Mh. Mkosamali: This week in perspective

Mh. Mkosamali: This week in perspective

"Shukrani kwa nyerere alicheza utadhani pele kuendeleza kiswahili mikoani na mbelembele tunamfagilia mzungu wakati tuna shida tele kingereza bila hela ni sawa na kupiga kelele"-L.A.N.G.A
 
Tatizo kubwa la Waafrika ni kujidharau baada ya kudharauliwa kwa miaka mingi na Wazungu. Waafrika ni watu pekee ambao hudharauliwa kuliko watu wengine wowote wale duniani. Dharau hiyo imeendelea hadi katika lugha zetu, lugha za Kiafrika zinaonekana si lugha za watu wasio na umuhimu wowote. Si walaumu watu wanaoona kuwa kutokujua Kiingereza ni tatizo kubwa... kwa sababu wamefanywa hivyo, si kwa matakwa yao, bali watu weupe wamewafanya wawe hivyo. UTUMWA WA KIAKILI na KUTAWALIWA KIAKILI. Ukoloni wa akili ni mbaya kuliko ukoloni tuliouzoea.
Nimewahi kuzungumza na watu wa mataifa mbalimbali kama vile Wajapani, Wakorea, Wajerumani, Wachina, Wahindi na Waafrika wanaotokea katika nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa. Baadhi yao wanazungumza Kiingereza vizuri wengine hawana uwezo mkubwa. Kwangu sioni tatizo lolote, wala sishangai. Namshangaa, kwa hakika, sana Mtanzania ambaye lugha yake ya taifa ni Kiswahili analinganisha ubora wa mtu kwa kutumia lugha ya Kiingereza.... LUGHA YA WAKOLONI WAKE...
Suala la ajabu kabisa ni pale Mzungu anapokea lugha ya Kiswahili, au Mtanzania anapokosea kuzungumza lugha ya Kiswahili na anaonekana hajafanya kosa kubwa, lakini akikosea Kiingereza tunalalamika.... Nasikitika kuishi kwenye jamii isiyojitambua na kuishi kama makopo matupu yenye mabaki makubwa ya ukoloni katika akili yake... HATARI!!!!
Nina wasiwasi na ubora wa elimu wa nchi yetu... haiwezekani miaka hamsini baada ya uhuru watu wake "huru" wana mawazo yaliyochakaa kiasi hiki... tuna safari ndefu ya kuutambua utu wetu, kuutambua utamaduni wetu na kuutambua Uafrika wetu.
MWAFRIKA USIPOJITAMBUA HUTATAMBULIKA... "Know thyself" Socrates.
 
watanzania tulio wengi tunajua english tena ilio sanifu ya KUANDIKA TU
ila kuongea ndio mgogoro kwani mfumo wetu wa elimu haukuturuhusu kujifunza lugha hii mapema tukiwa wadogo elimu ya msingi
lakini ukisoma presentation za watu na thesis utashangaa lugha iliyotumika kama kaandika Mtanzania.
Nyerere angekubali elimu ya msingi iwe kwa kiingereza yote haya yasingotokea. Sioni haja ya kuwakosoa viongozi eti lugha yao mbovu. hivi mnajua kuna wazungu ulaya ya kati na hata mashariki jawajui kabisa hata kusalimia kwa kiingereza sembuse sisi wabongo tulio mbali na wao.....
laumuni mfumo uliotufikisha hapa tulipo.
 
