Mh. Zitto kuna ukweli gani katika ripoti hii?

Semeni hivi: "Huyo mzungu katumwa na CCM na alikatiwa ticket na CCM kutoka alikotoka kuja kufanya thesis yake Tanzania na walimwambia nini cha kufanya na nani wa kumuona na pia alikuwa mgeni wa CCM kote alikotembelea" Nawashangaa sana kuwa hilo hamlisemi? Nangoja.

Ngoja niwape maujanja CHADEMA:

Ikiwa hiyo habari ndio kama ilivyo na huyo mzungu au sijui kabila gani, hajakutana na Zitto ku verify basi hiyo habari itakuwa haina maana kabisa. Ni porojo tu kama porojo zingine.
Kama itakua kama ulivyosema wewe basi thesis za ulaya ni rahisi mno.
 
Nimekubaliana na wewe kabisa na suala la kodi limekuwa msimamo wangu kwa muda mrefu. Mchango wangu kwenye Bajeti kuu na ile ya nishati na madini nilisema hili wazi kabisa.

The reference to 'ring-fencing' referred to the paper is the theory I explained to the researcher and it paid off as tulawaka declared profit last year.

I have acted very transparently in this matter, at arms-lenght. Nani kasema corporate social responsibility watu wa kigoma hawana haki nayo?

I have never benefitted personally to any gift given by Barrick or any other mining company in Tanzania.

I am happy msaada walioutoa umewezesha kijiji cha Mkabogo kukamilisha majengo ya shule na hivyo kuwafanya watoto wa kijiji kile na kata ya Kalinzi kupata elimu ya Sekondari.

Wanaotaka kulifanya hili jambo la kisiasa sitawazuia hata kidogo. Lakini naomba lionekane kwa picha pana zaidi. Hata hivyo kama ikithibitika nimefaidika kwa namna yeyote mimi binafsi, nitawajibika

Hapo nilipoweka nyekundu, unataka ithibitike mara ngapi? wakati wewe mwenyewe umekiri kuwa hili ni kweli.
Una maana kama jimbo lako limefaidika wewe hujafaidika binafsi? kwani huo msaada aliuomba nani kwa Barrick? na nani aliwapa anuani za kupeleka huo msaada huko jimboni kwako? Kwa nini wasipeleke kabla hujaanza kukemea mikataba na wapeleke huo msaada baada ya wewe kupiga kelele?

Halafu unasema utawajibika ikithibitika na ilhali imeshathibitika kuwa umefaidika jimboni kwako. Na wewe ndio mbunge wa hilo jimbo lako. Kwanini usiwajibike ukapisha uchunguzi wa kina ili ujisafishe? Ithibitike nini zaidi ya hivi?
 
Zitto hana muda wa kujibu pumba zako.

Kwa kukusaidia, Zitto pamoja na kupata msaada wa mabati amekuwa na msimamo wake ule ule kuhusu sector ya madini hata kwa bunge lililopita. Tatizo wewe mvivu wa kuangalia vipindi vya Bunge. Bado nakushauri uache uvivu wa kutembelea blog ya zitto utajua mengi. Una kichwa kigumu sijui tutor wako anapata shida kiasi gani.
kaka yuor love for zitto is blinding you,..you seem to defend him even where he(zitto)has admitted failure..we all admire his courage lakini tunapohisi anakosea lazima tumweleze ukweli only to make him a better leader,..pamoja na upungufu wake uzalendo wa zitto ni wajuu ukilinganisha wanaccm wote except nyerere..
whatever it is msaada kutoka barrick to our law makers una aina flani ya conflict of interest
 
Hapo nilipoweka nyekundu, unataka ithibitike mara ngapi? wakati wewe mwenyewe umekiri kuwa hili ni kweli.
Una maana kama jimbo lako limefaidika wewe hujafaidika binafsi? kwani huo msaada aliuomba nani kwa Barrick? na nani aliwapa anuani za kupeleka huo msaada huko jimboni kwako? Kwa nini wasipeleke kabla hujaanza kukemea mikataba na wapeleke huo msaada baada ya wewe kupiga kelele?

