Mgongano: Serikali Vs. Mwanahalisi - Mipaka ya Maoni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgongano: Serikali Vs. Mwanahalisi - Mipaka ya Maoni?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 9, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,818
  Trophy Points: 280
  Serikali yaiwakia MwanaHalisi
  Maulid Ahmed
  Daily News; Wednesday,October 08, 2008 @20:03

  Serikali imelitaka gazeti la MwanaHalisi kutoa sababu za kujitetea ili lisichukuliwe hatua kutokana na habari iliyoichapisha jana kuwa kuna njama za kumng’oa Rais Jakaya Kikwete asiweze kugombea urais mwaka 2010.

  Msemaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Jacob Tesha katika taarifa yake alisema kuwa agizo hilo limo katika barua iliyotumwa kwa Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo, Saed Kubenea ambapo ametakiwa awasilishe maelezo ya kina wizarani hapo kuhusu tuhuma hizo kabla ya kesho jioni.

  Katika gazeti hilo la kila wiki toleo la 118, kumeandikwa habari kuwa kuna kundi la mafisadi wakiongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa na Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz wamejipanga kuhakikisha Rais Kikwete asigombee urais mwaka 2010.

  Katika habari hiyo, mtoto wa Rais Ridhiwani anadaiwa kutumiwa na mafisadi hao katika njama hizo za kumng’oa baba yake pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao wamekuwa wakishiriki kuwaweka wafuasi wao watakaosaidia kufanikisha njama hizo.

  Tesha alisema kuwa kutokana na habari hiyo, serikali imesema kuwa ni ya uchochezi inayolenga kumgombanisha Rais Kikwete na viongozi wengine waandamizi wa CCM na kuleta mtafaruku katika familia yake.

  Taarifa hiyo ya serikali iliwaonya baadhi ya waandishi wa habari ambao kwa makusudi wamekuwa wakiandika habari zisizo sahihi na zenye kuchochea chuki miongoni mwa jamii na kusisitiza kuwa uhuru wa habari unaishia pale unapoingilia uhuru wa mtu mwingine.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa gazeti hilo, Saed Kubenea alilieleza gazeti hili kuwa hajapokea taarifa hiyo ya serikali hadi jana jioni na siku nzima ya jana alikuwa ofisini.

  Alisisitiza kuwa habari iliyoandikwa katika gazeti lake si mpya na imeshawahi kuandikwa na vyombo vingine vya habari lakini aliongezea kuwa gazeti lake limeiandika kwa undani zaidi.Hata hivyo alisema “taarifa hiyo ya serikali ikija tutaipokea, tutaijadili na kuitafakari kisha tutawajibu”.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,818
  Trophy Points: 280
  Hi sirikali kweli ni mufilisi. Hawajui Watanzania wengi tungefurahia ang'olewe leo badala ya kusubiri 2010 maana kuna ushahidi wa kutosha kwamba ni mwoga, ameweka mbele maslahi ya mafisadi badala ya Watanzania, ameweka mbele maslahi ya wageni 'wachukuaji' badala ya Watanzania (mikataba ya kuchimba dhahabu), hana ujasiri wa kuiongoza nchi na pia hana uwezo wowote wa kuiongoza nchi.
   
 3. Kipunguni

  Kipunguni Senior Member

  #3
  Oct 9, 2008
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nilishawahi kusema hapa kwamba TZ hivi sasa kuna serikali mbili; inayoongozwa na mafisadi (ambayo ndiyo ina nguvu zaidi) na ile inayoongozwa na Muungwana ... how right I was.
   
 4. Mzee wa Gumzo

  Mzee wa Gumzo Senior Member

  #4
  Oct 9, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli Kipunguni,
  Hakuna sababu yoyote ya kuwabana Mwanahalisi kuhusu taarifa hiyo, kila anayefualilia mambo atakubali kuwa kwa hali ilivyo CCM kuna maadui wengi kuliko marafiki.Mafisadi waliozaliwa na kulelewa ndani ya mfumo wa siasa za CCM wanaiongoza serikali kwa remote control
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Ufafanuzi huu ni muhimu....
   
 6. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hii ni Tanzania tu ndio mara tutasikia habari za kichochezi nchi nyingine watu wanaandika hoja na mawazo yao sio serikali wala rais au mawaziri utawakuta wanruka ruka eti kesi, mara ajieleze. Freedom of speech na freedom of expression ambazo serikali yetu inavifumbia macho sana.
   
