Mh. Hamad Rashid LIVE on Star TV

Hello Yahya, nina concern moja:

Jana wakati akiongea na vyombo vya habari, makamu wa rais wa Zanzibar (wa kwanza) alisema haoni kama ni busara kuzungumzia mambo ya chama kupitia vyombo vya habari hususani magazeti na badala yake watumie vikao vya chama; Jem Mh. Hamad Rashid haoni kwamba anatakiwa kutumia vikao vya chama kueleza madukuduku yake kuliko kuendeleza malumbano kupitia vyombo vya habari.
sasa mkuu wakifanya hivo sisi watu wa kawaida tutelewaje maana taarifa ya kuambiwa na mtu ni tofauti na kusikia mwenyewe.. Mi naona wako sawa ili hata sisi tujue kinachoendelea kwenye chama kuliko kusoma taarifa za magazeti
 
Swali kwa Hamad Rashid.
Ana maoni gani kuhusu kufukuzwa kwa Kafulila, na kama hili lingetokea kwake ndani ya CUF angefanyaje?
 
Ahsante Yahya
i) Kwa nini yeye amekuwa na mgogoro na Chadema na wakati vyote ni vyama vya upinzani?
ii) Kwa nini afikirie kuanzisha chama kingine cha upinzani,haoni kuwa ni kudhoofisha upinzani?
 
mh. Hamad rashid vp munalumbana kwenye vyombo vya habari lakini hivi jimbo lako unalipitia au ndo uchu wa madaraka
 
Kabla kipindi hakijaisha muulize:

Tujaalie maamuzi ya chama chako hatimae ni kukufukuza uanachama na hatimae ukapata ugumu wa kuanzisha chama kingine kwa sababu yoyote ile iwayo.Ikifikia hapo ni chama gani anaonelea atapendelea kujiunga nacho kati ya CCM na Chadema ?.
 
Kafulila na Hamad waliungana Bungeni, the same leo wanakua vinara wa migogoro CUF na NCCR mageuzi.
Kwanini hamadi hataki kukiri kua yeye ni mroho wa madaraka?
 
Yahya, baada ya kuona maswali yote yaliyoulizwa nimeona niache maana natambua kuwa muda wenu unakuwa umebana. Nishukuru kwa kutushirikisha na niwashukuru wote waliouliza maswali, mengi umeyasoma!
 
Asante sana Yahya,

Kutokana na Muda kutokuwa rafiki na wachangiaji wengi kuwa na maswali mengi, naomba umshaur Mheshimiwa Hamad Rashid ajiunge JamiiForums aje kutujibu maswali yale mengine ambayo hatoweza kuyajibu on air sasa.

By the way kuna maswali mengine anajibu kisiasa zaidi kama lile la kuanza mchakato bungeni ili kambi isiyo rasmi ya umbizani itambulike ni uroho wa madaraka, amejibu kisiasa zaidi hajakubali wala kukataa japo watu wazima tumejua amekubali ni uroho wa madaraka.
 
naona hamad anasema katiba ya jamuhuri ya muungano inasaidia kuleta migogoro kwenye vyama kwa kuwa inalazimisha watu wawe kwenye vyama ili waweze kuwawakilisha wananchi, matokeo yake ni kwamba watu ambao hawana interest na vyama wanalazimika kuwa wanachama wa vyama flani.

Hii ina maana analaumu kwanini mgombea binafsi hajaruhusiwa?

strong point toka kwa mzee hamad rashid,hii mi nimeipenda kwa kuwa tuko wengi ambao hatufungamani na upande wowote lakini katiba inatulazimisha eti lazima tuwe kwenye hayo magenge ndio tushiriki siasa sawasawa,very disturbing!
 
kuna huyu kibna sijui ni mtangazaji au nani anasema KATIKA WANASIASA TOP 5 TZ HAMAD NAYE YUMO sijui amepima kwa vigezo gani?
 
Hahahahahah,
invisible acha kuziba mid0mo watu
Kuna maswali ukimwuliza mtu unaweza kumfanya aweweseke au apotee kabisa kwenye hoja.

Swali hilo ni zuri, lakini nchi yetu tunaifahamu na uwezo wa kujibu maswali kama haya tunaufahamu pia!
 
Namshauri Hamad rashid kutaka nafasi ya uongozi ndani ya chama jaribu kuepuka marumbano na viongozi wengine ambao wanaonekana kama wanatumwa na viongozi wa juu mimi naona haya ya kwako ni kama ya LOWASA,chama kweli kina hitaji utendaji wa bara na visiwani
 
kwa ni nini vyama upinzani nchini vimekuwa vikiandamwa na migogoro,je inasababishwa na wana chama wenyewe ama mamluki kama wanavyodai wenyewe?
MGOGORO ULIOPO NDANI YA CCM UNAUONA KWELI? Dont focus on opposition only
 
Swali :
Hamadi atuhakikishie watanzania kwamba hatumiwi na watawala kupunguza nguvu ya upinzani.
 
kwanini Hamadi Rashid aseme ataanzisha chama kingne akifukuzwa?ameshaanza mchakato wa chama kipya? kwanini asijiunge na moja ya vyama vya upinzan vilivyopo kuliko kuongeza wimbi wa vyama na kuendelea kugawa kura za upinzani
 
Yahaya naomba muulize Hamad Rashid leo anaona umuhimu wa katiba ya mgombea binafsi . Vipi hawakushirikiana na CDM kihusu maswada wa katiba kwa ni kwa ilivyo Sasa CCM imeuteka na nafasi ya kubadilisha katiba itakuwa ndoto?
 
Usimsahau huyu mzee wa TADEA ndugu Yahya...

...........anatakiwa atueleze Watanzania seriousness ya ushiriki wake katika siasa za Tanzania, je anadhani amechangia chochote positively???
 
Back
Top Bottom