Mh. Hamad Rashid LIVE on Star TV

Mimi ni mwanaharakati wa mageuzi na naomba kumpa pongezi Mh. Hamad kwa kutetea heshima ya chama chake.

Naomba niseme waziwazi kwamba sioni tatizo kwa yeye kutamka nia ya kugombea uongozi ili ajaribu kukiimarisha CUF kinachoonekana waziwazi kupoteza mwelekeo. Tatizo ninaloliona hapa ni ulevi wa madaraka wa viongozi ndani ya vyama vya kisiasa na uoga wa kuwaachia wengine madaraka.
 
Nimependa msimamo wa Mh Hamad kwa kuwa mkweli juu ya muungano tofauti na baadhi ya wazanzibari wanaobeza umuhimu wa muungano.
Kauli ya Maalim Seif kwamba atafanya lolote kushinda ni kauli ya kimafya. Je katika hili cuf inajitofautishaje na ccm ambacho mmekuwa mkikilaumu muda mwingi kwa kujipangia ushindi?
 
Binafsi sitaki kumhukumu Ahmad Rashid kwamba ni mroho wa madaraka hata hivyo kauli yake kwamba yeye si mroho wa madaraka kwa sababu tu amehawahi kukataa vyeo kwangu ni hoja isiyo na mashiko! Historia inaonesha kwamba viongozi wengi wa kisiasa wanaanza vizuri lakini kadri wanavyoendelea kuwa madarakani ndipo wanapoanza kuyatamani zaidi madaraka!!!

By the way, ameshasema kwamba enzi hizo alikataa pendekezo la kuwa waziri wa mambo ya ndani kwavile alikuwa hajakomaa na alihitaji kujiifunza zaidi.....inawezekana anajiona ameshakomaa na hivyo kutamani zaidi madaraka tofauti na awali!
 
Kuna tetesi (rejea mahojiano ya Ismail Jussa na idhaa ya kiswahili ya ujerumani siku ya Jumanne tarehe 13/12/2011) pia kuwa Mhe. Hamad Rashid anatumiwa na CCM kuanzisha mgogoro CUF na ameahidiwa kuwa mgombea mwenza wa urais kwa ticket ya CCM mwaka 2015. Analizungumziaje hili?

kama kweli jussa alisema hivyo basi yule mhindi mpumbavu,kwani kuna hasara gani hasa kwa cuf wakiwa na makamu wa rais kwenye serikali ya muungano na wakati huo huo zanzibar nako wakishikiria nafasi hiyo hiyo?au kwa kuwa atakua hamad rashid basi yeye inamnyima usingizi
 
Swali kwa Hamad: Kwa nini usifikirie kuhama chama kwa vile ni dhahiri CUF hawakutaki, usin'gang'anie !!. Napendekeza uhamie Chadema, ni dhahiri utakiongezea nguvu na hasa upande wa visiwani.
 
hamad,cdm wanasema cuf ni ccm b.mbona hamuonekani kupinga hilo lakini kwenye madaraka mnatumia nguvu kubwa?
 
Hamad Rashid ni mroho wa madaraka, that is very clear, namuuliza swali moja kama ifuatavyo.
- walipitisha mswaada pale bungeni, je? walieenda ikulu kufanya nini hasahasa?
 
Mjadala wa Kipindi cha TUONGEE ASUBUHI upo hewani na Sinai Shaka undani kuhusu mgogoro unaofukuta ndani ya cuf utatolewa sura ya upande wa pili kwa kina. Fuatilia mjadala

1. Yahya mbona umeliacha swali la DT125 Pg3?

2. Huyu Rashid ana uwezo mkubwa kuliko Maalim - akili yake imetulia na ameonyesha umahili wake akiwa kiongozi wa upinzani bungeni. Huyu ni Mtanzania halisi - yu bara na visiwani
 
Swali la chipaka la kujua msimamo wa chadema ktk mchakato wa katiba ni mada tosha ambayo ya kujadiliwa ni kweli hawakutoa walitoka nje,yahaya ifanyie kazi hiyo
 
Mimi ni mwanaharakati wa mageuzi na naomba kumpa pongezi Mh. Hamad kwa kutetea heshima ya chama chake.