Halafu unasema utawajibika ikithibitika na ilhali imeshathibitika kuwa umefaidika jimboni kwako. Na wewe ndio mbunge wa hilo jimbo lako. Kwanini usiwajibike ukapisha uchunguzi wa kina ili ujisafishe? Ithibitike nini zaidi ya hivi?
sasa hapa ndo umerukwa na akili gafla, nia ya mfanya research nikuonyesha kuwa Zitto kahongwa that y kasema kama wewe FF na wenzako mnaamini ivyo na mtadhibitisha basi atawajibika, Mtu ukiwa unabwabwaja bila kufikiri matokeo yake ni kuandika upupu kama huu ulioandika, Think criticaly.
@ Zito. Usijibu hili tafathali nimeshalimaliza.
 
Simlaumu Zitto kwa hili kwasababu amechukuwa maamuzi ya kisiasa.First ili aweze kuchaguliwa tena,ni lazima ajitahidi kuwin hearts za wananchi anaowawakilishi.However only kama atakuwa na msimamo kuwa wananchi wa maeneo yenye migodi hiyo pia wanufaike.Na kwa upande mwingine ni issue ya polution inayotokana na shughuli hizo za uchimbaji dhahabu.Hii issue tulishaijadili humu na hao Barricks walifukuzwa huko South America kwasababu hiyo.Lakini viongozi wetu hawajali kuhusu well being ya wananchi hao.Kingine ni faida kubwa wanayoipata hao Barricks.Inawezekanakabisa kwamba tukizisimamia rasilimali zetu vizuri tunaweza hata kulipa deni letu la Taifa.

Meanwhile, the Tanzanian government doesn't raise enough tax revenue to do its job. There's still no paved road crossing the country, one in ten children dies before turning five and according to a speech by president Kikwete in November 2010, only 14 per cent of Tanzanians have electricity. Debt stands at $11 billion as of December 2010, up $800 million from the previous year.

Barrick has some big numbers of its own, but they barely affect the country's budget. Tanzania exported $1.5 billion worth of gold in 2009, 40 per cent of the value of all Tanzania's exports, and most of that gold was Barrick's. But Barrick only paid $37 million in royalties and levies that year about one per cent of Tanzania's total tax revenue of $3.27 billion. Employees paid another $37 million in taxes on their salaries.
 
kaka yuor love for zitto is blinding you,..you seem to defend him even where he(zitto)has admitted failure..we all admire his courage lakini tunapohisi anakosea lazima tumweleze ukweli only to make him a better leader,..pamoja na upungufu wake uzalendo wa zitto ni wajuu ukilinganisha wanaccm wote except nyerere..
whatever it is msaada kutoka barrick to our law makers una aina flani ya conflict of interest
Tafathali naomba tusiite huu ni msaada, huu ni wajibu, haiwezekani mzungu aje kuchukua madini ya matrilioni ya fetha wakati kijiji kilichopo 600 km kutoka kwenye mgodi husika hakina madarasa ya kusomea. Huu ni wajibu na sio msaada rethink plz.
 
Watanzania hebu acheni majungu kajengeni nchi inaliwa na mafisadi. Mh Zitto yuko very straight and just, hakuna hoja ya msingi dhidi yake, ingekuwa nchi inajengwa kwa maneno Tz ingekuwa juu sanA maana watu mna miwiiivu! Kuna mengi sana ya kumshukuru Zitto. Kwanza hao Barrick mbona wanasaidia sehemu kibao tu. Zitto Mungu aendelee kukutia nguvu.
 
Hii ya Zitto ni cha mtoto (even if true). Kuna mtu anaweza kusema kwanini hadi leo hii hakuna hata police invistigation kuhusu mauaji ya wale watu watano huko Nyamongo na baadae maiti kutelekezwa barabarani? Kwa nini hakuna uchunguzi hata kama utasema marehemu 'walikuwa na makosa'? Why?

Then wakati wa kikao cha bunge hili la bajeti lililoisha hivi karibuni kuna special 'events' mbili ambazo ni tata:
1. Ubalozi wa Canada waliandaa chakula maalum kwa wabunge wote huko Dodoma kwa kisingizio kuwa wanasheherekea Canada day. Hata hivyo siku waliyotoa huo mnuso haikuwa 'days before' the actual Canada day! Na kipindi hiki kulikuwa bado na majonzi ya Nyamongo. Wabunge wamepata mnuso, Nyamongo killings forgotten?