 7. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Saafi sana, hapo ni kumkabidhi tu rais notes za mkutano wa siri wa Morogoro, uliofanyika chini ya Acting Chairman Nchimbi, kutokana na Lowassa kuwa US sasa hao serikali wakipewa hizo notes waseme wazi wasigeuke mabubu,

  maana kuna ambao tuna copy tayari, Ohhh I love this yaani ushirika wa wachawi bwana kweli haudumu hata siku moja..
   
 8. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Ninavyoelewa hii pia inaweza kuwa mbinu ya muungwana ya kuwaleta wanaomhujumu mbele ya umma. JK ni mjanja sana katika matumizi ya vyombo vya habari, alifanya hivyo kwenye kampeni yake, akaendelea hivyo wakati wa Richmond, na sishangai kama anafanya hivyo sasa. Hii habari nadhani JK anayo, sasa hapo Tesha katumwa achokoze ili Kubenea amwage ushahidi wote apate sababu ya kuwashughulikia. Lau kama Tesha hajatumwa (kama bado anajidhania ni press secretary wa JK's ex rival Sumaye), basi amejiingiza mwenyewe kwenye kamtego, hapo mtu anaingia kingi kiulaini!
   
 9. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #9
  Oct 9, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kithuku... hisia zako hazipishani sana na za kwangu = JK anajua kucheza na vyombo vya habari. ILA.... kwanini isiwe ni mchezo wa kuigiza unaofanywa na JK mwenyewe na marafiki zake kina Lowasa ili kutafuta huruma kwa wananchi? Wananchi wakisikia story ya JK kutaka kungolewa wataona mafisadi hawampendi ndio maaana wanataka kumng'oa... hivyo watakuwa upande wake na atapita kiulani 2010...
   
 10. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #10
  Oct 9, 2008
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  wakuu hapa ni wazi kuwa ndg. Yetu kubenea ana kazi moja tu nayo ni kumfagilia mbali edward kutoka karibu na uso wa jakaya.

  Huenda huyu bwana ana baraka za jk ktk suala hili au la waislamu wa tz ambao wana dhamira ya kumuona mkuu jk aking'ara ktk 10 yrs yake ikulu huku wakiamini udhaifu uliojitokeza umesababishwa sana na edward lowasa na kidogo rostam.

  All in all tunachohitaji ni njema yenye amani na sura ya kuendelea kwa kweli.
   
 11. G

  Gulwa JF-Expert Member

  #11
  Oct 9, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 2,783
  Likes Received: 1,961
  Trophy Points: 280
  Mimi naanza kumtilia shaka Kubenea kwani mafisadi hawawezi kupanga kumg'oa fisadi mwenzao, JMK hakuwahi kukana hata mala moja tuhuma za ufisadi zinazomkabili. Hii ni njia anyotumia kujionyesha kwa uma kwamba yeye si fisadi ndio maana mafisadi wanamchukia. Habari ya MwanaHalisi na taarifa Ya Tesha yote ni maigizo tu
   
 12. W

  WildCard JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2008
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Lowassa anaijua CCM. Hawezi hata kuota kuandaa mipango ya AINA hiyo au hata inayofanana na hiyo!
   
 13. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #13
  Oct 9, 2008
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Ningekuwa mtu wa serikali, hoja ya MwanaHalisi ingekuwa kama 'tip' kwangu ya kuifanyia kazi na siyo ku'intimidate' mwandishi au gazeti lililoandika kuhusu kumng'oa Rais Jakaya Kikwete madarakani. Ndiyo maana Watanzania wanakuwa waoga kutoa 'tip' au kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola kwa jambo lolote lile kwa kuogopa kuwa watachukuliwa hatua au kusumbuliwa bila sababu za msingi.

  Serikali ingekuwa makini, ingefuatilia jambo hilo kisirisiri. Naamini kama gazeti hilo lingetunga uongo, lingeficha jina la mwandishi. Kwa vile mwandishi aliweka jina lake, ina maana ama ana ushahidi kuwa kuna njama hizo au amepata fununu fulani ambazo ameona aziweke wazi ili vyombo husika vifuatilie. Sasa kwa kufanya hivyo amekosea? Hapo ndipo inaponishangaza! NI lini Tanzania tutaheshimu uhuru wa kupata na kutoa habari?
   
 14. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #14
  Oct 9, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Mkuu,unajua Vasco da Gama wakati mwingine namuona genius wa siasa(Nisieleweke vibaya hapa,Genius wa siasa Chafu na si safi) maanke anatka kupata ushahidi kutoka ktk vyombo vya habari.Pia anweza kutumia ajenda ya kuwasulubu mafisadi ili apate sympathy from wananchi maanke so far watanzania hawataki kumsikia Lowasa labda viongozi waandamizi alio-wapick yeye enzi akiwa PM
   
 15. Z

  Zanaki JF-Expert Member

  #15
  Oct 9, 2008
  Joined: Sep 1, 2006
  Messages: 544
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Yule kijana inawezekana nae anajiona ni Kabila mwingine sasa...maana yule nae kulikuwa na fununu kuwa alitumiwa kummaliza baba yake.Mimi kwa kweli sishangai kabisa kuwa hii story ni ya kweli.

