Mh Rais, nakuomba tafadhali soma waraka huu... - Lema

Mh Rais, nakuomba tafadhali soma waraka huu... - Lema

Dah! ina maana hujauelewa huu waraka!!? sasa sijui tukusaidie vipi ndugu yetu. au wewe ni miongoni mwa wale >60% nini?

nimeuelewa sana, ila kuboresha jambo la kawaida

kama umesikiliza njia panda leo utaelewa namaanisha nini

tuna hoja nzuri lakini tunatakiwa kuzikandamizia na mfumo mzuri zaidi wa uandishi, ili hata wajukuu waelewe kwamba siku Lema anaandika ile waraka, taifa lilikua kwenye muktadha fulani

Kuhusu hiyo 60%, I am proud to say all my life nimekua kwenye ile 1% kuanzia darasa ka kwanza hadi vyuo vikuu vitatu vyenye shahada tatu zilizotukuka sana

na nilitembea matembezi ya mshikamano na jackson makweta ya kilomita nane nikiwa na ngoma mkononi kuchangisha pesa za majengo ya shule ya msingi ambayo ilikua na madarasa matatu tu, na tulifaulu kwenda for 1 asilimia zaidi ya 60 na kuweka rekodi

and I am not afraid to say anything
 
Hawa ndiyo wanaSiasa wetu.

Kwani ni kiasi gani kwa Mh. Mbunge kinaweza kumgharimu kutafuta Mwanasheria na mhariri mzuri ili kuweka waraka kama huu katika misingi, taratibu, kanuni na kisheria kabla hajautoa kwenye public domain.

It's all over the place mpaka hata kusudio la waraka linapotelea hewani.

Rais Jakaya kikwete ni taasisi ambayo inaendeshwa katika taratibu, kanuni na sheria hata kama kwa mawazo yake inaiona kama ni kibosera na haifanyi kama atakavyo.

Donald Rumsfeld said, "you go to war with the army you have, not the army you might want or wish to have at a later time"

This is the best we have. Nothing we can do until 2015

Ni angalizo tu.



Ujumbe wowote huangaliwa by form and content na vitu hivi viwili vikiwa confusing ndipo tunaweza kusema ujumbe uliokusudiwa kuifikia hadhira basi haukufika. Sasa by form ni wapi Mh.Lema amekosea? By content yeye anataka kufukisha ujumbe unaohusu udini na tiba yake. Ameonyesha vizuri katika hili na kuhoji kuwa kuna mambo mengi yanamkera Mwenyezi Mungu na binadamu tunashiriki kuyafanya tena tukishirikiana watu wa dini mbili. Ujumbe umefika na amekwenda kwenye empirical examples jinsi nchi za wenzetu wanavyofanya ili watu wake wasiwe damaged kiimani. His content is researched beyond doubt. Tuambie ulitaka mwanasheria amsaidie nini? Ujumbe na uaadishi ni mzuri na unakidhi. Wewe twambie nini mwanasheria angafanya kwenye editing unayotaka?
 
Kamanda Lema ni mkweli na kiongozi amejitoa haswa akimaanisha!!!

Kudos Lema
 
mkuu its gud to be critic nenda mbali zaidi kosa la lema na huo waraka nini?amemtusi mwandikiwa?au wewe ujapenda yeye kufanya hivyo?ujumbe upo kwenye signature yangu.

Mkuu inawezekana uelewa wangu ni mdogo.

Haihitaji hata elimu kujua kama ni mawazo yake kwa sababu CHADEMA kama chama is better than this. Cha muhimu tu ni kwamba, hatuwezi tukamtenganisha Mh. Lema na ubunge ndiyo maana ni makosa au kukosa adabu kuandika jina lake bila kuweka neno MHESHIMIWA.

Labda tu unisaidie, huu waraka ulikuwa unaenda kwa Rais Kikwete kama Rais au Kama Kikwete?. Huwezi vile vile tenganisha Rais Kikwete na taasisi ya Urais.

Tukubali kutokubaliana.