2. Asha Doctor Migiro bado anaonekana kuvutiwa sana na siasa za bongo na hivi majuzi (wakati wa kikao cha bunge la bajeti) alikuwa Dodoma kwa another set of special 'events'. Lakini moja alikuwa mgeni rasmi kwenye mkutano mkuu wa Tanganyika Law Society (TLS). Mpaka hapo hakuna shida. But guess who was the main sponsor? - Barrick!

Sasa jumlisha, Wabunge wamepata mnuso, wanasheria wamepata push! Kama haitoshi vile, Balozi wa Canada baada ya hizi shughuli mbili kaenda kuwatembelea Media Council!!! Sijui anawaatakia nini hawa media na sjui kama kuna mtu huko Media Council aliweza kuanganisha TIMING ya ujuo wa huyo balozi na matukio ya Nyamongo. Nadhani hawa ndugu zetu walifikiri amekuja kuwasifia kuhusu utendaji wao wa kazi!

Sasa hivi tunaona tunayoona, kodi hakuna, mahusiano na wakazi wa maeneo ya migodi ni mgogoro, na wenye nafasi ya kurekebisha wanakaa kimya.

Mwisho, someni hapo kwenye red: Kodi za wafanyakazi zinalingana na royalties & levies za kampuni. What a coincedence?

But Barrick only paid $37 million in royalties and levies that year about one per cent of Tanzania's total tax revenue of $3.27 billion. Employees paid another $37 million in taxes on their salaries.

Hahahaha,hapa kwa majumuisho,ni rahisi kusema yafuatayo:-

1.POSHO HAIWATOSHI WABUNGE,WAONGEZEWE ANGALAO 500,000/= KWA SIKU
2.SHIBUDA HANA TATIZO,ASIBUGHUDHIWE
3.KILA MWENYE KISU AKATE NYAMA KUTOKANA NA MAKALI YA KISU CHAKE.

over,....over,....over
 
sasa hapa ndo umerukwa na akili gafla, nia ya mfanya research nikuonyesha kuwa Zitto kahongwa that y kasema kama wewe FF na wenzako mnaamini ivyo na mtadhibitisha basi atawajibika, Mtu ukiwa unabwabwaja bila kufikiri matokeo yake ni kuandika upupu kama huu ulioandika, Think criticaly.
@ Zito. Usijibu hili tafathali nimeshalimaliza.

Wewe useme halafu uniambie nisijibu na tuko kwenye open forum hapa, kama hutaki kujibiwa kaa utazame tu na usichangie.

Kama sio rushwa hiyo ni nini? kapewa huo msaada baada ya kuanza kupiga kelele kuhusu Barrick na si kabla. Ajibu maswali niliouliza au mjibie wewe.

Halafu nakuomba tafadhali sana, jibu hoja zangu lakini usinitukane binafsi hapo nilipokuwekea rangi nyekundu. Hunijui sikujui hapa tunabadilishana mawazo na kila mtu ana yake. Tafadhali chunga heshima yako nawe uheshimiwe.
 
Zitto Kabwe kwangu bado ni mwanasiasa shujaa ndio shujaa wangu! Namkubuli yupo straight, kwenye ili jambo alivyojitokeza na kujibu kwa kweli ni ushujaa wa hali ya juu.
Wale maadui zake wote walikuwa wamepata pakusemea kujibu kwako imezidi kukujenga, hakuna mwanasiasa Tanzania hanaweza kujitokeza kujibu shutuma juu yake
 
gold.jpg 266656-2872-51.jpg

Hii habari ni ya kweli kabisa. Huyo mwandishi (mtafiti) alinihoji na mie ndio niliweka wazi kuwa Barrick mwaka 2008 walinunua mabati kwa ajili ya shule ya Sekondari Mkabogo katika Jimbo la Kigoma Kaskazini. Sikuwahi kushika mkononi pesa hizo wala kushiriki kuamua zitumike namna gani. Niliamua hivyo kwa uwazi kabisa na ndio maana sikuwahi kuficha suala hilo na hata kuliweka wazi kwa mwanafunzi huyu ambaye alinihoji mwaka 2010.

Sijawahi kuwa kimya kabisa katika suala la sekta ya madini. Nilisimamia kuandikwa kwa sheria mpya na kuhakikisha inakuwa na maslahi kwa Watanzania. Nimekuwa mkali kutaka kampuni za madini kulipa mrahaba wa madini wa sasa kwa mujibu wa sheria mpya. Ukitembelea blog yangu utakuta hotuba zangu Bungeni zenye misimamo yangu ya wazi kabisa kuhusu sekta ya madini.

