Mh. Rais, Wizara ya Afya ni ka "Empire" ka Madaktari, Kuna "Mfumo Daktari" Ulioota Mizizi

Kuna Dr alikua na duka la dawa sasa alimweka muuzaja Wa dawa hana elim ya dawa kiasi kwenye duka lake aliweka ad Huduma ya sindano.kuna mgonjwa alimwambia aende duka la dawa akachome sindano.sasa yule mhudum hana elimu yoyote alimchoma mgonjwa akaanza kuishiwa nguvu ad akapoteza fahamu
Aiseee
 
Uongozi unahitaji umekaa darasani miaka mingapi?

Kwahiyo kwakua MD anakaa mi5 ndio awe superior?

Kwahiyo Magu kwakuwa ni Chemistry iliyokaa darasani miaka 8 hawezi kuwa raisi mbele ya maprofessor wa Kemia?

#YNWA
Naona unachanganya mafaili kwa sana.
 
Yani hierrachy nzima ya wizara wameshika madaktari ndio matokeo yake haya.

Ukienda India kila hospitali ina kiwanda chake kidogo cha kutengeneza dawa, hakuna hospitali wananunua dawa nje na hapo. Hizi dripu na vizagavizaga vingine ni simple sana kutengeneza lkn nashangaa sijui tunakwama wapi.

Dripu nyingi tunazotumia hapa Tanzania zinatoka hapo Uganda tuu, pia niliwahi kuona Tumbi Hospital ya pale Kibaya mkoani Pwani wanatengeneza dripu zao.
Wafamasia wanafanya nini ? Wanatoa dawa tu pale dirishani ?
 
Naelewa vyotee, ILA nachouliza...
Is that a treating post or a leading post?

#YNWA
Liverpool unaniangusha kwenye kuelewa.. Kwenye hospital hakuna leading wala treating post. kuna job tasks,
Uongozi wa hospital unaendeashwa kwa Guidelines, Health management ambazo unakanidhiwa na wizara. you operate within the protocols. uwe na kipaji au usiwe,
leading imekaa kisiasa zaidi, maana inabidi uwe na ushawishi
 
Kwanza kwa heshima na taadhima nakusalimu na kukupa pole Mh. Rais kwa kazi nzito ya kuwaongoza watanzania na taifa kwa ujumla.

Mimi sio mwandishi mzuri saana Mh. lakini naomba nikupe hints chache tuu ili ujue na watu wajue ni kwa jinsi gani humo wizara ya afya kuna ki empire kimejengwa ambapo kwa namna moja ama nyingine kina negative impacts kwa jamii.

Kwanza kwenye wizara, nafasi za juu pale, yani top layer karibia yote wameshikilia madaktari, hakuna kada nyingine japokuwa wana vigezo sawa na hao madaktari.

Tukiachana na waziri pamoja na naibu wake ambazo ni nafasi za kisiasa (lakini wote ni madaktari), nafasi zingine za juu pale wizarani zimekaliwa na madaktari pia. Directors karibu wote ni madaktari.

Ukija kwenye hospitali zote pia wakuu wake wanakuwa ni madaktari. Sidhani kama kuna hospitali hapa nchini mkuu wake ni kada tofauti na udaktari. Mh. tukumbuke uongozi ni nafasi ya kuteuliwa haihitaji uwe umesomea kada fulani bali uwe na ujuzi na uwezo wa kuongoza. Lakini huko mahospitalini automaticaly madaktari wameshajiwekea dhana kwamba wao ndio wanapaswa kuongoza hospitali. Hakuna cha muuguzi, mfamasia wala mtaalamu wa maabara anayeruhusiwa kuongoza hospitali hata awe na sifa sawa na daktari.

Sio kwamba napinga wao kuwepo hapo, hapana. Ila najaribu kuwaza tuu ina maana kada zingine hamna wenye vigezo vya kushika hizo nafasi mpaka wao tuu washike.

Huu mfumo umepelekea maamuzi mengi sana yanafanyika kwa upendeleo na madaktari wanapeana favor zaidi kupita kada zingine. Angalia hata nafasi za kusoma level za juu wanaopata ufadhili wengi ni madaktari.

Pili, kutokana na "mfumo daktari" huu hapo wizarani, umepelekea wao kujiamulia mambo wanavyotaka bila kuogopa sababu wanajua hapo juu yupo wa kuwatetea hivyo hawagusiki.

Mathalani, ukienda hospitali nyingi za umma kwenye inpatients wards madaktari hawakai kabisa. Wakishapita ward rounds ile asubuhi kufika saa sita wanakuwa wameshapotea wanabaki wauguzi tuu. Hata ikitokea dharura yeyote wanaohangaika na mgonjwa ni wauguzi, na wagonjwa wengi sana wanafariki bila daktari kuwepo, mgonjwa akishafariki ndio daktari anaitwa kuja kuidhinisha kifo na sio kumuokoa mgonjwa. Mida ya usiku ndio hali ni mbaya zaidi kwani hata daktari akiitwa kuja ni mpaka asubuhi.

Tukija kwenye scenaria ya huyo daktari aliyekimbia hapo Tabora na kwenda Dar, kwanza kwa upande wangu Mh. naona kama amefanya fair kuweka wazi kaacha kazi. Mh. Rais naomba utambue 80% ya madaktari wa hospitali za umma wana vijiwe.