Ndo maana nimesema wewe inawezekana ni miongoni mwa wale >60%. Hapo Lema ameweka wazi, ameandika yeye na mkewe kama watanzania na wala sio mawazo ya CDM, kwahiyo wala hakuandika kama Mbunge vilevile, ameandika kama mtanzania mwengine yeyote ambaye angekerwa na yanayoendelea kwa sasa hapa Tanzania
 
Kwani hapo wewe hujaelewa nini, au ndo mnajifanya vichwa nazi ili kuhamisha wananchi mawazo kutoka kwenye hoja muhimu za kitaifa ili tuendelee kuongelea matatizo ya udini. Hebu rudia kuusoma taratiiiiiiiiiibu kwa kina kama usipouelewa basi sina shaka utakuwa miongoni mwa wale >60%

Sihitaji kusoma tena, kama wewe umeelewa, good on you.

Kwa hiyo matatizo ya kidini siyo hoja muhimu. Zipi hizo hoja muhimu unazofikiria. Kwani mimi ninakuzuia nini kuwa na hayo mawazo yako ya hoja muhimu.

Nilichoandika ni mawazo yangu. You can take it or leave it.

Tatizo langu, mimi siyo mpenda chongo
 
mkuu its gud to be critic nenda mbali zaidi kosa la lema na huo waraka nini?amemtusi mwandikiwa?au wewe ujapenda yeye kufanya hivyo?ujumbe upo kwenye signature yangu.

kila kitu wewe mpumbavu, sio kila anayetoa mawazo ya kuboresha ana chuki na Lema wewe

tatizo letu liko hapo, kila tunapotoa hoja ya kuboresha mnakuja kuwa wabishi na silly observations

ningekua nina chuki nisingesema aboreshe, ningesema ni waraka ----

nadhani kuna haja ya JF kupanga watu kwa uelewa na na elimu labda itapunguza kuchanganya wapuuzi kama wewe na watu wenye nia njema

nyambafff wahed

Kuboresha nini wewe nyambafu TIMING!!?, kama ungekuwa hujaelewa message sidhani kama ungetoa comment yoyote. Acha ujinga wewe muathirika wa mitaala mibovu
 
Kwani hujaelewa kilichoandikwa uone the positive side of the issue!
Hakina mpangilio, km kweli ni barua inayoenda Ikulu km ni ya hapa JF sawa

hivyo asilimia kubwa ni mashemeji wa Wachaga na mimi najiuliza wanaweza vipi kufanya Siasa za Ukanda na Ukabila wakati wao wenyewe ni familia moja ? kwa mfano , Mh Mwigulu Nchemba ,Mh David Mathayo ,Mh January Makamba , Mh Benjamin Mkapa , Mh Fredrik Sumaye , Mh Theo , Mh Dr Faustin Ndungulile , Mh Prof Ibrahimu Lipumba , Pro Mahalu , Mh Dr Hamis Kigwangala , Mh John Mgufuli , Mh Sospeter Muhongo ,Mh Jaji Warioba ,Idd Simba ,Mh Salmin Amour , na wengine wengi wote hawa wameoa Kilimanjaro . Sasa unajiuliza hawa wote ni Viongozi ndani ya CCM
kulikuwa hakuna haja ya kuwataja hao wote kina January Makamba na wengineo kwani kuna uhakika gani
Hata hii utaiingiza kwenye Grammer gani? Mh Rais , “ We are pressed on every side by troubles , but not crushed and broken . We are perplexed because we don’t know why things happen as they do .

km ujumbe ni kuchinja utakuwa umefika lakini hata kwa Rais lakini Advisor wa Mbunge basi aelewe nini nini wakati wa proof reading kwani Window 2007 hata nyingine zinarekebisha hata kiswahili
 
DU KWELI LEMA UKO SAWA KABISA. ILA HATA WAKRISTO TUPO AMBAO HATULI NYAMA YA NGURUWE. Kwenye katiba hakuna ibara inayozungumzia suala la utaratibu wa kuchinja pia twajua kuwa serikali yetu haifungamani na upande wowote. basi kila imani iwe huru.
 