Nakaribisha mtu yeyote aende Jimboni kwangu, kijiji cha Mkabogo akafanya uchunguzi kuhusu msaada ule. Nipo tayari pia Halmashauri ya Wilaya waweke wazi account iliyopokea pesa hizo na kuweka matumizi yao wazi.

Mimi binafsi sijawahi kupokea msaada wowote binafsi kutoka kampuni ya Barrick. Siku zote nimekuwa na misimamo isiyoyumba kuhusu sekta ya madini na nimekuwa nikiwa engage sana Barrick ili Tanzania ifaidike na madini yake.

Hata hivi sasa ukienda kwenye blog yangu zittokabwe.com utakuta nimewasema Barrick kwa kutolipa kodi ya mapato. Niliwasema katika interview na huyo kijana kutoka Canada kuhusu jambo hilo na niliwasema katika mijadala ya vyuo vya elimu ya juu kuhusu madini.

Ninaamini makampuni yana jukumu la kusaidia jamii. Kwamba Barrick walisaidia ujenzi wa shule ya Sekondari Jimboni kwangu, Jimbo ambalo lipo nyuma sana kimaendeleo ni jambo la kushukuru na sioni tatizo lolote la kimaadili.

Hapo kwenye Red ndipo kwenye umaana haswa,naijua sekta ya madini kwa kuwa mimi nae nimepita huko.Michezo michafu ya wamiki wa migodi duniani na haswa afrika ni style ya Use and abuses.Zitto ulikuwa mpiganaji sana kwa kuwa mama Tanzania alikuelekezea akitaka upaze sauti ili kuwaamsha watanzania kujua kuwa wanaibiwa,hata wale waliokuingilia wewe wakati unapiga kelele za kuwaamsha waibiwaji waliazibiwa na asili [Nature] kiasi kuwa walikuacha na kushindwa kuzuia kishindo na mlipuko wako.

Lakini kwa wacheza michezo michafu ya madini yaani diamond and gold dealers walijaribu kuona wewe uko upande upi wa shillingi ili waweze kukutumia yaani use and abuses.Nawe pasipo kificho polepole ulianza kupunguza mwangwi na sauti yako ikaenda na mawimbi mazito ya gharika ya utamu wa asali ya madolali.Ulipoteza usikivu wako kwa jamii na kuonyesha kabisa kile ulichopigia kelele sasa kimepoteza rubani kijana ambae uenda angesimamia dhamira yake ya mwanzoni uenda kwa mara nyingine Taifa lingepata a true son of the country.

Baba wa Taifa a true son of the Country alijua kuwa Nchi bado ni changa na kuwa alikuwa na wasomi wachache ambao wasingeweza kufanya utilization ya madini kwa elimu ndogo na ujuzi mdogo waliokuwa nao hivyo kuchukua jukumu la kuyalinda mpaka true sons wengine watakapozaliwa na kutambua umhimu wa madini hayo na faida zake kwa Taifa.Na kwa kuzingatia kuwa watakuta technlojia imekuwa na uongozi bora upo basi wangechuma mali hiyo kwa faida yao na vizazi vyao na kwa faida ya Taifa lao.

Lakini bidii za usaliti wa kutumiwa na kumsaliti mama Tanzania na watu wake,hakika kilio chake ni kikubwa na kwa kuwa what goes around comes around ni asilia [nature] na basi usaliti huo utawaludia wale wote waliopata support ya umma kiasi cha kuwa wale wote waliokuingilia Zitto wakati unapigania mali ya Watanzania waliazibiwa na sauti ya kilio chako na cha umma wa Watanzania waliokuwa nyuma yako daima wakati unapiga kelele za mwizi wa ,mali yetu.

