Mh Lema, tafadhali liangalie hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh Lema, tafadhali liangalie hili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by dropingcoco, Jun 16, 2011.

 1. d

  dropingcoco Senior Member

  #1
  Jun 16, 2011
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Najua unapita JF kwa hiyo sina wasiwasi na ujumbe wangu huu kwako. Arusha pale soko kuu kuna wimbi kubwa la watoto ambao umri wao unadhihirisha wazi kwamba wanatakiwa kuwa shule, na nahisi wengine wamekimbia shule ili wakafanye biashara ya kuuza mifuko na kubeba vifurushi vya wamama waliotoka kwenye manunuzi hapo sokoni. Wale watoto wanakera sana, na kama mtu unayependa taifa lako huwezi kuona kundi kubwa kama lile la watoto likiwa pale bila kupata elimu wakati tunasema watanzania tunapambana na Ujinga, Umaskini na Maradhi. Kwa mtindo huu ujinga hautakaa uishe hapa nchini. Chama cha magamba kimeshindwa kuwashughulikia, tuna imani na chama chetu cha ukombozi. hivyo basi tungeomba tuone unachukua hatua kama mbunge tulie na imani nae. Na pia sehemu zingine za nchi zenye sura kama hii basi nadhani kilio cha sisi watanzania wenye lengo zuri na nchi yetu kitakuwa kimesikika, na kuweza kuchukuliwa hatua ili tuweze kumshinda huyu adui Ujinga.

  Nawakilisha
   
 2. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nakupongeza sana kwani hii thread, ni issue na mbunge wetu tunaamini analimudu hata ikibidi atushirikishe.
   
 3. d

  dropingcoco Senior Member

  #3
  Jun 16, 2011
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pamoja mkuu, vita kama hizi lazima tuzipigane ili tuweze kushinda vita kubwa ya 2015
   
 4. M

  MAURIN Senior Member

  #4
  Jun 16, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbunge wetu ni mpiganaji wa ukweli kwa ARUSHA ndiye rais hilo halina ubishi,naamini LEMA anaweza kama ameweza kusomesha watoto 400 hatashindwa juu ya hao watoto waliopo hapo sokoni
   
 5. j

  jnuswe JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,271
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Asante kwa hilo anaweza pengine asipitie humu , unaweza pia kupata contact yake umpigie kumjuza , Mh. Lema ni msikivu
   
 6. d

  dropingcoco Senior Member

  #6
  Jun 16, 2011
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  contact zake kupata sio tatizo, ikishindikana kabisa ndio tutapiga simu, lakini naamini hapa JF kuna makamanda wa kutosha, kina Mnyika, Mdee, Regia na hata rais wetu mtarajiwa yupo, ujumbe utamfikia tu, hata wewe Nanyaro, Kilombero kunakuhusu
   
 7. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  Yah.....kuna ka ukweli
   
 8. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mkuu! Nakupongeza kwa thread kwani ina2gusa, na la nyongeza ni pale Mianzini nako ni karaha flu nalo si pa kuacha. NAWAKILISHA!!
   
 9. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  nawaonea raha arusha, mbunge wenu msikivu atawasikia. damn abood, sijui moro itabadilika lini.
   
 10. N

  Nicolas Member

  #10
  Jun 17, 2011
  Joined: Oct 12, 2007
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Touchlife - Moro mpaka mjivue magamba yote si leo !! Watoeni kabisa !
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kweli hii inaumiza kuona watoto ambao walipaswa kuwa shule na badala yake unawaona wanauza mifuko na kubebeshwa mizingo huku wakiambulia malipo ya 300 au 500...ukiwauliza watakupa sababu kama tumefunga shule, tumetumwa na wazazi, wengine wanasema hawana wazazi na wana wadogo zao wanao wategemea hivyo inabidi wahangaike, linalo niumiza ni wazazi kuhusika na hili swala kweli mwanao wa miaka 10 unamtegemea akuendeshee familia yako, hii ni aibu na kukwepa wajibu na kumnyima motto haki zake za msingi… wito wangu wananchi wa Arusha wote tunawajibike kwani tunajua fika elimu ya msingi ni lazima ingiwa hata waoenda wanarudishwa kisa hajatoa mchango wa 200 ya mlizi au ya choo hivyo tuisaidie serikali kwa kuya ripoti mambo haya kwa sehemu husika kama wenyeviti wa mita, madiwani na kwa wabunge…kwasababu tukiangalia sokoni tu tutakuwa hatusaidii sana kwani kuna wengine wanaponda kokoto kule majengo, wengine wana chuma kahawa msimu unapofika, wengine wanasomba maji mitaani hasa kwa watu wana jenga…
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Preta kuna kau-kweli siyo ukweli!?
   
