Mh Rais, nakuomba tafadhali soma waraka huu... - Lema

Mh Rais, nakuomba tafadhali soma waraka huu... - Lema

halafu jina lalalina fanana sana na kijiji nilichokulia! vipi leo umeamua kuweka akiliyao pembeni au iko likizo..

Mkuu,Kwani kitu gani kimekufanya mpaka ukafikiria akili yangu iko pembeni au likizo
Crashwise , Kijiji gani hicho ambacho sehemu ya maisha yako ulitumia.
 
Last edited by a moderator:
Kwa kuchangia mada ya lema nakumbuka miaka ya nyuma jinsi chama kimoja kilivyo dhofishwa na karibu watu wengi wasio kuwa wa dini ile waliamini hivyo kuwa kilikuwa chama cha kidini, lakini Mmungu ni mwingi wa matukio leo chadema kimesima imara bara kwa bahati mbaya Udini unatumika kukihujumu, chakushangaza wakati ule wakiristo walihamasishwa kuwa kile chama cha upizani kilikuwa cha kisilamu wasikiunge mkono na wengi wasiokuwa waisilamu walikikataa leo hii imetokea kwa chadema wasiokuwa waisilamu wanapigwa kampeni wakikatae chadema ,wanatumia fomula ile ile
 
Unafikiri Zitto alitakiwa kufanya hivi badala ya kuwalaumu wana JF kujadili!!!!!

sasa unafikiri zito angekuja na mawazo kama haya si kungekuwa na mgongano wa mawazo? hii ndo maana ya kuwa na wabunge wengi
 
yaani hadi pro lipumba ana toto la kichaga? na huyo mwigulu tena?
 
sasa unafikiri zito angekuja na mawazo kama haya si kungekuwa na mgongano wa mawazo? hii ndo maana ya kuwa na wabunge wengi

Sikuwa na maana alikuwa awe na mawazo sawa na Lema. Ninafikiri ingekuwa vema kama na yeye angemuandikia Rais badla ya kuishia kwenye Raia mwema.
 
Asante sana lema.
Mungu akubariki kwa upeo huu.
Ni wengi tunaunga mkono jambo hilo la 'halal' kwa kuwa katika nchi za wenzetu waliostaarabika...hutakuta wakiuana eti kwa haki ya kuchinja. Wenye kuongozwa na halal wale vya halal; na wale wengine wasiojali waachiwe uhuru wao.

Kamwe rais hapaswi kupuuza mawazo ya watu... Hatakama anayesema ni wa upinzani/humkubali....nk... Kubali hota yake au ipinge kwa hoja.
Mwalimu nyerere alisisitiza hili: Tusimkatae mtu...tukatae hoja yake kwa kutumia hoja...
 
Mh Rais Nakusalimu,

Wakati mwingine unapaswa kupewa pole na kuombewa na kufanyiwa dua kwani wewe ndie unatumikia ofisi kubwa kuliko zote Nchini na wakati huo huo unapaswa kupewa hongera kufikia malengo yako hayo ya kutumikia ofisi kubwa na ya Heshima kuliko zote Nchini , nimekuwa nikitafakari sana suala la Udini katika Taifa letu na huko Nyuma mwaka jana nilikuandikia pia waraka kuonya na kukumbusha hatua mathubuti kabla mambo hayajaaribika sijui kama ulisoma lakini naamini Usalama wa Taifa ambao siku hizi wanatumikia CCM watakuwa walisoma na Nape na wenzake pia walipata fursa ya kuusoma .

Mh Rais katika waraka hule nilisema hivi “ Mh Rais Taifa linahitaji Tiba “ siwezi leo kuandika kile nilichosema katika waraka ule ila niliweza kubashiri sumu ya udini inayoendelea katika Taifa lako na langu, Mh Rais , ukweli nakwambia ukifanya mchezo kidogo sana Taifa hili linapotea likiwa mikononi mwako kwani hali ya Nchi sio nzuri hata kidogo na watu waliokuwa wanaishi kwa umoja na upendo sasa wanaanza kutafuta mbinu za kugombana na kuuwana.

Mh Rais , Siasa ya Udini na Ukanda makusudi yake yalikuwa kudhoofisha vyama vya upinzani na yalifanikiwa kwa baadhi ya vyama kudhoofishwa sana na mkakati huo unaendelea dhidi ya Chadema lakini kinachosikitisha ni kuwa wale waliobuni mkakati huo walishindwa kutafakari au kuona madhara yake mbele .