Utawadanganya watu fulani wakati fulani bali utawadanganya watu wote wakati wote.ukweli utadhihili na uongo utajulikana,najua na nina hakika ufahamu michezo michafu ya diamond and gold dealers.Moja ya sifa zao ni use and abuses,japo uwezi kuona mahusiano ya kijana mhandishi kutoka canada na makapuni hayo ya madini ya kutoka huko kwao Canada ,lakini hakika hiyo ndio style yao.Wanakutumia kisha wanakumwaga kwa style ambayo uwezi kuunganisha matukio hayo kuwa wahusika ni wao.Ukiendelea kubisha dogo huyo atatumwagia mpaka account namba ya madolali kama sio ya uko kwao hata ujerumani ikibidi.Hiyo yote ni mikakati ya hawa wadau na michezo yao ambayo mala nyingi viongozi wengi wa africa uwa awaelewi pamoja na kuwa viongozi wengi wa Africa kama Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa Zabanga za Zaire ,Jonas Malheiro Savimbi wa Angola au Charles McArthur Ghankay Taylor wa Liberia hawa wote walitumika na wakaiishia kumwagwa na kutendewa unyama mkubwa.Hiyo ndio asili ya madini yetu ya Afrika,ni Baba wa Taifa letu na viongozi wachache wa sana wa Africa kama Festus Mogae walibaki na wanabaki kuwa true son wa Taifa na tunaendelea kuwaenzi kwa kuyalinda na kuyatumia kwa haki na kuleta ustawi kwa jamii usiotiliwa shaka hata kidogo na kwa faida ya wote.

Siko hapa kukuhukumu ila kama umetudanganya,what goes around comes around man.
Sasa hivi hizo ni mvua za lasha lasha zitakapoanza kunyesha ndio itafahamika.

Time will tell!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mkuu msaada kweli ni msaada tu hauna haki.Na ninajua kuwa migodi na rasilimali zingine ni lazima zinufaishe taifa kwa ujumla wake.Sipingi mgodi wa barick kusaidia jimbo la kigoma kaskazini kwani ni Tanzania pia.Concern yangu ni kwa kuzingatia historia ya zitto na barick zitto hakuona kuna kuonekana kama ananyamazishwa hata kama sio kweli?

Mkuu kweli unavyosema lakini nimejaribu kutokuwa biased na kutazama pande mbili za shlingi. Ningekuwa ziito najua ningefanya hivyo hivyo japo kw njia tofauti

Ndio maana nilimuuliza hili swali zito

Kwani nini hiyo proposal alinadika kwenye hiyo kampuni na sio wa NSSF CRDB, TBL, VICfish? NAona limekuwa gumu .
 
Aside from not receiving corporate income tax, Tanzania actually owes Barrick millions. In Tanzania, companies pay a "value-added tax" similar to Canada's GST when they buy goods and services and import fuel.As in Canada, the government owes a refund when companies pay more VAT than they collect from their customers. Barrick has no Tanzanian clients so it's entitled as of December 2010 to a total refund of $121 million that Tanzania over-collected over the years and can't afford to repay. It's more than one per cent of the country's official debt.
Huu kama si wendawazimu ni kitu gani?Yani kwanza eti wao ndiyo wana tudai,tena $121 millions.

Kweli hatuna viongozi.Ukiangalia hakuna tofauti kubwa na mangungo deals za back in a day.

Yani madini yenu lakini mnachezewa kama mijinga na sasa taifa linadaiwa na watu wanaochota rasilimali zetu. Ina maana sasa watazichota bure kwa muda mrefu sana.Kampuni ambayo total export yake inachukua 40% of the value of total National export halafu eti hawalipi corporate tax na pia total tax payment yao in terms of "royalties and levies" ni only 1% of total tax revenue.

Si ujinga huu ni kitu gani?Tunaliwa kote kote tu.Hawa waliotuingiza huu mkenge hawatufai kabisa.
 
Wewe useme halafu uniambie nisijibu na tuko kwenye open forum hapa, kama hutaki kujibiwa kaa utazame tu na usichangie.

Kama sio rushwa hiyo ni nini? kapewa huo msaada baada ya kuanza kupiga kelele kuhusu Barrick na si kabla. Ajibu maswali niliouliza au mjibie wewe.

Halafu nakuomba tafadhali sana, jibu hoja zangu lakini usinitukane binafsi hapo nilipokuwekea rangi nyekundu. Hunijui sikujui hapa tunabadilishana mawazo na kila mtu ana yake. Tafadhali chunga heshima yako nawe uheshimiwe.

He yamekuwaje tena? umkalim kama pilpili kichaa, hebu taratibu bibi wee. Unacheza na mbwa ingia nae msikitini usihamaki hee.
 
Hapo nilipoweka nyekundu, unataka ithibitike mara ngapi? wakati wewe mwenyewe umekiri kuwa hili ni kweli.