Na hivi vijiwe ndiyo wanavipa priority zaidi kuliko vituo vyao rasmi vya kazi. Asubuhi wakishapita round huko vituo vyao vya kazi basi kuanzia mida ya saa nne/tano wanaenda huko vijiweni(private hospitals) ambako wanakaa full-time. Sasa mimi naona bora huyu aliyeacha kabisa kuliko hawa wanaoendelea kula kodi zetu kwa geresha tuu huku muda mwingi wakiutumia huko private.

Pia hawa madaktari kingine kibaya zaidi wanachofanya huwa ni kuhama na wagonjwa kutoka hospitali za umma na kwenda nao huko vijiweni kwao. Mfano anaweza kuja mgonjwa kwenye hospitali ya umma akaonwa na daktari, lkn ataambiwa kwa vipimo na huduma kamili tuonane siku fulani kwenye hospitali fulani. Wakati anachoenda kufanyiwa huko private hospital pia kinafanyika kwenye hiyohiyo hospitali ya umma. Wanachoahidiwa huko private ni kwamba ukileta mgonjwa basi unakuwa na "cha juu".

Lakini haya yote hakuna wa kuyachukulia hatua madhubuti sababu kwenye uongozi mzima wameshikilia wao kuanzia wizarani mpaka huku chini kabisa. Hawa kada zingine hata wakijaribu kupeleka malalamiko wanaishia kuzimwa maana kote kuna "mfumo daktari".

Hivyo Mh ukitaka kuiponya hii sekta ya afya anza na kuvunja vunja huu "mfumo daktari" kwanza ndio tutapiga hatua kwenye hii sekta.

Ni hayo tuu kwa sasa Mh. Rais.
Shida siyo kuongozwa na daktari, issue ni watu kutokutimiza wajibu! Huko private haukuti madaktari wa umma bali kuna mafamasia, manurse, mateknishiani wa umma! Ni kutokutimiza wajibu kwa hao waliokasimiwa madaraka!
 
Sasa ata kama miongozo muhimu kwenye sekta ya afya hauijui sijui nikusaidieje. DMO is for medical officers, hadi pale itakavyoelekezwa vinginevyo.
Kwani kushare link itakuaje?

Maana mimi navyoona huku kwa Masters yangu tu kama naongoza idara ya Fedha nashindwaje kuongoza idara ya afya?

Ambacho amenishinda huyu DMO ni kujua medical nouns tu ambazo mi nina uhakika nilikaa ofisini kwake mwezi tuu naongeza hii ofisi ya DMO.

Kipi kinamfanya Nursing, Radiograph, N.k wasiwe leaders?

#YNWA
 
'Wabena' wanasema "Well said" !

Wafamasia nadhani ndio kundi la wataalam wa Afya wasiotambulika kabisa Tanzania licha ya kuwa ni kada muhimu sana! Nchi kama USA Wafamasia wanawapiku Madaktari kwa kukubalika kwa wananchi! Tz muulize mtu kuwa Mfamasia anafanya nini hajui!
Mimi nikiandikiwa dawa na daktari sinunui hadi nipate maelezo ya mfamasia.
 
Kwani kushare link itakuaje?

Maana mimi navyoona huku kwa Masters yangu tu kama naongoza idara ya Fedha nashindwaje kuongoza idara ya afya?

Ambacho amenishinda huyu DMO ni kujua medical nouns tu ambazo mi nina uhakika nilikaa ofisini kwake mwezi tuu naongeza hii ofisi ya DMO.

Kipi kinamfanya Nursing, Radiograph, N.k wasiwe leaders?

#YNWA
Hiyo documents haipo oinline isipokuwa unaweza ipata halmashauri,kwani muongozo ulivyotoka ilitumwa kwenye halmashauri zote.
Kuhusu wewe kuwa DMO unaweza tena vizuri tu, cha muhimu pambana kwanza kubadilisha muongozo ili utambulike.
 
Ye kauliza "Kwani MD anakaa darasani miaka mingapi?"

Kwahiyo alichomaanisha, kwakuwa MD anakaa miaka mi5 basi ndio maana yupo superior kuliko wenzake.

#YNWA
alafu ukaleta habari za chemistry sijui kuwa raisi sijui kuwaongoza PhD.
 
Hiyo documents haipo oinline isipokuwa unaweza ipata halmashauri,kwani muongozo ulivyotoka ilitumwa kwenye halmashauri zote.
Kuhusu wewe kuwa DMO unaweza tena vizuri tu, cha muhimu pambana kwanza kubadilisha muongozo ili utambulike.
Link tafadhali
afya.go.tz au tamisemi.go.tz AU ...........?

#YNWA
 
Nurse haujaelewa tu, haipo online ukitaka hard copy unaweza tumiwa tu inbox.
Bro every general rule has got it's exception.

Ulete hapa tujadili wazi kwenye post na raia wacomment.

Hakuna uchawi "Every thing is documented and IN EVERY GENERAL RULE THERE IS AN EXCEPTION""

#YNWA
 
Bro every general rule has got it's exception.

Ulete hapa tujadili wazi kwenye post na raia wacomment.

Hakuna uchawi "Every thing is documented and IN EVERY GENERAL RULE THERE IS AN EXCEPTION""

#YNWA
Haujakomaa, naona unabwanjabwanja tu, unawaaibisha nurse wenzako.
 
Back
Top Bottom