 13. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #13
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  huu uzi umenikumbusha hizo kero za pale sokoni, ukiingia tu watoto wanakuvamia kama inzi wanavyovamia nanihii......mimi hili jambo huwa linaniudhi sana na huwa nawauliza nyie watoto saa hii mnatakiwa muwe shule mnafanya nini hapa......ukishawauliza hivyo wanakuona kimeo taratibu wanapotea.......bila hili swala kuangaliwa kwa umakini watoto hawatasoma na wote watakimbilia sokoni.......na pale eneo la mianzini napo pamegeuka kero......watoto sijui wanavuta nini kwenye mikono ya makoti muda wote wanakuwa wamelewa......naamini mbunge wetu atashughulikia jambo hili
   
 14. W

  Wisson Member

  #14
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 45
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Yeah, this z very nice observation p'se Mr Mp of Arusha municipality work on that seriously. I'm in rock city and situation here z pathetic, yaani watoto wa mitaani ni so, wako wengi mno katikati ya Jiji hili la Mwanza na vitongoji vyake. wote wangetakiwa kuwa shuleni. TBC1 wamewai kuitoa hii situation recently kwenye taarifa yao ya habari.
  Natoa hoja kwa Waheshimiwa wabunge wa majimbo mawili ya Mwanza Mh. Wenje na Highness please lishughulikieni hili mkishirikiana na halmashauri ya jiji kwani hata Meya nadhani mnatakiwa kumshirikisha ili kuondoa hili tatizo. Naumia sana kila ninaposhuka kwenye hiace pale kituo cha Kauma napokewa na mikono karibu kumi ya watoto wanaomba hela ya chai au chakula. Siamini kuwapa chenji aliyonirudishia konda itawasaidia.
  Kwakuwa hii thread ina jina la Lema na naamini ataisoma na pengine Wabunge wa Mwanza hawataisoma yote, basi Mh. Lema na mashabiki wake watakaosoma mchango huu pelekeni huu ujumbe kwa Mh. Wenja na Mh. Highness wabunge wa Jiji la Mwanza.

  HAVE A NICE TIME
   
 15. M

  Maswa Member

  #15
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nichukue fursa hii kukupongeza mdau uliyeanzisha hoja hii muhimu sana, tusipokuwa makini hili taifa tunaloliita la kesho! halitakuwa kama tunavyolitarajia. Niombe jitihada kuhusu elimu kwa watoto zifanyike kwa kasi kubwa na isiwe Arusha tu, bali iwe ni mpango kwa nchi nzima. Kwa watoto ambao wako Arusha pekee hawataweza kuleta mageuzi na mabadiliko sahihi ya baadae kutokana na ukubwa wa nchi yetu. Sitii shaka kwa viongozi wetu makini wa nguvu ya umma watalishughulikia tena mapema. Nitoe mfano wa ugonjwa wa cancer, huwa cancer ikiingia sehem ya mwili hupashwa kufanyiwa huduma husika hiyo sehemu ya mwili ili isisambae sehemu nyingine, hivyo pia illiterancy ni kama cancer ambayo inaanza sehemu kidogo kwa baadae unajikuta imetapakaa taifa zima. Let us fight for changes all, we are the people whom we have been waiting for to bring changes. Nashauri pia mapambano dhidi ya hawa maadui watatu umasikini, ujinga na maradhi lazima tupambane nao wote na siyo kazi ya wachache "viongozi kazi yao ni kusimama mbele na kutoa mwonmgozo yaani kutoa mbadala kwa kila kinachofanyika" Pamoja sana mdau!
  Nimewasilisha ndugu wadau!
   
 16. papaa masikini

  papaa masikini Senior Member

  #16
  Jun 18, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 164
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mkuu,hilo limeonekana,na kwakuanzia na Bavicha Arusha,imeanza kujenga ukaribu na NGO's,zinazohusika na maswala ya Elimu,kwa ajili yakuanza kuliangalia hili tabaka lililosahaulika kwenye elimu,ile hali dunia inakwenda kwa kasi kwenye mabadiliko ya kiteknolojia!!
  Ukweli hakuna taifa lililoweza kuendelea,pasipokuwa na rasili mali watu,ambayo imejengeka kielimu zaid,na kimaarifa!!
   
Loading...