Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,694
787
Awali ya yote, kwa muda sasa nimejaribu sana kuangalia execution ya mamlaka na madaraka ya Rais na Waziri mkuu wa jamhuri kulingana na katiba ya sasa. Na kuna wakati nimeendelea kuona kwamba mara nyingi Marais wa Nchi yetu wamekuwa wakifanya kazi za waziri mkuu aidha kwa kupenda au kwa udhaifu wa Rais au udhaifu wa Waziri Mkuu au wote kwa pamoja.

Kwa nini?
Katiba inasema Waziri Mkuu ndio mtendaji/mtekelezaji wa kazi zote za kila siku za serikali. Katiba pia inasema Rais ndiye Amir Jeshi mkuu na Kiongozi wa Nchi... napenda kutafsi kama mtu wa mwisho kwenye organization hierarchy.

Utata na mazoea kama sikosei.
Leo utaona Rais ndiye mwenye kujibu masuala ya utendaji wa kila siku wa serikali mfano, hali ya mvua na chakula, umeme, etc. tena ati kila mwezi... ukiangalia hapo juu haya ndio mambo ya day-2-day ya serikali ambayo yangekuwa yanasemewa na Waziri Mkuu, na wahariri na waandishi wa Habari wangekuwa wanambana waziri mkuu kwa mujibu ya katiba yetu ya sasa.
Pili ieleweke wazi kwamba serikali kwa maana baraza lote la mawaziri likiwa dhaifu pale MJENGONI kuna kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu na kwa maana nyingine serikali ikiwa haitekelezi waziri mkuu ndiye wa kwanza kuondoka na baraza lake la mawaziri wakimuachia Rais tena kutea waziri mkuu na baraza lake jipya.
Kwa maana hiyo nilikuwa nitegemee zaidi kwa yale ya utekelezaji yatoke kwa Waziri Mkuu na sio kwa Rais.

Rais ni mtu wakutuambia mambo yaliyoshindikana, mambo ya community reconciliation, mambo ya utulivu wa nchi, mambo ya nje, mambo ya Macro Economics Policy and Framework especially pale zinapochenji....

Mfano Suala la Katiba sadakta limefanywa vizuri na Rais wetu JK, lakini simtegemei kuzungumzia mambo ya kila siku ya utekelezaji, kufungua benki zenye mitaji ya milioni mia mbili...etc. etc.

Majumuisho:
Mh. Rais tangu aingie hiki kipindi cha pili naona dalili kama ataachia baraza lake la mawaziri liwajibike na yeye abaki kama mkuu wa nchi, kwa maana nyingine hatuhitaji hotuba 12 kwa mwaka... lakini tunahitaji waziri mkuu aongee na wahariri na kadhalika mara kwa mara kuelezea serikali inavyotenda mambo yake.

Mh. Rais tunataka kukusikia pale tu ambapo Waziri Mkuu wako atakuwa ameshindwa jambo... au jambo lenyewe ni kubwa... ndio maana wizara zako ni Ulinzi, Mambo ya Nchi... Uchumi, Mahusiano ya Jamii etc.
 
thread nzuri..... ila sio rais wangu so nakuomba ubadilishe kila sehemu ambayo umeandika rais na kuweka jina lake la Kikwete please ...
Nitakugongea 10X
 
Asante kwa thread nzuri, hivi huyu jamaa hua anaskia na kuelewa kweli? hata hivyo kuna kujichanganya sana, kila mtu serikali ni mtoa kauli...katiba mpya hakuna, mwingine mpya inakuja, mwingine haiwezekani, pinda kabaki neutral, Jk katiba mpya inakuja! pambaf kabisa
 
Asante kwa thread nzuri, hivi huyu jamaa hua anaskia na kuelewa kweli? hata hivyo kuna kujichanganya sana, kila mtu serikali ni mtoa kauli...katiba mpya hakuna, mwingine mpya inakuja, mwingine haiwezekani, pinda kabaki neutral, Jk katiba mpya inakuja! pambaf kabisa

Kama umezoea kutukana wazazi wako hasa baba yako,basi usiendeleze tabia hiyo kwa wengine! Kikwete ni Rais wa Tz na anahaki ya kuheshimiwa! Tafadhali hiki sio kijiwe cha wavuta bangi,nenda huko kwenye face book ukatukane! sio ustarabu
 
Tatizo lake hapendi kufunikwa na PM

Pili PM wetu wa sasa ni Harmless nilitegemea angekuwa Magufuli ..lakini wapi?

Swadakta maelezo yako, PM anatakiwa atekeleze na hivyo anatakiwa mtu mkali siyo goigoi kama huyu wa sasa.
 
Haya jamani suala la ag jaji werema kusema mjadala wa dowans umefungwa alikuwa sahihi kutokana na hii thread?
Au waziri mkuu alikuwa right
 
Back
Top Bottom