Mh. Hamad Rashid LIVE on Star TV

Swali:

Mgogoro unaofukuta ndani ya CUF unatokana na ugomvi wako wewe Hamad na Maalim Seif, na kutokana na kutoelewana kwenu nyie wawili, hamuoni kwamba mnaweza kusababisha mpasuko ndani ya chama na kusababisha chama kusambaratika kwa maslahi yenu binafsi?

Na kwakuwa unatambua kuwa Mgogoro si mzuri kwa afya ya chama chenu, kwanini usijiweke pembeni na suala linalosababisha mgogoro na kubaki kuwa mwakilishi?
 
Unaweza litazama swali hili "migogoro ndani ya vyama vya siasa ina tija?" kwa sura mbili.

Ya kwanza ni ndio inatija endapo kiini cha mgogoro huo ni kutetea values za kidemokrasia zinazojikita katika kuimarisha demokrasia ndani ya vyama (intra party democracy).

Sura ya pili ni kwamba migogoro ndani ya vyama vya siasa haina tija endapo kiini cha mgogoro huo ni kudidimiza demokrasia ndani ya vyama.

Sasa vyombo vya habari ni juu yavyo kutujibu sisi nini ni vision na mission yao katika hili? Kuendeleza demokrasia ama kuididimiza? Katika kutekeleza hili vitujibu jee ni kwa namna gani vinajitahidi kuepuka kufungamana na maslahi fulani fulani?
 
Yahya uko makini, ahsante kwa kusoma swali langu. Japo tuna maswali mengi lakini hawa wanasiasa wanaudhi, wanatuona wananchi ni wa kutawaliwa tu
 
Mjadala wa Kipindi cha TUONGEE ASUBUHI upo hewani na Sinai Shaka undani kuhusu mgogoro unaofukuta ndani ya cuf utatolewa sura ya upande wa pili kwa kina. Fuatilia mjadala

Naomba kumuuliza Hamad Rashid.........Je,alipokuwa anapitisha mswada wa katiba tena kwa mbwembwe na kusema kuwa ni bora anadhani kuwa hii ni sahihi? na Je,adhani kuwa hii ndio laana toka kwa watanzania? na kwa hakika nadhani ajiandae kutumuliwa tu,Maalim seif hamad amakwisha sema hawata sita kuchukua maamuzi magumu kwa mwanachama anayeleta chokochoko na kwenda kinyume na taratibu za chama..
 
Maswali:
1. Kwanini mara nyingi ameungana na CCM kupiga vita CHADEMA hasa swala mchakato wa katiba mpya wakati tunajua ule mchakato una dosari nyingi tu?
2. Je huwezi ukawa mwanachama wa kawaida na ukajenga chama chako kwa kufuata utaratibu wa chama?
3. Inaonekana CUF ina ukaribu sana wa mahusiano wa kisiasa na CCM kuliko vyama vya Upinzani, analizungumziaje hilo?
 
Hamad yupo settled sana wakati anajibu maswali, nimefurahi kuwa naye anaona mapungufu ya upande wa mgombea binafsi.
 
Muulize tena:

Kabla hata hukumu dhidi yako ndani ya CUF haijatolewa umetangaza nia ya kuanzisha chama kipya. Je, huoni ni vyema mkasuluhishana na kubaki ndani ya CUF? Kwa upande mwengine mheshimiwa Hamad huoni kutakuwa na ugumu kupata wanchama na kutimiza masharti ya msajili. Au umejiandaaje na hilo ili yasije yakakukuta kama yale ya CCJ?
 
Hello Yahya, nina concern moja:

Jana wakati akiongea na vyombo vya habari, makamu wa rais wa Zanzibar (wa kwanza) alisema haoni kama ni busara kuzungumzia mambo ya chama kupitia vyombo vya habari hususani magazeti na badala yake watumie vikao vya chama; Jem Mh. Hamad Rashid haoni kwamba anatakiwa kutumia vikao vya chama kueleza madukuduku yake kuliko kuendeleza malumbano kupitia vyombo vya habari.
 
Mh.hamadi rashidi mimi sinashaka kwamba unania ya dhati kuongoza chama.je kupitia migogoro hii huoni shida kupata ushindi?
 
Hamad Rashid, anasema ametia nia ya kugombea, na kutia nia si mbaya kwa sababu ni haki ya kikatiba. Anasema hata Maalim Seif ameshasema kuwa atagombea, anasema Maalim Seif alisema kuwa yeye (Hamad) ni mgonjwa hivyo hafai.
 
Vyombo vya habari mmekuwa wapotoshaji, mnatakiwa mjitambue na mjitenganishe, maana kuna vyombo vya kuripoti habari na kuna vyombo vya kutengeneza habari sasa kati ya hv ni lazima muangalie ni habari ipi inatakiwa iripotiwe na habari ipi inatakiwa itengenezwe.

Mkitambua hivyo taaluma hii itakuwa nguzo kubwa katika kufikia malengo ya kuhudumia jamii na Waandishi wengi mmekuwa mnakurupuka tuu na wengine wanafuata upepo hii ni hatari sana, Haki ya kutoa habari hamuitumii vyema.
 
Kuna tetesi (rejea mahojiano ya Ismail Jussa na idhaa ya kiswahili ya ujerumani siku ya Jumanne tarehe 13/12/2011) pia kuwa Mhe. Hamad Rashid anatumiwa na CCM kuanzisha mgogoro CUF na ameahidiwa kuwa mgombea mwenza wa urais kwa ticket ya CCM mwaka 2015. Analizungumziaje hili?
 
SWALI KWA HAMAD:

Inavyooenekana hamadi unataka zaidi ya Ukatibu mkuu

1. Na kama unalengo la kuanzisha chama cha siasa kwanini usiondoke mapema CUF na ukaanzishe chama chako badala ya kukodi vibaka wenye mpanga kukatakata watu Chechnia?
2. Mbona umeanza kampeni za ukatibu wakati muda wa kampeni bado?
3. Lowassa amekupatia shilingi ngapi ili kukamilisha mkakati wake?
 
Mi sioni haja ya kumuuliza swali/maswali,hana lolote huyu.ni kigeugeu,haeleweki,yupo kama popo!muungano wao na ccm inawatafuna sasa,hawawezi pinga serikali ambayo wanashirikiana nayo.watatafunana mpaka watamalizana.
 
swali langu kwa bwana Hamad; kitendo cha Hamad kuonyesha nia mapema na kupinga uongozi wa uliopo wa chama chake haoni kuwa unahatarisha uhai wa chama chake? kesho na keshokutwa cuf ikisambaratika haoni kuwa yeye ndiye atakayekuwa chanzo cha matatizo yote hivyo kuatuaminisha kuwa anatumiwa na chama tawala ktk kudhoofisha upinzani kwani pia amekuwa mtari wa mbele kuwashambulia hata chadema?
 
Back
Top Bottom