Mgomo wa waalimu ni halali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa waalimu ni halali

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mzee wa Gumzo, Oct 13, 2008.

 1. Mzee wa Gumzo

  Mzee wa Gumzo Senior Member

  #1
  Oct 13, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jumamosi tulimsikia waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Prof.Jumanne Maghembe na waziri wa utumishi Hawa Ghasia wakitoa msimamo wa serikali kuhusu sakata la waalimu kutokulipwa malimbikizo yao yanayofikia bilioni 16.

  Katika maelezo ya serikali kwa umma mawaziri hao walidai kuwa waalimu wanaidai serikali bilioni saba na ushee tu kwa maana kuwa walishaanza kulipwa malimbikizo yao na serikali ingali inaendelea kulipa.Serikali ilitumia nafasi hiyo kuwataadharisha waalimu kutokugoma kwa madai kuwa mgomo utakuwa batili.

  Kwa upande mwingine, jana jumapili CWT imetoa tamko kuwa taarifa ya seriklali siyo ya kweli kuhusu mkataba unaodaiwa kufikiwa kati ya pande hizo mbili mapema mwezi huu.Vilevile CWT imepinga takwimu zilizotolewa kuhusu malimbikizo ya waalimu.

  Nia yangu hasa ni kutaka tufanye tafakari ya kina juu ya sakata hili na staili ya serikali yetu kuyashughulikia matatizo ya wafanyakazi wa umma nchini.Hii siyo mara ya kwanza kwa serikali kutoa vitisho kwa waalimu kuhusu kugoma kwao.Mara zote waalumu wamekuwa wakilalamikia hali iliyopo na wakati waot serikali imekuwa ikitoa ahadi kuwa inahakiki majina na madai yao kabla ya kuwalipa.

  Hali hii ya kuwapiga waalimu danadana kila wakati inapaswa kufika ukomo na waalimu wapewe heshima na umuhimu stahili.Serikali inaona njia ya kutatua matatizo ya waalimu ni kuwatishia kuwa watachukuliwa hatua za kinidhamu.Huu siyo mfumo mzuri wa uongozi.Kwa miaka siyo chini ya kumi sasa waalimu hawajaonja utamu wa fani yao na malimbikizo ya madai yao hayalipiki kwa urahisi.

  Mfano mzuri ni malipo yaliyofanywa mwezi wa nane mwaka huu.Serikali ilidhamiria kuwaficha ukweli waalimun kwa hazina kuchelewesha salary slip za waalimu mpaka leo lakini chakustaajabisha zile za septemba zilishatolewa.

  Kwa ujumla waalimu wanpaswa kufika pahala wakasema YATOSHA.Kama wazazi na walezi wanajukumu zito sana na kugoma kwao kuna athari kwa watoto wa taif hili lakini hawawezi kuendelea kufundisha wakati mioyo yao imejaa ukiungu wa sononeko na kukata tamaa.

  Vitisho haviwezi kuwa suluhisho, muhimu kwa waalumu kufikia azma yao ya kugoma na wasiwepo watakaowasaliti wenzao.Tanzania lazima tujifunze kudai haki zetu hata kama ni kwa kulala njaa na kuonekana wabaya.

  Haki ya mtu haiombwi inakuwepo tu.Usipoiona basi ujue kuna mtu kaificha na anataka umpigie magoti.Kataa kufanya hivyo.
   
 2. M

  MpiganajiNambaMoja Member

  #2
  Oct 13, 2008
  Joined: Sep 20, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Matitizo ya walimu na wafanyakazi wa serikali kwa ujumla yanatokana na mfumo mbovu wa utumishi serikalini. Mfumo wa utumishi wa serikali kuanzia mtu anapo ajiriwa hadi anapostafu ni ule ule toka wakati wa uhuru na auendani na mahitaji ya sasa. Idadi ya walimu imeongezeka sambamba na shule. Inahitaji mfmo madhubuti katika life cycle ya utumishi kuanzia kuajiri hadi mtu anapo stafu.

  Kwa mfano inachukua miezi 6 hadi mwaka mtumishi mpya kuanza kulipwa mshahara. Na anavyolipwa anaanza kulipwa kwa mwezi huo, na inabidi ajeze tena form nyingine ili kudai mshahara wake ambao haujalipwa (malimbikizo). Sasa kwa nini waajiri walimu/watumishi wapya kama fedha za kuwalipa zinakuwa hazipo? Kwa nini ichukue muda mrefu hivyo kuwalipa watumishi wapya.

  Kero nyingine ni Uhamisho. Mwalimu anapewa uhamisho bila malipo ya uhamisho. Anadai miaka na miaka. Hivi kwa nini umuhamishe mtu kama huna bajeti ya kuhamisha watu. Sitaki kuamini kuwa bajeti ya kuhamisha inakuwa haipo, ila fedha za walimu zinachezewa na watu.

  Ili matatizo kama haya ayasiendelee ni vyema mfumo bora zaidi ukatafutwa. Kompyuta kama zikitumika kikamilifu zitatatua matatizo mengi ya sasa.
   
 3. Matemu

  Matemu Member

  #3
  Oct 13, 2008
  Joined: Nov 29, 2007
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Walimu tupo nyuma yenu katika mgomo huu.Nimefurahi kusikia walimu mwaka huu hamna utani na serikali katika kudai stahili yenu.Kwanza huwa najiuliza hivi serikali inaona uzito gani kuwaomba msamaha walimu kwa kuwacheleweshea malipo yao halali? Halafu inakuja juu na kuwatishia kana kwamba wanadai kisichawahusu?
  Walimu hapa hamna jinsi pesa zenu nahakika zipo ila kunahitajika MGOMO MKUBWA ILI KUZIPATA tupo nyuma yenu WATANZANIA ingawa watoto wetu ndio watakaoathirika.
   
 4. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135  Watoto wataathirika iwapo waalimu hawatafanya mgomo.  .
   
 5. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2008
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Walimu ndio daraja la wanasiasa wetu; wamesoma toka huko kuondoa ujinga; sasa wanaongoza kama wanasiasa lakini hawawakumbuki waliowafikisha hapo; mbaya sasa unatishwa; kwa nini; nasikia CWT imejiandaa hata kulipa walimu watakaopata matatizo kama matoke ya mgomol hii ni hatua nzuri sana; CWT kaza booty; msilegee sis tuko pamoja na nyie; haki ya TZ haipatikani bila kulazimisha ( si mmeona hata TRL, NBC, TTCL nk). Watoto wataathirika zaidi kama walimu hawatalipwa; TZ amukeni jamani walimu wetu wanateseka
   
Loading...