Spika Makinda: Sasa tunaendelea na majadiliano kuhusu bajeti ya wizara ya miundombinu,Anayeanza kuchangia kwa asubuhi ya leo Mheshimiwa Diana Chilolo,Atafuatiwa na Mheshimiwa Peter Serukamba,Kangi Lugora na Suzanne Lymo.
Diana Chilolo: Mheshimiwa Supika,Nashukuru kwa kunipatia nafasi ya kuchangia kwenye bajeti hii ya wizara ya miundombinu.Kwanza kabisa napenda kumpongeza waziri Makufuri kwa Kazi nzuri sana anayoifanya ya kuhakikisha nchi yetu inapata miundombinu iliyo bora na ya kisasa kabisa,Kwakweli nampongeza kwa hilo waziri Makufuri kwani ni jembe hasa.
Mheshimiwa Supika,Pamoja na pongezi hizo lakini pia jimbo langu limekuwa katika kilio cha muda mrefu juu ya miradi ya barabara ambayo serikali yetu iliahidi kuikamilisha lakini huu mwaka wa kumi sasa hakuna kilichofanyika.
Mheshimiwa waziri we we mwenyewe ni shahidi mwaka Jana mwezi wa kumi na mbili ulikuja katika jumbo langu na nikakutembeza na nadhani mwenyewe umejionea hali ya barabara jinsi ilivyokuwa mbaya,Na uliniahidi kwenye bajeti ijayo miradi ya barabara kwenye jimbo langu itatengewa fungu la fedha lakini nikiangalia kwenye hiki kitabu cha bajeti ya wizara yako ninaona tu jina la jimbo langu lakini sioni fungu la fedha lilotengwa kwaajili ya miradi ya barabara ya jimbo langu,Sasa sijui ndiyo kusema umetudharau mimi na wale ninaowakilisha kwenye langu au Vipi?Baada ya kusema hayo niseme tu kwamba nakushukuru Mheshimiwa Supika kwa kunipatia fursa hii ya kuchangia kwenye hoja iliyoko mezani na ninamalizia kwa kusema...
Ninaunga mkoani hoja kwa asilimia mia moja (Anapigiwa makofi kwa nguvu ikifuatiwa na vigelegele kama vile wako kwenye SEND OFF wakiongozwa na Mheshimiwa Asha Bakari).