Mh, dhambi ya Uroda..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh, dhambi ya Uroda.....

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ngoshwe, Jan 20, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Wakati baadhi ya dini zinafundisha kuwa dhambi zote ni sawa, nimesikia kwa waumini wa dini fulani kuwa "dhambi mbaya kabisa kwenye vitabu vya Mungu" ni dhambi ya "kumegana" , "kura uroda" au "Kuzini".

  Watetezi wa hili wanadai kuwa dhambi hii inaambatana au kumalizikia na kuvunja amri zote kumi za agano kati ya Mungu na wanadamu kupitia Musa.

  Kwa dhambi ya kuzini, mtu anakuwa amesema uwongo kwa mwenzi wake na huyo atakaezini nae au watu wengine ili kuficha uovu nk. Kwa kupenda zinaa, mtu anakuwa hajamheshimu Mungu wake, wala hajaheshimu wazazi au wanaomzidi umri, anaweza kutoheshimu pia siku ya ibada kwa kuwaza zinaa kichwani hata akiwa kanisani au msikitini, anakuwa ametamani mali ya mtu mwingine (mke,gari, nguo, nyumba nk). Kwa zinaa mtu anaweza kuua (kupitia magonjwa au kuua mwenzake ili ampate huyo wa kuzini nae). Anakuwa ametamani mke asiye wake (wa jirani, rafiki nk) ili atende nae zinaa. Utamu wote wa zinaa kwa wanadamu ni uchafu na chukizo mbele za Mungu na Malaika wake.

  Kwamba, zinaa inahusisha mawazo, maneno na matendo na kushindwa kutimiza wajibu. Ikiwa Mzazi au mtu mwenye majukumu, anaweza kutelekeze familia kwa sababu ya kujikita kwenye fani ya kubwinya "tunda la katikati" nk. Aidha, tafsiri ya zinaa inakuwa imekamilika baada ya mwili na roho kukubaliana (kufanya agano la mapatano ya kutenda dhambi) kwa kukubali kukutanisah ndimi mbili ambazo pengine hazifkuwahi kufahamiani hata kidogo katika maisha na hata malaika walinzi wa ndimi hizo wanaweza kuwa na sifa zisizo sawa machoni pa Mungu.

  Kwa tendo hilo, zinaa inahesabika kuwa ni dhambi ya machukizo kwa Mungu wako na Malaika mlinzi na ndio maana baada ya tendo hilo, ubinadamu huwa unatoweka kwa sekunde kadhaa na hapo huwezi kutambua uzuri au ubaya wa tendo ulilolifanya na pengine ujutie moyoni mwako kwa nini umefanya vile na unapojitambua upo vile ulivyo aibu inakushika (upo uchi!).

  Wakati mwingine, inaweza kukupelekea kwenye ugomvi na huyo uliezini nae kwani maelewano yanakuwa yameisha (kw mf: ukipewa "invoice" ya kulipia huduma uliyopewa na kutoona hailingani na thamani halisi ya kupurudika kwako).

  Enyi wanazuoni, nini ukweli wa habari hii?.
   
 2. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  dhambi zote ni sawa mbele za mungu na zambi zote afanyazo mtu zipo nje ya mwili lakini azinie anafanya ndani ya mwili wake na azinie na mwanamke ana akili kabisa afanya jambo litakomwangamiza nafsi yake
   
 3. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Dhambi zote ni nje ya mwili, lakini zinaa ni juu ya mwili, na wote wanaofanya dhambi ya zinaa wanamuudhi roho mtakatifu. Ole wao wanaomuudhi Roho mtakatifu, maana dhambi zote zinasameheka isipokuwa ya kumtukana roho mtakatifu.
   
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Mungu ni fiction tupu, unawezaje kuthibitisha kwamba mungu yupo?
   
 5. A

  Amwanga JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 11, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  I can prove existence of Mungu. If you want!
   
 6. D

  Donrich Senior Member

  #6
  Jan 20, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mungu yupo,but it depend on what you believe,...Suala hili ni la kiimani zaidi kuliko hali halisi,yapo mambo yanayonifanya niamini kwamba Mungu yupo,kutaja machache ni pamoja na ...Creation ya dunia na vyote vilivyomo tukiwemo binadamu( mimi na wewe),Nyota,mwezi,na viumbe wengine ..sitaki kuamini vilijileta tu, na kwamba hata uhai wa binadamu na hatima ya maisha yake siamini kwamba ni kitu ambacho kipo kinachotokea tu...there must be somebody..na huyo ni Mungu.Bible which is the base of my faith says so,Quruan Say so and even Satan knows it...
   
 7. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Kwa kusema hivi tu umeonyesha huwezi ku prove.
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Kama ulimwengu umeumbwa, kwa sababu vitu complex haviwezi kutokea bila kuumbwa, basi it follows huyo aliyeumba ulimwengu naye ni complex kuliko ulimwengu, na yeye itabidi awe na muumba, na muumna wakeitabidi awe na muumba wake, ad infinitum.

  Ukisema mungu alipata exception kutoka sheria hii, kwamba yee hkuwa na muumba, unaonyesha kwamba hii sheria hiko absolute, kwamba hii sheria ina exception, then it follows kwa nini kma sheria hii inaruhusu exception kwa mungu isiruhusu exception kwa ulimwengu na binadamu?

  Ukisharuhusu mungu awepo bila kuumbwa unakuwa ushaacha loophole ya kwamba inawezekana binadamu na ulimwengu haujaumbwa.

