Hivi ni mimi peke yangu au kuna wengine wanaodhani kwamba wanafunzi nao kuandamana ni ujinga tu...
Taarifa kutoka mikoa kadhaa zinaonyesha kuwa polisi waliwakamata viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), ngazi za mikoa na wilaya, huku baadhi yao wakifikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuchochea mgomo ambao Serikali tayari imesema kuwa ni haramu. Kukamatwa kwa viongozi hao kulikwenda sambamba na tamko la baadhi ya wakuu wa mikoa na baadhi ya makamanda wa polisi ambao walionya kwamba wangewachukulia hatua za kisheria walimu ambao wangeendelea kugoma. Wakati Serikali ikichukua hatua hiyo, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), limeitaka Serikali kuacha kujitetea katika suala hilo na kulipa madai ya wanataaluma hao wa sekta ya elimu. Mkoani Dar es Salaam, FFU walitawanya maandamano ya wanafunzi katika eneo la Kunduchi, Kinondoni na kuwakamata baadhi yao. Waliandamana kwa madai ya kudai haki yao ya kufundishwa. Kundi kubwa la wanafunzi waliodaiwa kwamba walikuwa wakitoka katika shule mbalimbali za Manispaa ya Kinondoni waliandamana katika maeneo ya Mbezi Machimbo, huku askari wa FFU wakijaribu kuwazuia na kuwaelekeza kurudi nyumbani. NOTE: watoto ni haki yao kuendelezwa na haki huwa haiombwi inadaiwa . ni nani amesimama kuwatetea? wenyewe wameamua kujitetea |