Mh Rais, mkakati wa kudhoofisha Chama cha Siasa kwa Udini na Ukanda hauishi tu kuangamiza hicho Chama bali kuwagawa Watu na Taifa kwa Ujumla , Mtu anapojaribu kusema Chadema ni Chama cha Wakristo kimsingi matamshi hayo hayaangamizi Chadema tu bali yanagawa Watu kwa matabaka ya Udini wao na na kufanya Dini moja iamini kuwa Dini nyingine ni mbaya na hivyo mpango huo unafanya Watu waanze kutazamana kwa Udini na Ukabila na matokeo yake ndiyo haya tunaanza kuyaona leo .

Mh Rais , Taifa linahitaji tiba , Hivi karibuni Waziri Mkuu alienda Geita kwenye mgogoro wa Waisilamu na Wakristo na niliona mawazo ya Waziri Mkuu kwenye vyombo vya habari na kwa kweli nilisikitika kwa busara zile zilizokuwa zimejaa hofu kubwa . Tatizo lile lilianza na nani kati ya Mkristo na Muislamu anayepaswa kuchinja ?

Mh Rais , Nilipoona jambo hili nilianza kujiuliza maswali mengi sana , kwanza , umakini huu kwa pande zote mbili juu ya jambo hili umeletwa na nini na nani ? kwani yako mambo mengi yaliyokatazwa na Biblia na Msaafu ambayo watu wote wa dini hizi mbili wamekataa kuyatii au kuyafuata , kwa mfano waislamu na wakristo vijana kwa wazee wanakunywa pombe pamoja baadhi yao kujenga mahusiano hata ya kimapenzi yasio rasmi bila hata kufuata utaratibu wa Msaafu wala Biblia lakini hapa hutaona ugomvi mkubwa sana japokuwa ni masuala yanayo mkera na kumuudhi mwenyezi Mungu sana.

Mh Rais , ndio maana katika suala hili la nani achinje kati ya Muislamu na Mkristo niliposikia maafa yake nikakumbuka waraka niliokuandikia mwaka jana kuhusu ***** ***** za Udini ambazo zimeanza kuleta maafa ambazo Mwanzilishi wake ni CCM .

Mh Rais Chama chako unachokiongoza , Team yako imekuwa ikifanya sana propaganda hizi za ,Udini , Ukabila , na Ukanda usiku na mchana , lakini nimekuwa nikikerwa sana na Jinsi kabila la Wachaga linavyochukuliwa katika propaganda hizi na wanaofanya hivyo asilimia kubwa ni mashemeji wa Wachaga na mimi najiuliza wanaweza vipi kufanya Siasa za Ukanda na Ukabila wakati wao wenyewe ni familia moja ? kwa mfano , Mh Mwigulu Nchemba ,Mh David Mathayo ,Mh January Makamba , Mh Benjamin Mkapa , Mh Fredrik Sumaye , Mh Theo , Mh Dr Faustin Ndungulile , Mh Prof Ibrahimu Lipumba , Pro Mahalu , Mh Dr Hamis Kigwangala , Mh John Mgufuli , Mh Sospeter Muhongo ,Mh Jaji Warioba ,Idd Simba ,Mh Salmin Amour , na wengine wengi wote hawa wameoa Kilimanjaro . Sasa unajiuliza hawa wote ni Viongozi ndani ya CCM na wengine ndio mabingwa wa kufanya Siasa za Udini na Ukanda , je wake zao ndani ya nyumba wanajisikiaje wanapoona waume zao wanatukana kabila la ndugu zao kwa sababu ya Siasa ? hii ni hatari kubwa

Mh Rais kama kuchinja ni suala zito kiasi hicho katika Imani ya Kiislamu na pia ni neno kutoka katika Kitabu cha Imani yao basi ni haki na kweli kuwa wao wanapaswa kuchinja kwa Imani ya Dini yao na wala wasilazimishwe kumkosea Mungu wao kwani hakuna maarifa na Busara inayozidi imani , lakini vile vile Wakristo wasilazimishwe kushiriki Ibada ambayo sio yao. Waislamu kama wanaamini kuwa wao kuchinja ndio jambo lililoamrishwa katika vitabu vyao basi sasa Jambo hilo liheshimiwe na kutafutiwa utaratibu na vile vile Wakristo wasipuuzwe kugoma kushiriki jambo ambalo kwa wengine lina sura ya Imani.

Nini Kifanyike ?

