Black Mirror
JF-Expert Member
- Oct 17, 2019
- 829
- 1,034
Mheshimiwa Rais Magufuli wa Tanzania, wewe ndiye mwenye mamlaka ya mwisho kwa kila kitu hapa Tanzania. Mara nyingi umekuwa ukiwasihi watumishi wavumilie kuhusu kuongezewa mishahara kama inavyopaswa kuwa kwani sasa hivi unajenga nchi, lakini mheshimiwa unapaswa ukumbuke kuwa maisha hayasimami kwa watu kusubiria nchi ijengwe halafu yaendelee. Maisha yanaendelea wakati wote na wala hayasimami watu wanawaza mstakabali wa watoto wao, wake zao, ndugu zao na maisha yao.
Ukweli ulio hai ni kwamba sekta ya utumishi wa umma inapitia katika kupindi kigumu sana kuliko miaka yote na pengine kuliko tawala zote. Watumishi wa umma wana hali ngumu kimaisha, japo si wote maana wapo ambao wanakula keki ya Taifa sanjari na wewe.
Watumishi walio wengi uliwapunguzia mshahara kupitia kuongeza makato ya bodi ya mikopo kutoka 8% hadi 15% (haya ni maumivu makubwa sana). Mh Rais, mfano unapaswa ukumbuke bado watumishi hao hao wanakatwa kodi kubwa sana ya kutisha kuliko wafanya biashara, lakini wakirudi makwao bado wanakumbana na changamoto sawa na wananchi wengine mfno bei juu za vyakula na gharama nyingine kama kawaida.
Mh. Rais, juzi ulitoa kauli ya kuanza kufifisha tena matumaini ya watumishi wa umma uliposema kuwa hata wewe mshahara haukutoshi. Hii kauli inaashiria May 01/2020 hakuna tamko la kuongezewa mshahara. Hivyo basi nakuomba Mh Rais, Mei hiyo uruhusu watumishi waondolewe vikwazo vya kuhama. Hii ni kwa sababu kuwa miaka ya hivi karibuni kumekuwepo na wimbi kubwa la watumishi wa umma kutaka kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine, hasa walimu.
Walio wengi wanahitaji kuhama kutokana na ugumu wa maisha ulioimarishwa kipindi hiki. Hivyo, watumishi wanahitaji kuhama ili kupunguza ugumu huo kwani wengine wanajaribu kuchungulia mazingira rafiki ambayo walau yatawapa unafuu wa kuishi.
Mh Rais, basi walau siku hiyo waondolee vikwazo watu wahame tu bila bughudha zilizopo kwa sasa. Utakuwa umefanya la maana sana kwani tayari tunajua sasa hivi unajenga nchi; maslahi ya watumishi yanapaswa kusubiri japo maisha hayawasubiri na hata kodi tu twajua huwezi kupunguza pia.
Wasaidie watumishi tafadhali sana.