ilyas, njiwa, Nivea