  Sasa baba mwenyewe alimwachia mwanawe na mkewe wawe wajumbe wa NEC...si ni kujitafutia balaa huko? Matunda yake ndio hayo sasa
   
 16. Z

  Zanaki JF-Expert Member

  #16
  Oct 9, 2008
  Joined: Sep 1, 2006
  Messages: 544
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  ....ina maana basi Usalama wa Taifa wamekuwa pretty ineffective basi
   
 17. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #17
  Oct 9, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  1. Copy niliyonayo haina notes za mtoto wake kuhusika, sasa ninaamini Kubenea ana more than I have,

  2. Ze -Comedy ya kisiasa inayoendelea sasa katika serikali yetu ni lazima ifike mahali itakua na mwisho wake, sio siri tena kwamba sasa kuna makundi matatu, mawili makubwa na moja dogo, Moja la mafisadi, la pili la kutetea wanyonge, na kuna la tatu ambalo limekua liki function kwa siri sana na kwa muda mrefu sana sasa, hili linaanzia London na lina watu ambao wako very careful lakini recently limekua likijiegemea na hili la wananchi,

  3. According to the dataz, Muungwana analiunga mkono sana hili la wananchi, ingawa hapendi kuonekana hivyo mbele ya lile la mafisadi, na pia anaogopa sana kusababisha kumeguka kwa CCM, ndio maana kwenye uchaguzi wa mwisho wa NEC, ingawa Lowassa, Makamba, na Kingunge walishindwa uchaguzi wa NEC, Muungwana aliwaingiza anyways kuogopa kumeguka.

  4. Katika uchaguzi ule, Muungwana alimtoa uweka hazina Rostam bila ya kumfahamisha in advance, kilichompelekea Rostam aliyepigwa na mashangao mkubwa ndani ya kikao kumtumia ki-note Muungwana kumuuliza imekuwaje? Huku mama meghji, akihaha kwenye kiti chake, Muungwana alikisoma kile ki-note na kukitupa kwenye kikapu cha uchafu.

  5. All this yalimpelekea Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Musoma, Makongoro kuingiza hoja ndani ya NEC ya kutaka mafisadi wafukuzwe CCM tena mara moja, ilibidi Makongoro aitwe pembeni haraka sana na kundi la wananchi na kuombwa a-drop the ishu, sasa ikawa zamu ya wajumbe wa Zanzibar ambao mmoja baada ya mwingine walimtukana Muungwana, beyond anybody's belief kuhusiana na muafaka, so ugly kwamba Muungwana alihofia kifo cha muungano mle ndani, akanyamaza kimya na mwisho kuirudisha ile ishu mikononi mwa kamati ya CCM huko Zanzibar, hapa Karume alimzidi ujanja muungwana na muafaka wa Makamba. Sasa Zenji kuna hoja ya Karume kugombea term ya tatu!

  Kwa maoni yangu ni kwmaba inaelekea kuwa siku za finally ya this political Comedy zinaanza kufika mwisho, inasikitisha sana kwamba rais wetu amefikishwa mahali na mafisadi kwamba inabidi a-operate mawazo yake wka siri kwa sababu ya kuwaogopa, haya yote tunayalipia sisi wananchi kwa sababu kwa kuwa anawaogopa basi in the meantime mafisadi wana operate bila wasi wasi, tena as they wish.

  Sasa hivi the showdown ipo kwenye uchaguzi wa UWT, Sophia ni agent wa mafisadi, lakini the dataz ni kwamba Muungwana hawataki wote kuanzia Sophia mpaka Mama Janeti, in a private anasema angependa Mama Kilango agombee huko maana kwa maneno yake mwenyewe ".. yule ni kiboko atawasafisha huko kuanzia wafagiaji mpaka viongozi wabovu huko.." lakini mama Kilango amekataa kabisa kujiingiza huko na hivi majuzi tu ameshusha baiskeli za kisasa 30 kutoka US, kwa ajili ya walemavu wa jimbo lake jambo ambalo limewafanya kwa mara ya kwanza baadhi ya walemavu wa jimbo lake kuweza kuzunguka kijijini mbali na nyumba zao that is politically plus!