tatizo kubwa la waafrika ni kujidharau baada ya kudharauliwa kwa miaka mingi na wazungu. Waafrika ni watu pekee ambao hudharauliwa kuliko watu wengine wowote wale duniani. Dharau hiyo imeendelea hadi katika lugha zetu, lugha za kiafrika zinaonekana si lugha za watu wasio na umuhimu wowote. Si walaumu watu wanaoona kuwa kutokujua kiingereza ni tatizo kubwa... Kwa sababu wamefanywa hivyo, si kwa matakwa yao, bali watu weupe wamewafanya wawe hivyo. Utumwa wa kiakili na kutawaliwa kiakili. Ukoloni wa akili ni mbaya kuliko ukoloni tuliouzoea.
Nimewahi kuzungumza na watu wa mataifa mbalimbali kama vile wajapani, wakorea, wajerumani, wachina, wahindi na waafrika wanaotokea katika nchi zinazozungumza lugha ya kifaransa. Baadhi yao wanazungumza kiingereza vizuri wengine hawana uwezo mkubwa. Kwangu sioni tatizo lolote, wala sishangai. Namshangaa, kwa hakika, sana mtanzania ambaye lugha yake ya taifa ni kiswahili analinganisha ubora wa mtu kwa kutumia lugha ya kiingereza.... Lugha ya wakoloni wake...
Suala la ajabu kabisa ni pale mzungu anapokea lugha ya kiswahili, au mtanzania anapokosea kuzungumza lugha ya kiswahili na anaonekana hajafanya kosa kubwa, lakini akikosea kiingereza tunalalamika.... Nasikitika kuishi kwenye jamii isiyojitambua na kuishi kama makopo matupu yenye mabaki makubwa ya ukoloni katika akili yake... Hatari!!!!
Nina wasiwasi na ubora wa elimu wa nchi yetu... Haiwezekani miaka hamsini baada ya uhuru watu wake "huru" wana mawazo yaliyochakaa kiasi hiki... Tuna safari ndefu ya kuutambua utu wetu, kuutambua utamaduni wetu na kuutambua uafrika wetu.
Mwafrika usipojitambua hutatambulika... "know thyself" socrates.
nimeipenda mkuu, ni kweli hatujitambui kwamba na sisi waafrika tunahati miliki ya dunia hii, yote hii shauri ya kutawaliwa na wakoloni.....
 
Ukiamua kutumia lugha fulani itumie vizuri Kwa sababu hakuna anayekulazimisha kuongea. Kuna vipindi chungu nzima vya kiswahili Kwa nini alikubali kwenda kushiriki hiki cha lugha za wazungu?
 
Ukiamua kutumia lugha fulani itumie vizuri Kwa sababu hakuna anayekulazimisha kuongea. Kuna vipindi chungu nzima vya kiswahili Kwa nini alikubali kwenda kushiriki hiki cha lugha za wazungu?

umesomeka vyema dr mkumbo...!! bila shaka wahusika watalifanyia kazi
 
daktari
salamu na heshima zako
Lugha ni kiwezesho cha kuwasiliana.
Ingekuwa washiriki walikuwa kwenye mtihani wa kiingereza cha kuongea (oral English exam/interview) huu mjadala ungekuwa na mashiko.
Hakuna anayepinga kwamba walizungumza na wakaeleweka.
Hayo ya kutema yai wanayoyatafuta hawa wana JF hapa ni batili tu.
Wengine utaweza kuona hata kuandika kimombo kilichonyooka ni mgogoro!

Ukiamua kutumia lugha fulani itumie vizuri Kwa sababu hakuna anayekulazimisha kuongea. Kuna vipindi chungu nzima vya kiswahili Kwa nini alikubali kwenda kushiriki hiki cha lugha za wazungu?
 
I was impressed with the guy, he was competent and bold to raise some issues but i am dismayed as I visited this forum hoping to see discussion on what was raised in "This week in Perspective" unfortunately found two threads both discussing this same issue. does this discussion reflect great thinkers?
 
Ukiamua kutumia lugha fulani itumie vizuri Kwa sababu hakuna anayekulazimisha kuongea. Kuna vipindi chungu nzima vya kiswahili Kwa nini alikubali kwenda kushiriki hiki cha lugha za wazungu?

Ni kitu gani aliongea hakikueleweka mbona wewe unaenda kushiriki lugha za wazungu wakati sio mzungu. doctor kwa nini tusingejadili hoja zilizoibuliwa kwani kila kilichozungumzwa tulikielewa
 
Waheshimiwa wabunge wamezoea kuongea kiswanglish.. Hawajui Kiingereza wala Kiswahili
 
Ule haukuwa ni mtihani wa lugha ni mjadala wenye hoja..kwangu mimi sipati shida mswahili akikosea lugha ya kigeni,lakini kwa ukweli wa dhati huwa nasikitika sana na wakati mwingine kukasirika mswahili aliyekuta wazazi wake wanaongea kiswahili,akaenda shuleni na kufundishwa kwa lugha ya kiswahili anapofanya makosa dhahiri ya ama kuongea au kuandika kiswahili.