Hakina mpangilio, km kweli ni barua inayoenda Ikulu km ni ya hapa JF sawa

hivyo asilimia kubwa ni mashemeji wa Wachaga na mimi najiuliza wanaweza vipi kufanya Siasa za Ukanda na Ukabila wakati wao wenyewe ni familia moja ? kwa mfano , Mh Mwigulu Nchemba ,Mh David Mathayo ,Mh January Makamba , Mh Benjamin Mkapa , Mh Fredrik Sumaye , Mh Theo , Mh Dr Faustin Ndungulile , Mh Prof Ibrahimu Lipumba , Pro Mahalu , Mh Dr Hamis Kigwangala , Mh John Mgufuli , Mh Sospeter Muhongo ,Mh Jaji Warioba ,Idd Simba ,Mh Salmin Amour , na wengine wengi wote hawa wameoa Kilimanjaro . Sasa unajiuliza hawa wote ni Viongozi ndani ya CCM
kulikuwa hakuna haja ya kuwataja hao wote kina January Makamba na wengineo kwani kuna uhakika gani
Hata hii utaiingiza kwenye Grammer gani? Mh Rais , “ We are pressed on every side by troubles , but not crushed and broken . We are perplexed because we don’t know why things happen as they do .

km ujumbe ni kuchinja utakuwa umefika lakini hata kwa Rais lakini Advisor wa Mbunge basi aelewe nini nini wakati wa proof reading kwani Window 2007 hata nyingine zinarekebisha hata kiswahili

Hapo kwenye blue, mkuu kuna tatizo gana la grammar siyo (Grammer kama ulivyoandika) hiyo quote ilichukuliwa kama ilivyo kutoka kwenye kitabu kinachoheshimika kwa wakristo, nadhani ni vizuri kuheshimu mawazo ya maana, kuliko kuya crush kwa chuki binafsi mr Ukwaju
 
Last edited by a moderator:
Mh Rais Nakusalimu,

Wakati mwingine unapaswa kupewa pole na kuombewa na kufanyiwa dua kwani wewe ndie unatumikia ofisi kubwa kuliko zote Nchini na wakati huo huo unapaswa kupewa hongera kufikia malengo yako hayo ya kutumikia ofisi kubwa na ya Heshima kuliko zote Nchini , nimekuwa nikitafakari sana suala la Udini katika Taifa letu na huko Nyuma mwaka jana nilikuandikia pia waraka kuonya na kukumbusha hatua mathubuti kabla mambo hayajaaribika sijui kama ulisoma lakini naamini Usalama wa Taifa ambao siku hizi wanatumikia CCM watakuwa walisoma na Nape na wenzake pia walipata fursa ya kuusoma .

Mh Rais katika waraka hule nilisema hivi “ Mh Rais Taifa linahitaji Tiba “ siwezi leo kuandika kile nilichosema katika waraka ule ila niliweza kubashiri sumu ya udini inayoendelea katika Taifa lako na langu, Mh Rais , ukweli nakwambia ukifanya mchezo kidogo sana Taifa hili linapotea likiwa mikononi mwako kwani hali ya Nchi sio nzuri hata kidogo na watu waliokuwa wanaishi kwa umoja na upendo sasa wanaanza kutafuta mbinu za kugombana na kuuwana.

Mh Rais , Siasa ya Udini na Ukanda makusudi yake yalikuwa kudhoofisha vyama vya upinzani na yalifanikiwa kwa baadhi ya vyama kudhoofishwa sana na mkakati huo unaendelea dhidi ya Chadema lakini kinachosikitisha ni kuwa wale waliobuni mkakati huo walishindwa kutafakari au kuona madhara yake mbele .

Mh Rais, mkakati wa kudhoofisha Chama cha Siasa kwa Udini na Ukanda hauishi tu kuangamiza hicho Chama bali kuwagawa Watu na Taifa kwa Ujumla , Mtu anapojaribu kusema Chadema ni Chama cha Wakristo kimsingi matamshi hayo hayaangamizi Chadema tu bali yanagawa Watu kwa matabaka ya Udini wao na na kufanya Dini moja iamini kuwa Dini nyingine ni mbaya na hivyo mpango huo unafanya Watu waanze kutazamana kwa Udini na Ukabila na matokeo yake ndiyo haya tunaanza kuyaona leo .