  Muungwana sasa yupo stressed out, kwa wale mliomuona recently face to face mtakubaliana nami on this, urais umekua adhabu sasa lakini aliyataka mwenyewe, sasa behind hii Mwanahalisi's ishu ni the best opportunity kwa Muungwana ku-make up his mind, anataka nini hasa maana sasa sio siri tena kuhusu uwezekano mkubwa CCM kumeguka, na Muungano pia kufika mwisho,

  Sasa either Muungwana a-act na kutuokoa wananchi na hawa mafisadi, au akubali ku-undermined nao huku wakiliua taifa na ufisadi wao ambao unaendeela kwa kasi kubwa sana, kwa sababu according to the dataz accounts zao zote mafisadi zimezuiwa na serikali wasitoe hela kwa muda sasa, lakini wana uhuru wa kuingiza na wamekua wakiingiza kwa kasi kubwa sana bila kuogopa,

  Sasa Muungwana atafanya nini? Ni kusubiri tuone.

  Ahsante Wakuu.
   
 18. I

  Iga Senior Member

  #18
  Oct 9, 2008
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  HAPA hakuna siri yoyote wala uhaini wowote wala uchochezi wote maana vigezo vya wenye macho na masiko na ambao hawapewi bakshishi ya makombo ya CCM na serikali yake ni kwamba kiongozi wa sasa kashindwa kazi.

  Kweli ana jamali, anatoka sana nje na Bush anampenda sana na Marekani wanamtumia vilivyo na yeye ana huruma sana hata na wale wanaosababisha umasikini na vifo vya Watanzania wangali makinda lakini KUPENDA KUONGOZA KATU SIO KUWEZA KUONGOZA.

  Tanzania kama Afrika [na pengine dunia nzima] bado tuko mashakani kwani viongozi bora na safi wameadimika MNOOOOO! Masikini hatuna kiongozi na kina Ndimala na Kubenea hilo wanalijua fika. Na kila Mtanzania labda kwa wana CCM tu hawajui hili.

  Mheshimiwa kama kwa kweli hamjui hata kutumia senti za wananchi kwa hekima, uchungu na busara ndio tunashindwa kuwaelewa kabisa. Iweje utuwekee wizara ambazo ukishuka chini hazina uhusiano wowote wa kutuongezea uzalishaji mali wala sio tija wala sio demokrasia wala sio uhuru zaidi wala sio kuondokana na umasikini kwa haraka zaidi.

  Ama kweli sasa tunaelekea kwenye KASI MPYA YA KUBANA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI; NGUVU MPYA YA KUUKANDAMIZA NA KUUBOMOA UPINZANI NA ARI MPYA YA KUIBA KILA kilichoko hazina, kwenye ardhi zetu, kwenye misitu yetu ili kuneemesha CCM na mabwana zake na mamluki wao. Mola hakika kwa mabaya yenu lazima siku sio siku atawapatilizia mbali.

  Na laiti Wapinzani wangelikuwa na akili wakajiunga leo 2008 na kuanza kuhamasiha wananchi KUJUA KUWA UPINZANI ni kitu chema na sio jambo baya basi CCM 2010 itachechemea na inawezekana ikajikwaa na angalau tukawa na MSETO wa MUUNGANO hata kama kina mdwebedo Unguja hawautaki wao lakin ni huko kwao sio hapa!
   
 19. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #19
  Oct 9, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kama wanashida na wanadhani hakutenda sawa si waende mahakamani ili siri zote zitoke nje?
  Hii habari ya kutishana ya nini? Mkuchika bado anaota enzi za kutishana hapa?
  Shauri zake asubiri za kwake zikimwagwa hapo atakoma ubishi.
   
 20. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #20
  Oct 9, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu Field Marshal, Muungwana anajitakia mwenyewe matatizo haya kwa sababu kama angekuwa na nia ya kujitanzua kutoka kwa mafisadi, alikuwa na nafasi nyingi za kufanya hivyo. Yeye ni mwanajeshi na anajua zaidi mbinu za kumshitukiza adui; alizitumia alipomwondoa RA uwekahazina na alipomtosa EL alipojiuzulu.
  Moja ya mbinu ambazo angeweza kuachana na mafisadi ni kuwashitukiza kwa kuwamwaga wakati yeye akiwa ameshajiandaa na serikali yake; akumbuke kuwa alishatuambia kuwa urais wake hauna ubia, bado wananchi wanaamini hivyo.
  Yeye ndiye rais, ana kila nyenzo anayohitaji kujilinda yeye na serikali yake, kwa nini aliruhusu mafisadi wamshike kiasi kwamba hivi sasa ni kana kwamba anaoperate kutoka mafichoni?
   
Loading...