Kwanza Chama chako na Viongozi wake uwakanye mara moja kabisa kuacha propaganda za udini na ukanda , kwani katika hili hakuna namna Nchi inaweza kubaki salama , kwani hizo ***** ***** hazitokani na nia mbaya ya Waislamu na Wakristo bali ni siasa chafu iliyopandikizwa ili kuangamiza vyama vya Siasa na sasa imekwenda zaidi na imeanza kuwatesa wakati ambao Nchi ina matatizo mengi ,
Kwa mfano Chadema tulipoandama Arusha kupinga Uchaguzi wa Meya feki , Kiongozi mmoja wa Mkoa wa CCM hapa Arusha , alinukuliwa na vyombo vya habari akidai tunafanya maandamano hayo kwa sababu za Udini na ndio maana hatumtaki Meya , lakini kitu cha kushangaza huyu Meya Feki ni Mkristo tena Mchaga Kabila langu , lakini niliambiwa na tunampinga na Maaskofu wanampinga kwa sababu Chadema ni Chama cha Udini ‘ sasa najiuliza kama Meya huyu Feki ni Mchaga na ni Mkristo je hayo madai ya kijinga yanatoka wapi ? Kama Ukristo ni ajenda kubwa kwetu kwani nini tulimpinga sasa ? Huu ni mfano mmoja iko mingi sana inayoashiria mkakati wa makusudi wa kuangamiza Chadema na huku mkisahau kuwa maliangamiza Taifa , na ndio Mkuu wa Mkoa wa Arusha alipokuja tu alidai kuwa amekuja kupambana na Chadema na Wachaga , ila nimuhakikishie hataweza na asijaribu kamwe na mikutano ambayo amekuwa akiifanya aiche mara moja .

Pili ,Mh Rais, ninaamini kuwa wewe umesafiri Nchi mbali mbali kuliko mimi , Ukienda Marekani , Spain , Brazil , China , Hong Kong , Uk , Italy , Sweden, Botswana , Namibia , South Afrika , Zimbabwe, na Nchi nyiongi utaona Maduka au Mabucha ya Nyama yameandikwa (Halal ) au unanua bidhaa yeyote ya aina ya Nyama na kukuta imeandikwa “Halal” na ni ustarabu kwamba bidhaa hiyo machinjio yake yamezingatia maadili ya Dini ya Kiislamu na Waislamu wenye Imani thabiti na Imani yao hapo ndipo watakapofanya manunuzi yao katika bidhaa hiyo ya aina ya Nyama .Lakini maeneno hayo hayo unaweza kupata nyama katika maduka mbali mbali yasiozingatia utaratibu huo na kwa hivyo watu wasiojali sana masuala ya Imani wala hawatasumbuka kuuliza na kusoma kama Nyama hiyo imezingatia masuala ya matakwa ya Imani Fulani.

Hivyo, Mh Rais, nafikiri ni vyema utaratibu huu ukaletwa hapa kwetu ili tuonyeshe Kujali Imani ya Waislamu katika Jambo hili ambalo limekuwa kwazo katika Jamii hizi mbili kubwa na kama ufumbuzi wake hautakuwa kuzingatia hili basi tarajia uchungu kuendelea kutembea kwenye vifua vya watu bila kusema na siku moja hali inaweza kuwa mbaya na tukapoteza Taifa .

Mh Rais, naiona hofu isiyokuwa ya kweli ya Mh Waziri Mkuu kuwa tukiruhusu hilo kuwa Wakristo na Waislamu wataweza kutengana kwenye mambo mengine mengi haswa katika Biashara na mambo mengine , kitu ambacho nasema sio kweli kwani , Sukari ,Mchele , Soda na Juisi na bidhaa nyingi hazina makatazo na maelekezo katika Imani , Mfano kila Mkristo anajua kuwa Mwislamu hatumi Nguruwe na Nguruwe kwa mwislamu ni haramu na hivyo Mkristo hawezi kupika Nguruwe na huku akijua kuwa wageni wake siku hiyo ni Waislamu.
Kwa hiyo hofu ya kuligawa Taifa kwa kurusu jambo hili haliwezi kutokea kwani ni miiko ya Kiimani ambayo pande zote zinapaswa kuheshimiana ili upande mmoja usione umekandamizwa na kupuuzwa , na hofu ya kibiashara inayoweza kutokea katika suala hili inapaswa kupuuzwa kwani IMANI ni zaidi ya Biashara japokuwa sioni jambo hili likitokea .

Mh Rais, nisikuchoshe sana, lakini haya ni maoni yangu na Mke wangu na sio Chama changu tumeamka leo Asubuhi tukasema tukuandikie tena kwani wewe ni Mkuu wa Nchi , Najua unaweza kuwa busy sana kusoma waraka huu mrefu ila najua Mwigulu na Nape lazima wausome hivyo niwaombe wakufikishe ujumbe huu.

