Mgomo wa wahadhiri vyuo vikuu wanukia

Mgomo wa wahadhiri vyuo vikuu wanukia

Ni kufwatia kukamatwa na kupewa kesi ya ugaidi kwa wenzao wa UDOM
Vikao vya chama cha wahadhiri vyuo vikuu vinaendelea ili kuona namna ya kuchukua hatua stahiki za haraka
Eitha kutokana na hali ilivyo usiri umetawala na huenda wakatoka na azimio moja tu la mgomo.
Nani huyu anayetaka kuiangusha Tanganyika kwa kila eneo ? Hakuna aliyebaki na heshima zake aseme Stop. Stop. Stop.

Malechela ?, Msekwa ? Mangula ,? Kinana ? Sijui, sielewi.
 
Vyuo vipi unaongelea Boss, ni hivi vilivyong'olewa meno na kuwa " toothless au? Unazungumzia vyuo hivi ambavyo vimeshindwa ku- claim hata ile " university autonomy" yake?.

Ni hivi ambavyo maprofesa wake wanawafundisha wanafunzi na kuwatunuku degree kisha wakipewa viti vyeusi na vipaza sauti na wanasiasa wanasema wasomi wake hawaajiriki?...

Ni hivi Vyuo ambavyo miaka ya 2015 walifanya tafiti wakabaini kuwa wasomi wengi pamoja na kuwa na stadi ngumu "hard skills" kama vyeti na matokeo mazuri kitaaluma " good G.P.A hawana stadi laini " soft skills" ambazo ni muhimu zaidi kazini?

Teh!..ni hivi vilivyotunga Sheria mbovu ya kuwabana wahadhiri wake kufikia ngazi za U-profesa halafu vinawastafisha mapema na kuanza kuwatafuta tena kama "emeritus professors"?

Ni hivi ambavyo wasilisho la andiko la Profesa "Inaugural lectures" hufanyika kama masika ya jangwani?. Aiseee.....au..ni...

Ni vyuo hivi ambavyo maprofesa wake wakipewa ulaji wa kisiasa wanashukuru na kusema "wametoka mavumbini" Profesa anapaita Chuo mavumbini kweli?....tena Chuo kikongwe na kikubwa Afrika ,Bigiii mbona sikuelewi unazungumzia vyuo vipi?

Ni hivi ambavyo umoja wa wahadhiri unachukuliwa kama jukwaa la harakati za kisiasa na kuchukiwa, kiasi cha kutoa matamko yanayopungana na utawala?.. Unazungumzia Vyuo vipi Bigii?....

Hivi ambavyo wahadhiri wake badala ya kujitahidi kuwa sehemu ya kusukuma mabadiliko ya kijamii, kisiasa na kiuchumi wanakimbizana kusifia kila kitu ili kuandaliwa vyeo vya kisiasa?..

Unazungumzia vyuo vipi Bigii?.. Au hukumsika yule Profesa aliyesema degree holder warudi VETA?

My take; Vyuo hivi kwanza vinapaswa ku- claim autonomy yake kwa walioipoka kwanza ndiyo waje na masuala mengine. Tunafahamu Vyuo vina " code of professionalism na code of ethics" wasimamie hayo kwanza .
 
Nchi imeharibiwa kabisa na CCM.
Kila sehemu ni dhuluma ndiyo imetamalaki tu.
 
Hakuna muhadhiri anayeweza kugoma. Kwanza wahadhiri wengi ni machawa. Pili wananjaa sana.Wahadhiri wanaongeka kwa elfu 10, elfu 50 kirahisi tu. Yaani ndio utegemee wagome kwa sababau ya mwenzao.
Mkuu kuna jambo hulijui. Unafikiri Yuda janakaongea kwa bahati mbaya? Unafikiri Yuda yuko peke yake? Je unafahamu nani yuko nyuma yake?

Kuna mtego umeshawekwa unasubiriwa ufyatuke mtu anase humo.
 
Kama si mmoja wao basi ajiengue...90% ni michezo ya kila siku kuwachota wajinga wao wawe wapinzani na watu wao kwa pamoja.
Akisimama kiongozi 'A' azomewe akisimama mwingine ashangiliwe tena na hadhira ileile🙌
 
Ni kufwatia kukamatwa na kupewa kesi ya ugaidi kwa wenzao wa UDOM
Vikao vya chama cha wahadhiri vyuo vikuu vinaendelea ili kuona namna ya kuchukua hatua stahiki za haraka
Eitha kutokana na hali ilivyo usiri umetawala na huenda wakatoka na azimio moja tu la mgomo.
Inatakiwa na wanavyuo wa nchi nzima wagome na kukinukisha. Hii ni nfasi nzuri sana. Bila kufanya hivi hawa wauaji wataendelea kutuumiza. NB: Neno ''eitha'' umekosea kuandika na pia; hata ungepatia bado umelitumia vibaya.
 
Inatakiwa na wanavyuo wa nchi nzima wagome na kukinukisha. Hii ni nfasi nzuri sana. Bila kufanya hivi hawa wauaji wataendelea kutuumiza. NB: Neno ''eitha'' umekosea kuandika na pia; hata ungepatia bado umelitumia vibaya.
Vyuo havina meno Boss
 
Back
Top Bottom