Una maana kama jimbo lako limefaidika wewe hujafaidika binafsi? kwani huo msaada aliuomba nani kwa Barrick? na nani aliwapa anuani za kupeleka huo msaada huko jimboni kwako? Kwa nini wasipeleke kabla hujaanza kukemea mikataba na wapeleke huo msaada baada ya wewe kupiga kelele?

Halafu unasema utawajibika ikithibitika na ilhali imeshathibitika kuwa umefaidika jimboni kwako. Na wewe ndio mbunge wa hilo jimbo lako. Kwanini usiwajibike ukapisha uchunguzi wa kina ili ujisafishe? Ithibitike nini zaidi ya hivi?
Sitaki na sipendi kuamini kuwa kichwani mwako kuna ugoro badala ya ubongo kwa jinsi unavokuwa mgumu kuelewa aidha kwa makusudi au ndo kipaji chako cha kutoelewa! inaelekea we ni mtu mzima lakini bado unavaa nepi! hujui tofauti kati ya mtu kufaidika binafsi na manufaa ya jamii? hivi rais jk alipoomba msaada wa kujengewa udom ilikuwa kwa manufaa binafsi au kwa taifa? na ungesemaje kama angemmlikisha mkewe- mama salma au mwanawe ridhiwani?
 
Hii ya Zitto ni cha mtoto (even if true). Kuna mtu anaweza kusema kwanini hadi leo hii hakuna hata police invistigation kuhusu mauaji ya wale watu watano huko Nyamongo na baadae maiti kutelekezwa barabarani? Kwa nini hakuna uchunguzi hata kama utasema marehemu 'walikuwa na makosa'? Why?

Then wakati wa kikao cha bunge hili la bajeti lililoisha hivi karibuni kuna special 'events' mbili ambazo ni tata:
1. Ubalozi wa Canada waliandaa chakula maalum kwa wabunge wote huko Dodoma kwa kisingizio kuwa wanasheherekea Canada day. Hata hivyo siku waliyotoa huo mnuso haikuwa 'days before' the actual Canada day! Na kipindi hiki kulikuwa bado na majonzi ya Nyamongo. Wabunge wamepata mnuso, Nyamongo killings forgotten?

2. Asha Doctor Migiro bado anaonekana kuvutiwa sana na siasa za bongo na hivi majuzi (wakati wa kikao cha bunge la bajeti) alikuwa Dodoma kwa another set of special 'events'. Lakini moja alikuwa mgeni rasmi kwenye mkutano mkuu wa Tanganyika Law Society (TLS). Mpaka hapo hakuna shida. But guess who was the main sponsor? - Barrick!

Sasa jumlisha, Wabunge wamepata mnuso, wanasheria wamepata push! Kama haitoshi vile, Balozi wa Canada baada ya hizi shughuli mbili kaenda kuwatembelea Media Council!!! Sijui anawaatakia nini hawa media na sjui kama kuna mtu huko Media Council aliweza kuanganisha TIMING ya ujuo wa huyo balozi na matukio ya Nyamongo. Nadhani hawa ndugu zetu walifikiri amekuja kuwasifia kuhusu utendaji wao wa kazi!

Sasa hivi tunaona tunayoona, kodi hakuna, mahusiano na wakazi wa maeneo ya migodi ni mgogoro, na wenye nafasi ya kurekebisha wanakaa kimya.

Mwisho, someni hapo kwenye red: Kodi za wafanyakazi zinalingana na royalties & levies za kampuni. What a coincedence?

But Barrick only paid $37 million in royalties and levies that year about one per cent of Tanzania's total tax revenue of $3.27 billion. Employees paid another $37 million in taxes on their salaries.
Baada ya kusoma hayo, sasa naanza kuunganisha dots, Ni ubalozi wa Canada ndio main sponsors kwa study tour za abroad kwa Media Council.
Nilibahatika kuingia kwenye moja ya selecting panel ya kuchagua waandishi wa kwenda study nje ya nchi, kwanza hao Wacanada wakalazimisha lazima hiyo sponsorship ipitie MCT, MCT wakaleta majina ya wale wazee wao, mimi hili nililipinga kwa nguvu zangu zote nikisisitiza wapewe nafasi waandishi vijana ambao ni active kwenye media, niliwablend hao wazee wa MCT kuwa ni 'spent force', Wacanada wakang'ang'ana na wazee wale, sasa ndio naanza kupata picha!

Ile sherehe ya siku ya uhuru wa habari ya Mwaka juzi, iliyofanyika pale hoteli moja pale Mnazi Mmoja, main sposor ni ubalozi wa Canada na alikuja balozi mwenyewe!. Sponsor wa pili ni mzee wetu mkarimu mmiliki wa media house kubwa nchini. Nilipopata wasaa kuchangia, niliwabamiza MCT wao kama regulator, kwanini wafadhiliwe na media house moja, nikaorodhesha baadhi ya madudu ya hiyo media mbele ya mmiliki, nikazimiwa kipaza sauti na kuambiwa, kauli zangu zitaonyesha ukosefu wa shukrani kwa waliotoa fedha zao. Wakati wa kupata vinywaji balozi wa Canada alizungumza nani kujua kwa nini naiblast MCT, nilimweleza.

Mwaka huu katikati, nilikuwa approched na Ubalozi wa Canada wakanipa offer ya kuwa Political Advisor na kuahidi kunilipa pesa yoyote, very unfortunately I refused thier offer because I had other plans of my own, sisi wengine, tutajifia masikini na patriotic pride kwa taifa letu, nikiangalia kumbe mambo yenyewe ni haya, sijutii kuikataa job offer yao, najisikia heri kubaki masikini jeuri kuliko kuuza utu na utaifa wetu kwa shibe ya siku moja!.

Binafsi Zitto namuaminia sana, na pia niliamini yuko bold enough to stand any test in time, aliposhambuliwa mwaka jana kuhusu abrupt personal gain ya jumba masaki, hammuer, vogue na vx kadhaa, aliorodhesha income zake ku justfy ila pia akaisusa rasmi jf, nikamsisitia kwa boldness yake, hakuwa na sababu ya kususa, alisema bado hutembelea sana jf as a guest na atachangia pale tuu, patakapobidi sana.

Wakati tukiendelea kusubiri majibu ya Zitto, wana jf, naomba tukubali, kwenye mapambano, ukijiona huwezi kuwashinda adui zako, ama una surrender, ama una retreat. Ile formular ya no retreat no surrender, ni fomuler ya kupigana mpaka risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu limemwagika but at the end of the day, utasifiwa umekufa kishujaa but you are dead!. Inawezekana Zitto baada ya kujua hawezi kuwashinda, alitumia ile option ya "if you can't beat them, join them" tumpe benefit of doubt kuwa amekubali ili kuwainua wanaKogoma kielimu hivyo sasa Kigoma hawadanganyiki tena ndio maana CCM imepata kipigo, hivyo kujustify kupokea chochote kitu cha Barrick watoto wasome!.
 
Wewe useme halafu uniambie nisijibu na tuko kwenye open forum hapa, kama hutaki kujibiwa kaa utazame tu na usichangie.

Kama sio rushwa hiyo ni nini? kapewa huo msaada baada ya kuanza kupiga kelele kuhusu Barrick na si kabla. Ajibu maswali niliouliza au mjibie wewe.

Halafu nakuomba tafadhali sana, jibu hoja zangu lakini usinitukane binafsi hapo nilipokuwekea rangi nyekundu. Hunijui sikujui hapa tunabadilishana mawazo na kila mtu ana yake. Tafadhali chunga heshima yako nawe uheshimiwe.

Okey swali lako la awali nimeshamjibia Zitto, uliza swali lingine la msingi alafu acha jazba kijana.
 
Kama hili suala sio rushwa au harufu ya rushwa, basi rushwa imekwisha duniani! Kwanini community responsibility iwe kwa Barrick na sio TBL wenye mapato makubwa zaidi (yes, wanalipa kozi kubwa kuliko kampuni zingine)? Kwanini isiwe Vodacom, Airtel, Tigo? Barrick and Zitto-very convenient!
 
Baada ya kusoma hayo, sasa naanza kuunganisha dots, Ni ubalozi wa Canada ndio main sponsors kwa study tour za abroad kwa Media Council.
Nilibahatika kuingia kwenye moja ya selecting panel ya kuchagua waandishi wa kwenda study nje ya nchi, kwanza hao Wacanada wakalazimisha lazima hiyo sponsorship ipitie MCT, MCT wakaleta majina ya wale wazee wao, mimi hili nililipinga kwa nguvu zangu zote nikisisitiza wapewe nafasi waandishi vijana ambao ni active kwenye media, niliwablend hao wazee wa MCT kuwa ni 'spent force', Wacanada wakang'ang'ana na wazee wale, sasa ndio naanza kupata picha!