Mh Rais , “ We are pressed on every side by troubles , but not crushed and broken . We are perplexed because we don’t know why things happen as they do . But we don,t give up and quit , We are hunted down But God Never Abandon Us , We get knocked down But We get up again and keep going . The root of life need commitment and there’s a lot to suffer to get at the Climax ”

Don’t Give Up Mr President please we beg you to help our Country now .

Godbless Jonathan Lema

unavoandika kwa upole kama vile umepiga magoti, good boy. big up!
 
UWU ( Umoja wa Wabunge walioa Uchagani ) nasikia wanachama chao .
Watu wa aina yako, wenye mawazo finyu kama wewe ndio mliotufikisha hapa kwenye udini na ukabila wa kipumbavu. Hii hoja yako inatija gani kwenye mustakabali wa taifa letu?? tukisema ndio wana chama chao, wewe au wanajamvi watanufaikaje na hoja yako???? Kuna haja ya kuanzisha jukwaa la wambea, wanaopenda kuleta habari za "nasikia/nimesikia", umesikia wap??????????????????
 
Sikuwa na maana alikuwa awe na mawazo sawa na Lema. Ninafikiri ingekuwa vema kama na yeye angemuandikia Rais badla ya kuishia kwenye Raia mwema.
Mimi nadhan njia zote zilizotumika ni sahihi, haimaanish kuwa ni lazma waraka wa Lema utamfikia rais kwa vile ameudirect kwa rais, na wala haimaanish waraka wa zito hautamfikia rais kwa vile kauandika kwenye raia mwema. Rais anawajibu wa kusaka news zote zinazoihusu ofisi yake kwa mustakabali wa taifa analoliongoza. Naiman hata rais asipoziona nyaraka hizi in person, watu wa karibu naye watazisoma na may be wata incorporate mawazo yote haya kwenye kukarabati hali hii.
 
Great minds always makes history! it is well said, well addressed and well pinned to shake the lazy brains..Hakika tu wazawa wa fikra zetu.
 
Nimependa lema ametoa solution kabisa toafauti na wanasiasa wengine huishia kwenye malalamiko to.
Big up lema.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Mkuu,Kwani kitu gani kimekufanya mpaka ukafikiria akili yangu iko pembeni au likizo
Crashwise , Kijiji gani hicho ambacho sehemu ya maisha yako ulitumia.

Katika watu wenye ubishi wa Kijinga sana humu JF wewe ni namba moja, yaani unaweza soma post za watu wooote ukapata mtiririko mzuri wa michango, ila zako pekee zina huwa zina arguments zisizo za msingi...pengine huwa una-post bila kuwasoma wenzako
 
Mkuu inawezekana uelewa wangu ni mdogo.

Haihitaji hata elimu kujua kama ni mawazo yake kwa sababu CHADEMA kama chama is better than this. Cha muhimu tu ni kwamba, hatuwezi tukamtenganisha Mh. Lema na ubunge ndiyo maana ni makosa au kukosa adabu kuandika jina lake bila kuweka neno MHESHIMIWA.

Labda tu unisaidie, huu waraka ulikuwa unaenda kwa Rais Kikwete kama Rais au Kama Kikwete?. Huwezi vile vile tenganisha Rais Kikwete na taasisi ya Urais.

Tukubali kutokubaliana.

Kweli una uelewa na upeo mdogo tunashukuru umekiri mwenyewe!
 
Katika watu wenye ubishi wa Kijinga sana humu JF wewe ni namba moja, yaani unaweza soma post za watu wooote ukapata mtiririko mzuri wa michango, ila zako pekee zina huwa zina arguments zisizo za msingi...pengine huwa una-post bila kuwasoma wenzako

Good on you kwa Wewe mwenye ubishi wa kiakili kwa vile huwa unafuata mtiririko mzuri wa michango.

Sijakulazimisha kusoma soma michango yangu hapa JF. Halafu kama uligundua kama michango yangu ni ya ubishi wa kijinga, kwa nini bado unaendelea kuisoma soma. Huoni kama kufanya hivyo ni kupoteza muda wako wenye gharama kubwa na kuwa kama una umbea fulani. Hata hii post haikukuhusu wewe lakini cha kushangaza umeidandia ili utoe comment.

Ni kina nani hao walikupima wakagundua una uelevu wa kuweza kupima watu hapa JF pale unaposema "Katika watu wenye ubishi wa kijinga sana humu JF wewe ni namba moja".

Achana na mabandiko yangu kama hayana mashiko kwako kama nami nisivyo jishighulisha na mabandiko yako.
 
Back
Top Bottom