Mzalendo39
JF-Expert Member
- Apr 17, 2015
- 881
- 1,035
Ni katika viwanja vya Karimjee leo wakati bunge likimkabidhi Mh. Rais madawati kwa ajili ya watanzania
Mh. Mbunge wa Iringa alionekana akiwa kwenye ratiba hiyo na hata kupiga picha na Mh. Rais pamoja na wabunge wengine.
Kinachonishangaza ni vijana wa CCM na CHADEMA wanapomponda na kubeza kitendo hicho ambacho kinaonekana kwenda tofauti na msimamo wa chama chake, baada ya CHADEMA kutangaza msimamo wake kwa kutoshirikiana na serikali ya Chama cha Mapinduzi.
Msimamo huo ulianza wakati wa vikao vya bunge la bajeti vikiendelea Dodoma pale walipoonyesha msimamo wao wa kutoshirikiana na naibu spika na kuanza kususia vikao vya bunge ambapo ilifika mbali hata kisusia wabunge wa CCM na hata kupeana salamu na katika mwezi mtukufu wa ramadhani walisusia futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu pamoja na spika wa bunge
My take:
Huu ni wakati wa kuwa wamoja katika shughuli za maendeleo kwa watanzania.....tofauti za kichama zisituwawe watanzania
Naungana na Mh. Msigwa pamoja na watu wote wanaounga mkono utaifa kwanza vyama baadae.