Mgomo wa walimu wanukia, na wafanyakazi wa migodini kuacha kazi

Status
Not open for further replies.
naona mambo yanzidi kwenda mrama kila sehemu.. Ule mgomo wa walimu uliokuwa ukisuasua sasa ni dhahiri shairi umeibuka kwa nguvu.. Baada ya kutangaza kuanza mgomo wiki chache zilizopita.. Swala hilo lilipelekwa katika tume ya usuluishi ili kuumaliza mgogoro huo (madai yakiwa ni kuboresha mishahara yao, kuboresha mazingira ya kazi pamoja na posho), leo jibu limetoka kuwa usuluhishi umeshindikana baina ya walimu na serikali na hivyo basi tume ya usuruhishi imetoa cheti cha mgogoro huo kushindwa... Na hivyo basi walimu woote wanapaswa kupiga kura ya kuingia rasmi katika mgogoro na serikali kati ya tarehe 25-27/07 saa 3 kamili asubuhi... Ili jibu lipatikane

source taarifa ya habari ya itv.. saa 2.00 usiku tarehe 25/07/2012

wakati huhuo wawakilishi wa migodi mikubwa leo wametoa tamko la kutokukubaliana na sheria mpya iliyopitishwa ya nssf ya kuzui wanachama wake kujitoa, pamoja na kutopata mafao yao mpaka umri wa kustaafu (55-60) utakapowadia....pia wamewaandikia barua waajiri wao kuwa wanaacha kazi
muda si mrefu

naona mambo yanazidi kuwa magumu.... Karibuni tuyajadili haya kabla wakina mzee wa gombe na mzee wa kudadadaaaakeeee... Hawajaishauri serikali ya dhaifu kukimbilia mahakamani.....

kupitia waraka wa nyongeza ya mshahara, nimeona kwa mshahara umeongezwa just 38,000s. aisee nawaunga mkono, kabisa. ni chini ya silimia 9 ya mwaka jana yanyongeza
 
naona mambo yanzidi kwenda mrama kila sehemu.. Ule mgomo wa walimu uliokuwa ukisuasua sasa ni dhahiri shairi umeibuka kwa nguvu.. Baada ya kutangaza kuanza mgomo wiki chache zilizopita.. Swala hilo lilipelekwa katika tume ya usuluishi ili kuumaliza mgogoro huo (madai yakiwa ni kuboresha mishahara yao, kuboresha mazingira ya kazi pamoja na posho), leo jibu limetoka kuwa usuluhishi umeshindikana baina ya walimu na serikali na hivyo basi tume ya usuruhishi imetoa cheti cha mgogoro huo kushindwa... Na hivyo basi walimu woote wanapaswa kupiga kura ya kuingia rasmi katika mgogoro na serikali kati ya tarehe 25-27/07 saa 3 kamili asubuhi... Ili jibu lipatikane

source taarifa ya habari ya itv.. saa 2.00 usiku tarehe 25/07/2012

wakati huhuo wawakilishi wa migodi mikubwa leo wametoa tamko la kutokukubaliana na sheria mpya iliyopitishwa ya nssf ya kuzui wanachama wake kujitoa, pamoja na kutopata mafao yao mpaka umri wa kustaafu (55-60) utakapowadia....pia wamewaandikia barua waajiri wao kuwa wanaacha kazi
muda si mrefu

naona mambo yanazidi kuwa magumu.... Karibuni tuyajadili haya kabla wakina mzee wa gombe na mzee wa kudadadaaaakeeee... Hawajaishauri serikali ya dhaifu kukimbilia mahakamani.....
mimi nashauri mgomo wa WALIMU uwe reported hapa kuwa ulishaanza na unaendelea lakini vinginevyo tumezoea story kama hizi!!wa migodini hao nakubali wanaweza kuangusha kunji la nguvu lakin walimu????????????????????
 
Bwana mushi kaambiwa sisi ma miner tumesha chizi kama mlikuwa hamtujui sasa mtatujua sababu mmetugusa pabaya.
Pia kaambiwa ampelekee salamu mkurugenzi mkuu wa SSRA maamuzi wanayoyafanya yeye na mume wake asiyalete kwenye fedha za watu.sijui kama Bwana mushi atakubali kurudi hapa GGM.

mkuu mbna hapa kwetu kakola sijamwna hyo bwna mushi?kwa hili serikali imechemsha.
 
Napenda niwashauri walimu wenzangu tugome na tusifanye kazi ya sensa,serikali itatuangukia na kusikiliza shida zetu.Jana imetangazwa kwamba majadiliano yameshindikana na kuamua mwl aendelee kuishi kwa shida.
 
