RubbishAmeandika Professor FRANK JONATHAN PIUS.
Twende sawa mguu kwa mguu tuukate mzizi wa fitna juu ya CHADEMA kujiengua uchaguzi Serikali za Mitaa.
Ebu tutafakari swali moja kuu kiundani:
Kwanini Chadema wamejitoa/wamesusia uchaguzi wa Serikali za Mitaa? Je, ni mpango wa ndani wa chama au wamehujumiwa?
Twendeni sawa wanajukwaa hatua kwa hatua tutafakari baadhi ya mambo yafuatayo:
Wahenga walisema, ukitaka kushinda vita sharti ujue uimara pamoja na udhaifu adui yako. Ndugu zetu CHADEMA walijua wanashind ana na Serikali pamoja na Taasisi zake, kutwa kuinanga mitandaoni na kwenye vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa bila kujua kuwa SERIKALI haitaingia kwenye uchaguzi bali CCM ndio wataingia kwenye uchaguzi.
- Viongozi wa CHADEMA ndio walitakiwa kuwapa elimu viongozi waliotarajiwa kugombea uongozi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kutowaelekeza jinsi ya kujaza fomu za uchaguzi kwa usahihi/ufasaha.
- Makosa lukuki kwenye ujazaji wa fomu, kwa mfano: kwenye sehemu ya chama, mgombea anajaza CHADEMA ilihali kwa msajili wa vyama vya siasa chama hicho hakipo, kilichopo kwa msajili wa vyama ni CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).
- Viongozi wakuu wa CHADEMA wameshindwa kuwajenga viongozi wao wa ngazi za chini na kuishia kulalama kwenye mitandao ya kijamii kuhusu changamoto zinazowakabili.
- Viongozi wao wakuu wamejikita kutafuta huruma kwa ASASI za kiraia (kuomba kuungwa mkono kisiasa) badala ya kujikita kuwajenga viongozi wao wa chini kimbinu na kimkakati.
- Chuki za chini chini ndani ya CHADEMA juu ya uongozi, tuhuma za ufujaji wa fedha za chama na kung’ang’ania madaraka hali iliyosababisha kila mmoja kujiendea atakavyo chini ya mwavuli wa chama.
- Viongozi wao wa uenezi wameshindwa kuyatembelea matawi yao kwa kufanya mikutano ya ndani ili kujenga umoja na kupeana maarifa ya kimkakati ili kuukabili uchaguzi bali jukumu hili walimwachia MBOWE tu.
- Viongozi wa juu wa CHADEMA kutumia nguvu nyingi kupambana na Serikali hasa kuichafua kimataifa na kujenga chuki na kuifitinisha na wananchi na kusahau kuwa mpinzani wao mkuu ni CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) na si Serikali jambo ambalo imeipa CCM uwanja mpana kufanya shughuli za kisiasa na wao kuishia kuhudhuria kesi Mahakamani.
Kifupi tunaweza kusema jamaa walikuwa wanapambana na KIVULI wasichokijua wakihisi kuwa KIVULI hicho wataenda kushindana nacho kwenye chaguzi za Serikali za Mitaa na Chaguzi zijazo.
Mwanasiasa mmoja hapa nchini aliwahi kusema kuwa “KILA ZAMA NA KITABU CHAKE”, hili ina mapana yake. Huwezi kuwa kiongozi/mwenyekiti wa chama kwa muda mrefu huku umekosa mbinu za medani za namna ya kukabiliana na changamoto za chaguzi za Serikali za mitaa na ukaendela kujiita kiongozi mkuu wa chama ambaye silaha yake kuu ni kuweka mpira kwapani na kuacha timu pinzani uwanjani bila kuhesabu gharama na hasara za viongozi walizozipata kujiandaa na uchaguzi.
Nimalizie hapa kwa leo ili niwape muda mzuri wa kuyatafakari haya.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.