Ajabu ni kwamba hakuna mtu anayemlaumu au kumkejeli...ngoja aandike makosa kwenye lugha ya kiingereza utashangaa watu wanavyomshangaa kama alivyoshangaa huyu Dr Kitila.

Ukitaka kujua watu wanavyoabudu hii lugha -anagalia watu waliokosolewa kwa kupinda kiingereza humu kwenye posts zao...Wamekaa kimya pengine kwa kuona aibu.Lakini ingekuwa kiswahili wangelipuka kwa matusi.
 
bora mkosamali asiejua kingereza au mrusi asiejua kingereza?
 
Tatizo kubwa la Waafrika ni kujidharau baada ya kudharauliwa kwa miaka mingi na Wazungu. Waafrika ni watu pekee ambao hudharauliwa kuliko watu wengine wowote wale duniani. Dharau hiyo imeendelea hadi katika lugha zetu, lugha za Kiafrika zinaonekana si lugha za watu wasio na umuhimu wowote. Si walaumu watu wanaoona kuwa kutokujua Kiingereza ni tatizo kubwa... kwa sababu wamefanywa hivyo, si kwa matakwa yao, bali watu weupe wamewafanya wawe hivyo. UTUMWA WA KIAKILI na KUTAWALIWA KIAKILI. Ukoloni wa akili ni mbaya kuliko ukoloni tuliouzoea.
Nimewahi kuzungumza na watu wa mataifa mbalimbali kama vile Wajapani, Wakorea, Wajerumani, Wachina, Wahindi na Waafrika wanaotokea katika nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa. Baadhi yao wanazungumza Kiingereza vizuri wengine hawana uwezo mkubwa. Kwangu sioni tatizo lolote, wala sishangai. Namshangaa, kwa hakika, sana Mtanzania ambaye lugha yake ya taifa ni Kiswahili analinganisha ubora wa mtu kwa kutumia lugha ya Kiingereza.... LUGHA YA WAKOLONI WAKE...
Suala la ajabu kabisa ni pale Mzungu anapokea lugha ya Kiswahili, au Mtanzania anapokosea kuzungumza lugha ya Kiswahili na anaonekana hajafanya kosa kubwa, lakini akikosea Kiingereza tunalalamika.... Nasikitika kuishi kwenye jamii isiyojitambua na kuishi kama makopo matupu yenye mabaki makubwa ya ukoloni katika akili yake... HATARI!!!!
Nina wasiwasi na ubora wa elimu wa nchi yetu... haiwezekani miaka hamsini baada ya uhuru watu wake "huru" wana mawazo yaliyochakaa kiasi hiki... tuna safari ndefu ya kuutambua utu wetu, kuutambua utamaduni wetu na kuutambua Uafrika wetu.
MWAFRIKA USIPOJITAMBUA HUTATAMBULIKA... "Know thyself" Socrates.

Mkuu nimekuelewa sana lakini je hatuna uwezo wa kuikataa hii lugha kwa sababu inaweka vikwazo kwenye mawasiliano? Huyo mkosamali alikuwa ana point nzuri lakini lugha ilimzuia kuelezea kiufasaa kile anachokikusudia.
 
The use of English language inhibits comprehension, by many, of the issues discussed within Adam Simbeye’s “This week in perspectives” programme which to my opinion is designed for specific groups of urban, educated, family affluent, and middle- class citizens.
 
Itumike Lugha ya Kiswahili kujadili mambo yanayogusa watanzania wote na ili kuwezesha washiriki kuchambua mambo kwa Kina. Mawazo mazuri waliyonayo wanashindwa kuyawasilisha kwa jamii kwavile kiingereza kinasumbua
 
Back
Top Bottom