  It is impossible to advcate for creation on the basis of complexity, because it is a never ending pyramid of incosistencies.Kanuni itakayokufanya uamini binadamu kaumba ndiyo hiyo hiyo itakayokufunga uamini mungu naye kaumbwa ukisema umpe mungu upekee wa kusema yeye hajaumbwa, upekee huu huu utakusuta kwa kukuruda na kusema vipi kama upekee huu una apply kwa biadamu pia.

  Contraditions, contradictions.
   
 9. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  dhambi ya kuzini huanzia moyoni kwa kuwa hakuna mtu awazaye kwa mwilibali kwa ufahamu ambao hupeleka mawazo nafsini na nafisi kuamrisha mwili kutenda, na ndiyo maana injili inasema aliyekwisha kutamani mwanamke amekwisha kuzini naye, kwa sbabu kutamani kwatoka nafisini mwa mtu na si mwilini, hivyo mwili ni wa kuamulishwa kutenda kile ambacho nafsi ya mtu imeamua kutenda, kwa kuwa nafsi ya mtu inaongea kwa kutumia kinywa, ikiisha maliza kuongea mtu humalizia matendo ya kile ilichokiandaa nafsi kwa mwili. na ndiyo tendo la kuzini ni faida ya mwilini kwakuwa limeanzia ndani hivyo huishia mwilini halianzii mwilini na kuishia mwilini
   
 10. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Weweeee ni bora uamini tu kuwa yupo kuliko kuamini kuwa hayupo na siku yake ukamkuta huko juu..
   
 11. F

  Future Bishop Member

  #11
  Jan 20, 2010
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 75
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kiranga kama huamini kuwa Mungu yupo ni pole yako kwani wewe tu kuwepo duniani ni muujiza au sayansi ambayo yuko aliyepanga iwe hivyo na huyo ndiyo Mungu tunayeamuamini.

  Jaribu kujiuliza umekujaje duniani na siku ukimaliza safari yako ya hapa duniani unaenda wapi? Kumbuka haujafa ili ujue kitu gani kinatokea mtu akifa. Lakini maandiko matakatifu ambayo kwangu ni Biblia imenionyesha kuwa kifo cha mwili siyo mwisho wa maisha bali ni mwanzo wa maisha mengine ambayo yanategemea nimeishije hapa duniani. Na hapo ninaripoti mbele ya yule aliyeniumba kupata ujira wa maisha niliyoishi.

  Leo huna sababu ya kuuliza huyo naye Mungu nani aliyemuumba, swali hili linaweza lisikusaidie chochote leo na inawezekana unalileta/kujiuliza kwa sababu hutaki kuamini kuwa Mungu yupo.

  Naomba nikuhakikishie kuwa Mungu yupo na ataendelea kuwepo. Unahitaji IMANI kujua kuwa yupo lakini ukishamuamini unakuwa na HAKIKA. Siyo kitu cha kufikirika ni uhalisia kuwa tunamuamini Mungu aliye hai.

  Sijajua maana ya jina lako Kiranga lakini angalia lisiwe na maana ambayo ndiyo inafanya uamini hivi unavyosema!
   
 12. D

  Donrich Senior Member

  #12
  Jan 20, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mheshimiwa Kiranga,nimetangulia kwa kusema jambo hili ni la kiimani zaidi,kwa maana nyingine katika imani we dont need a proof,..ukishaanza kuproof hiyo si imani ni jambo lingine kabisa tunaweza kusema ni sayansi au sheria ukipenda,..Ndo maana wakristo wengi tunaamini kwamba kuna maisha baada ya kifo,lakini wanasayansi hawawezi kukuambia kwamba kuna maisha baada ya kifo kwani they cant proof..are you there Boss!
   
 13. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Afanaleki laila , oh My dog!

  Hapa ndo ushan'mix kuliko Maxists, ..toto..contractions, contractions x3 ....
   
 14. D

  Donrich Senior Member

  #14
  Jan 20, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kiranga upo wapi...rudi tujadili hili suala..ni muhimu sana...
   
 15. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #15
  Jan 21, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  Labda ameenda kujipanga upya, ni hatari sana kauli hizi labda uwe unatokea Urusi, Ireland na kwingineko ambapo napo japo baadhi hawamini uwepo wa "MUNGU" lakini bado wanataja mungu au kuamini "MIUNGU".
   
 16. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #16
  Jan 21, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280

  Ukishaongea imani unaweza kuongea chochote kile, mi nataka facts, testable tangible observable facts.

  Imani uanweza kuamini mungu anakaa misitu ya Kongo, poa tu kivyako.Ukitaka kuleta kama fact that is another matter.
   
 17. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #17
  Jan 21, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  afadhali Kiranga umerudi, ebu tupe uthibitisho mzee kwa kauli zako!
   
 18. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #18
  Jan 21, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Hakuna mungu wala miungu, dini yeyote inayoamini katika supernatural powers iko based on ignorance.
   
 19. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #19
  Jan 21, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Nimetoa kauli nyingi, unataka uthibitisho gani?

  Labda wanaoamini mungu yupo waanze kunithibitishia wao kwanza kwamba mungu yupo. Judeo Christian/ personal/supernatural god of course.
   
 20. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #20
  Jan 21, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145  There is no god, and Kiranga is his prophet. --Hii inamanisha nini kwa kiswahili Ndg Kiranga?.
   
Loading...