Ile sherehe ya siku ya uhuru wa habari ya Mwaka juzi, iliyofanyika pale hoteli moja pale Mnazi Mmoja, main sposor ni ubalozi wa Canada na alikuja balozi mwenyewe!. Sponsor wa pili ni mzee wetu mkarimu mmiliki wa media house kubwa nchini. Nilipopata wasaa kuchangia, niliwabamiza MCT wao kama regulator, kwanini wafadhiliwe na media house moja, nikaorodhesha baadhi ya madudu ya hiyo media mbele ya mmiliki, nikazimiwa kipaza sauti na kuambiwa, kauli zangu zitaonyesha ukosefu wa shukrani kwa waliotoa fedha zao. Wakati wa kupata vinywaji balozi wa Canada alizungumza nani kujua kwa nini naiblast MCT, nilimweleza.

Mwaka huu katikati, nilikuwa approched na Ubalozi wa Canada wakanipa offer ya kuwa Political Advisor na kuahidi kunilipa pesa yoyote, very unfortunately I refused thier offer because I had other plans of my own, sisi wengine, tutajifia masikini na patriotic pride kwa taifa letu, nikiangalia kumbe mambo yenyewe ni haya, sijutii kuikataa job offer yao, najisikia heri kubaki masikini jeuri kuliko kuuza utu na utaifa wetu kwa shibe ya siku moja!.

Binafsi Zitto namuaminia sana, na pia niliamini yuko bold enough to stand any test in time, aliposhambuliwa mwaka jana kuhusu abrupt personal gain ya jumba masaki, hammuer, vogue na vx kadhaa, aliorodhesha income zake ku justfy ila pia akaisusa rasmi jf, nikamsisitia kwa boldness yake, hakuwa na sababu ya kususa, alisema bado hutembelea sana jf as a guest na atachangia pale tuu, patakapobidi sana.

Wakati tukiendelea kusubiri majibu ya Zitto, wana jf, naomba tukubali, kwenye mapambano, ukijiona huwezi kuwashinda adui zako, ama una surrender, ama una retreat. Ile formular ya no retreat no surrender, ni fomuler ya kupigana mpaka risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu limemwagika but at the end of the day, utasifiwa umekufa kishujaa but you are dead!. Inawezekana Zitto baada ya kujua hawezi kuwashinda, alitumia ile option ya "if you can't beat them, join them" tumpe benefit of doubt kuwa amekubali ili kuwainua wanaKogoma kielimu hivyo sasa Kigoma hawadanganyiki tena ndio maana CCM imepata kipigo, hivyo kujustify kupokea chochote kitu cha Barrick watoto wasome!.
Kazi kweli kweli,ina maana Zitto amelegeza kamba dhidi ya udhalimu huu wa Barricks?
 
Ukali? Ukali wa namna gani sasa? Nilikuwa mkali kwenye mkataba wa Buzwagi. Hapajasainiwa mkataba mwingine wa madini toka Buzwagi. Kuna sheria mpya ya madini. Tulawaka wameanza kulipa kodi, resolute wameanza kulipa kodi.

Bungeni, hili Bunge la juzi tu nimetaka kuwe na windfall tax kwenye madini (hotuba yangu ipo zittokabwe.com).
Bungeni katika hotuba ya Wizara ya Nishati na Madini nimemtaka Ngeleja atoe notice kwa mining companies kuhusu new royalty rates waanze kulipa.

Hotuba yangu ipo katika blog yangu zittokabwe.com! Ukali upi unaousema sasa?
Lakini jambo la muhimu sana kujua katika siasa, a politician grows. I do. I must graduate from being a divisive figure to a uniting figure.

I must understand the sector and engage them. I have been doing that. Siwezi kuwa mpayukaji tu.

So far so good; but mind you the problem arises when you start engaging your so called adversaries and it is here that they start giving you saville Row suits [ mabati ya shule] as presents and they shut you up!! You call that growing up politically!! You are a corrupt politician pure and simple toka enzi za rushwa uliyopewa na DOWANS!!
 
Back
Top Bottom