Naomba niseme waziwazi kwamba sioni tatizo kwa yeye kutamka nia ya kugombea uongozi ili ajaribu kukiimarisha CUF kinachoonekana waziwazi kupoteza mwelekeo. Tatizo ninaloliona hapa ni ulevi wa madaraka wa viongozi ndani ya vyama vya kisiasa na uoga wa kuwaachia wengine madaraka.
Ndugu yangu mi mwenyewe namshangaa Maalim Seif... hana muda wa kufanya mambo ya chama kutokana na kutingwa na shughuli za ikulu ya zanzibar na hilo analijua,lakini bado anang'ang'ania aendelee kukishikiliwa cheo hicho ambacho kimekaa kiutendaji zaidi ndani ya chama.

Kama anaona hamad rashid hafai bora basi atafute mtu anaemuona anafaa kwake huko cuf ampigie debe ashinde uchaguzi wa ndani wa chama chake nafasi ya katibu mkuu kuliko kuing'ang'ania nafasi hiyo huku akijiua hana muda wa kuitumikia, huo ni ulafi na wapemba mi ntawashangaa sana wakiendelea kumuunga mkono hata katika jitihada yake hii ya kuimaliza kabisa CUF, naona ndio mana hata lipumba kaamua kumkimbia na kukaa nae mbali, nadhani nae kishamuona kwamba jamaa ni problem.

Haiingii akilini eti rais na pia uendelee kuwa katibu mkuu wa chama, ina maana hakuna watu wenye uwezo wa kufikiri kama wewe? CUF itakufa kama INKATHA FREEDOM PARTY ya BUTHELEZI, nae alikua na tabia kama za seif!
 
Yahya usitupe kapuni hili swali kwa Hamadi Rashidi, tafadhali muulize:

A. Hili suala tete la udini linalolinyemelea taifa letu yeye analichukuliaje kwa sasa?

B. Ikiwa yeye ameamua kujitutumua kumkabili Maalim Seif, aweze kuchukua nafasi ya uwenyeketi, je akipata ni nini cha tofauti atakachofanya ambacho Maalim Seif hakuwahi kukifanya kwa manufaa ya chama na taifa kwa kwa ujumla wake?
 
Asante Yahya kwa kuuliza maswali yangu yote ingawa swali langu la posho amelijibu kisiasa zaidi.
 
Ahsante wanaJF wote kwa kushiriki na Maswali yenu ya msingi muda haukuwa rafiki sana, ila hoja nyinyi za msingi zitakuwa zimejibiwa, ahsanteni na weekend njema
 
Amejibu kiujanjaujanja hamad anawanafunzi 18 anaowasomesha hv anaona kuongezwa kwa posho itamsaidia
 
Mjadala wa Kipindi cha TUONGEE ASUBUHI upo hewani na Sinai Shaka undani kuhusu mgogoro unaofukuta ndani ya cuf utatolewa sura ya upande wa pili kwa kina. Fuatilia mjadala
...Yahya, undani kuhusu huo mgororo haukuweza kutolewa, zimeletwa siasa zile zile za kinafki. Hamad Rashid hajataka kuwa mkweli, kuhusu hasa kinachoendelea CUF -anasema anamweshimu sana Maalim Seif, wakati huo huo akimchimba chini kwa chini- na ameendelea kujichanganya kuhusu msimamo wake juu ya mambo mbalimbali yaliyotokea mwaka huu. Amejichanganya juu ya kambi ya upinzani bungeni -ati sasa, Mbowe afikirie kuhusisha na vyama vingine katika kambi, muswaada wa katiba, suala la posho -kama mfumo mbovu, wao walikuwa wapi wenzao walipotaka kurekebisha mfumo?

...Nadhani, wana CUF wanamwona na kumwelewa Hamad Rashid kwa picha iliyo wazi. Wachukue tahadhari mapema na kufanya maamuzi sahihi.
 
Back
Top Bottom