Mchengerwa: Wanafunzi wote waanze masomo Januari

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa kutekeleza maagizo mbalimbali ili mchakato wa kuwapokea Wanafunzi wapya Shule za awali, msingi na sekondari uende kwa ufanisi kuanzia Januari 06,2024.

Mchengerwa ametoa agizo hilo leo December 30, 2023 wakati akiongea na Wakuu wa Mikoa katika kikao kazi kilichofanyika kwa njia ya mtandao ambapo Viongozi hao walieleza hatua zilizofikiwa katika miradi ya elimu na walivyojipanga kuwapokea Wanafunzi wapya.

Wakuu wa Mikoa hao kwa nyakati tofauti wakiwasilisha maelezo yao kuhusu utekelezaji wa miradi ya elimu wamemuhakikishia Waziri Mchengerwa kuwa hakuna Mwanafunzi atakayekaa chini au kukosa darasa na kuwa wote walioandikishwa na kufaulu wataanza masomo kwa wakati mmoja.

Aidha Waziri Mchengerwa ameagiza kuwa Wakuu wa Mikoa ambao bado hawajakamilisha ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya Elimu kuhakikisha wanakamilisha baadhi ya majengo ya vyumba vya madarasa ifikapo January 15 kama walivyoahidi wakati wanatoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya elimu katika mikoa yao.

Maagizo mengine aliyoyatoa ni pamoja na Shule zote mpya zinazojengwa zisajiliwe hususan ni zile za wasichana na baada ya mchakato huo kukamilika zianze kazi mara moja ya kupokea wanafunzi. Amesema baadhi ya mikoa ukiwamo wa Pwani wameanza mchakato huo.
 
Unakazania ukamilisuaji wa madarasa mapya kuonyesha wanafunzi watakua wengi, ila idadi ya walimu huongezi kwa wakati, hao wanafunzi, watadomaje effectively?

Acheni siasa.
 
Back
Top Bottom