soine
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 2,113
- 2,329
Teteh teteh! Wewe sio ma mkwe bali ba mkwe. Hakika ukweli unaumaa. Pole ee tena sana tu!
Waliomuweka madarakani waliona kuwa anawafaa, wewe sio mwanachama wa Udomasa, kwa ukerekwe? Kama sio madai ya msingi-kwa nini ofisi yenu ilipokea mishahara mipya ikipga kimya badala ya kutoa taarifa kwa wadau kuwa mishahara imekuja lakn ina makosa? Je, sio nyie mliotamka na kubandika kuwa 95% ya wafanyakazi hawastahili kupewa pesa za kujikimu? Sasa iweje leo mnapinga tamko lenu kuwa mtaanza kupunguza madeni kupitia OC? Kpnd hicho mlijigamba kweli hata baadhi yenu mlidiriki kusema Udom wameajiriwa watu 3 tu, wengne wote ni njaa ndo zilizowaleta. Tena mkieneza kasumba eti achaneni na washika chaki na njaa zao. Hamjui kuwa posho na mishara yenu ni kodi za hao hao washka chaki? Huenda ikawa hizo fedha na nyumba mnazojenga na kuhonga ndo hzo zinazodaiwa leo.
Mtabana na kujibinya wee ila katawaponyoka tu.
Anguko la mtu mzima ****** hulia mbwataaa!
Kweli itawaweka huru.
Poor Kikula & Kinabo, bila shaka haya yote hayapasi kuwakuta, anyway chachu kidogo huchachua donge nzima.

Wacha kudanganya watu. Wewe unaelewa fika unachosema si sahihi. Na ukweli unao.
I. Mishahara mipya
Unafahamu kwa takwimu ulizopewa na Menejimeti kuwa hayumkini kuwa HAZINA walileta mishahara mipya mwezi Novemba kama unavyodai.
Taarifa nilizonazo, umepewa copies za ex-chequers kuanzia mwezi wa saba zinazoonyesha kuwa UDOM imekuwa ikipokea fedha pungufu za mishahara toka HAZINA. Copies hizo zinaonyesha kuwa mwezi Oktoba na Novemba UDOM ilipokea kiasi cha fedha kinachofanana na hakuna ongezeko kama wewe na huyo jamaa wako wa HAZINA mnavyodai. Ushahidi huo unao.
2. Malipo ya fedha za kujikimu
Makamu Mkuu wa Chuo alishatolea maelezo kwenye mkutano wake na wafanyakazi kuwa Chuo kimeamua kutoa kwa awamu. Wewe hutaki wenzio walioanza kazi mwaka 2007 wapate pesa zao ndiyo maana unawadanganya.
3. Safari ya Msarifu na Mkurugenzi wa Rasilimali Dar es Salaam
Viongozi hawa wanaripoti UDOMASA au kwa Management? Uliambiwa baada ya kikao chenu kazi zote zilisimama. Wewe ni muongo, unajua kabisa kuwa viongozi hawa walikwenda Dar es Salaam kuwasilisha bajeti za mwaka ujao wa fedha. Kwa nini unataka kudanganya wenzio? Usitumie shida za wengine kujitafutia umaarufu.
4. Ulipwaji wa mishahara
Hakuna wizi kama unavyodai. Kama data clerk wa hazina alifanya makosa unataka na Menejiment ifanye makosa pia? Wewe una barua ya ajira inayoonyesha mshahara wako, unapopaswa kuanzia, nyongeza ya kila mwaka na kadhalika. Wewe mwenyewe umetia saini kukubali mkataba huo. Bila shaka unalipwa kulingana na barua yako ya ajira. Kama kuna kiasi kinazidi kutoka Hazina, Menejiment ya UDOM inapaswa kurudisha kinachozidi HAZINA. ukidai ulipwe haki si yako ni ufisadi. Mbona huzungumzii wafanyakazi wanaoletewa fedha pungufu za mishahara yao toka hazina kama wewe ni mkweli? Unavyowadanganya wenzako kuwa waendelee kudai tofauti ya kiasi cha mshahara unaotoka Hazina na unaolipwa na UDOM kwa mujibu wa mikataba yenu ya ajira unawapotezea muda. Hili haliwezekani hata kama utadai miaka 1000 wacha siku 2. Kulipwa tofauti unayodai ni kuvunja sheria na wewe unalijua hilo. Kwa kuwa serikali haiwezi kuvunja sheria, hata ukidai kwa rais wa jamhuri hawezi kusikilia upuuzi wako. Wewe unatia aibu wasomi wa nchi hii. Kumbe hujui hata sheria ndogo ndogo za kazi?
Sera ya Mazishi
Leo nimeona tangazo linalowataka wafanyakazi wasiotaka kuendelea na sera ya mazishi wajitoe, mbona hili husemi.
Bwana Paul Loisulie, wewe ulitumwa kwenda Dar kufuatilia masuala ya mishahara, umeshaieleza Menejimenti kilichojiri huko? Mmefikia muafaka gani na menejiment? Mbona husemi kama ulilipwa pesa za kwenda Dar kwa masuala hayo? Wewe ni mwizi, kwa nini umechukuwa michango ya wanachama wa UDOMASA wakati Menejimeti ya UDOM imekulipa zaidi ya laki nne kwa safari yako ya Dar kama posho ya kujikimu na nauli?
Sisi tunaipenda UDOM, tunataka watoto wetu wasomeshwe. Serikali ilishatangaza mishahara mipya na italipwa tu. Migogoro ya nini?
Mishahara kulipwa tofauti iachie Menejiment na HAZINA. Wewe kama ni Mzalendo kweli ifahamishe HAZINA ufisadi wa uongozi wa UDOM kisha waachie wenyewe washughulikiane. Kama una ushahidi zaidi wa ufisadi peleka TAKUKURU wafanye kazi zao. Mbona hili hufanyi?
Wewe umepoteza siku mbili bila kufanya kazi, je ukatwe mshahara? Kama sivyo, huu nao si ufisadi?
Menejiment ya UDOM ikikuchukulia hatua za kisheria utalia na nani? Usiwaponze wenzio bila sababu za msingi.
WEWE HUFAI KUWA MWENYEKITI WA UDOMASA. ACHIA WATU WENYE UWEZO NA UPEO NAFASI HIYO. KWA NINI HUTAKI KUJIFUNZA KUTOKA KWA MZEE SHIVJI AU MAREHEMU CHACHAGE ENZI ZA UDASA. HAWA HAWAJAHI KUWA NA MADAI YA KIPUUZI KAMA HAYA YAKO.