Mjadala wa Kipindi cha TUONGEE ASUBUHI upo hewani na Sinai Shaka undani kuhusu mgogoro unaofukuta ndani ya cuf utatolewa sura ya upande wa pili kwa kina. Fuatilia mjadala
Naona Hamad anasema Katiba ya Jamuhuri ya Muungano inasaidia kuleta migogoro kwenye vyama kwa kuwa inalazimisha watu wawe kwenye vyama ili waweze kuwawakilisha wananchi, matokeo yake ni kwamba watu ambao hawana interest na vyama wanalazimika kuwa wanachama wa vyama flani.
Hii ina maana analaumu kwanini mgombea binafsi hajaruhusiwa?
Ok, wao kama wanasiasa wanaionaje kasi na nguvu ya New Media (mitandao ya wavuti na simu n.k)? Wamejiandaaje kushiriki? Kama hajui maana ya New Media basi mwache usiendelee kumwuliza maana yawezekana anadhani inatakiwa kuwa controlled.
Naomba nimuulize Mzee wangu hapo Hamad Rashid, ni kwa nini ameanza harakati za kuwania ukatibu mkuu mapema kiasi hiki tofauti na taratibu za kichama? Je kwa sisi ambao tuliofuatilia kipindi cha mwanzo kabisa bungeni mara baada ya uchaguzi na kuona jinsi alivyokuwa anahangaika kubadili vifungu vya bunge ili kuwe na kambi isiyo rasmi bungeni,atatushawishi vipi kuwa yeye si mroho wa madaraka?
a} Ukizingatia ukomavu wa Mh.Hamad katika siasa, je ni sahihi kwa yeye kuanzisha chama kingine endapo atafukuzwa CUF???
b} Anaongeleaje muafaka wa CCM na CUF kwa sasa, umemaliza kiini cha tatizo Znz?
c} Muungano; una maslahi kwa Wazanzibari wa kawaida {tofauti na viongozi}?
Je yeye akiitwa mroho wa madaraka itakua anaonewa? Alipokuwa mkuu wa kambi ya upinzani hakusema kitu na alipokosa akaanza malumbano bungeni na kambi rasmi. Je, nikisema kuwa kwa sasa anataka ukatibu mkuu kwa nguvu itakuwa namuonea? Kama uchaguz ni 2014, mbona ameanza mapema? Kwani kampeni tayari? Na kwanini hayo madai asiyapeleke kwenye vikao?
Au kama CUF ni wazush, kwanin wasijitenge waanzishe chama chao?
mimi naomba nimuulize swali hili. Mh Hamadi Rashid wakati CUF inaingia ndoa na cccm hukuliona hili kwamba litadhoofisha chama chenu kisiwe tena chama cha upinzani, mbona hatukusikia ukipinga mfumo huu?
Mheshimiwa Ahmad Rashid apambane na asiogope hakuna mtu mwenye hati miliki ya siasa za nchi kila mtu ana haki ya kushiriki katika siasa za nchi. Maalim seif amekwisha nogewa.
Ila na wewe uache tabia ya kuwasakama wapambanaji wengine kama CHADEMA. Chama chenu kimepoteza mwelekeo na sasa kimeacha kuwatumikia wananchi na kuanza kugombea ruzuku ambazo ndio nahisi ni chanzo cha migogoro katika vyama vingi vya siasa.
Na nyie waandishi wa habari muache kutumiwa simameni katika taaluma wanasiasa huwa wanawatumia wakati wakiwa na shida ila mkitoa maovu yao wanawashambulia
swali kwa Hamadi. Je haoni cuf kuungana na ccm ndio chanzo cha mgogoro ? Maana imefanya Seif kuacha kufanya siasa za upinzani na kutekeleza sera za ccm? Ile ngangari iko wapi? Je ni lazima Hamad aanzishe chama au awe ktk chama?
Naomba umuulize Hamad; kwa maoni yake baada ya kutafakari sana mustakabari wa siasa na nchi ya Tanzania, kama angekuwa na uwezo wa kureshape au kuanzisha upya, nini angefanya tofauti na ni eneo gani linahitaji mabadiliko makubwa?
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.