Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

Nipo wilayani Misenyi mkoani Kagera. Sule ya msingi Kashekya.
Hapa walimu wamekuja shule ila hawafundishi.
Nimemuuliza Mwalimu mmoja wa hapa amesema wameamua kuja sio kufundisha bali ili wawe karibu waweze kupeana updates kwa urahisi.
 
Inasikitisha mno serikali kuwatelekeza waliotufikisha hapa. Serikali imeshindwaje kutumia akili za mbayuwayu hapa?
 
Upande wa Tunduma vurugu za wanafunzi zimetulia sasa (au niseme zimetulizwa); Hayo maandamano ya wanafunzi yalipelekea boarder ya upande wa Tunduma kusimamisha shuguli zake (sio kufungwa) kwa hofu ya usalama wa mali za wasafiri wanaotumia huo mpaka hasa magari ambayo huwa kwa wingi maeneo hayo.

Hata hivo so far shughuli zinaendelea kama kawaida kwa sasa katika offisi hizo za Migration hapo mpakani.
 
Hii kitu inakumbusha Soweto School boycott ndani ya Apatheid South Africa 1976. Maishani you can do nothing,or do something or do the right thing. Walimu hongera for doing the right thing.
 
Walimu Oyeeeeee,Walimu juuuuuu juu juu Kabisaaaa...Huku Swanga at least penyewe kimenuka.Shule za msingi ndo wanaongoza kutofika kabisa.Baadhi za Sekondari Makajanja wapo wapo wawili watatu,na halmashaur 4m2 ndo wanaanza mock.very gud
 
Taarifa tofauti niliyoipata sasa hivi ni kwamba Lushoto kuna kikosi kabisa kinapita mashuleni na Mwalimu anaekutwa shuleni anakula kibano
 
Nakapanya Mtazamo wako ni finyu sana kwa sababu hao walala hoi unaosema ndo wanategemea watoto wao wasome wawe waalimu na madaktari . Migomo hii ni alert kwa serikali kuboresha maslahi ya watoto wa walala hoi ambao wengi hugeuka kuwa asset au msaada kwa wazazi wao. Kama Maslahi yao hayataboreshwa watapata wapi kipato cha kuwasaidia wazazi wao ambao ni wakulima? fungua akili mkuu!!
 
Last edited by a moderator:
Watanzania waelewe kuwa kuwa Serikali haiwajali Watanzania hasa katika huduma za afya na elimu na ndiyo maana wanawalipa mishahara midogo. Watawala wameona huduma hizi siyo muhimu kwa Watanzania.
 
Magu nako kimenuka mbaya,shule za mjini nazo zimefungwa zikiwemo,nyalikungu,itumbili,uzalendo umetawala na wajinga wachache waliofoji vyeti ndio wapo kazini.
 
Wilayani Mbozi, katika maeneo ya VWAWA na Tunduma nako wanafunzi wako barabarani, hali ni mbaya zaidi Tunduma, kuna gari tayari imechomwa moto na hali inaweza uwa mbaya zaidi soon.
 
Aliyeripoti kuhusu Mgomo wa Walimu Same hakufanya Utafiti. Shule zote za Mjini walimu Wapo kazini. Afisa Elimu kazipitia na timu yake leo asubuhi.
 
Back
Top Bottom