Mh Rais , Taifa linahitaji tiba , Hivi karibuni Waziri Mkuu alienda Geita kwenye mgogoro wa Waisilamu na Wakristo na niliona mawazo ya Waziri Mkuu kwenye vyombo vya habari na kwa kweli nilisikitika kwa busara zile zilizokuwa zimejaa hofu kubwa . Tatizo lile lilianza na nani kati ya Mkristo na Muislamu anayepaswa kuchinja ?

Mh Rais , Nilipoona jambo hili nilianza kujiuliza maswali mengi sana , kwanza , umakini huu kwa pande zote mbili juu ya jambo hili umeletwa na nini na nani ? kwani yako mambo mengi yaliyokatazwa na Biblia na Msaafu ambayo watu wote wa dini hizi mbili wamekataa kuyatii au kuyafuata , kwa mfano waislamu na wakristo vijana kwa wazee wanakunywa pombe pamoja baadhi yao kujenga mahusiano hata ya kimapenzi yasio rasmi bila hata kufuata utaratibu wa Msaafu wala Biblia lakini hapa hutaona ugomvi mkubwa sana japokuwa ni masuala yanayo mkera na kumuudhi mwenyezi Mungu sana.

Mh Rais , ndio maana katika suala hili la nani achinje kati ya Muislamu na Mkristo niliposikia maafa yake nikakumbuka waraka niliokuandikia mwaka jana kuhusu ***** ***** za Udini ambazo zimeanza kuleta maafa ambazo Mwanzilishi wake ni CCM .

Mh Rais Chama chako unachokiongoza , Team yako imekuwa ikifanya sana propaganda hizi za ,Udini , Ukabila , na Ukanda usiku na mchana , lakini nimekuwa nikikerwa sana na Jinsi kabila la Wachaga linavyochukuliwa katika propaganda hizi na wanaofanya hivyo asilimia kubwa ni mashemeji wa Wachaga na mimi najiuliza wanaweza vipi kufanya Siasa za Ukanda na Ukabila wakati wao wenyewe ni familia moja ? kwa mfano , Mh Mwigulu Nchemba ,Mh David Mathayo ,Mh January Makamba , Mh Benjamin Mkapa , Mh Fredrik Sumaye , Mh Theo , Mh Dr Faustin Ndungulile , Mh Prof Ibrahimu Lipumba , Pro Mahalu , Mh Dr Hamis Kigwangala , Mh John Mgufuli , Mh Sospeter Muhongo ,Mh Jaji Warioba ,Idd Simba ,Mh Salmin Amour , na wengine wengi wote hawa wameoa Kilimanjaro . Sasa unajiuliza hawa wote ni Viongozi ndani ya CCM na wengine ndio mabingwa wa kufanya Siasa za Udini na Ukanda , je wake zao ndani ya nyumba wanajisikiaje wanapoona waume zao wanatukana kabila la ndugu zao kwa sababu ya Siasa ? hii ni hatari kubwa

Mh Rais kama kuchinja ni suala zito kiasi hicho katika Imani ya Kiislamu na pia ni neno kutoka katika Kitabu cha Imani yao basi ni haki na kweli kuwa wao wanapaswa kuchinja kwa Imani ya Dini yao na wala wasilazimishwe kumkosea Mungu wao kwani hakuna maarifa na Busara inayozidi imani , lakini vile vile Wakristo wasilazimishwe kushiriki Ibada ambayo sio yao. Waislamu kama wanaamini kuwa wao kuchinja ndio jambo lililoamrishwa katika vitabu vyao basi sasa Jambo hilo liheshimiwe na kutafutiwa utaratibu na vile vile Wakristo wasipuuzwe kugoma kushiriki jambo ambalo kwa wengine lina sura ya Imani.

Nini Kifanyike ?

Kwanza Chama chako na Viongozi wake uwakanye mara moja kabisa kuacha propaganda za udini na ukanda , kwani katika hili hakuna namna Nchi inaweza kubaki salama , kwani hizo ***** ***** hazitokani na nia mbaya ya Waislamu na Wakristo bali ni siasa chafu iliyopandikizwa ili kuangamiza vyama vya Siasa na sasa imekwenda zaidi na imeanza kuwatesa wakati ambao Nchi ina matatizo mengi ,
Kwa mfano Chadema tulipoandama Arusha kupinga Uchaguzi wa Meya feki , Kiongozi mmoja wa Mkoa wa CCM hapa Arusha , alinukuliwa na vyombo vya habari akidai tunafanya maandamano hayo kwa sababu za Udini na ndio maana hatumtaki Meya , lakini kitu cha kushangaza huyu Meya Feki ni Mkristo tena Mchaga Kabila langu , lakini niliambiwa na tunampinga na Maaskofu wanampinga kwa sababu Chadema ni Chama cha Udini ‘ sasa najiuliza kama Meya huyu Feki ni Mchaga na ni Mkristo je hayo madai ya kijinga yanatoka wapi ? Kama Ukristo ni ajenda kubwa kwetu kwani nini tulimpinga sasa ? Huu ni mfano mmoja iko mingi sana inayoashiria mkakati wa makusudi wa kuangamiza Chadema na huku mkisahau kuwa maliangamiza Taifa , na ndio Mkuu wa Mkoa wa Arusha alipokuja tu alidai kuwa amekuja kupambana na Chadema na Wachaga , ila nimuhakikishie hataweza na asijaribu kamwe na mikutano ambayo amekuwa akiifanya aiche mara moja .

Pili ,Mh Rais, ninaamini kuwa wewe umesafiri Nchi mbali mbali kuliko mimi , Ukienda Marekani , Spain , Brazil , China , Hong Kong , Uk , Italy , Sweden, Botswana , Namibia , South Afrika , Zimbabwe, na Nchi nyiongi utaona Maduka au Mabucha ya Nyama yameandikwa (Halal ) au unanua bidhaa yeyote ya aina ya Nyama na kukuta imeandikwa “Halal” na ni ustarabu kwamba bidhaa hiyo machinjio yake yamezingatia maadili ya Dini ya Kiislamu na Waislamu wenye Imani thabiti na Imani yao hapo ndipo watakapofanya manunuzi yao katika bidhaa hiyo ya aina ya Nyama .Lakini maeneno hayo hayo unaweza kupata nyama katika maduka mbali mbali yasiozingatia utaratibu huo na kwa hivyo watu wasiojali sana masuala ya Imani wala hawatasumbuka kuuliza na kusoma kama Nyama hiyo imezingatia masuala ya matakwa ya Imani Fulani.

Hivyo, Mh Rais, nafikiri ni vyema utaratibu huu ukaletwa hapa kwetu ili tuonyeshe Kujali Imani ya Waislamu katika Jambo hili ambalo limekuwa kwazo katika Jamii hizi mbili kubwa na kama ufumbuzi wake hautakuwa kuzingatia hili basi tarajia uchungu kuendelea kutembea kwenye vifua vya watu bila kusema na siku moja hali inaweza kuwa mbaya na tukapoteza Taifa .

Mh Rais, naiona hofu isiyokuwa ya kweli ya Mh Waziri Mkuu kuwa tukiruhusu hilo kuwa Wakristo na Waislamu wataweza kutengana kwenye mambo mengine mengi haswa katika Biashara na mambo mengine , kitu ambacho nasema sio kweli kwani , Sukari ,Mchele , Soda na Juisi na bidhaa nyingi hazina makatazo na maelekezo katika Imani , Mfano kila Mkristo anajua kuwa Mwislamu hatumi Nguruwe na Nguruwe kwa mwislamu ni haramu na hivyo Mkristo hawezi kupika Nguruwe na huku akijua kuwa wageni wake siku hiyo ni Waislamu.
Kwa hiyo hofu ya kuligawa Taifa kwa kurusu jambo hili haliwezi kutokea kwani ni miiko ya Kiimani ambayo pande zote zinapaswa kuheshimiana ili upande mmoja usione umekandamizwa na kupuuzwa , na hofu ya kibiashara inayoweza kutokea katika suala hili inapaswa kupuuzwa kwani IMANI ni zaidi ya Biashara japokuwa sioni jambo hili likitokea .

Mh Rais, nisikuchoshe sana, lakini haya ni maoni yangu na Mke wangu na sio Chama changu tumeamka leo Asubuhi tukasema tukuandikie tena kwani wewe ni Mkuu wa Nchi , Najua unaweza kuwa busy sana kusoma waraka huu mrefu ila najua Mwigulu na Nape lazima wausome hivyo niwaombe wakufikishe ujumbe huu.

Mh Rais , “ We are pressed on every side by troubles , but not crushed and broken . We are perplexed because we don’t know why things happen as they do . But we don,t give up and quit , We are hunted down But God Never Abandon Us , We get knocked down But We get up again and keep going . The root of life need commitment and there’s a lot to suffer to get at the Climax ”

Don’t Give Up Mr President please we beg you to help our Country now .

Godbless Jonathan Lema

Kumuonea tu Kikwete. Nyerere ndie aliandaa tabaka la UDINI hapa, akifatiwa na mkapa aliewaua waislam. Kosa la Kikwete ni kwamba wakati wake waliouwa wengi ni Wakiristo na sio waislam kama tulivyozoea
 
Waraka ungekuwa na tarehe na sahihi ya Mh LEMA ingependeza zaidi lakini naamini waraka utawafikia wahusika.

Ni waraka uliolaumu na kutoa mapendekezo. Nimevutiwa zaidi na mapendekezo lawama zitaturudisha nyuma zaidi.
 
Lema hana busara zozote wala rais hana muda wa kupoteza kumsoma Lema.
 
Hivi kwanini thread hii haijafungwa kama nyingine zenye ujumbe wa aina hii???
 
mkuu its gud to be critic nenda mbali zaidi kosa la lema na huo waraka nini?amemtusi mwandikiwa?au wewe ujapenda yeye kufanya hivyo?ujumbe upo kwenye signature yangu.

Lema hana busara zozote wala rais hana muda wa kupoteza kumsoma Lema.

Kwahiyo busara ni kwenda kutalii adis na kuacha minyukano mikubwa hapa nyumbani!? basi kama hizo ni busara hatuna kiongozi pale. Naisikitikia nchi yangu Tanzania kwa kuwa na kiongozi kama huyu
 
Ndo maana nimesema wewe inawezekana ni miongoni mwa wale >60%. Hapo Lema ameweka wazi, ameandika yeye na mkewe kama watanzania na wala sio mawazo ya CDM, kwahiyo wala hakuandika kama Mbunge vilevile, ameandika kama mtanzania mwengine yeyote ambaye angekerwa na yanayoendelea kwa sasa hapa Tanzania

Mbona umeng'ang'ania inawezekana, inawezekana, inawezekana ni wale >60%. Huwezi kuishi kwa kudhania na inawezekana. Kama hunifahamu, huna haja ya kukaa ukidhania.

Tatizo la watu kama wewe, mko desperate kupitisha point hata kama mnafahamu point yenyewe ni trash au bila kufahamu na kwa kufanya hivyo, inakuwa hata hamuwasaidii wanasiasa.

Bearing in mind that huwezi kulazimisha mawazo ya wengine yawe kama yako. Na kwa kufanya hivyo haiwezi pia kukupa haki ya kuanza classing people na wewe kujiona kama unazo nyingi akilini. Kwa lugha nyepesi, hiki unachokifanya ni ulimbukeni.

Mimi nimetoa mawazo yangu na wewe umetoa ya kwako. Fair enough.

Siko kwa kupenda chongo na kuita kengeza. Tukubali kutokubaliana.
 
Ujumbe mzuri lakini uliowataja wakapeleke ujumbe watabadilisha maneno kwani najua mkuu wa nchi hatausoma kwani maoni mengi anaambiwa yeye utamsikia tumia akili za mbayuwayu. Kazi kwleikweli. Lema god bless you umeandika kwa unyenyekevu kamanda haya maji ya udini yapo shingoni
 
Back
Top Bottom