Mgonjwa kutoa sadaka; Mchungaji yupo sahihi?

Mimi sijazama sana kwenye biblia na neno la Mungu.
Nina jirani yangu hapa mdogo wake anaumwa masuala ya uzazi na vidonda vya tumbo. Ana hali ngumu sana kiafya na safari za Bugando haziishi. Pamoja na madaktari Dada jirani amekuwa na option ya kwenda mchungaji kuombewa na kukabidhi swala lake kwa Mungu amponye.

Watu hawa nawaonea huruma sana kwa sababu hawana bima na matibabu ni ghali.

Sasa mchungaji amewashauri wamtolee sadaka Mungu ili awaponye. Amesema ni sadaka ya nathiri wamtolee sana Bwana na wamuombe awaponye. Mchungaji amewasihi wasisite kumtolea Bwana kama wafanyavyo hospitali.

Hii imekaaje wakuu. Maana hawa ndugu wanapambana kupata fedha ya matibabu halafu tena sadaka?!

Tujadili bila kashfa wala matusi. Ni kwa hoja tu
Sadaka ni shukrani kwa Mungu. Kwa hakika hata huyo mgonjwa ana jambo la kumshukuru Mungu. Lakini sio alazimishwe eti toa sadaka ili upone. Hucho kitu hakipo. Unamshukuru Mungu kwa aliyokutendea sio kwa kuomba akutendee jambo fulani. Au kulinganisha sadaka na kutoa gharama hospitali kwa kifupi huko ni kutomjua Mungu kabisa kabisa. Kama ni Mchungaji kweli anamwambia mgonjwa atoe sadaka kwa vile hata hospitali analipa gharama, huyo mchungaji ni wa kukwepwa kabisa.
 
Mimi sijazama sana kwenye biblia na neno la Mungu.
Nina jirani yangu hapa mdogo wake anaumwa masuala ya uzazi na vidonda vya tumbo. Ana hali ngumu sana kiafya na safari za Bugando haziishi. Pamoja na madaktari Dada jirani amekuwa na option ya kwenda mchungaji kuombewa na kukabidhi swala lake kwa Mungu amponye.

Watu hawa nawaonea huruma sana kwa sababu hawana bima na matibabu ni ghali.

Sasa mchungaji amewashauri wamtolee sadaka Mungu ili awaponye. Amesema ni sadaka ya nathiri wamtolee sana Bwana na wamuombe awaponye. Mchungaji amewasihi wasisite kumtolea Bwana kama wafanyavyo hospitali.

Hii imekaaje wakuu. Maana hawa ndugu wanapambana kupata fedha ya matibabu halafu tena sadaka?!

Tujadili bila kashfa wala matusi. Ni kwa hoja tu
Mwambie aende kanisan la wasabato Kama ikimpendeza amtafute pastor mbanga
 
sawa maombi mazuri yanasindikizwa na sadaka,ila mtu atoe kile ambacho ameguswa nacho,unaweza sindikiza maombi yako kwa elfu hata mbili na yakapokelewa
jamani nyie ugonjwa usikie kwa mwenzio,ukiumwa alafu usiwe na akili ya kupambanua jema na baya utapigwa sana
sitaki kukumbuka yaliyonipata
 
Yeye mchungaji akitaka gari wahumini mnachanga. Ila muhumini akitaka gari unaambiwa piga maombi.

Juzi nimeona twiti ya mtu kapost kumshukuru Mungu kwa kutoka salama katika ajali ya gari na kila mtu akasifia na kushukuru. Baada ya siku chache kasafariki sasa maombi na shukrani havikua na kweli au msaada
 
Yule mjamaa amekufa? Niliona ile post anashukuru
 
Kwa kweli,mamkubwa wangu aliumwa vichomi alikwenda kwa mganga...mganga akamwambia kunywa mkojo wako utapona...akakojoa kwenye kopo akanywa...nadhani imani ndo ilimponya
Alikunywa mkojo kwa maelekezo habari ya imani usiseme
 
Mganga namuona na kumka
Mkuu swala la imani lazima liambatane na sadaka. Bila sadaka na mambo mengine utachelewa sana.
Nakupatia mfano mdogo tu. Kwa shetani yan mganga ukiwa unaumwa waweza ambiwa mpeleke kuku mqwkundu au mweupe wa dawa. Kwa gharama ya haraka haraka ni tshs 10 000 kuku mmoja. Na kweli ukipeleka shida yako inaisha ila ukisema huna basi shida yako inabaki pale pale.
Swala la sadaka liko hivi, hakuna kitu kikubwa kama funga na sadaka kiimani. Tatizo la watu wengi tunamtolea Mungu kidogo sana ilihali sehemu nyingine tunapeleka kikubwa. Kwa mganga umepeleka kuku kwa Mungu si ndo ungepaswa upeleke mbuzi kabisaaa? Lakini kwa Mungu tunapeleka buku. Kwa mfumo huu tunajikwamisha sana katika maisha yetu. Sadaka inanguvu ya ajabu kama umesimama kiimani na ukatimiza yale yakupasayo.

Funga+maombi+sadaka+shukrani=miujiza mikuu juu ya mwombaji.
Tusimtolee Mungu chenchi na tutoe kwa mioyo yetu na si kwa kushurutishwa na mtu.
Mganga namuona na kumkabidhi chake, Mungu anayetaka sadaka kubwa anapatikana wapi?
 
Ungefuatilia kabisa tujue Mchungaji anasukuma Ndinga gani ili Msomaji apate picha kamili.

Kuhusu Mchungaji kudai sadaka kama ni sawa, Yes ni sawa maana sina Watu mnajipeleka wenyewe? sasa kumbe Mtu tayari upo kwenye matibabu Hospitali unafuata tena tiba kwa Mchungaji...ina maana huiamini tiba ya Hospitali?.
 
Mimi sijazama sana kwenye biblia na neno la Mungu.
Nina jirani yangu hapa mdogo wake anaumwa masuala ya uzazi na vidonda vya tumbo. Ana hali ngumu sana kiafya na safari za Bugando haziishi. Pamoja na madaktari Dada jirani amekuwa na option ya kwenda mchungaji kuombewa na kukabidhi swala lake kwa Mungu amponye.

Watu hawa nawaonea huruma sana kwa sababu hawana bima na matibabu ni ghali.

Sasa mchungaji amewashauri wamtolee sadaka Mungu ili awaponye. Amesema ni sadaka ya nathiri wamtolee sana Bwana na wamuombe awaponye. Mchungaji amewasihi wasisite kumtolea Bwana kama wafanyavyo hospitali.

Hii imekaaje wakuu. Maana hawa ndugu wanapambana kupata fedha ya matibabu halafu tena sadaka?!

Tujadili bila kashfa wala matusi. Ni kwa hoja tu
Hakuna Sala/Spiritual power inapokelewa bila kafara.
Toa kafara(sadaka) ili kupokea Uponyaji.
Sadaka kufunga na kusaidia Maskini ni sehemu ya kupokea spiritual power
 
Mganga namuona na kumka
Mganga namuona na kumkabidhi chake, Mungu anayetaka sadaka kubwa anapatikana wapi?
Iman mkuu kama unawezana na mganga unawnda kwake mnamalizana. Dunia inamachaguzi meng
 
Back
Top Bottom