Skillionare
JF-Expert Member
- Nov 6, 2011
- 1,190
- 523
Kamanda Lema ,jf honour u !
One thing about Godbless Lema, one distinct character, this just one that his enemies don't know about, is; HE RARELY SPEAKS OR WRITES, BUT WHEN HE DOES SO, THUNDER CAN BE HEARD FROM AFAR!!!!
Godbless Lema is one of the few MPs who writes few paragraphs whose content is that of book of Revelation.
.......Ohh...and he means what he says, always has...!!!
Naomba mtu anisaidie na summary ya ilichoandikwa hapo, nimesikia uvivu kusoma
Lema aende campaign kokote ila nae akae akijua Arusha kumedorora. Akae atulie, atulize vurugu kwa wafuasi wake afanye shughuli za maendeleo. Wabunge wenzake wa CDM tunaona wanayoyafanya yeye yako wapi? Ajue 2015 iko mlangoni inabisha hodi.......................... Hakuchagyuliwa kwenda mahakani kujibu kesi bli kuhamasisha maendeleo plz
Hata ukiandikiwa summary bado utasikia uvivu kufikiri.Naomba mtu anisaidie na summary ya ilichoandikwa hapo, nimesikia uvivu kusoma
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemshukia Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, kikisema kuwa ameanza propaganda za kukibeba Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki.
Tendwa alikaririwa na vyombo vya habari akimtahadharisha Mbunge wa CHADEMA katika Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, kutokanyaga kwenye kampeni za uchaguzi huo kwa tishio la kuuawa na viongozi wa kimila (Washiri).
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika, alisema kauli ya Tendwa ni ishara ya kutumia madaraka vibaya kujaribu kuibeba CCM kwenye uchaguzi huo mdogo baada ya wananchi wa Arumeru kuonyesha wanakipenda CHADEMA na kutaka mabadiliko.
"Tendwa akae pembeni aache uchaguzi kwa vyama vya CHADEMA na CCM. Alikwenda kufanya tathmini na amelizungumzia jambo moja ambalo amelifanya propaganda, mbona hazungumzii rushwa iliyofanywa na CCM kwenye kura za maoni?" alihoji Mnyika.
Alisema wadau mbalimbali wamelalamikia vitendo vya rushwa vilivyojitokeza CCM na kwamba yeye kama msajili kuna sheria tatu ambazo zinampa mamlaka ya kuzungumzia hayo.
Alisema kuna sheria ya vyama vya siasa ambayo moja kwa moja inampa wajibu wa kuzungumzia rushwa kadhalika ile ya gharama za uchaguzi ambayo inampa mamlaka ya kufuatilia vitendo hivyo.
"Kama ana nia njema, vitendo vya rushwa ambavyo pia vinazungumzwa na wana-CCM wenyewe angevitolea kauli, kuacha hayo ni kutumia madaraka vibaya. Kuyaacha mambo ya msingi na kulizungumzia moja tu ni propaganda za kuibeba CCM," alisema
Katika hilo, Mnyika alimtaka Tendwa afanye mambo mawili; kwanza atoe ripoti ya kina ya tathmini aliyokwenda kufanya Arumeru na ijulikane wazi na pili, kwa sababu ameitaja CHADEMA awakabidhi nakala ya ripoti kamili aliyoifanya, vinginevyo watachukua hatua.
Mnyika aliwatahadharisha wananchi wa Arumeru Mashariki, kukumbuka kuwa wakati wa kampeni, viongozi wa serikali wamekuwa na kawaida ya kutumika propaganda kusaka ushindi.
"Wanataka wananchi wa Arumeru, wajifunze kilichotokea Tarime mwaka 2008, waliamua kuwa na mshikamano, wakapuuzia propaganda wakaamua kuchagua CHADEMA," alisema Mnyika.
Kwa mujibu wa Mnyika, Machi 3-4 watafanya uteuzi na si kuangalia propaganda kama za Tendwa. Hivyo kuwataka wazee wa Arumeru Mashariki kuwaunga mkono ili kazi waliyoianza mwaka 2010 ilete manufaa.
Source:Tanzania Daima
chadema au lema hawana wanasheria?
tendwa ni wakufungulia mashtaka,ushahidi uko wazi,kama ametumwa na wazee wa washiri yeye ni shahidi nakama ni propaganda yeye ni mtuhumiwa.
katika nchi inayodai inafuata utawala wa sheria haiwezekani mtu amtume mtu mwingine kupeleka taarifa za kumwua mtu na akaachwa hivihivi.
chadema wasiligeuze hili kuwa la kisiasa hili ni kosa na linatakiwa kuwa mahakamani.nitawashangaa sana kama wataenda kwenye kampeni huku tendwa akiwa akiwa uraini.
Jeshi lililo makini lingeweza kuchukulia serious hi taarifa za Tendwa, tusisibiri mpaka mauaji yatokee ndiyo wachukue hatua, na hii ndio udhaifu wa jeshi la polisi wanashughulikia reaction. Mwiteni Tendwa aeleze ni wazee gani hao na wao waitwe kwa mahojiano na karipio kali
Tafsiri ya Udini ni Masaburi kama wewe na MOU yenu mnayoihubiri kila sikuSasa apa udini ni upi? hivi kwako tafsiri ya udini ni nini?
Huo ndio ushujaa na ukomavu wa kisiasa, mapambano yaendelee mpaka Demokrasia ifunguke
na kufikia percent 100% tupo karibu sana kwa pamoja tutaweza.
Naomba mtu anisaidie na summary ya ilichoandikwa hapo, nimesikia uvivu kusoma
Msikubali kudanganywa.