Unapoteza muda wako bure, hawa walimu tangu mwezi wa 5 wanapiga hadithi ya mgomo mpaka leo hamna kitu.
Walimu na kuhusu kugoma itabaki story.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
mkuu mbna hapa kwetu kakola sijamwna hyo bwna mushi?kwa hili serikali imechemsha.

mkuu hii serikali naona imetuchoka, kila kitu wanachoamua ni kwa maslahi yao tu... ninawasisiwasi kama hili swala la nssf linawagusa mawaziri na wabunge.... coz lisingepita fasta hivi.... mi nadhani wakati umefika wa kusema hapana ... naona kila siku afadhali ya jana.... sijui pia wakina mwigulu kwa haya yanayotokea wayesema ni chadema pia??
 
mimi nashauri mgomo wa WALIMU uwe reported hapa kuwa ulishaanza na unaendelea lakini vinginevyo tumezoea story kama hizi!!wa migodini hao nakubali wanaweza kuangusha kunji la nguvu lakin

walimu????????????????????

mkuu huu mgomo ulishaanza zamani sana... ni silenti but serious sana...... tangu 2005 mambo ni hovyo... unaona madogo wanaingia form 1 wamefaulu hawajui kusoma na kuandika, zaidi ya 60% wanaomaliza form four ni dv four na ziro dogo wa form threee unamuuliza 1-2 anakwambia haiwezekani hiyo ticha......yaaani nibalaaa tupu... lakini hawa ndio watakaoleta mapinduzi coz ni watoto wa maskini kwasababu MASKINI HAFILISIKI
 
Mgomo wa walimu umenukia mda mrefu sana mpaka umeacha kunukia sasa unanuka.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Mimi kama mfanyakazi naunga mkono mgomo wa kugomea Kiunua mgongo changu nilipwe nikiwa na miaka 55 au 60. Huo ni uwiz wa Mchana.
 
Mimi kama mfanyakazi naunga mkono mgomo wa kugomea Kiunua mgongo changu nilipwe nikiwa na miaka 55 au 60. Huo ni uwiz wa Mchana.

Tunaposema Chadema ni waasisi wa migomo mnakataa; kama hamkubaliani na sheria ya kiinua mgongo zipo njia sahihi kwa nini kila kitu iwe ni migomo tu hamna njia nyingine sahihi ya kutafuta haki?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
mkuu huu mgomo ulishaanza zamani sana... ni silenti but serious sana...... tangu 2005 mambo ni hovyo... unaona madogo wanaingia form 1 wamefaulu hawajui kusoma na kuandika, zaidi ya 60% wanaomaliza form four ni dv four na ziro dogo wa form threee unamuuliza 1-2 anakwambia haiwezekani hiyo ticha......yaaani nibalaaa tupu... lakini hawa ndio watakaoleta mapinduzi coz ni watoto wa maskini kwasababu MASKINI HAFILISIKI
huo sasa ndio ujinga nisioupenda sasa hawa madogo unawaumiza unaharibu maisha yao kimya kimya kama ni kugoma wagome hadharani shule zifungwe mambo yakiwa sawa walimu na wanafuzi warudi elimu bora itolewe na madogo wafaulu wawe na maisha bora!hii inafnana na madaktari sasa wagoma kimya kimya watu wanakufa watu wanateseka afadhali wagome wazi hospital zifungwe ili wananchi tuiwajibishe serikali kwa kushindwa kutupa huduma za afya!!
 
Hata serikali wakienda mahakamani kuomba mahakama kusitisha mgomo wa walimu, hatukubali. Tutaigomea hata mahakama haki ya Mungu tena.
 
1.) Mgomo wa walimu ni sawa na wasirudi nyuma,2.) Kuhusu mafao:Falsafa nzima ya mzunguko wa maisha inasema hivi: JANA NI HISTORIA, KESHO NI MAJALIWA, LEO NI ZAWADI. Sasa iweje mtu uishi kwa kutegemea KESHO? ili hali maisha ni sasa(leo),? je nani kaiona KESHO?
 
By lwayo.nawaomba walimu popote pale walipo muungane ili muweze kupigania haki zenu bila kufanya hivyo mtaendelea kunyanyaswa.
 
Mkuu kama mnaandamana kwa maslahi yenu fanyeni, lakini kama comment zetu zinawachochea basi jueni sisi pia tunataka hizo kazi zenu,sasa ngoja mtimuliwe kazi ndio mtajua kama sisi tuko nanyinyi

Mkuu tunaandamana kudai haki yetu na kamwe usiwe na mawazo ya kupata kazi yangu hata kama nimeondoka hapa mgodini. kazi za migodini imesomewa na kamwe kama wewe ni afisa kilimo hutakuwa geolgist au Mining Eng. Hata hiyo kazi ya operator si ya kuajiri leo na kesho ukatinga. Waulize drillers wamejifunza kwa muda gani. Usifananishe kazi za kuunganisha za serikali zetu kuwa ndizo zipo huku..hata ukipewa kumonitor magari yapi na lini yaingie service tu utatoroka kazi mwenyewe hivyo tunaposema tunagoma si sisi tu wa migodini bali wate wanaoguswa na hii sheria tunahitaji kuwa kitu kimoja. Haya mawazo ya fulani agome ili afukuzwe niingie hayatakusaidia.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom