Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 58
Ninataka niamini kuwa ni kweli kuwa CHADEMA kuna mgongano kuhusu uteuzi wa zitto kwenye kamati/tume/jinalolote ya JK ya madini. Kama hizi habari ni kweli, basi hii ni dalili nzuri sasa kuwa watanzania wamegundua kuwa kabla ya kukubali au kupitisha jambo lolote kubwa na lenye kugusa maslahi ya watu wengi nchini ni lazima kuwepo na mjadala na mchanganuo wa kutosha.
Ninashawishika pia kusema kuwa kama chama tawala, bunge, halmashauri zetu zingefanya maamuzi kwa msingi wa kuruhusu mawazo ya wengi yasikilizwe ikiwemo wale wanaopinga kabla ya kupitisha vitu haraka haraka Tanzania ingekuwa bila IPTL, Kiwira na maovu mengi yaliyopitishwa na watu wachache sana kwa manufaa yao binafsi.
Hii ni nafasi kwenu viongozi wa CHADEMA kuonyesha nchi hii kuwa mko tayari kutunza demokrasia na kuruhusu utofauti wa nia na mawazo ndani na nje kwa nia ya kujenga kitu kikubwa na chenye manufaa kwa watanzania wa leo na wajukuu zao.
Fanyeni mjadala wazi na kila kitu kiweke pamoja ili mwishoni ikiamuliwa nini kifanyike kunusuru taifa na mafisadi wanaouza nchi, kila mtanzania azidi kujenga imani kwenu na kwa watanzania wote ndani na nje ya serikali waliochoshwa na uozo unaondelea.
Zitto ameshafanya uamuzi wa kuingia katika kamati/? hii na mie naona kuwa ni vyema aingie huko kama hivyo ndivyo anashawishika kufanya. Zitto ameahidi kuwa ataendeleza kulinda maslahi ta Tz kwa hiyo ni vyema apewe nafasi kufanya na kuthibitisha hilo. OK Zitto, kafanye mambo huko ila ukisalimu amri afadhali uombe kazi huko ikulu or something. Kwa sasa GOOD LUCK - NENDA KAFANYE KAZI