King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 55,290
- 77,651
Umofia Kwenu Wana JF,
Kuna kero Kubwa sana hasa kwenye viwanja vilivyopimwa vya halmashauri,Wakishauza viwanja vyao wanasahau kabisa kuwaletea miundombinu kama kurekebisha barabara,kupeleka umeme,maji n.k barabara walizochonga wakati wanaviuza ndio hizo hizo hazijawahi kurekebisha hata mara moja,Kuna mradi mmoja wa manispaa ya Temeke umeme kwenda kwenye block ni kama zinahitajika nguzo kama 3 kufika kwenye mradi lakini huu ni mwaka umepita hata nia hawana,kwa kero hizi sidhani kama skwata zitapungua.
Kero ya pili ni vibali vya ujenzi,Yaani mtu unaomba kibali cha ujenzi inapita hadi miezi minne ukifatilia kibali unaambiwa bado hakijatoka mara ooh baraza la madiwani halijakaa,sasa anayetoa kibali cha ujenzi ni Diwani au Engineer? Cha kushangaza sasa ukisema ngoja nianze kuchimba msingi nianze haipiti dakika sifuri washakuja na migari yao ya SM eti kwanini unajenga bila kibali huu ni Upuuzi,Waziri Lukuvi tunaomba ututatulie hii kero(Jipu),Kwanini kibali cha ujenzi mmzungushe mtu?
Kero ya tatu ni watu wananunua viwanja wanaweka vichaka bila hata kukiendeleza,utakuta mtu tangia anunue hajawahi hata kufyeka nyasi,ningependa watoe tamko mtu asiyeendeleza kiwanja chake anyang'anye apewe mwingine,mkifanya hivyo maendeleo yatawahi kuja kwenye miradi mipya ya viwanja,kuna wengine wananunua lengo lao ni kuviacha wakisubiri thamani ipande wauze,hao sio wakuwapa wanyang'anywe wapewe wenye uhitaji.
Nawasilisha Straighta outta Minjingu Near Koromije.